JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Ndugu zangu kuna taarifa nimezipata kuwa inadaiwa kuna Mgodi umetitia kutokana na mvua zinazoendelea Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu na Watu kadhaa kufukiwa.
Mgodi upo Kijiji kinaitwa Ikinabushu, details za jina na kilichotokea zaidi bado sijazipata.
Mliopo karibu na Bariadi tupeni taarifa zaidi.
======
WATU ZAIDI YA 10 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA
SIMIYU: Tukio la kutitia kwa kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa Ikinabushu uliopo Wilayani Bariadi linadaiwa kusababisha watu zaidi ya 10 kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Mkoa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine wa Wilaya na Mkoa wote wapo eneo la tukio.
Hali hiyo imetokea wakati mvua zikiendelea kunyesha kwa wingi Mkoani #Simiyu. Taarifa zaidi zitafuata.
=====
UPDATES
Zoezi la kufukua miili ya wachimbaji waliofukiwa na kifusi katika mgodi wa IKINABUSHU uliopo kijiji cha Ikinabushu Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu imefikia 22 hadi kufikia usiku wa Jumamosi January 13.
Mkuu wa Wilaya Bariadi Simon Simalenga amethibitisha idadi hiyo Usiku huu wakati akizungumza na #CloudsDigital