Spika Sitta: Kelele za Kingunge hazininyimi usingizi

sijawahi kuanzisha mgogoro chadema na inshaallah ninamwomba mungu kila siku nisiwe chanzo cha mgogoro chadema. In fact nilizuia mgogoro chadema. I will defend this movement (CHADEMA) to the best of my courage, help me GOD.
Thanks Zitto for all.
Also politics sometimes its a game of oportunities, whoever seizes the oportunity at the most oportune moment wins the game, please please please Chadema!, seize this moment and capitalize on this.
 
Thanks Zitto for all.
Also politics sometimes its a game of oportunies, whoever seizes the oportunity at the most oportune moment wins the game, please please please Chadema!, seize this moment and capitalize on this.

Ingawa mimi ni mwumini wa siasa za kupanga na sio za kuvizia. Hata hivyo, ushauri umepokelewa
 
sijawahi kuanzisha mgogoro chadema na inshaallah ninamwomba mungu kila siku nisiwe chanzo cha mgogoro chadema. In fact nilizuia mgogoro chadema. I will defend this movement (CHADEMA) to the best of my courage, help me GOD.

Mhh,

Ohh kweli, kwa mawazo yako kuna chadema au kuna wewe upande mmoja na chadema upande mwingine?

BTW - ni mgogoro upi uliouzuia chadema?
 
Mhh,

Ohh kweli, kwa mawazo yako kuna chadema au kuna wewe upande mmoja na chadema upande mwingine?

BTW - ni mgogoro upi uliouzuia chadema?

CHADEMA ni taasisi na hakuna aliye juu ya movement hii. Msimamo wangu umekuwa hivyo siku zote na utaendelea kuwa hivyo. Hata wale waliojaribu kutaka kuonyesha eti mimi ni maarufu zaidi ya chama niliwakatalia waziwazi mbele ya umma.

Nimezuia migogoro mingi sana katika movement yetu. Mingi sana and out of that we build institutions sio?
 
hapana hawezi. Akilivunja na yeye anapoteza Urais!

Akivunja Bunge uchaguzi unaitwa wa Rais na wabunge. Hivyo naye habaki. Lakini yeye kama mkuu wa nchi (head of state) yupo juu ya Bunge. Rais ni sehemu ya Bunge kwa kusaini miswada kuwa sheria. Akikataa kusaini, amekataa. Nchi nyingine Bunge laweza kupitisha na kum over rule Rais. Kwetu hapana. Bado yupo juu ya Bunge constitutionally
 
hapana hawezi. Akilivunja na yeye anapoteza Urais!
.

Anaweza kwa mujibu wa katiba, yes na yeye anapoteza urais kwa kuitisha uchaguzi mkuu mpya ndani ya siku 90, ila kumbuka baada ya kuvunjwa bunge, the loosers ni wabunge, rais anaendelea kuwepo madarakani mpaka siku ya kuapishwa rais mpya, hivyo he has nothing to loose.
 
No hatubishani kwenye hiyo fact (btw - hatukubishana kwa lolote lile). Nimeuliza tu audacity ya kuonyesha wengine hekima ambayo wewe mwenyewe uliiweka mfukoni wakati wa mgogoro wako uliouanzisha chadema.
Jamani watu tunahitaji kusoma maandiko tu tukaelewa. Hapa ubishi wa nini?
Kesi imekwisha kwa utetezi wa Zitto na case closed!
 
Akivunja Bunge uchaguzi unaitwa wa Rais na wabunge. Hivyo naye habaki. Lakini yeye kama mkuu wa nchi (head of state) yupo juu ya Bunge.

Hili nimelikataa mwanzoni kwenye mada nyingine. Rais wa Tanzania hayuko juu ya Bunge. Sijui unaipata wapi hii nadharia?

Rais ni sehemu ya Bunge kwa kusaini miswada kuwa sheria. Akikataa kusaini, amekataa.

Hapana. Akikataa mara ya kwanza mswada unarudishwa Bungeni na unasubiri miezi sita kupita halafu unarudishwa kwake tena. Na kama umepata kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge basi unaweza kurudishwa ndani ya miezi hiyo sita na Rais atatakiwa kuukubali (overuling ya presidential veto). Asipofanya hivyo Bunge linavunjika na Bunge linavunjika na yeye anapoteza Urais; habaki.

Nchi nyingine Bunge laweza kupitisha na kum over rule Rais. Kwetu hapana. Bado yupo juu ya Bunge constitutionally

Nimeielezea hiyo kwa mujibu wa Ibara 97:4. Rais hayuko juu ya Bunge. Ukisema yupo "juu ya Bunge" ni kama kumaanisha kuwa Rais anaweza kuendelea na madaraka bunge likivunjika; kwa vile yeye ni sehemu hiyo hiyo ya Bunge (siyo juu yake) akilivunja na yeye anapoteza Urais; so logically it is impossible for a person to sit on a branch and still hang on it after cutting it.
 
.

Anaweza kwa mujibu wa katiba, yes na yeye anapoteza urais kwa kuitisha uchaguzi mkuu mpya ndani ya siku 90, ila kumbuka baada ya kuvunjwa bunge, the loosers ni wabunge, rais anaendelea kuwepo madarakani mpaka siku ya kuapishwa rais mpya, hivyo he has nothing to loose.

He has everything to lose; kwa sababu akilivunja Bunge anatarajia kupata wabunge wapya kutoka wapi? Itakuwaje kama wote wanarudi tena Bungeni? Na wakiona anachezea hivyo wanaleta mashtaka ya kibunge ya abuse of power na kumvua Rais madaraka? Ndio, wabunge wanaweza kumvua Rais madaraka - hivyo hayuko juu ya Bunge!
 
Asante MKJJ kwa darasa la separations of powers. Nimekubali nimekuelewa. Rais wetu ni sehemu ya Bunge, ni kweli hawezi kumvua madaraka spika akiwa kama rais, bali anaweza kumfanza kwa kumnyang'anya kadi yake ya chama hivyo kuupoteza uspika na ubunge instantly.

true; but the same can be said about the President; Chama chake kikiamua kumvua uanachama anapoteza na Urais wake!
 
Hili nimelikataa mwanzoni kwenye mada nyingine. Rais wa Tanzania hayuko juu ya Bunge. Sijui unaipata wapi hii nadharia?

Hapana. Akikataa mara ya kwanza mswada unarudishwa Bungeni na unasubiri miezi sita kupita halafu unarudishwa kwake tena. Na kama umepata kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge basi unaweza kurudishwa ndani ya miezi hiyo sita na Rais atatakiwa kuukubali (overuling ya presidential veto). Asipofanya hivyo Bunge linavunjika na Bunge linavunjika na yeye anapoteza Urais; habaki.

Nimeielezea hiyo kwa mujibu wa Ibara 97:4. Rais hayuko juu ya Bunge. Ukisema yupo "juu ya Bunge" ni kama kumaanisha kuwa Rais anaweza kuendelea na madaraka bunge likivunjika; kwa vile yeye ni sehemu hiyo hiyo ya Bunge (siyo juu yake) akilivunja na yeye anapoteza Urais; so logically it is impossible for a person to sit on a branch and still hang on it after cutting it.

Kaka, chukua katika soma sura ya Bunge. Halafu soma sura ya Rais. Tanzania kikatiba haina Rais wa mpito. Akivunja Bunge anabaki kuwa Rais mpaka Rais mpya atakapoapishwa. Anabaki na mamlaka yale yale kana kwamba hakuna lililotokea.

Watungaji wa katiba yetu waliitunga katika hali ya kuhakikisha kuwa hakutakuwa na ombwe. Mfano chukua Rais anapofariki, hatangazwi mpaka atangazwe na Rais (unaipata hiyo? Makamu anaapa kwanza kuwa Rais kisha ndiyo anatangaza kuwa Rais (aliyekuwapo kafariki).

Niliwahi kuandika humu JF kuwa Rais ana kofia mbili tofauti zenye majukumu mawili tofauti na yamefafanuliwa na katiba.

  1. Rais kama Mkuu wa nchi
  2. Rais kama Mkuu wa Serikali
Kama Mkuu wa Serikali hayupo juu ya Bunge.
Kama Mkuu wa nchi, yupo juu ya Bunge.
 
Speaker 6 usishindane na mjinga utakuwa mjinga pia. Kambla ya elimu uzee ulikuwa busara lakini kwa wakati huu s hivyo tena. Wazee wengine huongeza umakini wanapozidi kuzeeka lakini wengine hurudi kuwa kama watoto. Kingunge ni mzee anaeelekea kwenye mawazo ya kitoto.
 
true; but the same can be said about the President; Chama chake kikiamua kumvua uanachama anapoteza na Urais wake!

Katiba inasemaje hapo? Katika sifa za kupoteza Urais kuna kuvuliwa uanachama wa chama?

Pili, turudi kwenye ile hoja ya kuvunja Bunge na kubaki na Urais. Mwanakijiji yupo sahihi.
 
Katiba inasemaje hapo? Katika sifa za kupoteza Urais kuna kuvuliwa uanachama wa chama?

Pili, turudi kwenye ile hoja ya kuvunja Bunge na kubaki na Urais. Mwanakijiji yupo sahihi.

Mheshimiwa Zitto, ningependa nielewe kidogo kuhusu huu utaratibu wa kumvua mwanachama uanachama. Kuna rules zozote zinazotakiwa kufuatwa kabla ya kumvua mwanachama uanachama, au inategemea tu "busara" ya mwenyekiti wa chama.

Kuna namna yoyote inayotumiwa na vyama vya siasa kudhibiti nguvu ya mwenyekiti, kufanya maamuzi kama anavypenda. Au mwenyekiti akiamka na kusema ananivua uanachama ndio basi imetoka?
 
.
Unakumbuka Sakata la Vituo vya Mafuta Moro?. Mahakama ilitoa uamuzi, Spika akaucrass , Jaji Mkuu akasema Spika Ameghafilika, Spika akatangaza Bungeni, Jaji Mkuu ndiye ameghafilika.

Sakata lenyewe lilikuwa hivi, Sumatra walifanya surprise check ya usafi wa mafuta, ikakuta mafuta yamechanganywa kwenye vituo 6. Ikavifungia right there and them. Wamiliki wakaenda mahakamani, mahakama ikavifungulia kwa hoja kuwa sheria zilikiukwa, Sumatra haikufuata sheria kuvifungia.
Kwanza kabisa kosa lako lilikuwa kuchanganya pumba na mchele.

Pumba ni pale ulipo sema kuhusu speaker na suala la serikali kutekeleza maamuzi ya serikali, ya kwamba anataka anacho taka yeye ndio kiwe, wakati serikali mpaka sasa hivi bado hawajatoa tamko lao rasmi la utekelezaji wa maazimio ya bunge.

Sasa hapa ni kwamba umetaka kwa makusudi mazima kupotosha ukweli.

Sasa ukija suala la kituo cha mafuta unatakiwa uangalie substance ya kitu.

Moja matumizi ya Stop order, kwa tanzania imekuwa ikitumika vibaya kama solution ya matatizo badala ya kuwa temporary relief kwa muhusika, stop order imekuwa ikitumuka kupitiliza kipinda cha busara cha situation. kingereza wanasema beyond reasonable time, sasa reasonable time kwenye sheria inatafsiri yake kutokana na situation. mfano wewe kwenda huko kwenu reasonable time inaweza kutafsirika ni siku tatu na sio 7, mwezi au mwaka.

sasa kwa mfano hilo la kituo cha mafuta walikuwa wanataka stop order ya siku ngapi? pili wameshikwa readhanded je hilo suala lina hitaji stop order? wakati mafuta ni bidha inayotoka kila siku, si ndio mwanzo wa kupoteza ushahidi?

Tatu nini mamlaka ya eura ikiwa sheria inasema ukimpata mtu mwenye mafuta machafu adhabu yake ni kufungiwa kituo pale pale? sasa yeye defence yake ni kupeleka ushahidi mahakama kwa kutumia hati ya dharura, na hata mahakama ya biashara zimewekwa ili kuharakisha mambo kama hayo, sasa wao kesho yake ni kupeleka sampuli ya stock yao ambayo ni nzuri, na ewura nao kupeleka sampuli chafu, then indepent side watapeleka sampuli yao hao wanaopingana, within three to one week suala limetatuliwa, sasa wewe kutafsiri yako ulitaka hiyo stop order ikae zaidi ya hapo wakati hao watu wanaweza kuharibu ushahidi, ndio ufanisi unaotaka kubariki.

Sasa kama jaji mkuu kapotoka interested parties tusiseme hivyo, iwe ni barabarani au kwenye sehemu zinazo husika?

Unajua sheria zingine huwa zinapingwa kwa sababu uwepo wake ni kwa ajili ya kuntyima wengine haki? mfano hiyo ya mgombea binafsi na yule wa chama. nini Nyalali alisema, au Kamati ya Jaji Kisanga? mbona walipuuzwa na Serikali mpaka leo hilo jambo halina tafsiri iliyo sahihi?

Unajua Tanzania tumewaachia wanasiasa kutuamulia mambo mengi mpaka ya kitaalumu, sasa wewe , nina hisi nimwana taaluma kwa njaia moja au nyingine, hivyo unatakiwa kuwa na mawazo endelevu na si mgando.

na hili la sheria mbovu mbovu sio tanzania tu hata nchi zilizo endelea sema wenzutu, mahakama haina uoga wakuiambia serikali hapo mlipotoka.

Tanzania limesemwa lakini utkelezaji hakuna.
 
Mwanakijiji,

(natumia katiba toleo la mwaka 2000, lile la mwaka 2005 ambalo lina mabadiliko makubwa sina)

Ukisoma ibara ya 38(2) unapata hoja yako ya kwamba akivunja na yeye habaki.

Ukisoma ibara ya 42(3) unaona kuwa akivunja anabaki kuendelea na kazi.

Ibara ya 42 - 3 ipo juu ya ibara ya 38-2 kwa sababu hii ya 38 imeanza na maneno bila kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii............ Masharti yanayotajwa ni yale ya 42-3.

Akivunja anabaki
 
Asanteni sana kwa somo la separation of powers. Thread kama hizi inatakiwa wabunge wetu wawe wanazipitia maana wako wengine ambao hawaelewi kama jinsi wachangiaji wetu wanavyoshusha nondo za somo la uraia.

Huu ni mjadala wenye afya kwa taifa na raia wa Tanzania. Taratibu, lakini tutafika tu. Wale ambao walikuwa hawaelewi, nao itafika mahali wataelewa.

Baadhi ya wabunge wakisoma hoja za Mzee Kingunge kwenye magazeti hawa-take trouble ya kufuatilia ili waone kama hoja zake ni za msingi ama ni ubabaishaji tu ili kuitetea serikali iliyo madarakani.
 
Back
Top Bottom