Paul Makonda atembelea na kuweka maua katika kaburi la Hayati Samuel Sitta

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,277
9,717
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Paul Makonda Mwamba na Jabali wa siasa na kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara. Hii leo asubuhi ametembelea na kuweka maua katika kaburi la marehemu Samuel Sitta, ambaye alikuwa speaker wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 2005 na kuachia 2010 baada ya kuwa ilitakiwa iwe zamu ya mwanamke kuongoza mhimili huo wa Bunge.

Speaker Marehemu Samuel Sitta anakumbukwa sana kwa kulibadilisha bunge na kulifanya kuwa la viwango. Ni wakati wake ambapo moto ulikuwa unawaka kweli kweli. Ni wakati ambapo Tanzania ilishuhudia waziri Mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania akitangaza kujiuzulu mbele ya macho ya watanzania.

Bunge hili lilikuwa na watu machachari sana ambapo CCM ilikuwa na watu kama Dr. Hallisoni Mwakyembe, Ole Sendeka na Anna kilango Malecela.

Wakati upinzani kulikuwa na watu kama Dr. Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe pamoja na Halima mdee aliyekuwa binti mbichi kabisa kwa wakati huo. Ni wakati huo ambao zitto kabwe alisimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge na kuja na kitu kinachoitwa operation sangara.

Katika bunge hilo makashifa mengi sana yalikuwa yakiibuliwa na kulikuwa na minyukano mingi sana ndani ya bunge kutokana na kuwa makundi na mikakati ilikuwa ikipangwa na kusukwa kiustadi sana katika mbio za kumrithi Rais Kikwete 2015. Kwa hiyo kila kundi lilijitahidi sana kutupa makombora mazito mazito kwa yule aliyeonekana kuwa tishio kwa kundi lao.

Mpaka inafika 2015 minyukano ilikuwa imepigwa ya kutosha na mabomu yamerushwa ya kutosha na wengine kuachwa na majera ya kisiasa ambayo bado wanayo mpaka leo mioyoni mwao. Naamini wakati huo hakuna aliyekuwa anaacha glasi ya maji na kuirudia kuinywa baadaye, maana kila mtu alikuwa makini sana katika kujirinda na kutomuamini mtu.

Ni wakati huo wa kuanzia wakati wa marehemu samueli Sitta mpaka wakati wa Anna Makinda ambapo vijana walitokea kuipenda sanaa tena sanaa siasa na pia kila mahali ilikuwa ni kawaida kukuta watu wamejaa wanafuatilia vikao vya bunge pale Dodoma kupitia runinga.mimi mwenyewe nilikuwa nafuatilia kila kitu kinachoendelea katika Bunge letu.

Kwa hakika kila kitu na wakati wake.wakati huo umepita na siamini kama itakuja ijirudie tena kwa watu kuwa na hamasa na mwamko wa kisiasa kama ule nilioushuhudia kwa macho yangu mwenyewe na kushiriki pia moja kwa moja katika mijadala mitaani.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Hii ni mara yake ya kwanza kwenda au ashawahi fanya hivyo wakati mwingine?
 
Back
Top Bottom