Tanzia: Madame B na Kijino wamefiwa na Baba yao

I know for certain that we never lose the people we love, even to death. They continue to participate in every act, thought and decision we make. Their love leaves an indelible imprint in our memories. We find comfort in knowing that our lives have been enriched by having shared their love. POLE SANA MADAME B.:doh:
 
Mwenyezi Mungu awajalie shufaa katika kipindi hiki kigumu, may your dad RIP
 
poleni sana madme b na kijino kwa msiba!
Habari za muda huu waungwana?
Nimepokea taarifa asubuhi hii kuwa member wenzetu Madame B na Kijino wamefiwa na baba yao.

Taarifa niliyoipata toka kwa Madame B mwenyewe inafafanua zaidi kuwa Mzee alikuwa anaumwa. Amefariki asubuhi ya leo tarehe 25-10 2012.

Msiba upo Chama, Mbezi Mwisho{Ya Kimara}. Ni njia ya kuelekea Maramba Mawili..

Mipango ya mazishi inaendelea sasa hivi eneo ambalo msiba upo{Chama. Njia ya kwenda Maramba Mawili}

Taarifa zaidi zitaendelea kuwafikia kadri ambavyo itakuwa imepangwa. Wana JF tuungane pamoja katika kipindi hichi kuwafariji wenzetu {Wafiwa} kwa kuwapa Moyo na kuwaombea faraja na nguvu toka kwa Mungu.

Kwa taarifa na maelezo zaidi jinsi ya kufika eneo la tukio{Kwa wale watakaohitaji kwenda msibani} piga namba hii ya 0716394882..

Updates:

Nimepata taarifa muda huu kutoka kwa Madame B kuwa eneo la msiba limebadilishwa. Msiba umehamishiwa nyumbani Kinondoni B Mtaa wa Dunga. Sio kule Mbezi kama ambavyo taarifa ya awali ilieleza... Namna nzuri ya kufika na kupitia njia ya kuelekea Mwananyamala hospital kutokea Kinondoni Biafra.

Tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
 
Asanteni sana,sana tena sana jamii yote ya wana Jf kwa kutufariji ktk kipindi hiki kigumu.
Ila hatutaweza kuupindisha ukweli kuwa Baba yetu Kipenzi hayupo tena nasi hapa Duniani.
Ameondoka wakati bado tunamuhitaji Baba.
Mbele yetu,Nyuma yako,sote tu wapitaji na Kwake Tutarejea.
Nawashukuru woote kwa Kutufariji.
Asanteni sana.
Pole wangu rafiki najua inaumiza sana najua vile unajisikia zidi kumwomba MUNGU ampe baba rehema ya kuuona uso wake!
love yu SIS!
TUPO PAMOJA mamie,si unajua my dear!
 
jamani poleni sana kwa kuondokewa na mzee wenu Mungu awape nguvu kwa kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana Madame B na Kijino, Mungu awape faraja na nguvu wakati wote wa msiba...
 
Asanteni kwa kutufariji wanajamii wenzetu, ndio hvyo tumefiwa, na tumebaki yatima, mama yetu alitangulia miaka 4 nyuma, mimi ndio mkubwa, nimebaki na jukumu la kuwalea wadogo zangu, tunaomba muendelee kutufariji
Pole sana Kijino MUNGU awape nguvu kupita hapa salama na wadogo zako.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana Madame B, Kijino pamoja na ndugu jamaa na marafiki wote wa familia ya marehemu.
Nawaombea kila la kheri na moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu mlichompoteza baba mpendwa.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana wadau na familia nzima kwa msiba huu mzito wa kuondokewa na nguzo muhimu katika familia, Mungu awajalie uvumilivu na kuwawezesha kumpumzisha mzee wenu salama.
 
Poleni sana kwa kufiwa. Madame B, ukimaliza msiba nna maswali yangu kadhaa.
Mungu awape nguvu.
 
Back
Top Bottom