Spika Sitta: Kelele za Kingunge hazininyimi usingizi

Jamaa wametuweza kweli, wamefanikiwa kututoa kwenye objective yetu ya kuikomboa nchi hii sasa tumebaki tunarumbana rumbana kuhusu nani kasema hili au lile.

hawa wote wanaogombana ni chama kimoja basi tuwafungie pazia na kuanza kupanga jinsi ya kyuuikomboa nchi hii. Tuna watu wengi sana wa kuweza kuikomboa nchi hii na wengine hata hawajingia kwenye siasa bado sasa. Tunaitaji kuwasha roho ya mapinduzi na siyo mipasho.

Ukiangalia kwa karibu sana utaona kuwa strategy ya mafisadi inaanza kushinda kwani wanatuchagulia topic za kudiscuss na muda wa kuwa kwenye marumbano, sisi wenyewe hatuwezi kupanga chochote cha kuikomboa nchi hii.

Vibaraka wao wakutuchanganya tunawajua na wanakuja hapa na matusi na kejeli nasi tunahamaki na kuanza kupoteza muda kujibishana nao tukizani kuwa tunajibu mapigo kumbe ndiyo tunacheza wimbo wanautaka. Mali zetu wanaendelea kutuibia na uchaguzi watashinda. Halafu wataleta drama za kuwa kuna makundi kati ya wapiganaji na mafisadi cha ajabu wote wanang'ang'ania kuwa katika chama kimoja si kituko hicho. malaika anapotaka kuendelea kushare table na Lucifer
 
Acheni watu wawe na uhuru wa mawazo. Mtakimbiza watu humu halafu mbaki kama chama kimoja - zidumu fikra za mwenyekiti.

Pasco anao uhuru wa mawazo yake na wala hajashambulia Bunge. Kwa nini mnakosa ngozi ngumu ya kusoma usichopenda?

Tulianzisha JF ili watanzania wapate pa kusemea bila kuogopa. Huu mwenendo wa kutovumilia mawazo ya wengine unaota mizizi sasa hapa.

Jibu hoja kwa hoja. Kama huna jibu na hoja huipendi kajifungie msalani ulieeeeeeeeeeeee, ujifute machozi urudi kukata ishu na sio kuanza kutukanana hapa.
...I salute mh. but wakati mwingine uvumilivu una mipaka,vile yeye haoneshi kuheshimu yaliyo ya kweli!
 
Kingunge kachemsha, amesahau kuwa wakati wake umeisha, hizi ni zama zingine. Mh Simba keshawaanzishia, wao wamalizie watu tujue pumba zp,mchele upi tuujue ukweli..
 
Hawa wazee wameongea mambo yao huko ndani ya vikao vyao, kwa nini wanajibizana kwenye magazeti? Hekima imewaishia kabisa?

Wewe mbona hoja zako za kutaka uenyekiti ulikua unapenyeza kwenye magazeti?

Na hata habari ya wewe kuitwa na kupokwa nafasi ya kugombea uenyekiti kimizengwe,kikao kilikua cha siri,lakini mabishano ya kambi zenu tuliyaona kwenye magazeti.

Muheshimiwa hii ni VITA!
 
Kaka nakuelewa kabisa. Tujadili hoja hii kwa kumtoa Sitta na Kingunge ili tuwe objective.

Ibara ya 63 ya katiba - kushauri na kusimamia! Ushauri ukikataliwa na unayemshauri na unaamini kuwa ni ushauri bora, unatangaza kuwa huyu hashauriki. Hivyo, unamtoa na kwenda kwenye uchaguzi mwingine. Kama hutaki kumtoa, unaendelea naye mpaka uchaguzi ulio kwenye ratiba kwa mujibu wa katiba na kelele zinaishia hapo.

Bunge kama mwakilishi wa wananchi kwa kupitia mbunge mmoja mmoja nguvu yetu ni kura ya kutokuwa na imani na Rais.

Jambo kubwa la kuzingatia hapa ni kwamba KATIBA ndio ipo juu ya kila kitu (constitutional supremacy) na hakuna mhimili ulio juu ya mhimili mwingine. Sisi wabunge tuna hangover ya Parliamentary supremacy!

Kina Kingunge wao wanahangover ya Party supremacy

Mkuu tupo pamoja katika hii elimu ya uraia,

Sasa kaka, ukiangalia paragraph yako ya kwanza ni dhahiri kabisa kwamba bunge lipo kuishauri na kuisimamia serikali. To supervise and advice. Sasa chief tatizo linakuja pale ambapo..watu wanataka kuendeleza status quo. In otherwords kama bunge limeishauri serikali ifanye kitu ikakataa basi serikali inabidi iondolewe kwa kura ya kutokuwa na imani. Sasa who will do that in CCM? Sasa what we are seeing from CCM stalwarts...they want to have their own cake and eat it at the same time. In other words wanataka..mapendekezo ya bunge wayakatae harafu status quo iendelee. Asiwajibishwe yeyote. Demokrasia gani hiyo? Labda ya Karzai na wamarekani!

Harafu kwanza tuangalie hayo mapendekezo ya bunge yalihusu nini? Kuwachukulia hatua walioiba pesa ya umma kwa kutumia madaraka yao! Simple! Hapa tunaongelea akina Mwanyika, Hosea, Lowassa etc...sasa hili swala..hata kama siyo bunge lingekuwa limesema hivyo, ni criminal offence within itself. Kama ingekuwa ni nchi yenye misingi ya demokrasia..ni dhahiri FBI au Special Crimes Unit..wangewadaka hawa jamaa wakawa tayari jela. Lakini ushangae..hapa tunajadili...kamati ya bunge..tunasahau walichokipendekeza..kwamba it would be in the national interests..kama serikali ingekitekeleza. Sasa huoni kwamba serikali inayokataa kuwachukulia hatua wabadhirifu..hata credibility yake ni zero? Kinachotokea hapa..serikali inatetea wezi wa kodi zetu..and we are busy here spinning..bila kuangalia bigger picture na impact. Ohh..nearly forgot what Africans are good at. Everybody is spinning to get his cut of the slice.

In all, politics is a complicated game..especially in banana republic kama yetu, ambako party survival madarakani inategemea ujinga wa wananchi wake. Sorry to be brutal, lakini wanategemea kwamba wananchi hatuelewi so they can do anything and go away with it. And CCM has successfully done that since its creation.

Ufisadi, uzembe na woga wa bunge letu has nothing to do with any governance model, ni ujinga wetu sisi wananchi ambao ndo tunawaajiri na kuwatuma kule. Harafu baada ya kuangalia yote haya..next elections, issues zitakuwa on personalities...and that will be another day, another win for the currupt in our midist. Simply put, we arent responsible citizens.

Kifupi, katika siasa zetu za vinchi vyetu masikini..hakuna kitu kama common good. Its everybody for himself. Yet watu tunataka, maendeleo kupitia njia ambayo haileti maendeleo. Mkuu itakuchukua miaka mingi sana kufika Kigoma, kama badala ya kuchukua reli ya kati unaamua kupanda mashua kwenda Madagascar.

Zitto, you are bold enough, than most of us, labda ndo maana uko kwenye politics (perhaps thats a personal calling you made). Lakini kwangu mimi, naamini Africa na Tanzania..tutapata demokrasia ya kweli (hence uwajibikaji na maendeleo) kama WANANCHI tukiamka kutoka kwenye usingizi pono! Tujue kabisa kwamba kuwa RAIA ina entail responsibilities. So far..tunaonekana kuwalaumu viongozi, wakati sisi hatujiangalia..ni vipi tunaweza ku-influence hali iliyopo ikabadilika. Tukiendelea hivi tulivyo, we can dream, whine and lament, but poverty and all social ills are here to stay with us.

Masanja,
 
.
Mh.zito,
Tunakushukuru sana kwa ufafanuzi wako mzee.
Tatizo kubwa hapa ndani ni ushabiki.
Mwanakijiji ni mshabiki sana wa akina mwakyembe pasipokuwajua wao ni akina nan.Ukiangalia post zake kwa Lowasa ni majembe tu.Lakini hajawahi kusema kuwa ile kamati ya Mwayembe ilijaa siasa na wivu na uroho wa madaraka.

Halafu kitu kingine hapa.Ni kwamba kila anachoandika mwanakijiji basi wana jf wanaona ni sawa ata kama ni pumba.

Wewe nimefuatilia post zako zote ni za kuwajenga mafisadi! Bila shaka unanufaika moja kwa moja na wachafu hawa! Hoja za Mzee Mwanakijiji zipo wazi na ndio maana zinaungwa mkono na wengi humu. Wewe ndio mwenye matatizo...
 
Ndugu yuo got it very wrong, Speaker hawezi kupingana na mahakama?
hilo lazima ulielewe tena saana, hukumu yoyote inayotolewa na mahakama ni halali mpaka itakapotenguliwa na mahakama au mamlaka ya juu zaidi wenye mandate ya kufanya hivyo.
.
Unakumbuka Sakata la Vituo vya Mafuta Moro?. Mahakama ilitoa uamuzi, Spika akaucrash , Jaji Mkuu akasema Spika ameghafilika kuuingilia Mahakama, Spika akatangaza Bungeni, Jaji Mkuu ndiye ameghafilika!.

Sakata lenyewe lilikuwa hivi, Sumatra walifanya surprise check ya usafi wa mafuta, ikakuta mafuta yamechanganywa kwenye vituo 6. Ikavifungia right there and them. Wamiliki wakaenda mahakamani, mahakama ikavifungulia kwa hoja kuwa sheria zilikiukwa, Sumatra haikufuata sheria kuvifungia.

Spika amjibu Jaji Mkuu

2009-02-10 09:44:38
Na Boniface Luhanga, Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Samuel Sitta, amezitaka Mahakama na taasisi za sheria nchini kufanya maamuzi yenye maslahi kwa taifa.

Spika Sitta aliyasema hayo jana muda mfupi baada ya kumalizika kwa kipindi cha Maswali na Majibu kwenye kikao cha Mkutano wa 14 wa Bunge unaondelea mjini hapa.

Alisema Mahakama zipo kwa ajili ya kuisadia jamii kwa ujumla na kwamba ni matarajio kwamba hata maamuzi yake yatakuwa yakilenga walio wengi badala ya wachache.

Spika Sita aliongeza kuwa, Bunge kama moja ya mhimili wa serikali, haliwezi kukaa kimya katika maamuzi yasiyo ya haki yanayofanywa na mhimili mwingine yaani Mahakama pamoja na mingine.

"Naelewa wapo wanaoweza kusema naingilia Mahakama Lakini wanapaswa kuelewa kuwa, wapo pale kwa ajili ya wananchi waliowafanya wawe pale," alisema.

Aliongeza kuwa, wanapaswa kufahamu pia kuwa, maamuzi yao mengine yanawaumiza wananchi wasio na hatia kwa faida ya wachache.

Hata hivyo, Spika Sitta alisisitiza kuwa, siku zote Bunge litasimama mstari wa mbele kutetea haki za watu na haliwezi kuendelea kubaki kimya kama mambo yakienda tofauti.

Alitolea mfano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ambayo imefungia baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta mkoani Morogoro kutokana na kugundulika kuuza mafuta machafu mkoani humo.

Katikati ya mwaka jana, Ewura ilivisimamisha kutoa huduma vituo kadhaa vya kuuza mafuta kwa tuhuma za kuuza bidhaa hiyo ikiwa chini ya viwango.

Spika Sitta alisema Mahakama moja mkoani Morogoro, ilishirikiana na wafanyabiashara wa mafuta na kuweka pingamizi mahakamani dhidi ya amri hiyo ya Ewura.

"Katika hali kama hii, mahakama ilikuwa sambamba na wafanyabiashara wanaouza mafuta yasiyofaa kwa wananchi. Na kwa hali hiyo, Mahakama ilijali zaidi maslahi ya wafanyabiashara na kuwaacha walio wengi," alisisitiza Spika Sitta.

Alisema yeye akiwa ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, hawezi kukaa kimya kwa sababu watu hao ndio wanaoteseka ama kuumia kutokana na maamuzi kama hayo.

Aidha, Spika Sitta, alisema leo anatarajia kutoa maelezo kuhusu madai ya Jaji Mkuu dhidi ya Bunge.

Jaji Mkuu Augustine Ramadhani, alikaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni akisisitiza umuhimu wa kuendeleza utamaduni wa mgawanyo wa madaraka ambapo alionya mhimili mmoja wa serikali kuingilia mwingine na hususan alikuwa akililenga Bunge.
 
Wewe nimefuatilia post zako zote ni za kuwajenga mafisadi! Bila shaka unanufaika moja kwa moja na wachafu hawa! Hoja za Mzee Mwanakijiji zipo wazi na ndio maana zinaungwa mkono na wengi humu. Wewe ndio mwenye matatizo...
.

Ziko wazi kwako wewe na ufinyu na upeo mdogo wa kuelewa.Haukatazwi kuzifuata,lakini sio kuwalazimisha wote wazifuate.
 
Huyu Pasco naye kwa kwenda chakani!... Unafanya makusudi kupotosha mambo au ndio matunda ya kufikia hoteli moja na Rostam Dodoma hayo?

Waganga njaa kina Pasco hawatakuja kuisha kwenye vi nchi masikini kama hivi, mpaka mwisho wa dunia.

Kina Kingunge na Pasco wanataka kutumia Ignorance ya watu on parliamentary systems wanatumia Half-Truths kutaka kulinda maslahi yao ya matumbo njaa!

Thanks
 
Rais hawezi kumvua madaraka Spika au kuwavua madaraka wabunge!.
Asante MKJJ kwa darasa la separations of powers. Nimekubali nimekuelewa. Rais wetu ni sehemu ya Bunge, ni kweli hawezi kumvua madaraka spika akiwa kama rais, bali anaweza kumfanza kwa kumnyang'anya kadi yake ya chama hivyo kuupoteza uspika na ubunge instantly.

Rais akitofautiana na Bunge, anaweza kulivunja bunge as he pleases.
 
Jaji Mkuu Augustine Ramadhani, alikaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni akisisitiza umuhimu wa kuendeleza utamaduni wa mgawanyo wa madaraka ambapo alionya mhimili mmoja wa serikali kuingilia mwingine na hususan alikuwa akililenga Bunge.

Pasco, we are all Tanzanians and we know very well who is doing what when it come to interfearing with the matters of the other pillar of the government.

Unajua inasikitisha sana kuona hata wakati mwingine jaji mkuu anaongea kama vile anaogopa kusema ukweli, au anaongea kwa kudhani kuwa watanzania wote ni wajinga.

Unajua hizi system za kuletewa zinatusumbua sana, na kuna wakati zinatufanya tuonekane wajinga. We have a lot of evidences of Exective Branch kuingilia Mahakama, kuipuuza na hata kuidindia mahakama.

Sitta mwenyewe akiwa waziri wa sheria na katiba anaweza kukumbuka vizuri issue ya mgombea huru, mahakama ilifafanua vizuri sheria iliyotungwa na bunge, lakini serikali ikaipinga mahakama, na ikalihonga bunge na kufanya ujanja mpaka leo issue hiyo iko kimya. Ukweli ni kuwa hakuna separation of powers Tanzania, hata huo uamuzi wa vituo vya mafuta morogoro haukuwa uamuzi wa mahakama ulikuwa ni uamuzi wa wenye pesa na kuitaka mahakama ifanye maamuzi kwa manufaa yao, the order came from executive.

Let us fool no one, we do not have sepation of powers. Kila kitu kinaamuliwa na executive, tumeshituka sasa baada ya kuona wenye hela wawili au watatu wanajua kuwa wakinunua au wakiweka hisa kwenye executive watakuwa wamemaliza kila kitu.
 
Yaani CCM ni nani zaidi. Hivi Mwenyekiti au makamu hawapo warudishe nidhamu ya chama?
 
Pasco, we are all Tanzanians and we know very well who is doing what when it come to interfearing with the matters of the other pillar of the government.

Let us fool no one, we do not have sepation of powers. Kila kitu kinaamuliwa na executive, tumeshituka sasa baada ya kuona wenye hela wawili au watatu wanajua kuwa wakinunua au wakiweka hisa kwenye executive watakuwa wamemaliza kila kitu.

- Mkulu Bongolander, maneno mazito sana hayo, Tanzania hatujawahi kuwa na separation of power, Msekwa alijaribu sana kulitenganisha bunge na Ikulu, lakini walipomgundua wakaanza kumpa nafasi kamati kuu, wakamfanya kuwa watatu on the line kwenye urais, na wakampa sana kukaimu urais enzi zile Mkapa na Shein wanapishana Airport wakibadili ndege za kwenda nje na kabla hajashituka wakamtupa nje ya uspika,

- Akaingia Sitta, ambaye kwanza walikuwa pamoja na Mtandao baadaye akaona upuuuzi wao umezidi kipimo, akaanza kutaka kutenganisha bunge na Ikulu ndio huyu sasa wamemkaba kooni, Judicila naomba hiyo msiitaje kabisa maana ni kama haipo, huwa tunaisikia pale tu jaji mkuu ana-retire, anarusha maneno mengi ya ki-coward of how much alikuwa kiingiliwa na Bunge na Ikulu, blah! blah! wanampa kamati ya kula na pensheni nzito basi yameisha, hakuna cha separation of power wala nothing.

- Tukishaona wazungu wamekuja toka nje kufuatilia hela zao wanazotupa za misaada ndio tunaanza kujidai na sisi tuna three branches of government, three branches my foot!

FMeS!
 
Hawa wazee wameongea mambo yao huko ndani ya vikao vyao, kwa nini wanajibizana kwenye magazeti? Hekima imewaishia kabisa?
Mara nyingine hasira hufanya mtu akafanya kitu ambacho baadaye hujutia kwa nini alikifanya.
Tatizo la wazee hawa ni kama lile la kwako wewe kwani ulifanya kitu hicho hicho kwa ajili ya hasira tu wakati wa uchaguzi wa Chadema. Wengi tunaokupenda na kukuthamini hatukuamini kitu tulikuwa tukikisoma hapa jf. Nadhani ulijutia baadaye.
Hata wao baadaye najua watayamaliza na kuendelea kuwa kitu kimoja ili waendelee kuikandamiza demokrasia.
 
Sijitetei. Kilichotokea kimetokea. Hakikupaswa kutokea na haikuwa nia yangu itokee. I regret.
 
Hawa wazee wameongea mambo yao huko ndani ya vikao vyao, kwa nini wanajibizana kwenye magazeti? Hekima imewaishia kabisa?

Wakati mwingine inachekesha sana kumsoma Zitto.

Yaani leo Zitto anashauri watu watunze mambo ya vikao vya ndani ya chama? Zitto ya kwenu huko chadema ulishindwa kuyatunza ndani ya chama na ukayaleta hapa na magazetini kote Tanzania BUT leo unapata audacity ya kuonyesha watu hekima?

Kamalize kwanza mgogoro wako uliouanzisha huko chadema kabla ya kuleta unafiki wako ccm
 
two wrongs never make it a right. If i was wrong i was wrong, it doesnt give others a licence to commit the same.

Hao wazee hawana hekima kama ilivyokuwa mimi kijana sikuwa na hekima. Tunabishana kwenye fact hii?
 
No hatubishani kwenye hiyo fact (btw - hatukubishana kwa lolote lile). Nimeuliza tu audacity ya kuonyesha wengine hekima ambayo wewe mwenyewe uliiweka mfukoni wakati wa mgogoro wako uliouanzisha chadema.
 
Acheni watu wawe na uhuru wa mawazo. Mtakimbiza watu humu halafu mbaki kama chama kimoja - zidumu fikra za mwenyekiti.

Pasco anao uhuru wa mawazo yake na wala hajashambulia Bunge. Kwa nini mnakosa ngozi ngumu ya kusoma usichopenda?

Tulianzisha JF ili watanzania wapate pa kusemea bila kuogopa. Huu mwenendo wa kutovumilia mawazo ya wengine unaota mizizi sasa hapa.

Jibu hoja kwa hoja. Kama huna jibu na hoja huipendi kajifungie msalani ulieeeeeeeeeeeee, ujifute machozi urudi kukata ishu na sio kuanza kutukanana hapa.
Zitto asante sana kwa comment yako hii.
Mungu akubariki.
 
No hatubishani kwenye hiyo fact (btw - hatukubishana kwa lolote lile). Nimeuliza tu audacity ya kuonyesha wengine hekima ambayo wewe mwenyewe uliiweka mfukoni wakati wa mgogoro wako uliouanzisha chadema.

sijawahi kuanzisha mgogoro chadema na inshaallah ninamwomba mungu kila siku nisiwe chanzo cha mgogoro chadema. In fact nilizuia mgogoro chadema. I will defend this movement (CHADEMA) to the best of my courage, help me GOD.
 
Back
Top Bottom