Mwanakijiji,
(natumia katiba toleo la mwaka 2000, lile la mwaka 2005 ambalo lina mabadiliko makubwa sina)
Ukisoma ibara ya 38(2) unapata hoja yako ya kwamba akivunja na yeye habaki.
Ukisoma ibara ya 42(3) unaona kuwa akivunja anabaki kuendelea na kazi.
Ibara ya 42 - 3 ipo juu ya ibara ya 38-2 kwa sababu hii ya 38 imeanza na maneno bila kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii............ Masharti yanayotajwa ni yale ya 42-3.
Akivunja anabaki
Ndiyo maana tunahitaji Katiba Mpya ili kuondoa hizo contradictions, na inawezekana wameziweka makusudi ili kutuchanganya na kutudanganya sisi ambao ni layman wa sheria.