Tanzia: Madame B na Kijino wamefiwa na Baba yao

pole sana mzee wetu! MUNGU wetu akusamehe makosa yako, upumzike kwa amani, AMEN!
 
Poleni sana Madame B na Kijino
Mungu awape nguvu kuvumilia maumivu na misukosuko yote ya msiba!
Mungu ailaze roho ya mzee wetu mahala pema peponi!
Amina!
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana Wandugu!

MUNGU MWENYE MAMLAKA AWAPE NGUVU KTK KIPINDI HIKI KIGUMU!

Nitawaseach hewani soon!
 
Aise poleni sana wafiwa; kwakweli kuondokewa mzazi ni pigo kubwa sana. Mungu awape faraja na moyo wa kuyapokea, hayo kwa ustahimilivu. Mungu alituazima baba yetu na sasa amemchukua kwake kusipokuwa na shida wala magonjwa.

RIP baba Madame B na Kijino
 
Last edited by a moderator:
Mungu awape roho ya ustahimilivu wafiwa wote ktk kipindi hiki kigumu.
 
Madame B na Kijino poleni kwa msiba huu mkubwa... Mwenyezi Mungu awajaalie wepesi katika shughuli zote za mazishi na awazidishie Imani na Amani katika nyoyo zenu.

Nicas asante saaana kwa taarifa, na kutuhusisha katika huu msiba. Pamoja saana.
 
Pole sana shosti na miss mwenzangu Madame B! Pole sana Kijino!
Nitakuwepo leo baada ya mida ya kazi kuwafariji.
Mungu ampe taji ya uzima mzee wetu!
 
Asanteni kwa kutufariji wanajamii wenzetu, ndio hvyo tumefiwa, na tumebaki yatima, mama yetu alitangulia miaka 4 nyuma, mimi ndio mkubwa, nimebaki na jukumu la kuwalea wadogo zangu, tunaomba muendelee kutufariji
 
Usijali Kijino. Tuko pamoja katika kipindi hiki kigumu.. Poleni sana kwa kumpoteza Baba.
 
Last edited by a moderator:
Asanteni kwa kutufariji wanajamii wenzetu, ndio hvyo tumefiwa, na tumebaki yatima, mama yetu alitangulia miaka 4 nyuma, mimi ndio mkubwa, nimebaki na jukumu la kuwalea wadogo zangu, tunaomba muendelee kutufariji

Aisee...Poleni sana.. Mtayashihda haya.....simama tu upande wa Mungu, tenda haki na utashinda Kijino. Poleni nilitamani sana nifike huko ila sitaweza kwa sasa nipo mbali kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Nawashukuruni wana Jf Woote kwa Kutufariji katika kipindi hiki kigumu.
Hatuwezi kuupindisha ukweli kuwa Baba yetu Mpendwa ametuacha wakati bado tunamuhitaji sana.
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe.
Asanteni sana,sana,sana.
 
Asanteni sana,sana tena sana jamii yote ya wana Jf kwa kutufariji ktk kipindi hiki kigumu.
Ila hatutaweza kuupindisha ukweli kuwa Baba yetu Kipenzi hayupo tena nasi hapa Duniani.
Ameondoka wakati bado tunamuhitaji Baba.
Mbele yetu,Nyuma yako,sote tu wapitaji na Kwake Tutarejea.
Nawashukuru woote kwa Kutufariji.
Asanteni sana.
 
Nawashukuruni wana Jf Woote kwa Kutufariji katika kipindi hiki kigumu.
Hatuwezi kuupindisha ukweli kuwa Baba yetu Mpendwa ametuacha wakati bado tunamuhitaji sana.
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa,
Jina Lake Lihimidiwe.
Asanteni sana,sana,sana.

Poleni sana Madame B na Kijino. Mungu awape uvumilivu katika kipindi hki kigumu kwenu.. Kazi ya Mungu haina makosa.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana wafiwa. Mungu Aiweke pema roho ya marehemu.
 
Back
Top Bottom