Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,032
- 2,769
Bila unafiki, ushambenga, uchawa na ukurung'unzu wowote. Nasimama kusema katika umri wangu spika Bora niliyewahi kumuona na kumkubali alikuwa Samweli Sitta mzee wa viwango! Lakini kwa sasa nchi ipo mikono salama chini ya spika Tulia Ackson Mwansasu.
Huyu mtu sio tu ni spika bali tumepata hazina mpya ya kujivunia! Huyu ni zaidi ya homa ya jiji kwa maana hakuna kiunzi Wala mtego ambao unaweza kumnasa kwa urahisi. Ni spika Bora kuwahi kutokea na chenji inabaki.
Labda Kuna mtu atanuna lakini hata kama yupo aliyenuna basi ni uzembe tu wa kufikiria sio kosa lake!
Nawaambieni tujifunze kuheshimu tulichopewa kabla ya kufikiria ambacho hatunacho. Tujifunze kutunza hazina zetu.! Spika Samweli Sitta bunge lake halikuwa na upendeleo wowote na alihimili vishindo vyote na dhoruba ngumu bila kuumiza upande wowote.
Na bunge lilikuwa na furaha sana ! Naamini bunge hili tungeanza na dk Tulia tangia mwanzo tungekuwa tumepiga hatua kubwa zaidi ya hapa na mengi yaliyotokea yasingetokea.
Kelele nyingi zinasikika kwamba awaondoe wabunge 19 bungeni nikama yeye ndiye aliwaweka mle ndani ya bunge . Nachokumbuka Mimi aliyewaapisha akina mdee sio dk Tulia aksoni ni job ndugai .
Hata yeye naamini yale yalikuwa maagizo Toka juu .lakini ngoja ni waambie kitu hata chadema upande wao Kuna mahali waliyabananga .
Halima Mdee na Esther Bulaya wasingeamua kukisaliti chama kilichowalea na ambacho wanahistoria kubwa ndani yake ikiwa mchakato wa kupata wawakilishi wa viti maalumu ungefuatwa'.
Kilichokuwepo ni uongozi kupendekeza majina ya wake zao na wapenzi wao na ndio maana mdee na ether na wenzao wakaliamsha. Spika Tulia hahusiki popote na chochote kuhusu wabunge 19 .
Jambo la pili katika historia ya uumbaji kwa mara ya kwanza dunia nzima Iko chini ya mikono ya spika hodari mwana mama kutoka milima ya rungwe. ! Eeh kwani nani anabisha ? Yeye ndio Rais wa mabunge duniani IPU,. maana yake nchi imeaminiwa sio tu spika Tulia .
Najua nabii hakubaliki nyumbani lakini dk Tulia kafanya mengi . Ana moyo wa pekee na ni mtu asiye yumbishwa .Kwa sasa tunashuhudia utulivu wa Hali ya juu sana kwenye mhimili wa bunge!
Tutarajie bunge la viwango zaidi 2025 - 2030 chini ya mwamba huyu, mwanamama shupavu ! Dada na rafiki yetu mkubwa dk Tulia aksoni ! Homa ya jiji !!