Namshauri Ummy Mwalimu Waziri wa Afya kutengua Kauli ya kuruhusu Clinic binafsi katika hospitali za umma

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,330
9,750
Ndugu zangu watanzania,

Muda mfupi nimetoka kumsikiliza Waziri wa Afya mh Ummy mwalimu kiongozi mchapa kazi na ambaye siku zote na wakati wote amefanya kazi kubwa Sana na ya kutukuka katika kila Wizara aliyopelekwa na kuaminiwa . Kauli ya Waziri inatoa ruhusa kwa madaktari kuwa na private clinic ndani ya hospitali za umma. Binafsi kauli hii nilipokuwa na msikiliza Waziri wangu nimejikuta moyo na mwili wangu vikipigwa ganzi,mwili ukitetemeka ,moyo ukisononeka na macho yangu yakififia huku sauti ya Waziri wangu ikijirudia masikioni mwangu muda wote na kuninyong'onyesha.

Ndugu zangu kauli ya mh Waziri italeta athari kubwa Sana katika secta ya Afya na kutuathiri sisi watanzania wanyonge wa kipato Cha chini.katu na kamwe huwezi ukaweka hospitali ndani ya hospitali,mfumo ndani ya mfumo, Mfumo na utaratibu wa hospital ya private ndani ya mfumo na utaratibu wa hospitali ya umma pasipo maandalizi Wala mashauriano Wala kupima athari.Tutadhorotesha utolewaji wa huduma Bora za Afya kwa watanzania.kutakuwa na haja na sababu ipi ya mtanzania kwenda hospitali za umma? Kimbilio la mnyonge litakuwa wapi? Tumaini la watanzania masikini itakuwa wapi? Yatima,wazee na watu wasio jiweza Nani atawafuta machozi?

Ni Daktari yupi ataacha kuwekeza nguvu zake muda wa ziada ili ajipatie pesa yake binafsi? Hatuoni suala hili litapunguza ufanisi wa madaktari na kujituma vyema muda wa kawaida? Hatuoni itakuwa Ni mashindano kwa madaktari kutumia muda wa ziada? Hatuoni vifaa Tiba vilivyo nunuliwa kwa Kodi za watanzania wanyonge vinaweza kutumika zaidi muda wa ziada kuliko ule wa kawaida? Ni vipi Daktari atafanya kazi kwa ufanisi ikiwa muda mwingi anautumia muda wa ziada na usiku kucha na kuamka huku akiwa amechoka mwili na akili muda anaohitajika kuwahudumia wagonjwa katika mfumo wa hospitali ya umma unavyokuwa? Hatuoni hapa wagonjwa watakosa haki ya kupokewa vizuri,kusikilizwa na kuhudumiwa vyema ikiwa watakuta daktari alikesha anafanya kazi zake za kuwahudumia wagonjwa binafsi.

Utaratibu wa vifaa Tiba na madawa ya serikali utakuwaje ikiwa mapato haya ya ziada yanakwenda kwa mtu binafsi? Hatuoni pia utaratibu huu unaweza ukawagawa madaktari. Vipi vifaa Tiba vya serikali vikiharibika muda wa ziada ambao mapato ni ya mtu binafsi? Nani atabeba jukumu na gharama za kutengeneza ? Nani atakubali kuwa viliharibika muda wa ziada? Hatuoni hata madawa ya serikali yanaweza kutumika hovyo na kwisha mahospitalini na kuwanyima haki ya kupata dawa wanyonge? Sasa Kuna haja gani ya kupiga marufuku maduka ya Dawa ya watu binafsi kuwa karibu na hospitali za umma? Au Nini tofauti yake katika haya mawili la kuruhusu private clinic ndani ya hospitali za umma na kupinga maduka binafsi karibu na hospitali za umma?

Unaweza kufanya majaribio katika mambo mengi lakini siamini Kama unaweza ukafanya mzaha na majaribio katika Afya za watanzania,Afya ndio mtaji wetu watanzania,ndio Tumaini letu,ndio Taa yetu ,ndio uchumi wetu,ndio maendeleo yetu,.huwezi ukacheza na uhai wa watu,uhai haununuliwi Wala hautengenezwi kamwe. Kama lengo Ni kuwaongezea mapato na vipato Jambo ambalo nami naliunga mkono ,Basi serikali iwaongezee mishahara na marupurupu,kuwalipa fedha za over time, kuwaboreshea mazingira ya kazi ,kuwapa fursa za kujiendeleza kielimu na kuwalipa stahiki kulingana na Elimu zao,kuwapandisha vyeo na madaraja kwa wakati na kuongeza watumishi wa Afya zaidi ili waliopo wasielemewe na wingi wa wagonjwa na hivyo kuchoka kimwili na kiakili katika kuwahudumia, Kuwa na mfuko maalumu wa kuwasaidia kupata mikopo kwa haraka na kwa riba nafuu na mengine mengi.

Tusiyaweke rehani maisha ya watanzania wanyonge.,wazee wetu ,wajane ,yatima na watu mbalimbali wasiojiweza wanategemea hospitali za umma Sana ,ndio kimbilio Lao na ndio Tumaini Lao,ndio faraja kwao na ndio mkombozi wao.sasa tukiwatelekeza tutakuwa tunawaua na kuwaangamiza kabla ya wakati wao uliopangwa na Mwenyezi MUNGU na tutakuwa tunaua Taifa na nguvu kazi ya Taifa . Tufanye kwa kadri iwezekanavyo kuhakikisha ya kuwa secta ya umma inaleta matumaini kwa watanzania kila Siku,tuwafanye watanzania waone hospitali za umma ndio nafuu zaidi na wakati wote waongoze huko ambako ndiko kuliko na Kodi zao.

Huwezi ukawatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja,huwezi ukatumikia mifumo miwili tofauti kwa ufanisi ndani ya eneo moja la umma ,yaani asubuhi mjamaa na jioni bepari.hiyo haiwezekani. Nashauri Utaratibu huu usitishwe mpaka wadau washilikishwe nasisi wananchi Tutoe mawazo yetu.

Nawapendeni Sana madaktari wetu lakini katika hili itakuwa Ni kuwaweka majaribuni Sana na kufifisha utolewaji wa huduma za Afya kwa wagonjwa muda wa kazi na tutasikia malalamiko mengi Sana kutoka kila Eneo

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Soma:
- Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi

- Ummy: Madaktari Bingwa kufanya kazi ya Kliniki binafsi katika Hospitali za umma baada ya saa za kazi sio jipya
 
Nieleweshe tu badala ya kunishambulia kwa kejeri maana sipo hapa kushindana na serikali yangu mwenyewe iliyoundwa na chama changu.
 
Wewe ni mnyonge hakika...ungefupisha hadithi ..mimi.sijasikia Hilo Tangazo ,IL Kwa Unyonge na Uandishi huu nahisi kama hukumweleea Waziri!
 
Acha wivu wewe, punguza kiranga. Wewe una akili kuliko waziri? Unadhani katamka kwa bahati mbaya?
 
Kuandika mambo meengi yaliyostahili kundikwa kwa paragraph mbili tu ni dalilli za kutafuta mantiki wakati unaandika!

Kaa chini, tengeneza hoja kwa weledi kisha andika unachokusudia. Kisha sasa weka namba yako ya simu
 
Acha wivu wewe, punguza kiranga. Wewe una akili kuliko waziri? Unadhani katamka kwa bahati mbaya?
Ndo Wazalendo uchwara hawa. Kuhangaika tu na Mambo yasiyo muhimu na kuacha mambo yenye mslahi kwa nchi. Hilo jitu ni jinga sana
 
MAWAZIRI HAO WAUZA BANDARI?KM WANAAKILI KWANN HUDUMA NI MBOVU KWENYE MAHOSP ZETU ZA UMA
Kwa Sasa hospitali za umma zimeboreshwa na zinaendelea kuboreshwa kila leo,ndio maana unaona hata bajeti ikiongezeka kila mwaka wa fedha ili kuhakikisha kuwa watanzania wanapata huduma Bora.
 
Waziri Ummy Mwalimu ameruhusu madaktari wa serikali kutumia hospitali za umma kama private clinics baada ya saa za kazi. Jambo hili lina ukakasi lakini ndiyo hivyo tena sisi wananchi hatuna namna bali kukubali kwa kuwa hoja ikisha kubaliwa na kupitishwa na CCM ndiyo maamuzi ya mwisho.

Sasa kwa kutumia busara hizo hizo za CCM basi uamuzi huo usiishie kwa madaktari tu bali pia watumishi wote wa serikali waruhusiwe kutumia mali na ofisi za umma kwa shughuli zao binafsi. Waalimu wafanye tuition mashuleni baada ya muda wa kazi, wahandisi, madereva, wahasibu nk.

Serikali isifanye ubaguzi wala upendeleo katika hoja hii. Wananchi wote wanalipa kodi hivyo wana haki ya kutumia rasilimali za umma kwa usawa. Ikiwezekana shughuli zote za umma zibinafsishwe kwa sababu serikali imeshindwa kuzisimamia.
 
Back
Top Bottom