Fahamu kuhusu Destination Marketing Business

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,504
5,539
Habari za wakati huu;
Ni matumaini yangu kwamba mnaendelea salama na juhudi zenu za ujenzi wa taifa.
Leo ninawaletea mjadala kuhusu model ya biashara inayoitwa Destination Marketing Services(DMS).Kampuni zinazofanya shughuli hizi huitwa pia kama Destination Marketing Corporation(DMC)

Destination Marketing ni nini?Hii ni biashara au huduma inayohusika zaidi na kupromote eneo au maeneo fulani kwa ajili ya kuwavutia watu kwa ajili ya utalii,biashara,uwekezaji au kuishi.Lengo kubwa la Destination Marketing ni kumpatia mtu ambaye ni mgeni taarifa mbalimbali kuhusu eneo fulani ili kumvutia kwa ajili ya ama uwekezaji,utalii,biashara na hata kuishi.Inahusisha ukusanyaji na usambazaji wa taarifa mbalimbali kuhusu eneo fulani ikiwamo utamaduni,huduma,gharama za maisha,hali ya kiuchumi na biashara,hali ya hewa pamoja na fursa mbalimbali na vivutio vilivyopo katika eneo husika.Fursa zinaweza kuwa katika sekta rasmi na hata katika sekta isiyokuwa rasmi.

Nyingi kati ya kampuni zinazofany Destination Marketing zimejikita zaidi katika vivutio vya utalii ingawa unaweza kufanya destination marketing kwa ajili ya uwekezaji, biashara n.k. cha muhimu ni kuhakikisha unakuwa na taarifa za uhakika kuhusu eneo fulani na unakuwa na namna ya kutengeneza fursa na kuwasaidia wageni katika eneo hilo.

Jinsi ya kuanzisha/kufanya shughuli za Destination Marketing
Kufanya shughuli za destination marketing unaweza kufanya kama Local/Mwenyeji au kufanya kma Expert yaani mtaalam.Unapofanya kama local unakuwa ni mtu unayeishi na kufanya kazi katika eneo unaloishi na hivyo unakuwa unalipromote eneo hili.Unaweza pia kufanya kama expert ambapo unatembelea eneo husika na kuangalia maeneo yanayohusiana na utaalamu wako kwa kutegemea pia eneo lako la uzamifu.

Kwa mfano ukiamua kufanya DMS kwa mkoa wa Mwanza unaweza Kujii ta Mwanza GUIDE na ukawa unatoa taarifa mbalimbali kuhusu mkoa wa Mwanza na ukawapa watu taarifa za wakati huu na maeneo na fursa mbalimbali za mkoa mwanza.Vili unaweza kuamua tu kuwa unajihusisha na suala la uwekezaji katika mkoa wa Mwanza ambapo kazi yako zaidi ni kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa wa mwanza na ukawa ni mtaalamu katika hilo.

Katika zama hizi za Utandawazi unaweza kutumia teknolojia mbalimbali kama mitandao ya kijamii na tovuti kutengeneza maudhui yanayohusu eneo husika na kuandika maandiko mbalimbali kwa ajili ya kuonesha uzuri na fursa zilizopo.
Karibu tujadili zaidi namna ambavyo tunaweza kutumia fursa hii ya DMS kwa ajili ya kutengeneza kipato na fursa kwa ajili yetu na maendeleo ya biashara zetu.

Je kuna fursa gani za kibiashara,kiutalii au hata kiutamaduni katika eneo lako ambalo unaweza kutumia kama mwanzo wakuingia katika biashara ya DMS

Iwapo unagependa kufahamu zaidi unaweza kuwasiliana kwa email:masokotz@yahoo.com
 
Back
Top Bottom