Serikali Kutoa kauli Kuhusu Mgomo wa Madaktari kesho

Mnyika kaomba kwanini tunasikiliza upande mmoja tu wa serikali mbona kamati ya bunge na madaktari hawasikilizwi?
Na hii ndo njia nzuri ya kutatua mgogoro huu!!!! Siyo kusikiliza serikali hii tata ambayo kila kukicha wanatoka na empty promises. Waje na open debate kati wa Madaktari na hiyo serikali!!!
 
Hivi ile hoja ya kutokuwa na imani na Pinda (serikali) imeishia wapi?

Au lile changa la macho (baraza jipya la kiini macho) ndio hitimisho?
 
Serikali dhaifu imemshindwa hata Dr Ulimboka! he iz alive and kicking

Mungu ni mwema
 
mimi sio mtabiri ila nasema kwamba kauli iliyotolewa na waziri mkuu wa serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya mgoma wa madaktari katika chombo kikubwa cha nchi yaani Bunge itapelekea hitimisho la kuanguka kwa serikali serikari ya CCM. Nasema asante Pinda kwa kutusaidia kuiondoa hii serikali mapema.
 
mimi sio mtabiri ila nasema kwamba kauli iliyotolewa na waziri mkuu wa serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya mgoma wa madaktari katika chombo kikubwa cha nchi yaani Bunge itapelekea hitimisho la kuanguka kwa serikali serikari ya CCM. Nasema asante Pinda kwa kutusaidia kuiondoa hii serikali mapema.
Umenena haswa
 
Liwalo na liwe, Ccm watashinda uchaguzi mwaka 2015.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
Hisia zangu ni hizo jamani -- maana mtoto wa mkulima ameshindwa kutatua mgomo huo, kwa sababu tu hana mamlaka ya kuamua mambo, mamlaka yote yako kwa JK, the playboy.
 
He is difeating his moral? If his integrity is high he should resign mbona Lowasa aliresign.
 
"Liwalo na liwe" sasa limekuwa.Tuseme tuna kiongozi ama screen sever. Kwa kutamka hivyo alikua ana maana gani. Hili ndio tatizo la viongozi wetu kupewa madaraka kama njugu ikfikia hatua ya kutatatua matatizo makubwa ktk jamii kama hili lla madaktari ili kunusuru maisha ya Watanzania tunabakia kusema liwalo na liwe. Serikali ikiambiwa ni dhaifu na legelege wanaona wametukanwa. Unapokuwa na viongozi wanaoongoza nchi mithili ya kucheza mcheźo wa kujificha basi ujue hali sio nzuri hata kidogo. Mbaya zaidi hili limetokea waakati huu serikali inavutana na madaktari hadi kufikia hatua ya mgomo brk. Sijuui hali na afya za watanzania wenzetu hazijulikani hatma yake.
 
Hili hili ndilo litamuondoa. mimi nimeanza kuchoka naye -- kumbe hana lolote. Mtu mzima..hovyo..!
 
Mbona alipotaka kupogiwa kura ya kutokua na imani bungeni hakusema liwalo na liwe matokeo yake akawa anakesha kwenye vikao mpaka usiku wa manane ili kuokoa ulaji wake. Ama kweli mtoto wa mkulima amepoteza mvuto.
 
Kauli za ajabu kama hizo sio za kwanza kutolewa na viongozi wakubwa wa nchi hii lakini hakuna effect yeyote(ya kujiuzulu au kuanguka) so msitegemee lolote jipya.
 
katika mgomo uliopita mkuu wa nchi aliahidi kulishughulikia madai ya madaktari,na kuwaahidi watanzania kwamba hali kama hii haitatokea tena,cha kushangaza ni kwamba kabla hata miezi 4 haijaisha mgomo wa madaktari umejirudia tena.hii imetokana na kutokutekeleza ahadi na kile alichoamini kwamba ni suluhisho la kudumu. matokeo yake ndiyo haya sasa,pamoja na vitisho vya waziri mkuu.WATANZANIA tunaamini kwamba vitisho na suluba havijengi bali ni mwanzo wa machafuko.nadhani ni wakati mwafaka kwa serekali kufanya maamuzi ya busara na kuacha kejeli za LIWALO NA LIWE.
 
Back
Top Bottom