Spika Sitta: Kelele za Kingunge hazininyimi usingizi

Zitto sijakuelewa hapa, labda umeeleza kwenye post zingine. Ninavyoelewa ni kuwa kama Mswadaumekataliwa kuasiniwa na Rais utarudihwa tena bungeni kujadiliwa na kufanyiwa marekebisho, na kama wabunge wa tabaki na msimamo wao ule ule wa kutokuubadirisha mswaada wakaupeleka tena kwa rais kusianiwa ili iwe sheria na rais akaukataa kama itatokea Rais akaukataa mswaada mara mbili basi hakuna mjadala either of the two inatakiwa vitokee, Rais ajiuzuru na serikali yake, au Bunge kuvunjwa na uchaguzi mkuu kufanywa.

Kwa hiyo kusema kuwa Rais akikataa mswada then Bunge halina namna nadhani sio sahihi, labda kama sijakuelewa.

Upo sahihi na mwanakijiji amefafanua pia hivyo hivyo. Mantiki yangu ni kuwa muswada hautakuwa sheria iwapo Rais akikataa kusaini. Uganda na nchi nyingine zenye mfumo kama wetu, Rais akikataa anaurudisha Bungeni na sababu za kukataa, na Bunge likiendelea na msimamo wake na wakapiga kura ya theluthi mbili muswada ule unakuwa sheria. Tanzania hapana - Bunge linavunjwa! Ndio mantiki yangu hiyo
 
Sasa naona Kisheria nimewaelewa wote wewe, Mkjj, Pasco et al. sasa nikirudisha suala la utekelezaji wa maazimio 23 ya kamati teule ya Bunge kwenye mkataba wa ufuaji wa umeme wa serikali na Richomond Ltd, hili tutasema limekaaje? Bunge limepitisha maazimio na kuitaka serikali itekeleze, serikali imeleta report mara ya kwanza ikiwa nusu nusu na bunge halikuridhika lakini serikali iliomba muda zaidi kwa ajili ya utekelezaji.

Wiki hii kama itawezekana serikali italeta report ya utekelezaji mathalani ikaeleza bayana kuwa haijaona sababu za msingi za kutekeleza mazimio kadha wa kadhaa (km kumuwajibisha Hosea) Na wabunge wasiridhike, nini kitatokea?

Kwenye mpira (soka) wachezaji wakiumia au kutolewa kwasababu yoyote ile mpaka wakawa chini ya wachezaji 7 (kwa timu moja) Refa humaliza mchezo. Tuchukulie technically kuna idadi kubwa ya abunge hawajaridhishwa na utekelezaji wa maaazimio ya bunge, wakaamua kujiuzuru mmoja mmoja, je kuna sheria yoyote inayolazimisha either bunge kuvunjwa au serikali kujiuzuru kutokana na uwingi wa wabunge walio jizuru?

(samahani kwa typo mijadala mitamu)
 
mkuu tiba

si swala la kushangaza hata yesu alisema nabii aaheshimiki nyumbani kwake...na ndio maana hutomwona m'kijiji akijibizana na hoja kama hizi
.
Mbumbu.
Hiyo sio hoja.
angalia alivyoandika mwenzio tiba kwa ustarabu.Idiot
 
Nilidokeza hapo juu kuwa unazungumzia kile kinachoonekana na siyo kile kilichopo kisheria na kikatiba.

Rais anapotekeleza mamlaka yake kama mkuu wa nchi ni DOLA na sio mhimili wa dola.

Kwanza, hakuna hiyo tofauti Kikatiba kati ya "Dola" na "Mhimili wa Dola". Lakini zaidi hata neno "dola" tunavyolielewa sisi halitumiki katika Katiba yetu. Mara nyingi tunapozungumzia Dola tunazungumzia "State" na wakati huo huo tunapozungumzia Mkuu wa Nchi tunazungumzia "Head of State" ambayo yaweza kutafsiriwa kama "Mkuu wa Dola" au "Mkuu wa Nchi".

Lakini pia kuna kitu tunachokiita "serikali" yaani government. Dola siyo serikali tu ni zaidi ya serikali iliyoundwa. Dola tunavyolielewa neno hilo linamaana nyingi na linachukua karibu maana zote za Kiingereza. Neno lenyewe asili yake ni Kiarabu. Hivyo Dola ukiileta kwa kiingereza inatafsiriwa kama "mamlaka(authority), himaya(empire-dola ya Mwanamutapa), nchi(country), taifa(nation), na serikali (government).

Hivyo nasema hayo ili kufuta hii tofauti tuliyoitengeneza kati ya "dola" na "serikali" au "dola" na "nchi" au "dola" na taifa". Kwa mantiki hiyo, tunapozungumzia "vyombo vya dola" hatuzungumzii vitu tofauti na "vyombo vya serikali" au "vyombo vya mamlaka ya nchi".

Hata hivyo naelewa watu wanaojaribu kutofautisha "Serikali" kutoka "Rais na Baraza na watumishi wanaomsaidia kutekeleza wajibu wake wa kikatiba" na "Serikali" kama "jumla ya mamlaka zote na vyombo vyote vya kisiasa na kiutendaji, kisheria na kimadaraka vya nchi".

Kwa ajili ya mjadala huu basi nitatumia neno "serikali" kumaanisha "sehemu ya madaraka ya uongozi wa nchi ambayo si mahakama wala Bunge". Yaani sehemu ile inayotumika na utendaji (executive).

Maana yangu hii inajengwa na tafsiri ya Katiba juu ya serikali kuwa ni "pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka
au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote." (Ibara 6)

Utaona kwenye kichwa cha sura hiyo ya Katiba kwenye Kiswahili linatumika neno "serikali" lakini kwenye toleo la Kiingereza inatumika "State" na hivyo kuendelea kuweka wingu kwenye maneno haya.

Hivyo basi tunapozungumzia serikali tukwepe inapowezekana kuchanganya vitu ambavyo ni kimoja na tunapotaka kuvitofautisha basi tuvitofautishe kwa umakini kabisa (precise) kwani maneno yanatuchanganya sana.

Yeye mwenyewe Rais ni dola. Rais anakuwa mhimili pale tu anapotekeleza mamlaka yake kama Mkuu wa Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu.

Katiba haitambui tofauti hii. Rais SIYO dola - serikali, nchi, mamlaka, himaya etc. Na Rais siyo Mhimili kama ofisi moja bali Urais ndiyo Mhimili. Yaani, Rais kama mtu mmoja hatengenezi Mhimili bali Rais kama Mkuu wa sehemu ya Utendaji (Executive) wa serikali yetu ndiyo Mhimili. Hivyo, hakuna wakati wowote ambapo Rais SIYO sehemu ya Mhimili wa Utendaji. Kwa kadiri ya kwamba upo Utendaji, upo Mhimili wa Utendaji unaoongozwa na Rais.

Na ndio maana hatuwezi kusema Spika ni Bunge lakini ni Mkuu wa Bunge na ndiye anasema kwa niaba yake. Vivyo hivyo Mahakama; Jaji Mkuu siyo Mahakama bali ni Mkuu wake na anapewa haki ya kuwa mkuu wa mhimili huo na haachi kuwa Mkuu wa Mhimili huo akienda nje ya mahakama.
This is what ought to....... Bunge letu halina mamlaka ya kutoa amri wala kuiagiza Serikali (what is). Bunge limepewa mamlaka ya kikatiba kuishauri Serikali (ibara ya 63) na KUISIMAMIA serikali. Katika katiba ya Kiingereza neno hili limeandikwa 'to oversee'.
Kwanza niseme kwamba Katiba ya Kiswahili ndiyo yenye nguvu ya kisheria kwa mujibu wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya Uhaini dhidi ya Zanzibar. Kwa hiyo neno la Kiingereza la "oversee" halina umuhimu katika mjadala huu labda kutupa mwanga tu wa kuelewa mambo fulani. Lakini neno "kusimamia" katika Kiswahili lina nguvu kuliko la "Kuoversee".

Hivyo Bunge halina mamlaka yeyote ya kutoa amri, kuagiza wala kuelekeza.

Bunge limepewa mamlaka ya Kuidhinisha mipango yoyote ya muda mfupi au mrefu ya JMT. Katika kuidhinisha linanguvu ya kukataa kubadilisha au hata kutoa maelekezo ya nini kifanyike. Na likikataa (nguvu yake ya kusimamia) serikali (RAis) hawezi kuendelea na mpango huo. Wabunge wasipojua nguvu yao hii ndio sababu serikali wakati mwingine inajifanyia tu mambo yake.

Msingi wa nguvu hii ni kuwa Bunge ndio wawakilishi wa watu siyo Rais. Falsafa nzima ya utawala wa demokrasia ni kuwapa nguvu watu siyo mtu mmoja. Ndio sababu ya Magna Carta, mapinduzi ya Ufaransa na yale ya Marekani.

Katika Tanzania wabunge wetu wanataka kupoteza nguvu hii na kumwachia Rais cheki isiyojazwa. Hatuwezi na hatupaswi kuwaacha wabunge waache jukumu lao la kuisimamia serikali na hata kuilazimisha serikali kufanya kile sisi wananchi tunataka wafanye. This amounts to relegation of duty.

Kama serikali inaweza kufanya lolote bila kulazimishwa au kusimamiwa na Bunge, basi hatulihitaji Bunge! what for? kupitisha bajeti tu? Rais si anaweza kufanya hivyo yeye mwenyewe?
Mfano huu hauendani na mjadala. Bajeti imewekewa taratibu za kisheria za utekelezaji wake (public finance act and appropriation acts). hivyo mfano wako hapa sio penyewe.

Hapana ni mfano mzuri.

Serikali inaweza kukataa agizo la Bunge iwapo Bunge likisema toa 100bn kwenye dampo na weka kwenye nishati. Serikali inaweza kusema sitaki na Bunge halitafanya kitu.

Basi kuanzia Spika hadi mbunge mgeni kabisa wanatakiwa kupangwa mistari mbele ya wenye mitutu ya bunduki na mmoja mmoja kupopolewa kama ndege kwenye mti. Kama Serikali inaweza "at will" kukataa maelekezo ya Bunge juu ya fedha za walipa kodi na ikajiamulia ipendavyo na wawakilishi wawalipa kodi hao wakabakia kusema "well amekataa hivyo hatuna la kufanya" basi Bunge halistahili kabisa kuwepo kwani kimantiki halina umuhimu! Bunge lisiloweza kusimamia serikali na kuhakikisha serikali inatekeleza matakwa ya wananchi limepoteza uhalali wake. I'm very serious on this point.

Katika mchezo wa siasa, Bunge litasubiri shughuli za serikali nalo kusema hatutekelezi shughuli zenu. Huu ndio utaratibu ambao ulikuwa unatumika sana Ulaya ambapo mabunge yalikuwa yanagomea miswada ya Serikali mpaka serikali itekeleze mambo yao.

Well hata kwetu linawezekana; tatizo letu wabunge wetu wanafikiria Rais yuko juu yao hivyo wanahitaji kumbembeleza awasilikilize. Jamani hata Marekani hapa tunayaona Rais inabidi aende kubembeleza Bunge kupitisha mswada na wakati huo huo Seneti imetuma ujumbe kuwa kwa kadiri mswada uko ulivyo wala hauna nafasi - Rais mwenye nguvu zaidi duniani anapigishwa magoti na wawakilishi wa wananchi. The people rule supreme.

Bunge la Tanzania hutumia njia hii kwenye masuala ya maslahi ya wabunge tu. Njia hii ingetumika katika Richmond tungekuwa tumemaliza sinema hii mapema sana.

Ni kwa sababu wabunge hawajui nguvu waliyonayo isipokuwa yanapokuja maslahi yao; well said.

Unatafsiri vibaya neno kusimamiwa. Hakuna serikali inayoweza kukataa kusimamiwa kwani ni jukumu la Bunge kikatiba. Kusimamia sio kuamrisha wala kuagiza. Ninaamini walioandika katiba walichagua sana maneno maana neno hili ni dhaifu sana (the weakest - oversee?).

Nimeligusa hili hapo juu

Serikali ya Tanzania inaweza kulikatalia Bunge ushauri wake na Bunge lisiwe na la kufanya

Zitto this is very dangerous position. Serikali haiwezi, haipaswi na haitakiwi kukataa madaraka ya wananchi juu yao. Serikali isiporidhika na maamuzi ya Bunge inaleta hoja Bungeni na kutaka kura za kupindua, it can not refuse the parliament abirtrarily. No sir.

maana hata kura ya kutokuwa na imani ina taratibu zake na lazima iwe hoja mahususi. Hoja mahususi haiwezi kuwa ' wamekataa ushauri wetu, basi hatuna imani. Itagonga mwamba maana lazima AG atataka tafsiri ya mahakama.
KUKATAA UAMUZI WA BUNGE NI HOJA YA KUTOSHA KABISA.. Mahakama italiona hilo kiurahisi kweli, kwa sababu sovereignty belongs to the people. Mahakama haiwezi kuiacha serikali kutotii madaraka ya wananchi! Jaribuni na utaona how easy the courts will side with the people.
Narudia Bunge letu halina mandate ya kutoa maelekezo kwa serikali.

Wananchi wasipokuwa na uwezo na haki ya kuielekeza serikali yao kupitia wawakilishi wao then tumekubali kuishi kwenye utawala wa kifalme ambapo neno la Mfalme ndio sheria. Lakini kwa kadiri ya kwamba tumeamua kufuata utawala wa Kikatiba na kutambua kuwa hakimiya inatoka kwa watu, basi Bunge lina uwezo na madaraka ya kuiigiza serikali.

Ndugu yuo got it very wrong, Speaker hawezi kupingana na mahakama?
hilo lazima ulielewe tena saana, hukumu yoyote inayotolewa na mahakama ni halali mpaka itakapotenguliwa na mahakama au mamlaka ya juu zaidi wenye mandate ya kufanya hivyo. mfano hili la Zombe hata Raisi kaliongelea lakini haimanishi anapingana na mahakama bali ni mtu kuona au kuzania haki haijatendeka.

Sasa ukija mazungumzo yaani vitu vilivyo nje ya ukumbi wa bunge au mahakama havina authority yoyote. Mfano Dr Sengondo Mvungi anapoongelea kitu, mimi au wewe au hata Jaji mkuu ikiwa ni nje ya eneo la mahakama litabaki ni neno au ushauri nk ambao yoyote yule anaweza kukubaliana nao au kutokubaliana nao. na ndio maana hata leo hii Raisi anaweza sema kitu, lakini wengine wakakipinga. Au AG anaweza kuwa na muono tofauti wa jambo la kisheria na mwanasheria mwingine hata awe Jaji Mkuu, lakini wakiingia mahakamani final say ni ya Judge.

Inabidi utofautishe mambo yanayo ongeleawa na watu kwenye semina, barabarani, warsha, kongamano, kwenye forums, blog nk na kile kinachoongelewa kwenye sehemu mahususi.

Mfano watu wanaona kwenye kesi ya Zombe haki haikutendeke, hizo zitaitwa kelele mpaka pale mahakama ya Juu au mamlaka zingine zitakapo liongelea suala hilo ndani ya mipaka yao.

Hili la serikali na Bunge bado serikali haijapeleka utekelezaji wake, hivyo huwezi kupinga kitu ambacho hakipo, ndio maana hata unapotaka kukata rufaa ni lazima uwe na uamuzi wa mahakama sau mwenendo wa kesi .

Na zaidi ya hapo si suala la Sitta kupinga au kukubali, bali hiyo report inatakiwa iwasilishwe na serikali kwa kamati husika na kusomwa bunge ili wabunge waridhie au la.

Kaka huyu pasco ndo anakua sasa, tafsri zinamshinda sana, halafu toka lini Sitta alibishana na jaji mkuu, mimi sijawahi kusikia sita anabishana na jaji mkuu, ila nilisikia sita aliongenlea suala fulani kama maoni yake na wala kulikuwa hakuna ubishi wala mgongano wa mawazo.
 
Bahati mbaya uchambuzi wetuu mara nyingi kuhusu Richmond unaegemea sana kwenye hisia na kukosa uhalisia wake.

Bunge limeheshimika baada ya Ripoti ya Richmond ambayo Lowassa aliamua kujiuzuluuu kwa heshima ya chama na serikali yake. Kwangu Lowasa ni shujaa kwani wengine wanoujiuzuluu lazima wanalazimishwa au kuombwa kufanya hivyooo lakini EL aliamua mwenyewee.. HUU NDIO UONGOZI.

Kama ilivyoo katika nchi nyingine kulikotokea mabadilko, huwa yanachochewaa na watu wanaojitoa.
 
MJ big up man, maelekezo yako yanatosha na ni mwanga kwasio fahamu wajibu wa Bunge nini, am sure kila mtu akisoma hiyo article, maana iko kama article ataelewa jinsi gani Bunge letu lilivo na mandate ya kuishauri na kuilekeza Serikali hii ya bwana JK. Watanzania wengi to be honest hatujui katiba ya nchi yetu, katiba imefungiwa kwenye madroo as a result most us dont have an access to it, nikifika Bongo itabidi niitafute ili niisome, na kama unayo soft copy please MJ tupostie kamanda
 
Wiki hii kama itawezekana serikali italeta report ya utekelezaji mathalani ikaeleza bayana kuwa haijaona sababu za msingi za kutekeleza mazimio kadha wa kadhaa (km kumuwajibisha Hosea) Na wabunge wasiridhike, nini kitatokea?

Mbona kwenye ripoti iliyowakilishwa Bungeni inaeleza wazi kuwa Dr. Hosea ameshawajibishwa kwa kuandikiwa barua ya onyo kwa kutokuwa makini katika uchunguzi wake ingawa ripoti pia inakubaliana na serikali kwa kusema haya ..“..Hata hivyo, hapakuonekana dalili za mazingira ya rushwa wakati wa kufanya kazi hiyo. Hivyo, Mamlaka yake ya Nidhamu imetoa onyo kwake kwa kutokuwa mwangalifu katika eneo hilo. (Makofi)”.

Labda tukubaliane kuwa "kuwajibishwa" mawazoni mwetu ni kufukuzwa au kuhamishwa ofisi lakini siyo kupewa onyo la maandishi. Shida ni kuwa mtekelezaji ni mwingine na mpedekezaji wa adhabu hana uwezo wa kuchagua aina ya adhabu. Kwa mantiki hiyo Ndugu Madata aliyesimamai mchakato na Hosea aliyesimamia uchunguzi wa kuwepo kwa rushwa, wote serikali ilishauriwa "iwawajibishe" na wote wamepewa barua za kuonywa. Labda mjadala uwe kuwa adhabu yao ni ndogo na hailingani na makosa yao na siyo kuwa hawajawajibishwa.
 
two wrongs never make it a right. If i was wrong i was wrong, it doesnt give others a licence to commit the same.

Hao wazee hawana hekima kama ilivyokuwa mimi kijana sikuwa na hekima. Tunabishana kwenye fact hii?

Asante sana Zitto, hili jibu lako limenirudishia tumaini na imani kwako - nilikuwa nimekacha JF kwa muda.
Tukirudi kwenye mada, ukweli ulio mchungu lakini ambao lazima tuukubali ni kuwa nchini Tanzania hadi hii leo hatuna separarion of powers bali bado tuna party supremacy. Katiba, serikali, bunge na mahakama ni tools tu zinazotumiwa kuhakikisha CCM inabaki madarakani au kwa lugha nyingine ni subordinate organs za CCM. Matokeo yake ni kuwa ikitokea katiba ya nchi ikapingana na katiba ya CCM, zitatafutwa njia za kuhalalisha hali hiyo kwa kuzitumia mahakama au bunge - mfano wagombea binafsi.

Mwaka 1992 tulishuhudia serikali ya CCM ikiihujumu demokrasia kwa kuridhia mfumo wa vyama vingi lakini kwa kuongozwa na katiba ya CCM bila kufanya marekebisho ya kukidhi katika katiba ya nchi. Matokeo yake ni kuanzishwa kwa vyama vilema visivyojiweza kwa kufungwa na kubanwa na hiyo hiyo katiba ambayo ingevilinda. Hivyo badala ya kukua na kusitawi vimejikuta vikizidi kudhoofika kwa kukosa rutuba na nyenzo ambavyo vimeatamiwa na chama tawala - ndani ya katiba.

Tatizo la wananchi kwa upande mwingine ni kule kuiamini CCM kuwa kuna wakati utafika kwa hiari yao watabadilika na kutanguliza maslahi ya taifa mbele ya Chama. Hili halitawezekana, si kwa sasa na si kwa siku za karibuni na kama wote tungeweza kulitambua hili tungeanza kwa kutafuta njia ya kulitatua bila hiari yao. Bahati mbaya wengi wetu hatuko tayari kwa jukumu hili - tumezoea vya kunyonga, vya kuchinja twaogopa tusichafue suti zetu kwa damu.
 
Nilidokeza hapo juu kuwa unazungumzia kile kinachoonekana na siyo kile kilichopo kisheria na kikatiba.

Kwanza, hakuna hiyo tofauti Kikatiba kati ya "Dola" na "Mhimili wa Dola". Lakini zaidi hata neno "dola" tunavyolielewa sisi halitumiki katika Katiba yetu. Mara nyingi tunapozungumzia Dola tunazungumzia "State" na wakati huo huo tunapozungumzia Mkuu wa Nchi tunazungumzia "Head of State" ambayo yaweza kutafsiriwa kama "Mkuu wa Dola" au "Mkuu wa Nchi".

Lakini pia kuna kitu tunachokiita "serikali" yaani government. Dola siyo serikali tu ni zaidi ya serikali iliyoundwa. Dola tunavyolielewa neno hilo linamaana nyingi na linachukua karibu maana zote za Kiingereza. Neno lenyewe asili yake ni Kiarabu. Hivyo Dola ukiileta kwa kiingereza inatafsiriwa kama "mamlaka(authority), himaya(empire-dola ya Mwanamutapa), nchi(country), taifa(nation), na serikali (government).

Hivyo nasema hayo ili kufuta hii tofauti tuliyoitengeneza kati ya "dola" na "serikali" au "dola" na "nchi" au "dola" na taifa". Kwa mantiki hiyo, tunapozungumzia "vyombo vya dola" hatuzungumzii vitu tofauti na "vyombo vya serikali" au "vyombo vya mamlaka ya nchi".

Hata hivyo naelewa watu wanaojaribu kutofautisha "Serikali" kutoka "Rais na Baraza na watumishi wanaomsaidia kutekeleza wajibu wake wa kikatiba" na "Serikali" kama "jumla ya mamlaka zote na vyombo vyote vya kisiasa na kiutendaji, kisheria na kimadaraka vya nchi".

Kwa ajili ya mjadala huu basi nitatumia neno "serikali" kumaanisha "sehemu ya madaraka ya uongozi wa nchi ambayo si mahakama wala Bunge". Yaani sehemu ile inayotumika na utendaji (executive).

Maana yangu hii inajengwa na tafsiri ya Katiba juu ya serikali kuwa ni "pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka
au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote." (Ibara 6)

Utaona kwenye kichwa cha sura hiyo ya Katiba kwenye Kiswahili linatumika neno "serikali" lakini kwenye toleo la Kiingereza inatumika "State" na hivyo kuendelea kuweka wingu kwenye maneno haya.

Hivyo basi tunapozungumzia serikali tukwepe inapowezekana kuchanganya vitu ambavyo ni kimoja na tunapotaka kuvitofautisha basi tuvitofautishe kwa umakini kabisa (precise) kwani maneno yanatuchanganya sana.

Katiba haitambui tofauti hii. Rais SIYO dola - serikali, nchi, mamlaka, himaya etc. Na Rais siyo Mhimili kama ofisi moja bali Urais ndiyo Mhimili. Yaani, Rais kama mtu mmoja hatengenezi Mhimili bali Rais kama Mkuu wa sehemu ya Utendaji (Executive) wa serikali yetu ndiyo Mhimili. Hivyo, hakuna wakati wowote ambapo Rais SIYO sehemu ya Mhimili wa Utendaji. Kwa kadiri ya kwamba upo Utendaji, upo Mhimili wa Utendaji unaoongozwa na Rais.

Na ndio maana hatuwezi kusema Spika ni Bunge lakini ni Mkuu wa Bunge na ndiye anasema kwa niaba yake. Vivyo hivyo Mahakama; Jaji Mkuu siyo Mahakama bali ni Mkuu wake na anapewa haki ya kuwa mkuu wa mhimili huo na haachi kuwa Mkuu wa Mhimili huo akienda nje ya mahakama.
[/SIZE][/I]Kwanza niseme kwamba Katiba ya Kiswahili ndiyo yenye nguvu ya kisheria kwa mujibu wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya Uhaini dhidi ya Zanzibar. Kwa hiyo neno la Kiingereza la "oversee" halina umuhimu katika mjadala huu labda kutupa mwanga tu wa kuelewa mambo fulani. Lakini neno "kusimamia" katika Kiswahili lina nguvu kuliko la "Kuoversee".

Bunge limepewa mamlaka ya Kuidhinisha mipango yoyote ya muda mfupi au mrefu ya JMT. Katika kuidhinisha linanguvu ya kukataa kubadilisha au hata kutoa maelekezo ya nini kifanyike. Na likikataa (nguvu yake ya kusimamia) serikali (RAis) hawezi kuendelea na mpango huo. Wabunge wasipojua nguvu yao hii ndio sababu serikali wakati mwingine inajifanyia tu mambo yake.

Msingi wa nguvu hii ni kuwa Bunge ndio wawakilishi wa watu siyo Rais. Falsafa nzima ya utawala wa demokrasia ni kuwapa nguvu watu siyo mtu mmoja. Ndio sababu ya Magna Carta, mapinduzi ya Ufaransa na yale ya Marekani.

Katika Tanzania wabunge wetu wanataka kupoteza nguvu hii na kumwachia Rais cheki isiyojazwa. Hatuwezi na hatupaswi kuwaacha wabunge waache jukumu lao la kuisimamia serikali na hata kuilazimisha serikali kufanya kile sisi wananchi tunataka wafanye. This amounts to relegation of duty.

Kama serikali inaweza kufanya lolote bila kulazimishwa au kusimamiwa na Bunge, basi hatulihitaji Bunge! what for? kupitisha bajeti tu? Rais si anaweza kufanya hivyo yeye mwenyewe?

Hapana ni mfano mzuri.

Basi kuanzia Spika hadi mbunge mgeni kabisa wanatakiwa kupangwa mistari mbele ya wenye mitutu ya bunduki na mmoja mmoja kupopolewa kama ndege kwenye mti. Kama Serikali inaweza "at will" kukataa maelekezo ya Bunge juu ya fedha za walipa kodi na ikajiamulia ipendavyo na wawakilishi wawalipa kodi hao wakabakia kusema "well amekataa hivyo hatuna la kufanya" basi Bunge halistahili kabisa kuwepo kwani kimantiki halina umuhimu! Bunge lisiloweza kusimamia serikali na kuhakikisha serikali inatekeleza matakwa ya wananchi limepoteza uhalali wake. I'm very serious on this point.

Well hata kwetu linawezekana; tatizo letu wabunge wetu wanafikiria Rais yuko juu yao hivyo wanahitaji kumbembeleza awasilikilize. Jamani hata Marekani hapa tunayaona Rais inabidi aende kubembeleza Bunge kupitisha mswada na wakati huo huo Seneti imetuma ujumbe kuwa kwa kadiri mswada uko ulivyo wala hauna nafasi - Rais mwenye nguvu zaidi duniani anapigishwa magoti na wawakilishi wa wananchi. The people rule supreme.

Ni kwa sababu wabunge hawajui nguvu waliyonayo isipokuwa yanapokuja maslahi yao; well said.

Nimeligusa hili hapo juu

Zitto this is very dangerous position. Serikali haiwezi, haipaswi na haitakiwi kukataa madaraka ya wananchi juu yao. Serikali isiporidhika na maamuzi ya Bunge inaleta hoja Bungeni na kutaka kura za kupindua, it can not refuse the parliament abirtrarily. No sir.

KUKATAA UAMUZI WA BUNGE NI HOJA YA KUTOSHA KABISA.. Mahakama italiona hilo kiurahisi kweli, kwa sababu sovereignty belongs to the people. Mahakama haiwezi kuiacha serikali kutotii madaraka ya wananchi! Jaribuni na utaona how easy the courts will side with the people.

Wananchi wasipokuwa na uwezo na haki ya kuielekeza serikali yao kupitia wawakilishi wao then tumekubali kuishi kwenye utawala wa kifalme ambapo neno la Mfalme ndio sheria. Lakini kwa kadiri ya kwamba tumeamua kufuata utawala wa Kikatiba na kutambua kuwa hakimiya inatoka kwa watu, basi Bunge lina uwezo na madaraka ya kuiigiza serikali.

Nashukuru kwamba Mh. Zitto ameisoma post hii.
MUNGU aingalie nchi yetu kwa jicho la huruma na aingilie kati.
THIS IS VERY SERIOUS COMRADES.
 
Yale niliyasema huko nyuma kuwa Sophia Simba alikuwa mouthpiece tu wa Jakaya leo yamedhihilishwa na Kingunge alipokuwa anahojiwa na TBC1; amesema kuwa ilikuwa sahihi kwa Sophia kuwaumbua wale wanaojifanya kuwa wao ni safi kuliko wenzao na kwamba baada ya report ya THREE CCM WISE MEN kuwasilishwa kwenye NEC yao na kujadiliwa anauhakika CCM itakuwa safi na kuanza upya!! Wanajanvi uelewa wangu wa maneno ya mzee huyu ni kwamba huko kwenye NEC yao nadhani wale wanaojipambanua kuwa wapiganaji watafukuzwa chama na CCM kuanza upya na MAFISADI wakipeta! Tungoje tuone kitakachotokea kwenye NEC ijayo.
 
Tokea asubuhi nimesoma hii topic ndo nimeimaliza.
Nakushukuru Mwanakijiji na Mh. Zitto tumepata changamoto kubwa
sana ambazo zinakuza uelewa wa hii mihimili mitatu ya utawala.

Lakini nimegundua kuwa kwa maelezo yote aliyoelezea MJJ kwenye
hii topic inaonekana bado tunahitaji somo kubwa kwa wabunge wetu wote na watanzania kwa ujumla.

Sasa ebu angalia Mh. Zitto ambaye ni Msomi, Mhelewa, na mbunifu bado nayeye anababaika, sasa ebu fikiria wale wabunge walioko huko bungeni hivi vitu kweli wanavielewa kweli? Bado watanzania tunahitaji somo kubwa
ili kupata mwanga wa kuelewa Bunge ni nini.
 
Hapa ipo kazi jamani nawashukuru wote waliochangia hii mada maana na mimi nimeisoma nimepata mambo mengi ambayo sikuwahi kuyajua
 
Sasa naona Kisheria nimewaelewa wote wewe, Mkjj, Pasco et al. sasa nikirudisha suala la utekelezaji wa maazimio 23 ya kamati teule ya Bunge kwenye mkataba wa ufuaji wa umeme wa serikali na Richomond Ltd, hili tutasema limekaaje? Bunge limepitisha maazimio na kuitaka serikali itekeleze, serikali imeleta report mara ya kwanza ikiwa nusu nusu na bunge halikuridhika lakini serikali iliomba muda zaidi kwa ajili ya utekelezaji.

Wiki hii kama itawezekana serikali italeta report ya utekelezaji mathalani ikaeleza bayana kuwa haijaona sababu za msingi za kutekeleza mazimio kadha wa kadhaa (km kumuwajibisha Hosea) Na wabunge wasiridhike, nini kitatokea?

Kwenye mpira (soka) wachezaji wakiumia au kutolewa kwasababu yoyote ile mpaka wakawa chini ya wachezaji 7 (kwa timu moja) Refa humaliza mchezo. Tuchukulie technically kuna idadi kubwa ya abunge hawajaridhishwa na utekelezaji wa maaazimio ya bunge, wakaamua kujiuzuru mmoja mmoja, je kuna sheria yoyote inayolazimisha either bunge kuvunjwa au serikali kujiuzuru kutokana na uwingi wa wabunge walio jizuru?

(samahani kwa typo mijadala mitamu)
Ukweli unabaki kuwa Bunge halina nguvu ya kuweza kuilazimisha serikali au kutunishiana misuli na serikali.

Linaweza kukwamisha Bajeti na kutoa mapendekezo yoyote kwa serikali. Ila serikali ina uwezo wa kuyakubali au kuyakataa (kikatiba).

Vile vile, kuhusiana na suala la Richmond, serikali inaweza kurudi Bungeni na kutamka kuwa mapendekezo yote au baadhi yake hayakubaliwi na serikali na kutoa sababu za kutoyakubali. Kinachotegemewa kwa serikali (katika suala hili) ni kufikia hatua ya kusema hivyo. Katiba inaitaka serikali iseme sababu za kutoyatekeleza mapendekezo ya serikali.

Lakini pia, kama Bunge likiona Katiba ya nchi inahitaji marekebisho, ina mamlaka ya kufanya marekebisho ya Katiba hiyo (isipokuwa mabadiliko ya sheria au utaratibu unaohusu masuala ya fedha ambayo inabidi yapitishwe na Baraza la Mawaziri).

Kuhusiana na Wabunge kujiuzuru ama kupungua Bungeni kwa sababu nyingine zozote, Katiba inaruhusu shughuli za Bunge kuendelea bila kujali idadi ya wabunge walioweza kuhudhuria.

Ibara ya 95:

Bunge laweza kutekeleza shughuli wakati wa vikao vyake bila ya kujali kwamba kuna kiti kilicho wazi miongoni mwa viti vya Wabunge (iwe kiti hicho kimekuwa wazi tangu Bunge lilipokutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu au kimekuwa wazi baada ya Mkutano huo wa kwanza) na iwapo katika shughuli hizo atashiriki mtu yeyote ambaye hana haki ya kushiriki au kama wakati wa shughuli hizo atakuwapo mtu yeyote ambaye hana haki ya kuwapo, basi kushiriki kwa mtu huyo au kuwapo kwake hakutabatilisha shughuli hizo.
 
Tokea asubuhi nimesoma hii topic ndo nimeimaliza.
Nakushukuru Mwanakijiji na Mh. Zitto tumepata changamoto kubwa
sana ambazo zinakuza uelewa wa hii mihimili mitatu ya utawala.

Lakini nimegundua kuwa kwa maelezo yote aliyoelezea MJJ kwenye
hii topic inaonekana bado tunahitaji somo kubwa kwa wabunge wetu wote na watanzania kwa ujumla.

Sasa ebu angalia Mh. Zitto ambaye ni Msomi, Mhelewa, na mbunifu bado nayeye anababaika, sasa ebu fikiria wale wabunge walioko huko bungeni hivi vitu kweli wanavielewa kweli? Bado watanzania tunahitaji somo kubwa
ili kupata mwanga wa kuelewa Bunge ni nini
.

Tatizo ni kwamba, Zitto aliingia kwenye hii debate as usual - akijiamini kuwa anajua kila kitu. Imetia moyo kuona shule (twisheni) aliyopewa hapa maana itamsaidia yeye na Wabunge wengine ndani ya bunge letu.
 
sijawahi kuanzisha mgogoro chadema na inshaallah ninamwomba mungu kila siku nisiwe chanzo cha mgogoro chadema. In fact nilizuia mgogoro chadema. I will defend this movement (CHADEMA) to the best of my courage, help me GOD.

Mh. thanks, big up
 
Upo sahihi na mwanakijiji amefafanua pia hivyo hivyo. Mantiki yangu ni kuwa muswada hautakuwa sheria iwapo Rais akikataa kusaini. Uganda na nchi nyingine zenye mfumo kama wetu, Rais akikataa anaurudisha Bungeni na sababu za kukataa, na Bunge likiendelea na msimamo wake na wakapiga kura ya theluthi mbili muswada ule unakuwa sheria. Tanzania hapana - Bunge linavunjwa! Ndio mantiki yangu hiyo

Naomba kufahamishwa jamani. HIVI?

BUNGE, SERIKALI NA MAHAKAMA vinaitwaje kwa Umoja wake ni nini hasa vyombe hivi?

Asante
 
Back
Top Bottom