Tanzia: Madame B na Kijino wamefiwa na Baba yao

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,556
7,084
Habari za muda huu waungwana?
Nimepokea taarifa asubuhi hii kuwa member wenzetu Madame B na Kijino wamefiwa na baba yao.


Taarifa niliyoipata toka kwa Madame B mwenyewe inafafanua zaidi kuwa Mzee alikuwa anaumwa. Amefariki asubuhi ya leo tarehe 25-10 2012..


Msiba upo Chama, Mbezi Mwisho{Ya Kimara}. Ni njia ya kuelekea Maramba Mawili..


Mipango ya mazishi inaendelea sasa hivi eneo ambalo msiba upo{Chama. Njia ya kwenda Maramba Mawili}


Taarifa zaidi zitaendelea kuwafikia kadri ambavyo itakuwa imepangwa. Wana JF tuungane pamoja katika kipindi hichi kuwafariji wenzetu {Wafiwa} kwa kuwapa Moyo na kuwaombea faraja na nguvu toka kwa Mungu.


Kwa taarifa na maelezo zaidi jinsi ya kufika eneo la tukio {Kwa wale watakaohitaji kwenda msibani} piga namba hii ya 0716394882..


Updates:


Nimepata taarifa muda huu kutoka kwa Madame B kuwa eneo la msiba limebadilishwa. Msiba umehamishiwa nyumbani Kinondoni B Mtaa wa Dunga. Sio kule Mbezi kama ambavyo taarifa ya awali ilieleza... Namna nzuri ya kufika na kupitia njia ya kuelekea Mwananyamala hospital kutokea Kinondoni Biafra.

Tunawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Updates.

Taarifa ambayo imetolewa mda huu ni kwamba Mwili wa marehemu utasafirishwa Jumapili tarehe 28-10- 2012 . Mwili unasafirishwa kwenda Lushoto.

Taarifa zaidi zitawajia kadri ambavyo zitatokea..


Update

Mda huu ndo shughuli ya kuaga inamalizika. Safari ya kuelekea Lushoto kwa ajili ya mazishi ndo inaanza. Tuwekane kwenye maombi

Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake libarikiwe.

Pumzika kwa Amani Mzee George.
 
Dah pole sana wafiwa Mungu awape nguvu kwenye wakati huu mgumu. R.I.P mzee George
 
Poleni sana,
nitakutafuta kwa kweli kesho I should be there,
poleni sana, Mungu azidi kuonekana katika maombolezo yenu.
 
Oooh my god very bad news kwa siku ya leo pole Madame B na Kijino
Mungu awape moyo wa ujasiri katika kipindi hiki kigumu
Mavumbini tulitoka na mavumbini tutarudi
Jina la bwana lihimidiwe
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana Madame B na @ Kijino, Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu. . .
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe!
 
Last edited by a moderator:
Habari za muda huu waungwana? Nimepokea taarifa asubuhi hii kuwa member wenzetu Madame B na Kijino wamefiwa na baba yao Mzee George William Shemndolwa.

Taarifa niliyoipata toka kwa Madame B mwenyewe inafafanua zaidi kuwa Mzee alikuwa anaumwa. Amefariki asubuhi ya leo tarehe 25-10-2012..

Msiba upo Chama, Mbezi Mwisho{Ya Kimara}. Ni njia ya kuelekea Maramba Mawili..

Mipango ya mazishi inaendelea sasa hivi eneo ambalo msiba upo{Chama. Njia ya kwenda Maramba Mawili} taarifa zaidi zitaendelea kuwafikia kadri ambavyo itakuwa imepangwa.

Wana JF tuungane pamoja katika kipindi hichi kumfariji wenzetu{Wafiwa} kwa kuwapa Moyo na kuwaombea faraja na nguvu toka kwa Mungu.

Kwa taarifa na maelezo zaidi jinsi ya kufika eneo la tukio{Kwa wale watakaohitaji kwenda msibani} piga namba hii ya 0716394882.

pole sana Madame B Mungu akupe nguvu ktk kipindi hk kigumu, may he RIP.
 
Last edited by a moderator:
Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani.Amina.
 
Madame B & Kijino kabla ya leo sikutambua ni mna relation.
Aidha poleni sana na tanzia Rip mz Shemndolwa.
 
What a bad news! Poleni sana Madame B na Kijino kwa msiba wa baba yenu! Poleni ndugu jamaa na marafiki! Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe!
 
Last edited by a moderator:
Ni njia yetu sote, MUNGU awape ujasiri katika kipindi hiki kigumu. R.I.P baba!
 
Pole sana Madam B, na Kijino kwa msiba mzito wa kuondokewa na mzee wenu.
Mwenyezi Mungu atawapa nguvu kutokana na msiba huu mzito, tupo pamoja..............
 
Habari za muda huu waungwana? Nimepokea taarifa asubuhi hii kuwa member wenzetu Madame B na Kijino wamefiwa na baba yao Mzee George William Shemndolwa. Ni Afisa Kodi Mamlaka ya Mapato {TRA} Musoma Mjini Mkoani Mara.

Taarifa niliyoipata toka kwa Madame B mwenyewe inafafanua zaidi kuwa Mzee alikuwa anaumwa. Amefariki asubuhi ya leo tarehe 25-10-2012..

Msiba upo Chama, Mbezi Mwisho{Ya Kimara}. Ni njia ya kuelekea Maramba Mawili..

Mipango ya mazishi inaendelea sasa hivi eneo ambalo msiba upo{Chama. Njia ya kwenda Maramba Mawili} taarifa zaidi zitaendelea kuwafikia kadri ambavyo itakuwa imepangwa.

Wana JF tuungane pamoja katika kipindi hichi kumfariji wenzetu{Wafiwa} kwa kuwapa Moyo na kuwaombea faraja na nguvu toka kwa Mungu.

Kwa taarifa na maelezo zaidi jinsi ya kufika eneo la tukio{Kwa wale watakaohitaji kwenda msibani} piga namba hii ya 0716394882.

BWANA alitoa BWANA ametwaa jina lake lihimidiwe.R I P mzee wetu.
poleni wafiwa wote.
 
Last edited by a moderator:
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom