Serikali Kutoa kauli Kuhusu Mgomo wa Madaktari kesho

makunyazi.jpg mzee wa makunyanzi akiwa anatabasamu
 
PM amepoteza nguvu... Kauli zake zinatatanisha,you know why?
Kama kiongozi mkuu wa serikali bungeni ktk majinu yake alitakiwa simply kujibu kidiplomasia,lakini kauli yake ya liwalo na liwe na kilichomtokea Dr SU ni ushahidi wa nia ovu kutoka ktk kauli yake
Pia kwa kusema kwake eti serikali iliona iache mambo mengine katika mgomo ili wapishe masuala ya kisheria,does it mean kuwa kulikuwa na undisclosed agenda na sasa ndio wameamua kuachana na masuala ya kisheria na kuendelea na hayo mambo mengine?
kwa kusema atatoa kauli kesho hiyo pia imemshusha kuwa hawezi kama yeye kutamka kitu mpaka akapewe maelekezo ya juu na hasa ukikumbuka kauli zake ktk mgomo uliopita jinsi zilivyoyeyuka kama moshi
Je yeye kama kiranja wa mawaziri alishamtuma ama kumuuliza Dk Mwinyi ktk appointment yake mpya ameshakutana na madaktari na kuwasikiliza au kuendeleza pale raisi alipoishia?
Kuenda mahakamani pia ni UDHAIFU..ile ni jumuia ya madr na walijua wakiunda legal entity watakuwa subjected na utawala wa sheria(mahakama) sasa wakaunda jumuia,ambayo kimsingi serikali itakuwa ngumu kuwabana,sasa serikali inashtaki kivuli??
tuangalie kiini cha mgomo then tusonge mbele.katika meza ya majadiliano sio kila dai lazima litekelezwe kwa 100 percent,unaweza kugawanyisha kilichopo kikaingia katika madai yote na wadai wakaridhika kuwa angalau umewaconsider rather than to remain silent as if you are not responsible
Tunasubiri kauli ya kesho na isije kugeuka.
 
Nilikuwa sijui,kumbe sura ya mtu ina reflect roho yake na akili yake pia!
 
Mzee wa kulia huyo,mnakumbuka alilia bungen kuhusiana na ma albino?. Sasa leo katoa tena kaul tata kuhusu ma dr nadhan akibanwa atatoa machoz tena. Na hiv hampendagi dr ulimboka, sijui.
 
mimi sio mtabiri ila nasema kwamba kauli iliyotolewa na waziri mkuu wa serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya mgoma wa madaktari katika chombo kikubwa cha nchi yaani Bunge itapelekea hitimisho la kuanguka kwa serikali serikari ya CCM. Nasema asante Pinda kwa kutusaidia kuiondoa hii serikali mapema.

Uongozi as we know it si lele mama!...MP ame-demostrate the highest level of incompetence kwa cheo shake.
 
Yametimia yale aliyowaambia Mh. Mnyika bungeni Juzi. ila kwa sababu ni sikio la kufa.
 
Hii ndiyo Serikali ya CCM ikijibu hoja ya Mgomo wa Madaktari mbungeni kupitia Kaimu mkuu wa kaya ndani ya Jumba la Viyoyozi.
1. Liwalo na Liwe
2. Kama Noma na iwe Noma
3. Weka Mboga mi namwaga ugali
4. Weka Ugoko mi naweka Chuma
5. Bwai Bwai tu
 
Huyo ndio pinda bwana na kauli zake tata, akibanwa anaanza kulia na kutoa machozi. Au mmesahau kauli ya kuhusu wauwaji wa maalbino?. Alibanwa bungen akatoa machozi. Subirini.
 
Pinda ni shokabuzoba ya serikali ya JK

Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 22 December 2010

KATIKA gari kuna chombo kiitwacho shock absorber (shokabzoba); madereva mitaani wanaziita ‘shokap’. Kazi kubwa ni kuongeza mneso wa gari na kupunguza mtikisiko mkubwa likiingia kwenye mashimo mashimo au barabara mbovu.

Shokap zikiharibika mneso kwenye ga...ri unakosekana na hivyo likiingia kwenye mashimo hudunda na kurusha sana na huweza kusababisha vifaa vingine kuharibika.

Rais Jakaya Kikwete aligundua kwamba gari (serikali) alilokuwa anaendesha halikuwa na shokap bora (Waziri mkuu madhubuti) ndiyo maana lilishindwa kuhimili katika barabara iliyojaa mashimo ya EPA na kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Mwaka 2008 Kikwete akiwa ameelemewa na shutuma dhidi ya gari lake kwamba lilikuwa linajigonga ovyo na kurusha roho za abiria (wananchi), alituliza akili mwaka 2008 akaagiza shokap mpya. Alimteua Mizengo Peter Kayanza Pinda kuwa waziri mkuu.

Pinda ametumika kama shokap mwenye jukumu kubwa la kuzuia mihemuko ya watu iliyokuwa inatikisa serikali yake katika kashfa za Meremeta/ Tangold, pamoja na madai ya Mahakama ya kadhi na Katiba mpya.

Staili ya Pinda kwanza ni kusoma hoja zinazotolewa na wananchi dhidi ya serikali, kupima uzito wake, kusoma aina ya watu wanaotoa hoja ili ajibu kulingana na kaliba yao. Pili husoma kiwango cha mhemko wa wananchi katika uwasilishaji hoja.

Halafu huingia kwenye kabati la majibu na kuchomoa anayoona yanafaa kwa wakati ule. Majibu yake huwa hayatoi ufumbuzi wa mwisho ila kuteka hoja iliyopo na pale anapokuwa amezidiwa ‘humwaga chozi’ basi.

Katika baadhi ya maeneo Pinda huwalainisha wakosoaji wa serikali kwa kukubali udhaifu au husema serikali imeliona hilo na inalitafutia ufumbuzi wa kudumu huku akitoa angalizo baadhi ya mambo huhitaji muda mrefu.

Pinda, hjajatoa ufumbuzi wa kudumu juu ya matatizo makubwa ya kifisadi yaliyoikumba serikali isipokuwa kauli njema ya matumaini.

Kwa staili hiyo Pinda amefanikiwa kupunguza kelele au kuziba kwa viganja shutuma au malalamiko. Mpaka lini?

Pinda maarufu kama Mtoto wa Mkulima amefanya kazi Ikulu hivyo anajua mambo mengi ya kiutawala, mazuri na mabaya.

Anajua kampuni nyingi bomu zilivyoruhusiwa kama Meremeta, namna ilivyoingizwa nchini IPTL na hata mkubwa mmoja alivyojigawia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira kwa kisingizio cha uwekezaji.

Baadaye akaingia katika siasa, akateuliwa Waziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi). Hivyo wakati inaibuka kashfa ya Richmond iliyoporomosha heshima ya gari la Kikwete hadi kumwangusha mtangulizi wake Edward Lowassa, yeye alikuwa serikalini.

Mwanasheria Pinda ndiye msaada pekee katika serikali ya Kikwete kuzima, kupoza, kulainisha mioyo ya watu waliochoshwa na ufisadi unaopaliliwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kikwete alimteua Pinda katika kipindi ambacho watu walikuwa wakihoji kama kweli mkuu huyo wa nchi ni ‘Chaguo la Mungu’ kama walivyosema maaskofu.

Pinda aliteuliwa katika kipindi ambacho shokap ya kwanza ilivunjika na kuharibika kabisa baada ya kuingia katika shimo la Richmond. Kwa mwonekano serikali iliporomoka pale.

Pinda alilainisha mioyo ya wabunge na wananchi kwa kukiri udhaifu wa serikali kiutendaji, akaahidi kufanyia kazi mapendekezo ya Bunge. Badala yake kilichofanyika ni kusafisha baadhi ya watuhumiwa, na hata waliopaswa kuadhibiwa waliachwa ufike muda wao wa kustaafu.

Kuhusu wizi wa mabilioni ya fedha uliofanywa kupitia kampuni ya Meremeta, alidai suala hilo linahusiana na siri za Jeshi la Wananchi na kwa hiyo hawezi kutoa siri hizo. Hii ni mbinu inayotumiwa na serikali kuficha, maana hata wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje ‘EPA’ ilidaiwa fedha zilichukuliwa kwa masuala ya usalama wa taifa.

Alitoa majibu hayo kunyamazisha wabunge huku akijua muundo wa kampuni hiyo haukuwa unahusiana na jeshi. Vilevile alitoa majibu hayo akijua uchimbaji wa madini si siri. Wabunge wamebaki wakijiumauma!

Kuhusu mkuu wa nchi mstaafu kujiuzuia Kiwira, Pinda alisema jamii ichunguze kwanza dhamira ya kiongozi huyo kama kweli alikuwa na nia ya ufisadi. Alisema kwa kadri anavyojua yeye zile zilikuwa juhudi za kuokoa mgodi huo!

“Kama kweli ni fisadi ilitakiwa tuone ana madege mangapi, ana mabilioni katika mabenki. Jamani, mimi naamini kwamba dhamira ya kiongozi huyu ilikuwa safi tu na kuondoa kiwingu hiki serikali inauchukua tena mgodi huo,” alisema Pinda.

Majibu hayo hayakufuta mtikisiko bungeni ila yalisaidia kufunika udadisi wa wabunge maana mpaka mtu awe na madege ndipo astahili kuitwa mhujumu uchumi.

Kikwete mwenyewe aliwapa msamaha waliokwapua mabilioni ya fedha katika EPA kwamba warejeshe ili wasishtakiwe. Hata hivyo watu wanaendelea kuhoji mpaka leo iweze wezi wa mabilioni wasamehewe wakati sheria hiyo inatumika kuwafunga wezi wa kuku?

Pinda alitumika kama shokap serikali ilipowasilisha Bajeti ya mwaka 2009/ 2010 ikifuta msamaha wa kodi ambao taasisi za dini zilikuwa zinanufaika. Ukaibuka mtikisiko mkubwa nchi nzima na bungeni.

Pinda alihangaika usiku na mchana kufanya vikao na maimam na maaskofu Dar es Salaam na Dodoma kwa lengo la kupata ufumbuzi. Alituliza hasira za watu kwa kuahidi kumshauri rais urejeshwe utaratibu wa zamani —alifanikiwa.

Kuhusu shutuma dhidi ya kauli yake kwamba aliruhusu watu wajichukulie sheria mkononi kuua wauaji wa maalbino, Pinda hakuwa na jibu wala utetezi muafaka isipokuwa kulia kwa nia ya kuonyesha uchungu wa alichokiona Mwanza.

Katikati kipindi ambacho watu wanajadili hoja nzito juu ya mustakabali wa nchi, Pinda, kwa busara na umakini, ameibuka na kuteka hoja ya katiba mpya kwa lengo la kupunguza hasira za watu dhidi ya serikali na hasa Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani aliyedai suala la katiba mpya halipo na wanaotaka ni watu wa barabarani watembeao kwa miguu.

Pinda amejitokeza tena na kusema kuwa hata serikalini wanalijadili na hakuna kigugumizi akisema atamshauri Rais kuunda timu ya kushughulikia suala la katiba kama wananchi wanavyojadili.

Bila shaka Pinda amepima kasi na wingi wa maoni ya watu mashuhuri nchini, wasomi, viongozi wakuu wastaafu, majaji na wanasiasa akaona mjadala huu haukwepeki.

Amepima uzito wa hatua iliyochukuliwa na wabunge wa Chadema kumsusia Rais Kikwete alipozindua Bunge mwezi uliopita ikiwa ni njia ya kushinikiza Katiba mpya na kuundwa upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Akarejea nyuma jinsi hoja ya katiba mpya ilivyojadiliwa kwa kina mwaka jana wakati wa kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Baba wa Taifa, Nyerere iliyoandaliwa na Tasisi ya Mwalimu Nyerere.

Hapa Pinda amefanya kazi yake kama shokap kutuliza munkari tu ili watu wadhani serikali yao ni sikivu. Kama serikali imeliona na inataka kulifanyia kazi Pinda ajue kinachojadiliwa, kupendekezwa na kuhitajika kwa sasa ni KATIBA MPYA, siyo VIRAKA kama anavyodai.
 
I dont know what is this. Is the country crazy? Where is everyone? Am i crazy? Haki ya nani kipindi hiki watajua daktari ni nani? Yote waliyofanya nimesamehe ila siyo hili la leo. Kama alivyowahi kusema the late founder of the nation he jk nyerere. Hii ni kama kula nyama ya mtu. Dhambi hii itawafuata milele

Kwenye nchi kama Tanzania ambayo kwa muda wa miaka mingi tulikuwa na chuo kikuu kimoja tu kinachotoa fani ya udaktari mtu kuwa daktari kwa namna fulani ni tunu. Ni nafasi ambazo walikuwa wanapata watanzania wachache baada ya baba na mama zetu kujiminya katika vipato vyao kuchangia kodi za nchi. Wapo wengi waliokuwa na uwezo na mapenzi ya kusomea fani hiyo bali walikosa fursa kutokana na uchache wa nafasi na hata mazingira ya familia zao. Mategemeo ya watanzania wengi ni kwamba hawa watanzania wenzetu wachache waliopata bahati ya kusomea fani nyeti ya udaktari wataitumia kwa kuweka uhai wa binadamu juu ya kila kitu.


Sasa mtu hata kufikia kumbuluza daktari na kumpiga kinyama ni jambo la kusikitisha sana na linapaswa kupatiwa ufumbuzi. Lakini kwa upande wa pili, haitarajiwi kwa madakatari wetu kutumia tukio hilo la kusikitisha lililomfika mwenzeti kutishia maisha ya watanzania wengi wasio na hatia. Kuzidisha mgomo kwa sababu ya unyama aliyofanyiwa daktari wetu na mtu asiojulikana hakumukomoi wala kumuathiri huyo mtu bali kunatuathiri sisi walala hoi tunaotegemea hospitali za umma zilizowaajiri. Daktari aliefanyiwa unyama ana thamani sana lakini hao watu wanaopoteza maisha kutokana na migomo yenu wana thamani zaidi.
 
He is difeating his moral? If his integrity is high he should resign mbona Lowasa aliresign.

Mimi sioni kama kujiudhuru au kutojiudhuru Pinda kutasaidia lolote katika kuondoa mgomo wa madaktari. Mwanzoni madaktari na wanaharakati walisema asipojiudhuru Waziri Wa Afya na Katibu wake migomo itapelekea maandamano ya nchi nzima. Serikali ikasikia na kuwaondoa wote. Sasa tunataka Waziri Mkuu awajibike. Akishawajibika tutasema Raisi nae awajibike na labda utakuwa ndio mwisho wa mgomo. Sasa tatizo halisi hasa hapo ni nini?

Tukiitizama historia ya Tanzania, ni kipindi gani katika histroria ya Tanzania madaktari walikuwa wanapata maslahi mazuri zaidi ya kipindi hiki cha uwaziri mkuu wa Pinda na Uraisi wa Kikwete? Kama kuna mtu anadata ya kupinga ukweli huu aweke hadharani. Atuambie maslahi ya madaktari yalikuwa ni moja kati ya maslahi ya juu katika taaluma zote kama ilivyo sasa? Madaktari walikuwa na nafasi ya kuwa na ajira zaidi ya moja licha ya maslahi kuwa juu kuliko kabla? Tukumbuke tena kwamba wakati huo walikuwa wachache sana kulinganisha na sasa.

Kwa kusema hivyo sikusudii kumaanisha kwamba madai yao hayana msingi. Hoja yangu ni kwamba hayahalalishi migomo kama hii inayoletea kupotaza maisha yetu kila siku. Mimi naona pia kwamba uzalendo umepungua sana. Watu tunaangalia sana maslahi ya kidunia kuliko asili yetu. Sikuona sababu ya kuendelea na migomo na vitisho hata baada ya Mahakama kutoa zuio la muda wakati mgogoro kati ya madaktari na mwajiri wao unaendelea kutafutiwa suluhu.
 
...mtoto w mkulima amesahau alipotoka naye ni wale wale waishio kwenye familia dhaifu:sad:

Hii changamoto iwe ni kwa watoto wa wakulima wote na sio mtoto wa mkulima Pinda. Maana kama madaktari watoto wa wakulima watakumbuka walikotoka hawawezi kuwa tayari kuwaona ndugu zao wanakufa kwa sababu ya mapambano na mwajiri wao ya kimaslahi ya dunia
 
Liwalo na liwe.........
ndugu zanguni

hakuna aneunga mkono kupigwa na kuteswa kwa Dr ulimboka! lkn aliefanya hivyo hajulikani. suala la madaktari limekua la kisiasa. siasa ni mchezo mchafu


NIMEJIFUNZA JAMBO MOJA

Nimejifunza kuwa DAKTARI HARUHUSIWI KUGOMA KUTOKANA NA KAZI YAKE INAYOHUSU UHAI. mbona huyu dr ulimboka amekimbizwa mhimbili!!! kwa nini? jibu ni rahisi, KUOKOA MAISHA YAKE. sasa kwa nini wanagoma!? ina maana wantaka watanzania wafe? mboa serikali imetatua maombi yao kwa 70% bado TC SCan pekee na mambo madogo madogo. WANATAKA NIN HAWA MADAKTARI? WANATUMWA NA IFRITI (JINI) YUPI? waziri mkuu amesema bungeni kuwa serikali kesho itatoa msimamo wake.


USHAURI WANGU
Nashauri waziri wa utumishi awafukuze wote ambao HAWATARIPOTI KESHO ASUBUHI KAZINI. tuache kuvuruga nchi yetu yenye amani kwa MAMBO YA UCHU WA MADARAKA
 
Kwakweli mimi inaniumiza kichwa kweli. Sielewi hasa wanataka nini? Maana kasi yao haiowani hata kidogo na hoja za kuunga mkono madai yao. Naona kasi ya serikali kushughulikia madai yao imekuwa kubwa pasipo mfano lwkati kazi ya mgomo nayo inaenda juu zaidi.
 
Declaration of Geneva (1948)
Physician's Oath[h=4]Adopted by the General Assembly of the World Medical Association, Geneva, Switzerland, September 1948 and amended by the 22nd World Medical Assembly, Sydney, Australia, August 1968.[/h][h=3]CIRP Introduction[/h]The World Medical Association is an association of national medical associations. This oath seems to be a response to the atrocities committed by doctors in Nazi Germany. Notably, this oath requires the physician to "not use [his] medical knowledge contrary to the laws of humanity." This document was adopted by the World Medical Association only three months before the United Nations General Assembly adopted the Universal Declaration of Human Rights (1948) which provides for the security of the person.

[h=3]Physician's Oath[/h]At the time of being admitted as a member of the medical profession:

  • I solemnly pledge myself to consecrate my life to the service of humanity;
  • I will give to my teachers the respect and gratitude which is their due;
  • I will practice my profession with conscience and dignity; the health of my patient will be my first consideration;
  • I will maintain by all the means in my power, the honor and the noble traditions of the medical profession; my colleagues will be my brothers;
  • I will not permit considerations of religion, nationality, race, party politics or social standing to intervene between my duty and my patient;
  • I will maintain the utmost respect for human life from the time of conception, even under threat, I will not use my medical knowledge contrary to the laws of humanity;
  • I make these promises solemnly, freely and upon my honor.


Citation:
  • Declaration of Geneva (1948). Adopted by the General Assembly of World Medical Association at Geneva Switzerland, September 1948.
 
Ikiwa kesi ipo mahakamani basi mgomo huu una walakini?. Tutasema sababu zoote lakini subra jamani subra.. Kesi ya kina Yona, Mramba imechukua miaka mingapi mbona hatujavanmia nyumba zao na magari yao.Maadam kesi ipo makahamani kitakachopingwa ni uamuzi wa mahakama kama sheria imepindishwa lakini kugoma wakati kesi ipo makahamani inaonyesha wazi kutokuwa na imani na mahakama zetu, hivyo tunajichukulia sheria mkononi...Let's be ready for consiquences ndio inapoingia - Na Liwali liwe!
 
Ndugu zangu hivi tukitizama kiapo ambacho Daktari anatakiwa kujifunga nacho hawa madaktari kweli wanayohaki ya kuendelea kugoma licha ya kupoteza maisha yetu. Hivi kweli consideration ya juu kuliko yote ni maisha yetu au maslahi yao ya kifedha? Ndugu zangu madaktari tujitahidi kurudi nyuma na kuangalia kama bado tupo ndani ya maadili ya fani zetu. Hatutakiwi kutumia taaluma yetu ya udaktari kinyume cha kanuni za ubinadamu. Unapoapa na kusema "the heath of my patient will be my first consideration" unaweza kugoma kuwatibu wagonjwa hata kama watapoteza maisha yao ili mradi upate maslahi yako ya kimapato?
 
Hivi kweli sisi wapiga kura tuko wapi, kodi tutoe wenyewe, waende kukaa nazo mjengoni na kusema LIWALO na LIWE kwa uhai wa walipa kodi na wapiga kura wa nchi hii ili hali wao wakienda kutibiwa nje ya nchi hata malaria tu; wakati umefika wa kuchukua hatua. Nawaunga mkono madaktari klatika hili.

View attachment 57746
Wakati unawaunga mkono hao Madaktari zingatia na hiyo picha hapo juu yeye mmoja anafanyiwa hivyo hao waliowengi wanakufa tu
Je huyo mmoja ni muhimu kushinda hao wengi?

Think twice.....
 
Back
Top Bottom