Tanzia: Madame B na Kijino wamefiwa na Baba yao

Kila nafsi itayaonja mauti mzee wetu katangulia na sisi tunafuata.. Mwenyezi Mungu awape faraja na awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu...
 
Habari za muda huu waungwana?
Nimepokea taarifa asubuhi hii kuwa member wenzetu Madame B na Kijino wamefiwa na baba yao.

Taarifa niliyoipata toka kwa Madame B mwenyewe inafafanua zaidi kuwa Mzee alikuwa anaumwa. Amefariki asubuhi ya leo tarehe 25-10 2012..

Msiba upo Chama, Mbezi Mwisho{Ya Kimara}. Ni njia ya kuelekea Maramba Mawili..

Mipango ya mazishi inaendelea sasa hivi eneo ambalo msiba upo{Chama. Njia ya kwenda Maramba Mawili}

Taarifa zaidi zitaendelea kuwafikia kadri ambavyo itakuwa imepangwa. Wana JF tuungane pamoja katika kipindi hichi kuwafariji wenzetu {Wafiwa} kwa kuwapa Moyo na kuwaombea faraja na nguvu toka kwa Mungu.

Kwa taarifa na maelezo zaidi jinsi ya kufika eneo la tukio {Kwa wale watakaohitaji kwenda msibani} piga namba hii ya 0716394882..

Updates:

Nimepata taarifa muda huu kutoka kwa Madame B kuwa eneo la msiba limebadilishwa. Msiba umehamishiwa nyumbani Kinondoni B Mtaa wa Dunga. Sio kule Mbezi kama ambavyo taarifa ya awali ilieleza... Namna nzuri ya kufika na kupitia njia ya kuelekea Mwananyamala hospital kutokea Kinondoni Biafra.

Tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Poleni sana ndugu zangu na asante kwa taarifa. Swali, mazishi yanatarajiwa kufanyika lini?

Mungu wetu ni mwema sana, atawalinda na kuwaongoza kila hiitwapo leo.Tuna tumaini ata wapa faraja katika kipindi hiki kigumu, nasi tutaendelea kuwaombea kila leo!

Wote wata waacha lakini Baba yetu aliye mbinguni hawezi kuwaacha kamwe.
 
Poleni sana Madame B na Kijino mwenyezi Mungu awape moyo wauvumilivu katika hiki kipindi kigumu, Wana JF wa daa tushikamane kwenda kuwapa pole na kuwafariji wenzetu.
Ndio njia yetu sote tukeshe tukiomba hatujui siku wa saa..
 
Poleni sana MadameB na Kijino.Mungu akawape faraja na moyo wa uvumilivu. Rest in Peace baba yetu.
 
Poleni sana wafiwa Madame B na Kijino.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya mzee wetu mahali pema peponi apumzike kwa amani.
Poleni sana sana.
 
Last edited by a moderator:
Habari za muda huu waungwana?
Nimepokea taarifa asubuhi hii kuwa member wenzetu Madame B na Kijino wamefiwa na baba yao.

Taarifa niliyoipata toka kwa Madame B mwenyewe inafafanua zaidi kuwa Mzee alikuwa anaumwa. Amefariki asubuhi ya leo tarehe 25-10 2012..

Msiba upo Chama, Mbezi Mwisho{Ya Kimara}. Ni njia ya kuelekea Maramba Mawili..

Mipango ya mazishi inaendelea sasa hivi eneo ambalo msiba upo{Chama. Njia ya kwenda Maramba Mawili}

Taarifa zaidi zitaendelea kuwafikia kadri ambavyo itakuwa imepangwa. Wana JF tuungane pamoja katika kipindi hichi kuwafariji wenzetu {Wafiwa} kwa kuwapa Moyo na kuwaombea faraja na nguvu toka kwa Mungu.

Kwa taarifa na maelezo zaidi jinsi ya kufika eneo la tukio {Kwa wale watakaohitaji kwenda msibani} piga namba hii ya 0716394882..

Updates:

Nimepata taarifa muda huu kutoka kwa Madame B kuwa eneo la msiba limebadilishwa. Msiba umehamishiwa nyumbani Kinondoni B Mtaa wa Dunga. Sio kule Mbezi kama ambavyo taarifa ya awali ilieleza... Namna nzuri ya kufika na kupitia njia ya kuelekea Mwananyamala hospital kutokea Kinondoni Biafra.

Tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Updates.

Taarifa ambayo imetolewa mda huu ni kwamba Mwili wa marehemu utasafirishwa Jumapili tarehe 28-10- 2012 . Mwili unasafirishwa kwenda Lushoto.

Taarifa zaidi zitawajia kadri ambavyo zitatokea..

poleni sana wafiwa,tupo pamoja katika kuomboleza msiba wa baba yetu mpendwa,R.I.P BABA
 
Back
Top Bottom