Ummy: Madaktari Bingwa kufanya kazi ya Kliniki binafsi katika Hospitali za umma baada ya saa za kazi sio jipya

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema suala la Madaktari Bingwa kufanya kazi ya Kliniki binafsi katika Hospitali za umma baada ya saa za kazi sio jipya na tayari linafanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, JKCI, Ocean Road na Taasisi ya Mifupa MOI ambapo lilianza kutekelezwa zaidi ya miaka 15 iliyopita (IPPM-Intramural Private Practice).
WhatsApp Image 2023-07-12 at 11.35.59.jpeg

Waziri Ummy amesema lengo ni kutoa muda zaidi kwa wananchi kuweza kupata huduma za matibabu ya kibingwa kutoka kwa wataalam hao na pia kutoa motisha kwa kuongeza kipato cha madaktari bingwa na bobezi walioajiriwa na Serikali.

“Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwenye Sekta ya Afya, sasa tunataka kushusha utaratibu huu kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa ili kubakiza Madaktari bingwa waendelea kufanya kazi mikoani, hili jambo lina tija katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa Mikoani, Daktari bingwa anapata na Hospitali inapata, muhimu kuweka utaratibu mzuri na wa wazi” amesema Waziri Ummy.

“Tuna uhaba wa Madaktari bingwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, Mwezi uliopita tulitangaza nafasi 35 walioomba ni 15 tu, kama Wizara tutaendelea kuweka mikakati mbalimbali ili kuvutia Madaktari bingwa kufanya kazi katika Hospitali za umma hasa za Mikoani” amefafanua Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa utaratibu huo utawezesha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wanaohitaji kuhudumiwa kwa uharaka na kuwatuliza Madaktari kwenye vituo vyao vya kazi na kuwapunguzia adha ya kukimbia kwenye vituo binafsi(maarufu vijiwe au vioski) baada ya muda wa kazi.

“kukimbia kimbia maeneo tofauti hii kunashusha heshima ya kitaaluma kwao na wengine kulazimika kufanya kazi katika mazingira hatarishi na yenye uwekezaji mdogo wa miundo mbinu na vifaa Tiba kuliko alivyoviacha katika Hospital yake ya Rufaa ya umma” amefafanua Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amebainisha kuwa utaratibu huo utaongeza mapato ya Hospitali za Rufaa za Mkoa. “Mapato yatasaidia kuongeza faida na uwekezaji utakaowafaidisha wagonjwa wote, unachangia kuwezesha hospitali kuhudumia wagonjwa wa msamaha, kuongeza motisha kwa watumishi wote kutokana na mapato hayo ambayo hugawanywa watumishi wote wa Hospitali husika"

Pia, soma:

1. Namshauri Ummy Mwalimu Waziri wa Afya kutengua Kauli ya kuruhusu Clinic binafsi katika hospitali za umma
2. Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi
 
Kwahiyo serikali imekili imeshindwa kutoa motisha ya kutosha kwa hao madakitari bingwa wachache? Ili wa achane na clinic binafsi kama mbuge moja analipwa wastani wa 20m kwa mwezi. Kwanini wasipunguze idadi ya ya bunge kama hao covid 19 huo mshahara ulipwe hao madakitari bingwa 20m kila moja kwa kila mwenzi tuone kama kuna atakae enda na private clinics, wizara ina poor planning policy TZ nzima haina madakitari bingwa zaidi ya 100 ni wacheche sana ila mnashindwa kuwa motisha vya kutosha...... .
 
WAZIRI UMMY MWALIMU ATOA UFAFANUZI WA KLINIKI ZA MADAKTARI BINGWA BAADA YA SAA ZA KAZI

“Utaratibu wa kutoa huduma za afya binafsi baada ya masaa ya kazi sio jambo jipya” amesema Waziri Ummy na kuongezea kuwa utaratibu huo umekuwa ukifanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Mifupa MOI na Taasisi ya Saratani Ocean Road.

Waziri Ummy amesema kuwa utaratibu huo unasimamiwa na miongozo mahususi iliyopitishwa na bodi za Hospitali husika.

“Muhimbili utaratibu huu Muhimbili wanauita Intramural Private Practice at Muhimbili, (IPPM), Wizara inaona kwamba ni jambo lenye tija kushusha utaratibu huu kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa” ameeleza Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema utaratibu huo utawezesha wananchi kuhudumiwa kwa haraka lakini kwa kulipia kwa ziada, kuwatuliza madaktari kwenye vituo vyao vya kazi pamoja na kuwapunguzia adha ya kukimbia kwenye vituo vingine vya kazi 'vijiwe' baada ya muda wa kazi.

“Zoezi hili haliendi kuathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi badala yake linakwenda kuboresha upatikanaji wa huduma za kibingwa kwa wananchi katika maeneo yao.

“Utaratibu huu unalenga kuhakikisha tunavutia madaktari bingwa kufanya kazi mikoani, tumetangaza nafasi za madaktari bingwa 35 mwezi Juni 2023 wakaomba madaktari 15, 11 walikidhi vigezo, wakaripoti madaktari bingwa 6 tuu”

Waziri Ummy amesema ni wajibu wa Serikali kuweka mazingira ya kuvutia madaktari bingwa kufanya kazi katika hospitali za umma.

Amesema kuwa utaratibu huo utazinufaisha Hospitali kwa kuongeza mapato kwakuwa watu wanaofika kwenye kliniki binafsi watalipia kwa gharama ya juu tofauti na wale wa muda wa kazi za mwajiri.

Soma:
- Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi
 
Kwa hiyo madaktari watatumia vifaa vya serikali bila kuvilipia?

Wizara haioni kuwa huu ndio mwanzo wa madaktari kujimbonjisha makusudi wakati wa kazi na kuambia wagonjwa wawaone baada ya saa za kazi?
 
Kuna tetesi za uwepo wa ugonjwa wa kipindu pindu wilaya ya kinondoni - Bunju - wataalamu wa afya fwatilieni
 
Hivi hawa watu ni kwa nn wanang'ang'ania kutuongoza ili hali wameonesha kushindwa kutatua kero zetu?
Badala ya kutatua matatizo always wanayaongeza
Tunaomba CCM mtupishe sasa aingie hata Hashim Rungwe
 
Kazi ndio hizo za udaktari bingwa jamani!

Ualimu siyo kazi. Mwalimu akifundisha twisheni kwenye majengo ya serikali atakipata cha mtema kuni.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema suala la Madaktari Bingwa kufanya kazi ya Kliniki binafsi katika Hospitali za umma baada ya saa za kazi sio jipya na tayari linafanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, JKCI, Ocean Road na Taasisi ya Mifupa MOI ambapo lilianza kutekelezwa zaidi ya miaka 15 iliyopita (IPPM-Intramural Private Practice).
View attachment 2685696
Waziri Ummy amesema lengo ni kutoa muda zaidi kwa wananchi kuweza kupata huduma za matibabu ya kibingwa kutoka kwa wataalam hao na pia kutoa motisha kwa kuongeza kipato cha madaktari bingwa na bobezi walioajiriwa na Serikali.

“Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwenye Sekta ya Afya, sasa tunataka kushusha utaratibu huu kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa ili kubakiza Madaktari bingwa waendelea kufanya kazi mikoani, hili jambo lina tija katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa Mikoani, Daktari bingwa anapata na Hospitali inapata, muhimu kuweka utaratibu mzuri na wa wazi” amesema Waziri Ummy.

“Tuna uhaba wa Madaktari bingwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, Mwezi uliopita tulitangaza nafasi 35 walioomba ni 15 tu, kama Wizara tutaendelea kuweka mikakati mbalimbali ili kuvutia Madaktari bingwa kufanya kazi katika Hospitali za umma hasa za Mikoani” amefafanua Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa utaratibu huo utawezesha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wanaohitaji kuhudumiwa kwa uharaka na kuwatuliza Madaktari kwenye vituo vyao vya kazi na kuwapunguzia adha ya kukimbia kwenye vituo binafsi(maarufu vijiwe au vioski) baada ya muda wa kazi.

“kukimbia kimbia maeneo tofauti hii kunashusha heshima ya kitaaluma kwao na wengine kulazimika kufanya kazi katika mazingira hatarishi na yenye uwekezaji mdogo wa miundo mbinu na vifaa Tiba kuliko alivyoviacha katika Hospital yake ya Rufaa ya umma” amefafanua Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amebainisha kuwa utaratibu huo utaongeza mapato ya Hospitali za Rufaa za Mkoa. “Mapato yatasaidia kuongeza faida na uwekezaji utakaowafaidisha wagonjwa wote, unachangia kuwezesha hospitali kuhudumia wagonjwa wa msamaha, kuongeza motisha kwa watumishi wote kutokana na mapato hayo ambayo hugawanywa watumishi wote wa Hospitali husika"

Pia, soma:

1. Namshauri Ummy Mwalimu Waziri wa Afya kutengua Kauli ya kuruhusu Clinic binafsi katika hospitali za umma
2. Ummy Mwalimu: Ruksa Madaktari kutumia hospitali za Serikali kama private clinic baada ya muda wa kazi
Kwahiyo ni Hapana kupumzika kwa hao wataalamu...... Sasa muda wa kufanya kazi za mshahara wa mwisho wa mwezi watakua wana sinzia mwanzo mwisho.....
 
Back
Top Bottom