Baba na mwana wanapoacha majonzi katika jiji la Washington DC

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,107
52,832
GiZA LAANZA KUTAWALA - 1
Matumizi ya nyaraka za vitambulisho na
umuhimu wa kushirikisha jamii katika kupambana na uhalifu.

Watu 17 walikufa ndani ya siku chache, na wengine 23 walijeruhiwa.
Oktoba 2002 wakazi wa jimbo la Washington DC na maeneo ya jirani walijikuta kwenye wakati mgumu wa
matishio ya mauaji, ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu kulipuliwa kwa kituo cha biashara cha kimataifa mjini New York. Kila mtu hakudhani kama yupo salama. Mauaji hayo ya kufululiza yalianza asubuhi ya tarehe 2 Oktoba kwa mwanaume wa miaka 55 aliyekuwaa meegesha gari yake maeneo ya Wheaton, Meryland.

Baada ya kufanya manunuzi ndani ya
'Supermarket, James Martin alitoka nje kuelekea mahali alipoegesha gari yake. Mkewe na mtoto wake wakiume mwenye umri wa miaka 11 walikuwa wakimsubiri ndani ya gari. Lakini James Hakufika. Haikujulikana nini kimetokea, bali watu walishtukia tu mtu amedondoka huku akivuja damu nyingi kifuani. Mke wa
James alipiga kelele za kuomba msaada huku akijitahidi kupiga simu kitengo cha huduma za dharura. Haikusaidia. Dakika chache baadaye James Martin alikata roho.

Uchunguzi wa awali ulionesha James alishambuliwa kwa risasi. Mgongoni mwakwe palionekana tundu dogo ilipoingia risasi na tundu kubwa lilionekana kifuani ilipotokea risasi, hii iliashiria kwamba alishambuliwa kwa silaha yenye nguvu kubwa. Ni silaha ya kivita.

Maofisa wa polisi walijitahidi kutafuta
viashiria vya ushahidi wa uhalifu huu ikiwa ni pamoja na maganda ya risasi, lakini hawakupata chochote katika eneo lile.
Ni nani huyo aliyeamua kukatisha maisha ya James Martin, na kwanini aliamua hivyo?

Kabla swali hilo halikupata majibu, asubuhi ya saa 1:40 siku iliyofuata, yaani Oktoba 3, ugumu wa swali uliongezeka. Sunny Buchanan, kijana wa miaka 39
alianguka ghafla na kugalagala wakati akifanya kazi ya kufyeka nyasi kwa kutumia mashine ya kukatia nyasi.

Watu wa karibu walifikiri amejiumiza mwenyewe kwa mashine hiyo. La! Haikuwa hivyo, wala haikuwa ajali. Muuguzi mmoja miongoni mwawa hudumu wa dharura waliofika kumchukua Sunny alisema, hakuwahi kuona mtu akivuja damu vibaya
kama huyo tangu kazi ya kutoa huduma za dharura miaka zaidi ya kumi iliyopita.
Sunny aliuawa kwa risasi iliyotoka
kwenye silaha nzito. Na huo ulikuwa mwanzo tu wa asubuhi ya damu katika kaunti ya Montgomery –Washington DC.

Dakika chache baadaye, saa 2:07 asubuhi, taxi moja iliingia kujaza mafuta kwenye kituo kimoja cha mafuta kando ya barabara ya Connectcut, kilometa takribani 8 kutoka alipouawa Sunny. Mwanamke mmoja kwa jina Caroline naye alikuwa amefika kabla
ya taxi hiyo. Wakati akiweka mafuta, taxi ilikuwa ikisubiri amalize. Ghafla, mlio wa bunduki ukasiskika.

Caroline alipagawa kidogo, lakini alipotazama huku na kule, alimuona dereva wa taxi ile iliyoegeshwa nyuma yake akiwa anatapatapa nyuma ya usukani. Damu nyingi ilikuwa imetapakaa kwenye vioo vya taxi ile. Nini kinaendelea?

Watu wawili walikuwa wameuawa kwa risasi yenyebnguvu ndani ya dakika 31 tu, umbali wa kilometa nane kutoka tukio moja hadi lingine. Na bado haikutosha. Dakika chache baadaye, muuaji alifanya tena kazi yake. Sarah Ramos alikuwa akisubiri usafiri nje ya
makazi ya watu mashuhuri mahali palipoitwa Leisure World. Mwanafunzi huyu wa sheria aliingia Marekani akitokea El Salvadol. Akiwa mwanafunzi wa sheria,
aliamua kufanya kazi za usafi wa ndani ili apate kipato cha kumsaidia kuunganisha siku. Sarah hakujua, si yeye bali roho yake ndiyo ilikuwa ikisubiri safari pale Leisure World. Safari hii hakukusikika mlio
wa bunduki, lakini mashushuda walishtukia mtu amedondoka huku akivuja damu nyingi kichwani na shingoni. Risasi ya kaliba 223 ililengwa kwa Sarah Ramos, ikatoboa paji la uso na kutokea eneo la nyuma ya kichogo, ikapiga kwenye ukuta wa mgahawa uliokuwa karibu na marehemu, ikadondoka sakafuni.

Idara ya dharura ya Montgomery ilikuwa
bize siku hiyo, lakini waliokusudiwa na muuaji wote waliaga dunia. Na bado haikutosha.
Asubuhi hiyohiyo, Lori Luis Rivera alikuwa akifuta vumbi kwenye gari yake eneo la kituo kimoja cha mafuta. Naye alikufa papohapo baada ya kushambuliwa kwa risasi kutoka kwa muuaji asiyeonekana.

Matukio yote matano ya mauaji
yalitokea ndani ya eneo la kilometa za mraba 25 tu, sawa na eneo la upana wa kilometa 5 na urefu wa kilometa 5. Yawezekana pia muuaji aliwashambulia
watu wengine lakini aliwakosa – kutokana na taarifa za kuonekana alama za matundu yaliyosababishwa na risasi kwenye kuta za baadhi ya majengo.

Mauji yote yametokea maeneo ya wazi yanayotumiwa na watu wote. Hakuna misitu mikubwa, hakuna milima, hakuna eneo la kujificha. Huyu muuaji alikuwa wapi?

Maofisa wa upelelezi wasio na sare
walimwagwa kwenye maeneo yote ya matukio ya mauaji kujaribu kupata taarifa zinazoweza kusaidia. Taarifa moja iliyopatikana kutoka kwa shuhuda wa eneo la Leisure World alipouawa Sarah Ramos, ilihusu gari moja jeupe lenye bodi
iliyofunikwa pande zote. Ni gari ambalo
liliondoka ghafla baada ya Sarah kuanguka chini na kuvuja damu. Lakini magari ya aina hiyo yalikuwa mengi ndani ya kaunti ya Montgomery na shushuda hakuweza kukariri namba za gari aliyoiona.

Miili mitano ya marehemu ilichunguzwa kwa umakini. Maofisa wa polisi walitaka kujua asili ya majeraha waliokuwa nayo marehemu – ili wapate picha ya mahali muuaji alipokuwa.

Je! Mdunguaji alishambulia kutoka juu ghorofani, au akiwa ardhini?

Wakati maofisa hao wakikuna vichwa kutafuta majibu ya maswali yao, huku
wakisubiri majibu ya uchunguzi wa kitabibu
muuaji aliwarudisha tena kwenye mshtuko.

Baada ya kuwa ameshambulia asubuhi, mchana alipumzika. Ilipofika usiku muuaji alimuua Pascal Shalom, muhamiaji kutoka Haiti aliyekuwa akivuka barabara eneo la mpaka wa kaunti ya Montgomery.

Asubuhi ya tarehe 4 wakazi wa kaunti ya
Montgomery na jimbo lote la Washington DC waliamka wakiwa na mtazamo mpya. Maisha ya kila mtu yalionekana kuwa hatarini kwani muuaji hakuchagua rika, rangi wala jinsia katika malengo yake.

Miongoni mwa watu sita walio uawa ndani ya masaa48 walikuwamo wanaume, mwanamke mmoja na mtoto, tena watu hao walikuwa wa matabaka tofauti; wazungu kwa weusi.

Muuaji hakuchagua wa kumuua.
Uchunguzi wa majeraha kwenye miili ya marehemu sasa ulitoa majibu kadhaa. Majeraha yote yalitokana na risasi yenye nguvu iliyorushwa kwa bunduki ya kivita inayotumika kwa udunguaji kutoka mbali.
Yawezekana ni bunduki aina ya Bushmaster. Ni bunduki yenye nguvu kubwa inayoweza kurusha risasi itakayoharibu eneo kubwa la ndani ya mwili ingawa inapoingia huacha katundu kadogo.Taasisi ya taifa ya kuratibu Pombe, Tumbaku na Silaha za Moto ilifanya uchunguzi wake na kugundua kuwa muuaji hakulenga risasi kutoka sehemu ya juu bali usawa wa ardhini. Maana yake, muuaji hakuwa juu ya ghorofa, au juu ya mti, bali alilenga kutoka chini.

Uchunguzi huu hufanywa kwa kutazama majeraha ya wahanga, namna jeraha la
kuingia risasi inavyohusiana na jereha la kutoka kwa risasi. Ikiwa muuaji alikuwa juu ghorofani, bila shaka jeraha la kuingia risasi litakuwa sehemu ya juu ya mwili kuliko
jeraha la kutoka risasi. Lakini kama majeraha yote mawili yapo kwenye usawa au yanakaribiana usawa basi ni wazi muuaji alikuwa ardhini.

Alikuwa wapi? Alikuwa anajificha wapi?

Kutokana na taarifa hiyo, na kwa namna matukio yalivyotokea maeneo tofauti ndani ya muda mfupi, maofisa wa upelelezi waliamini muuaji anatumia usafiri wa gari.

FB_IMG_17084993901690552.jpg
FB_IMG_17084993809504115.jpg
 
HOFU YAZIDI WASHINGTON DC - 02

Wazo hilo la kwamba muuaji anatumia gari lilizua hofu zaidi na woga ulisambaa kama moto wa msituni. Kila mtu alihofia maisha yake. Je! ni ugaidi mpya baada ya ule wa Septemba 11?

Mchana wa tarehe 4 Oktoba, muuaji alibadili mbinu. Sasa alisafiri hadi kusini mwa Washington DC. Mwanadada Caroline alishambuliwa kwa risasi kwenye eneo la maegesho ya magari wakati akitoka dukani kununua mahitaji yake. Akiwa amelala chini, Caroline alisali kwa ajili ya watoto wake wadogo aliowaacha nyumbani. Bahati nzuri wahudumu wa dharura waliwahi kufika na kumpatia msaada wa haraka. Huyu alikuwa mtu wa kwanza kunusurika kifo kutoka kwa mdunguaji wa washington DC asiyeonekana.

Tutafanya nini? Polisi walijiuliza. Hakuna shahidi wala ushahidi. Hakuna kiashiria cha maana cha kusaidia uchunguzi. Nini kifanyike kuunasa mzimu huu?
Aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa kaunti ya Montgomery, Charles Moose aliamua kukusanya timu yake yote ya wachunguzi ya kaunti hiyo, ikiwa ni pamoja na wale waliokaribia kustaafu waingie mzigoni kumsaka muuaji. Pia aliomba msaada kutoka kwa kila mtu mwenye taarifa zinazoweza kusaidia. Lakini Loh! Hakukuwa na msaada.
Kulikuwa na maoni zaidi ya 100,000 lakini hakuna lilosaidia. Baadhi ya watu walijifanya wao ndio wahusika wa mauaji lakini polisi waligundua ni watu waliokuwa wanatafuta umaarufu tu. Polisi waliendelea na uchunguzi. Walifanya tathmini ya matukio yaliyotokea na kupata majibu kwamba muuaji atakuwa anatumia zaidi barabara zisizo na msongamano ili anapofanya matukio yake aweze kutoroka haraka. Polisi waliamini kama muuaji au wauaji wangetumia njia zenye msongamano basi asingeweza kufanya matukio yote ndani ya muda mfupi. Kwa sababu hiyo, Polisi walimiminika katika maeneo ya barabara za pembeni ya mji wakiwa na nguo za kiraia, wakaweka vizuizi kila walipohisi panafaa kuzuiwa, akilini mwao wakiwa na mchanganyiko wa hofu ya kushambuliwa na mdunguaji lakini pia matumaini ya kumnasa mdunguaji. Hata hivyo, muuaji alikuwa anafikiria mbele zaidi. Hawakumnasa.

Siku tano zilikuwa zimepita na watu saba walikwisha shambuliwa. Hakuna aliyejua nani anayefuata kushambuliwa kwa risasi ya mzimu wa Washington DC. Polisi walianza kuhisi wanashindwa kuilinda jamii yao inayowaamini na walioapa kuilinda. Shirika la uchunguzi la ndani ya Marekani FBI, likaamua kuongeza nguvu kwa polisi wa Montgomery. Fedha taslimu dola za kimarekani laki mbili ziliahidiwa kutolewa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana muuaji. Wakati huo, wakazi wa jimbo la Washington DC wakaanza kujiuliza kama waruhusu watoto wao waende shule au la!
Aron Brown, mwanafunzi wa miaka 13 alikuwa amezuiwa kutumia gari la shule kwa sababu ya usumbufu wa kulakula ndani ya gari. Mama yake akaamua kuwa anampeleka shule yeye mwenyewe. Siku hiyo ya tarehe 8 Oktoba, mama alimshusha Aron karibu na shule. Mara tu baada ya kugeuza gari na kuanza kuondoka akashtuka kumuona Aron kupitia kioo cha pembeni (side mirror) akiwa amelala chini, damu zinamvuja. Kwa jitihada za haraka na bahati, mama yule alifanikiwa kumuwahisha mwanaye hospitali, na baada ya siku 15, madaktari waliona uwezekano wa Aron kuishi. Aron akawa mnusurika wa pili wa shambulio la muuaji asiyeonekana. Kwa kuwa eneo la shule aliposhambuliwa Aron lilikuwa tofauti na maeneo waliposhambuliwa wengine kutokana na kuwa pembeni ya mji na uwepo wa miti mingi, maofisa wa polisi waliona haja ya kufanya uchunguzi wa eneo hilo kwa kina.

Kama bahati, polisi walifanikiwa kupata vitu vitatu; ganda la risasi, ambalo karibu yake kulikuwa na kizibo cha kalamu na karata moja. Karata hiyo ilikuwa imeandikwa kwa kalamu; ‘Dear Policemen, call me God, don’t tell the press’ – maana yake, Rafiki mapolisi, niiteni Mungu, msitangaze kwenye vyombo vya habari.

Wapelelezi waligundua kuwa muuaji ameacha ujumbe huo makusudi na bila shaka anataka kuwasiliana na polisi. Kwanini awasiliane na polisi baada ya kuua watu wengi? Anataka pesa?
Kizibo cha kalamu kilichukuliwa na kupelekwa maabara kupimwa alama za vidole na DNA, lakini hakukuwa na alama za vidole kwenye kizibo hicho. Karata iliyokuwa na ujumbe nayo ilipelekwa maabara kufanyiwa uchunguzi wa alama za vidole, haikuwa na alama zozote. Ganda la risasi lilibaki kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa silaha na matokeo yake yaliashiria kuwa bunduki iliyotumika ni aina ya Bushmaster Riffle. Bunduki hii inaweza kusababisha maafa makubwa hata ikitumiwa na mtu asiye mzoefu. Polisi hawakufikiria haraka kupelekea ganda la risasi maabara kwa ajili ya kutafuta alama za vidole baada ya kuwa zimekosekana kwenye kizibo cha kalamu na karata. Hapo walifanya kosa kubwa.

Oktoba 9, Veterani wa jeshi la Marekani ambaye pia alikuwa muhandisi wa majenzi aliyetunikiwa tuzo kedekede wakati wa vita vya Vietnam, alikuwa akisafiri kutoka Virginia kwenda Maryland. Alisimama njiani maeneo ya Montgomery ili ajaze mafuta. Risasi ya ukubwa wa kaliba 223 ikapasua kichwa chake na kukatisha ndoto zote za uzeeni alizowahi kuota. Siku mbili baadaye, yaani Oktoba 11 Ken Bridges naye aliuawa eneo lingine la kituo cha mafuta huko Virginia. Oktoba 14 muuaji alishambulia tena hukohuko Virginia. Mwanamama Linda Franklin alikuwa amesimama nyuma ya gari lake liloegeshwa nje ya duka kubwa (Supermarket), wakati mumewe alikuwa akirekebisha siti. Risasi ya kaliba 223 ikapasua kichwa na kukatisha maisha ya Linda papo hapo. Kichwa cha Linda kilipasuka vibaya kiasi kwamba ingekuwa ngumu kuitambua sura yake. Lakini wakati huu, shuhuda alitokea. Mathew Doud aliwaambia maofisa wa upelelezi kuwa alimuona muuaji wakati akitoka nje ya duka. Mathew anasema hakumuona sura, lakini ni mwanaume mwenye asili ya watu wa mashariki ya kati akiwa na gari ndogo ya rangi nyeupe, yenye bodi lilofunikwa pande zote. Haraka, polisi walitoa taarifa hiyo hadharani ili kila mtu aweze kutoa taarifa. Siku iliyofuata, mpelelezi mmoja alikuwa akirudia kutazama video zilizonaswa kwenye tukio la mauaji ya Linda. Kwenye video mojawapo, alimuona shuhuda Mathew Doud akitoka nje ya duka dakika tatu baada ya mauaji kufanyika. Aah! Inawezekanaje? Shuhuda Mathew Doud alikuwa muongo. Dakika tatu ni muda mrefu wa kutosha kukimbia maili kadhaa lakini Mathew alidai alimuona muuaji akimshambulia Linda. Wapelelezi wakajiridhisha kuwa ushuhuda huo haukuwa na faida yoyote kwao. Rekodi zote za ushuhuda wa Mathew Doud zikafutwa.

Oktoba 19, Jeff na Stephanie Hopper walikuwa wakisafiri kuelekea Florida. Wakiwa umbali wa kilometa zaidi ya 150 kusini mwa Washington wawili hao waliamini wapo nje ya eneo la hatari. Wakaegesha gari eneo la mgahawa wa Ponderosa ili wapate chakula cha jioni. Punde, ikasikika sauti ya mlio wa bunduki! Baada ya sekunde kadhaa Jeff alianguka chini akiwa anavuja damu eneo la tumboni. Muuaji wa Washington aliibuka tena mahali pasipotarajiwa, kilometa 150 kutoka anapotafutwa. Hatahivyo, huduma za dharura zilisaidia kuokoa maisha ya Jeff baada ya kufanyiwa operesheni tano kwa muda wa siku 18.

Polisi walifika na kufanya uchunguzi katika eneo la mgahawa wa Ponderosa na maeneo ya jirani. Mbwa wa polisi aliyepewa mafunzo ya kunusa harufu ya vilipuzi alifanikiwa kupata ganda la risasi eneo lenye kichaka karibu na mgahawa. Karibu na mahali palipokutwa ganda la risasi kulikuwa na mfuko mdogo wa plastiki uliotundikwa kwenye mti, ndani yake kulikuwa na karatasi yenye ujumbe uliosomeka; ‘Enyi polisi. Niiteni Mungu. Nahitaji dola milioni 10 kwenye akaunti yangu ya benki. La sivyo watu wengi watakufa’.

Pamoja na mahitaji hayo ya fedha, muuaji aliahidi kupiga simu kwenye mgahawa wa Ponderosa alipomrushia risasi Jeff Hopper usiku uliopita.
Asubuhi ya Oktoba 21 maofisa wa polisi na waandishi walikusanyika kwenye mgahawa wa Ponderosa, kisha askari polisi wakatangaza kupitia vyombo vya habari kuwa wapo mahali hapo kwa ajili ya muuaji aliyeahidi kupiga simu kuongea nawo. Hatimaye, polisi walijikuta wakizungumza na muuaji kwa mara ya kwanza. Muuaji alipiga simu na kuwataka polisi wafuate matakwa ya kwenye ujumbe alioacha, la sivyo watu wengi watakufa. Aliwaambia pia wasikilizaji wengine kwamba watoto wao hawapo salama. Wakati akizungumza na simu, polisi walitumia mbinu ya teknolojia ya mawasilino kujua mahali alipo muuaji huyo. Wakagundua simu ilikuwa ikitoka mahali fulani kwenye kituo cha mafuta mbali kidogo kutoka mgahawani pale. Dakika 33 baadae, polisi waliwakamata watu wawili waliokuwa ndani ya gari ndogo nyeupe, ya kubebea mizigo. Lakini watu hao walikuwa ni wahamiaji haramu tu, hawakuwa wahusika wala hawakuwa na mahusiano yoyote na muuaji wa Washington DC.

Hatahivyo, mdunguaji wa Washington DC alifanya kosa moja kubwa wakati alipopiga simu kuzungumza na polisi; alitumia sauti yake halisi wakati polisi na vyombo vya habari vilikuwepo na kurekodi sauti hiyo.
Wakati huohuo wachunguzi wa maabara walijitahidi kupata alama za vidole kwenye mfuko wa plastiki uliokutwa kwenye mti usiku wa shambulio la Jeff kwenye mgahawa wa Ponderosa. Alama za vidole zilipatikana, lakini hazikufanana na mtu yeyote kwenye mfumo wa kanzi data ( database) wa taifa. Kwa mantiki hiyo, polisi walipata alama za vidole, lakini alama hizo ni za nani miongoni mwa mamilioni ya wanadamu waishio juu ya ardhi ya Washington? Hawakuweza kujua!

FB_IMG_17084993963791453.jpg
 
NURU YAREJEA WASHINGTON DC - 3
Umuhimu wa matumizi ya vitambulisho na kushirikisha jamii katika kupambana na Uhalifu!

Sehemu iliyopita tuliona maofisa wa uchunguzi wa kimaabara walipata alama za vidole za mtuhumiwa, lakini hawakiweza kutambua ni alama za nani. Kwenye uchunguzi wa kimahakama (Forensic investigation), alama za vidole ambazo mwenye nazo hafahamiki zinaitwa 'Finger Marks', hadi pale alama hizo zinapotambulika kuwa ni za fulani ndipo huitwa 'Finger Prints'. Kwahiyo wataalamu walipata 'Finger Marks' ambazo msaada wake ni mdogo sana.

Ili alama za vidole ziwe na msaada wa haraka inabidi kuwepo na alama za vidole za huyo muhalifu kwenye kanzi data (database) ya alama za vidole ya taifa. Kwa bahati mbaya, hakuna taifa duniani lenye kanzidata inayojumuisha hata asilimia 20 tu ya raia wote. Hata Marekani wenyewe hawajafikia hiyo asilimia 20.

Maana yake ni kwamba hata kama muhalifu akiacha alama za vidole, hawezi kupatikana kwa kutumia alama hizo ikiwa alama zake hazikuwahi kuwepo kwenye kanzidata, ila anaweza kupatikana kwa njia zingine halafu atachukuliwa alama za vidole ili kulinganishwa na zile zilizopatikana awali – kuhakiki kama ni yeye au la.

Tuendelee...
Bila kuchoka, polisi waliendelea kumtafuta muuaji. Sasa kila mbinu inayowezekana ilipaswa kutumika. Kule Montgomery, eneo la shule aliposhambuliwa mtoto Aron kulipatikana ganda la risasi, kizibo cha kalamu na karata yenye ujumbe. Mamlaka za kaunti ya Montgomery hazikuwa zimechunguza alama za vidole kwenye ganda la risasi iliyodhaniwa kumshambulia Aron kule shuleni kwa sababu ganda hilo lilikuwa kwa wataalamu wengine wa vilipuzi waliotaka kuchunguza aina ya silaha inayotumiwa na muuaji.

Kizibo cha kalamu na ile karata yenye ujumbe havikuwa na alama za vidole, vipi kuhusu ganda la risasi?
Kama bahati, alama za vidole zilipatikana kwenye ganda la risasi iliyomshambulia Aron. Na sasa alama hizo zilikuwa tofauti na alama zilizokutwa kwenye shambulizi la Jeff kwenye mgahawa wa Ponderosa.

Muhimu zaidi, alama hizi za sasa zilikuwapo kwenye kanzidata ya taifa – mwenye nazo aliitwacLee Boyd Malvo – kijana wa miaka 17, muhamiaji kutoka Jamaica. Kijana huyo alichukuliwa alama za vidole katika kituo cha Bellingham, jimboni Washington. Hili ni jimbo tofauti na lipo mbali na jimbo la Washington DC; Kwahiyo, kuna jimbo la Washington na Washington DC ambalo ndio makao makuu ya serikali ya Marekani.

Picha ya kijana Malvo ilipatikana papo hapo kwenye kanzidata, lakini haikuwekwa hadharani.
Polisi waliamini kwamba kijana huyo hakuwa peke yake, bali alikuwa na mtu mwingine ambaye alama zake zilipatikana kwenye ganda la risasi la mgahawani Ponderosa, ambazo hazikuwapo kwenye kanzidata ya taifa. Upelelezi ulikuwa unaanza kuleta matokeo. Lakini muuaji hakupoa.

Oktoba 22 ilikuwa zamu ya Conrad Johnson, dereva wa basi aliyeuawa katikati ya mji wa kaunti ya Montgomery. Katika eneo la tukio, ujumbe mpya ulitundikwa kwenye mti ukisema; ‘Ujinga wenu umegharimu maisha ya mtu mwingine’. Muuaji aliwaona polisi wajinga kwa kushindwa kumpatia fungu aliloomba la dola milioni 10 ili aache kuua watu. Na sasa alituma ujumbe ili kuwachefua zaidi. Hakujua, siku zake zipo ukingoni. Polisi walifanya siri kubwa juu ya taarifa za alama za vidole za kijana Lee Boyd Malvo ili zisivuje. Muuaji akijua kama alama za vidole zimepatikana anaweza kujificha na kufanya uchunguzi uwe mgumu zaidi, au anaweza kuamua kuua watu wengi zaidi akijua siku zake zinakaribia.

Zaidi ya kuwa muhamiaji kutoka Jamaica, huyu kijana Lee Boyd Malvo ni nani?
Kijana huyu alizaliwa Jamaica na baadaye alihamia Marekani akiwa chini ya ulezi wa mama yake aliyeitwa Midred. Mama huyo alisaidiwa kuingia Marekani na mwanaume wake aliyeitwa John Muhammad. Ndio kusema John Muhammad alikuwa mume wa Midred na pia baba mlezi wa Lee Boyd Malvo.
Mtu aliyeitwa Robert Holmes kutoka New Jersey alipiga simu kwenye namba maalum iliyotolewa na polisi lakini simu yake haikupokelewa. Rober Holmes alikuwa na ujumbe muhimu kuhusu sauti ya mtu aliyezungumza kwa simu na polisi kwenye mgahawa wa Ponderosa akitaka fedha kiasi cha dola milioni 10. Ilikuwa sauti ya kijana Lee Boyd Malvo. Lakini Robert Holmes hakusita kujaribu kupiga simu tena na tena na hatimaye, baada ya siku tano ndipo polisi walipokea simu yake. Robert aliwaeleza polisi ya kuwa anaamini sauti ya mtu aliyezungumza na polisi ni sauti ya kijana Lee Boyd Malvo ambaye anaishi na John Muhammad.

Robert aliifahamu vema familia hii. Yeye na John Muhammad walikuwa marafiki wakubwa tangu walipokuwa jeshini na anajua masaibu yanayomsibu rafiki yake sasa. Robert aliwaambia polisi kuwa John Muhammad alishaachana na mkewe Midred, na baada ya kuachana alianza kumtishia kumuua. Midred alikimbia vitisho vya John, akabeba watoto wake wadogo na kwenda kuishi Washington DC. John Muhammad naye alimfuata Midred huko Washington DC. Kwakuwa John Muhammad na mwanaye wa kambo Lee Boyd Malvo walipatana sana, si ajabu John na Malvo ndiyo wanaofanya huo ujambazi.

Robert Holmes alimwagika zaidi, akawaambia polisi anajua kuhusu tabia ya John na Malvo ya kujifunza shabaha kwa bunduki tangu walipokuwa wakiishi huko Florida.
Taarifa hizo zilikuwa msaada mkubwa kwa maofisa wa polisi na sasa walikuwa na matumaini ya kumkamata muuaji wa Washington DC. Polisi walifuatilia mara moja taarifa za John Muhammad kwenye mfumo wa usajili wa magari, wakagundua anamiliki gari aina ya Chevy (Chevrolet) Caprice yenye rangi ya blue na namba za usajili za New Jersey – NJ 08104.

Hapa kunaonekana umuhimu wa kuwa na nyaraka za vitambulisho zenye taarifa za kutosha za mtu. Vitambulisho vya uraia, vya kupiga kura, leseni za udereva na hati za umiliki wa mali na hati za kusafiria zinapaswa kuwekwa kwenye mfumo mmoja wa mawasiliano. Haina maana kuwa mtu awe na kitambulisho kimoja, hapana, bali nyaraka zote hizo zifanane na taarifa zake ziweze kupatikana kwenye mfumo mmoja. Kwa mfano, mtu mmoja anayeitwa John Muhammad, taarifa zake zote zifanane kwenye vitambulisho na hati zote ili iwe rahisi kumpata anapohitajika.

Kufikia hapo maofisa wa polisi hawakuona tena haja ya kuficha kitu. Taarifa za gari hiyo ziliwekwa hadharani na picha za John Muhammad pamoja na Lee Boyd Malvo pia ziliwekwa hadharani ili mtu yeyote, atakayewaona au atakayeona gari hiyo popote atoe taarifa kwa jeshi la polisi.

Wakati huo kikosi maalum cha makomandoo wa SWAT kilikuwa kikijiandaa na mapambano ya kurushiana risasi na muuaji endapo watapewa taarifa za mahali alipoonekana.

Oktoba 24, shuhuda mmoja aliyeitwa Whitney alitoa taarifa juu ya gari ndogo aina ya Chevrolet Caprice, rangi ya blue yenye namba NJ 08104. Whitney alimiliki gari ya aina hiyohiyo, kwahiyo ilikuwa rahisi kuitambua. John Muhammad na Lee Malvo hawakujisumbua kurusha risasi tena walipogundua hawana pa kukimbilia. Kitendo cha polisi kuwatangaza hadharani kwa sura na gari yao kiliwamaliza nguvu wakawa kama wamepigwa sindano ya ganzi. Hawakuwa na cha kufanya, walisubiri tuli humo kwenye gari wakisubiri kukamatwa na kufunguliwa mashitaka. Wangejaribu kujibizana kwa risasi na kikosi cha SWAT wasingeweza.

Siku saba zilipita bila watuhumiwa kuzungumza chochote. Hatimaye Malvo akafunguka. ‘John ni rafiki yangu, pia ni baba yangu. Kila anachofanya na mimi nafanya’ – alisema Lee Malvo. Akaendelea, ‘nilikuwa nafunga kula chakula kabla ya kuua mtu, kwani hilo lilinisaidia kuongeza shabaha’.

Lee Malvo alitoa taarifa za kila mauaji waliyofanya, walipokosea na walipopatia. Alitoa taarifa za mauaji mengine waliofanya miji mingine kabla ya kuhamia Washington DC. Akasema walikuwa wakijifunza pamoja namna ya kulenga shabaha huko Florida. Walitumia gari yao ndogo kwa namna ya pekee ili wasipatikane kirahisi, walitoboa tundu dogo upande wa nyuma ya gari mahali panapokaa namba za usajili, halafu wakaondoa siti za nyuma ili kuwepo nafasi ya kutosha ya kujilaza wakati wa kulenga mtu. Wakati Lee Malvo akilenga shabaha kupitia tundu hilo, John Muhammad alikuwa kwenye usukani. Ilikuwa ni vigumu kugundua kuwa risasi imetoka nyuma ya gari kupitia tundu dogo lisiloonekana sawasawa.

Mwaka 2004, John Muhammad alihukumiwa kifo wakati Lee Malvo alihukumiwa kifungo cha maisha. John alikata rufaa, na miaka miwili baadaye alibadilishiwa kifungo na kuhukumiwa maisha bila msamaha.

Mwisho!
FB_IMG_17085001613242363.jpg
 
View attachment 2910874
Wape credit investigation discovery
 
Back
Top Bottom