Masanja
JF-Expert Member
- Aug 1, 2007
- 4,820
- 8,886
Kwa kusaidia mjadala ili uwe na afya zaidi, jee Kingunge alisema nini?
Alisema, Bunge la Tanzania linafuata mfumo wa Wenstminister wa Bunge la Uingereza unaoheshimu sana mipaka ya separation of powers baina ya mihimili mitatu ya dola, Bunge (The Legistlature), Serikali (The Executive) na Mahakama (The Judiciary).
Kingunge akamshambulia Spika Sitta kwa kuika mfumo huo na kuingilia uhuru wa Mahakama na Serikali huku akikikumbatia kikundi kinachoisulubu serikali huku yeye mwenywe akiingilia uhuru wa mahakama.
Swali ni jee tuhuma za Kingunge zina ukweli, au nao ni utetezi wa mafisadi.
Kwa maoni yangu ni kweli na mifano ipo. Spika Sitta amekuwa anapractice perliamentary supremacy over and above mihimili hii mingine miwili ya Dola. Amewahi kubishana na Jaji Mkuu wazi wazi kupinga uamuzi halali wa mahakama which is wrong.
Na katika maazimio 23 ya bunge kuhusu kamati ya Mwakiembe, anataka kuilazimisha serikali iyatekeleze kama yalivyo hata kama serikali inaona hakuna hatia, ndio maana Hosea bado yuko madarakani.
Lengo la separation of powers ni checks and balance kati ya mihimili hii kuzuia mmoja usiende kwenye extreme, Bunge litunge sheria, mahakama izitafsiri sheria hizo na serikali isaidie utekelezaji.
Sita amekuwa mtunga sheria, anataka kuhukumu kama kwenye Richmond, na kuilazimisha serikali kutekeleza. Kamati ya Bunge imeona kuna hatia Richmond, serikali meona hakuna hatia. Kikao hiki cha Bunge kilipanga kuisulubu tena serikali. Baada ya Sitta kusulubiwa kwenye kamati ya Mwinyi, sasa kaufyata ni heshina na adabu, mpaka kaliahirisha Bunge huku kuna ishu kibao muhimu kwa taifa.
Ili kuilinda heshima yake, Sitta lazima ataita press conference next week kutueleza kwa nini, na mkiona kimya, mjue Sitta kwisha habari yake, King Maker na timu yake in full control.
Chief,
With due respect. You better revisit your constitutional law class!
Otherwise, ukiamua kufanya uchambuzi wa issues kama hizi itabidi uwe makini. Si kwamba wote humu ni vilaza wa hilo darasa la Westminster. By far, our parliament in Tanzania is no where in exercising the powers of the parliament as espoused by the Westminister model. Kifupi ni kwamba Sitta is doing ambacho Msekwa na waliomtangulia ingebidi wawe wamefanya. Lakini kwa vile Msekwa na waliomtangulia walikuwa stalwarts wa CCM, ndo leo tunamuona Sitta kwamba anaingilia uhuru wa mihimili mingine. HE IS SIMPLY DOING WHAT HE SUPPOSED TO DO. KULIWEZESHA BUNGE KUISIMAMIA SERIKALI.Kitu ambacho kiko kwenye katiba yetu.
Hivi kweli Mkuu Pasco, kwa akili yako mkuu..unaweza kushika computer yako na kuandika kwamba Serikali haikutekeleza maamuzi ya bunge kwa vile "iliona hawana hatia wahusika". Really? kwa lugha nyingine kutekeleza yale maazimio ilikuwa ni OPTION YA serikali? C`on brother. Surely you can do better. Maana nakuaminia kichwa chako.
In all, Kingunge et al..wanakimbia vivuli vyao. Wanataka status quo. Maana hawajazoea kuwajibishwa. And precisely hicho ndo kinatuumiza nchi zetu za dunia ya nne. Viongozi wamezoea kuendesha nchi kama kampuni binafsi..akitokea mtu akataka kufuata sheria-tena zilizokwenye vitabu vyetu. Mwanzo wengi tunakuwa hostile kwa watu kama hao.
again I say, Kingunge, perhaps hajui nini maana ya Westmnister model. After all alisoma elimu ya ukomunisti, kwa hiyo simlaumu.
Tuendelee kuelimishana,
Masanja