Serikali Kutoa kauli Kuhusu Mgomo wa Madaktari kesho

Kuna tetesi kwamba mtoto wa mkulima kesho anaachia ngazi kwani tatizo la madaktari limekuwa gumu kwake na kwa kifupi limemshinda hivyo ni bora akaachia ngazi kwani mpaka sasa hawezi kubadili lolote na hivyo watanzania wataendelea kupoteza maisha asipofanya hivyo.
My take
Tusubiri kesho lakini mwishi Vipi?

Pinda ange solve vipi mgomo wa madaktari wakati mkuu aliudaka juu kwa juu na kunywa juice na madaktari Ikulu baada ya hapo akatumia wazee wa DSM kujijenga kisiasa
 
yeah
kunakipindi ni lazima serikali ifanye maamuzi magumu ili kunusuru maisha ya watu wake

ukisikia mtu mzima anasema NA LIWALO NA LIWE tutegemee maamuzi magumu kutoka kwa serikali

Watarudisha zile trilioni tatu kutoka bodeni na hizi za uswizi, hayo ndio maamuzi magumu.
 
Ikitokea Pinda anajiuzuru nitafanya bonge la party nakesha kwa siku 2 :pray2: itokee kweli ajiuzuru
 
Nani ajiuzulu wewe?Nilikuwa naunga mkono mgomo laki kwa sasa naupiga kwa nguvu zote kwa sababu zifuatazo:
1. Mamia ya wananchi wasio na hatia wanaumia na pengine kupoteza maisha kwa sababu ya mgomo
2. Madai mengine ni unrealistic kwa mfano kudai mshahara wa milioni 3,kwa madaktari peke yao,vipi kuhusu idara zingine?
3.Nimegundua viongozi wa mgomo wanawatumia madaktari kugoma kwa maslahi yao binafsi.Angalia kitendo cha Dr Ulimboka kuitwa na watu asiowafahamu na yeye akaenda tena peke yake.
4.Huyo Dr Ulimboka anaweza kununuliwa na akawasaliti wenzake.Vipi alipoenda kwa hao asiowafahamu wangeamua kumpa KITITA???kama aliweza kwenda peke yake,uko wapi uadilifu wa kukataa rushwa kama angepewa?
 
Hana jipya,

Mh. Zambi anahoji kuwa japokuwa kesi mahakamani madaktari wameendelea kugoma serikali inasemaje?

Pinda kasema kesho watalitolea maamuzi na kasema LITAKALO KUWA NA LIWE. Hivi kwa kauli hii tuna waziri mkuu kweli??

Majibu yake kama sura yake ilivyo.
 
mtoto wa mkulima hana jinsi ya kujitetea katika hili kwani kauli zake zinamtokea puani. ushauri wangu ameonesha udhaifu wake na serikali yake legevu kwani wanaamini kuwa matumizi ya nguvu kwenye vita vya intelectual ni suruhisho. tunaomba waje na mkakati wenye mashiko ktk mgogoro wa ma dr tz. ukiweza baba JIUZURU KABLA HAIBU HAIJAKUKUTA
 
Baada ya Mhe. Zambi kutaka majibu ya Serikali (leo Bungeni) Waziri Mkuu ameahidi kesho serikali italitoa majibu/tamko kesho. Tutarajiwe nini Great Thinkers?
Atakuja na kusema kuwa hakusema chochote kama ilivyokuwa wakati wabunge walivyohatarisha kibarua chake bungeni walipoungana kuwawajibisha mawaziri kwa kujihusisha na ufisadi.
 
Huyu Pinda Amepinda na kauli zake! Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa!

By Mpendamabadiliko

Watanzania wenzangu hizi kauli tunazozitoa zinaweza kuonekana ni nyepesi sana lakini madhara yake yanaweza kuwa makubwa sana na yakaathiri watu wengi wasiokuwa na hatia. Tuhuma ya kuteka mtu kwa nia ya kumuuwa kijasusi ni shutuma kubwa sana. Ni lazima mtu anayetoa kauli kubwa kama hiyo awe na ushahidi wa kutosha.

Sijui kati yetu tunaongea kwa kumsisitizo tuna ushahidi wowte wa kuonesha ni nani kutoka serikali na kwa amri ya nani kahusika na utekaji huo? Kama hatuna ushahidi kwa nini tusifanye uchunguzi kwa chini chini na hatimaye tukipata ushahidi ndio tuwe na haki ya kuzungumza?

Mbali ya kusoma magezetini na kusikia katika maredio na vyombo vingine vya habari ni ushahidi gani mwingine tulionao wa kueleza chimbuko la utekaji na sababu zake?

Kwa nini tusingoje vyombo vya usalama vikafanya uchunguzi na hatimaye tukawa na sauti ya kusemea? Muenendo huu tunaoanza kuuzoea ni mbaya sana na unaleta dalili mbaya katika mstakbari wa amani yetu. Ni bora moderator kama yupo akachuja habari kama hizi.

Mimi ni mmoja kati ya waliosikitishwa na kuhuzunishwa na tukio lililompata ndugu yetu. Natoa changamoto kwa vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kupata chanzo na wahusika katika tukio hili la kinyama na ambalo liko tofauti na mazingira ya Tanzania. Naungana na watanzania wenzangu pia kumtakia matibabu mema ndugy yetu na Mungu amponeshe mapema
 
I dont know what is this. Is the country crazy? Where is everyone? Am i crazy? Haki ya nani kipindi hiki watajua daktari ni nani? Yote waliyofanya nimesamehe ila siyo hili la leo. Kama alivyowahi kusema the late founder of the nation he jk nyerere. Hii ni kama kula nyama ya mtu. Dhambi hii itawafuata milele
 
Kadiri unavyofanya uonezi kwa mtu fulani ndivyo unavyozidi kumpa ujasiri wa kurevange. Na kadiri unavyozidisha maumivu yake ndivyo unavyokoleza chuki yake kwako. Rebers ni wapigania haki waliochoka kunyanyaswa na siku zote huo wanaungwa mkono na wananchi waliochoshwa na utawala wa mabavu. Nawaona Rebers haoooo wanakuja kwa kasi ya umeme Tanzania.
 
Hamna anayeweza kupinga kwamba madakatari kwamba wanahaki ya kutetea haki zao. Ni jambo la msingi lakini kuzingatia kwamba kazi ya udaktari kutokana na asili yake ina sura tofauti sana na kazi nyingine. Mtu yoyote anapoamua kuingia kazi ya udaktari ni lazima awe amefikilia na kukubali changamoto za lazima zinazofungamana na kazi ya udaktari.

Mimi mwalimu leo nikigoma hata kwa wiki mbili madhara nitakayosababisha yanaweza kufidika. Kama wanafunzi hawakusoma vipiti ishirini ninaweza kufidia kwa kuongeza masaa na siku za kufanya kazi na wanafunzi wakaelewa na kufaulu pengine hata zaidi. Lakini mimi daktari nikigoma kwa masaa kumi na mbili tu hasara yake siwezi kufidia hata kama nikifanya kazi kwa masaa ya ziada zaidi ya mwaka.

Ni ndugu zenu, watoto wenu na mama zenu wangapi wamepoteza maisha yao toka mlipogoma. Jaalia kwama mgogoro wenu na serikali unaisha na mnalipwa fedha zote mnazozidai manaweza kutumia miujiza gani kurejesha maisha ya watu yaliyopotea kutokana na mgomo wenu.

Kama binaadamu wa kawaida tena watoto wa kikiristo na kiislamu hivi kwa akili zenu za kawaida hamtegemei kwamba migomo yenu itapelekea vifo vya watanzania wa kawaida ambao kodi zao na za baba zao ndio zinalipa mishahara yenu na mafuta ya magari zenu na kodi za nyumba zenu. Watanzania hawa hawa ambao kodi zao ndizo zilizokutoweni katika utoto wa wakulima na kuwa madaktari bingwa?

Mtambue kwemba sheria ilipoweka vikwazo katika migomo ya madaktari tofauti na watu wengine haikulenga kuwabagua madakatari bali ilizingatia unyeti na umhimu wa fani yenu. Hayo yalipaswa kuwa mambo ya kwanza kabla hamjachagua kuwa madaktari. Kama mngekuwa wabunge au wafanyabiashara migomo yenu isingetunyima usingizi.

Ni bora pia tujue kuwa maisha ya leo hapa duniani ni m,wanzo tu na njia ya maisha ya baadae yasiyo mwisho. Ni vizuri tungetafuta namna ya kupigania haki zetu isiyoghalimu maisha yetu. Vinginevyo sio vibaya kama tukijiuliza mara mbili kama tulikuwa sahihi kuchagua fani hii takatifu ya udaktari.

Wapo marafiki zetu ambao zamani walichagua kazi za upadri na ushehe lakini baada ya kuona changamoto na mitihani katika kazi hizo waliondoka kwa heshima na kuwaacha wenye mioyo thabiti kuendelea na kazi hiyo. Sio vibaya kama mtu atajiuliza mara mbili na kuona kama anaweza kuhimili changamoto ya kazi ya udaktari na akiona la akatafuta kazi nyingine kuliko kuwa chanzo cha ukengeufu katika fani
 
Acha uoga, uko nyumbani jisikie huru.
Watanzania wenzangu hizi kauli tunazozitoa zinaweza kuonekana ni nyepesi sana lakini madhara yake yanaweza kuwa makubwa sana na yakaathiri watu wengi wasiokuwa na hatia. Tuhuma ya kuteka mtu kwa nia ya kumuuwa kijasusi ni shutuma kubwa sana. Ni lazima mtu anayetoa kauli kubwa kama hiyo awe na ushahidi wa kutosha.

Sijui kati yetu tunaongea kwa kumsisitizo tuna ushahidi wowte wa kuonesha ni nani kutoka serikali na kwa amri ya nani kahusika na utekaji huo? Kama hatuna ushahidi kwa nini tusifanye uchunguzi kwa chini chini na hatimaye tukipata ushahidi ndio tuwe na haki ya kuzungumza?

Mbali ya kusoma magezetini na kusikia katika maredio na vyombo vingine vya habari ni ushahidi gani mwingine tulionao wa kueleza chimbuko la utekaji na sababu zake?

Kwa nini tusingoje vyombo vya usalama vikafanya uchunguzi na hatimaye tukawa na sauti ya kusemea? Muenendo huu tunaoanza kuuzoea ni mbaya sana na unaleta dalili mbaya katika mstakbari wa amani yetu. Ni bora moderator kama yupo akachuja habari kama hizi.

Mimi ni mmoja kati ya waliosikitishwa na kuhuzunishwa na tukio lililompata ndugu yetu. Natoa changamoto kwa vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kupata chanzo na wahusika katika tukio hili la kinyama na ambalo liko tofauti na mazingira ya Tanzania. Naungana na watanzania wenzangu pia kumtakia matibabu mema ndugy yetu na Mungu amponeshe mapema
 
Acha uoga, uko nyumbani jisikie huru.

Suala sio owoga bali ustaarabu wa kauli. Kama kuna ushahidi wa madai ni bora tukauweka wazi. Hatuwezi kuzigeuza hisia na speculation zetu kuwa ukweli hata kwenya tuhuma nzito kama hizi. Kwani kuna faida gani tunapata kwa kutoa tuhuma ambazo hatuwezi kuzithibitisha hata kama zinaleta uchochezi ndani ya nchi?
 
Back
Top Bottom