Pupa ya kutaka kushika madaraka, itaiangusha CHADEMA tena

I knew it .... huna data za kusapoti maelezo yako na yet unataka watu wakuchukulie serious.

Nilianza kukuona myeyushaji baada ya kuanza kujibu as if wewe ni Antari Sangari (mwandishi wa hii habari). Huwezi kutoa credit mwanzoni mwa thread na ukaanza kuchukua credit kati kati ya thread unless unataka kusema kuwa wewe ni Antari Sangari (which of course you are not).
Have you ever heard of something called "Editor in Chief"...? Kama unajua maana yake/responsibilities zake, then utajua ni kwanini na defend hii article kwa nguvu zote, ingawa mwandishi wake ni Antar Sangali.
 
No, umasikini wa watanzania unachangiwa na watanzania wenyewe kuwa wavivu. Nani anakuzuia kujiajiri mwenyewe kama unashindwa kupata ajira serikalini ama kwenye private sector. Watanzania wanachokijua ni kukaa vijiweni na kupiga porojo siku nzima wakitegemea kuwa serikali itawafanyia kila kitu. Hizo zama za zamani zimepitwa na wakati. There ain't no such thing as a free lunch hapa duniani. Na kuhusu "jiji la Dar es Salaam kunuka kinyesi kila siku," unategemea Kikwete ndo' aje kukusafishia? C'mon! Mbona watu mnaongea pumba sana humu jukwaani. Serikali haiwezi ikawafanyia kila kitu. Wewe unachafua jiji mwenyewe, unategemea matokeo yake yawe nini? Jiji lijisafishe lenyewe????
Duh, mkuu wangu sasa umekwenda nje kabisa ya kuelewa jukumu la serikali ktk kuongoza. Na laukama ingekuwa hivyo Marekani au nchi za Ulaya wasingewalalamikia viongozi wao pindi ajira zinapopungua au kukosekana.

Leo hii Obama yuko ktk msukosuko wa kiutawala kwa sababu ya ajira hali wao wana kila kitu kinachomwezesha mtu kujiajiri mwenyewe. Nafikiri ni bora tu stick na swala lako kuliko kwenda ktk fani ambazo huzifahamu.
 
Mkuu, again, I think umekurupuka kutoa hoja bila ya kutafakari kwa kina nilichokisema hapo juu. Pole sana. Well, Obama yuko kwenye msukosuko in large part wasababu base yake (liberals) wako kinda frustrated na jinsi alivyotumia mandate yake vibaya. Yes, alifanikiwa kupitisha sheria mpya ya healthcare, lakini liberals hawakuipenda kwasababu haikuwa na vitu walivyokuwa wanavitaka (i.e. public option). Pili, Stimulus package aliyoipitisha mara tu baada ya kushika madaraka, haikuenda mbali kama ambayo liberal economists wengi walivyotarajia. Tatu, independents wengi wamemkimbia kwasababu the whole wing of democratic part wanaonekana kama wimps fulani (they don't stand in what they believe/wanacompromise mno!). Ni kweli kuwa suala la ajira liko juu (9.6%), lakini nikukumbushe kuwa Ronald Regan aliface the same thing kipindi cha utawala wake miaka ya 80 (high unemployment ya 9.5%), lakini bado alikuwa re-elected, why? Kwasababu economy ya marekani jinsi ilivyokuwa structured, kazi nyingi zinateng'enezwa na private sector, na Regan alichofanya at that time, ilikuwa nikuwashawishi wamarekani kuwa sera zake zakukata tax, zitateng'eneza mazingira mazuri kwa private sector kuzalisha kazi hivyo ku-rejuvenate economy.... And so, Obama kitu kingine kinachomfanya awe kwenye msukosuko ni blowback ya kucheza nice na republican wingnuts na kuwaachia nafasi wajenge narrative bandia kwenye mainstream media na kwenye pysches za wamarekani kuwa yeye ni socialist, sio mkristo, and stuff like that... Moreover, you can't deny the fact that, there's such pure form of racism toka kwenye segment kubwa ya electorate.
 
Mkuu, we may agree to disagree on that one... I mean seriously, do you really believe kwamba watanzania wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 43,000,000 wana give a damn kuhusu kile (wana JF wasiozidi 10,000) wanachofikiria humu jukwaani? Yeah, wewe na wasomi wachache hapa JF mnaweza kuwa mmelizika na sera za Chadema na mko very ethused na candidancy ya Dr. Slaa, lakini ukweli ni kwamba, sio watanzania wote wanoshare the same enthusiasm.
BongoTz,
Can you please substantiate your statement (with emphasis on the red font)?
 
Have you ever heard of something called "Editor in Chief"...? Kama unajua maana yake/responsibilities zake, then utajua ni kwanini na defend hii article kwa nguvu zote, ingawa mwandishi wake ni Antar Sangali.

Haya si maandishi yako BongoTz ....... tatizo hapa sio kudefend article, tatizo ni wewe kuandika as if wewe ndiye mwandishi wa hii article (and you are not).
 
Mkuu, again, I think umekurupuka kutoa hoja bila ya kutafakari kwa kina nilichokisema hapo juu. Pole sana. Well, Obama yuko kwenye msukosuko in large part wasababu base yake (liberals) wako kinda frustrated na jinsi alivyotumia mandate yake vibaya. Yes, alifanikiwa kupitisha sheria mpya ya healthcare, lakini liberals hawakuipenda kwasababu haikuwa na vitu walivyokuwa wanavitaka (i.e. public option). Pili, Stimulus package aliyoipitisha mara tu baada ya kushika madaraka, haikuenda mbali kama ambayo liberal economists wengi walivyotarajia. Tatu, independents wengi wamemkimbia kwasababu the whole wing of democratic part wanaonekana kama wimps fulani (they don't stand in what they believe/wanacompromise mno!). Ni kweli kuwa suala la ajira liko juu (9.6%), lakini nikukumbushe kuwa Ronald Regan aliface the same thing kipindi cha utawala wake miaka ya 80 (high unemployment ya 9.5%), lakini bado alikuwa re-elected, why? Kwasababu economy ya marekani jinsi ilivyokuwa structured, kazi nyingi zinateng'enezwa na private sector, na Regan alichofanya at that time, ilikuwa nikuwashawishi wamarekani kuwa sera zake zakukata tax, zitateng'eneza mazingira mazuri kwa private sector kuzalisha kazi hivyo ku-rejuvenate economy.... And so, Obama kitu kingine kinachomfanya awe kwenye msukosuko ni blowback ya kucheza nice na republican wingnuts na kuwaachia nafasi wajenge narrative bandia kwenye mainstream media na kwenye pysches za wamarekani kuwa yeye ni socialist, sio mkristo, and stuff like that... Moreover, you can't deny the fact that, there's such pure form of racism toka kwenye segment kubwa ya electorate.

Ona unavyojichanganya .. ndio tatizo la kuingilia profesheni za watu wengine.
 
Ebu acha vuvuzela zenu hivi mapinduzi au serikali za kijeshi uanza na matawi? Hizi ni habari au mawazo ya watu mfu!!! Nyoooooo.
 
Mkuu, again, I think umekurupuka kutoa hoja bila ya kutafakari kwa kina nilichokisema hapo juu. Pole sana. Well, Obama yuko kwenye msukosuko in large part wasababu base yake (liberals) wako kinda frustrated na jinsi alivyotumia mandate yake vibaya. Yes, alifanikiwa kupitisha sheria mpya ya healthcare, lakini liberals hawakuipenda kwasababu haikuwa na vitu walivyokuwa wanavitaka (i.e. public option). Pili, Stimulus package aliyoipitisha mara tu baada ya kushika madaraka, haikuenda mbali kama ambayo liberal economists wengi walivyotarajia. Tatu, independents wengi wamemkimbia kwasababu the whole wing of democratic part wanaonekana kama wimps fulani (they don't stand in what they believe/wanacompromise mno!). Ni kweli kuwa suala la ajira liko juu (9.6%), lakini nikukumbushe kuwa Ronald Regan aliface the same thing kipindi cha utawala wake miaka ya 80 (high unemployment ya 9.5%), lakini bado alikuwa re-elected, why? Kwasababu economy ya marekani jinsi ilivyokuwa structured, kazi nyingi zinateng'enezwa na private sector, na Regan alichofanya at that time, ilikuwa nikuwashawishi wamarekani kuwa sera zake zakukata tax, zitateng'eneza mazingira mazuri kwa private sector kuzalisha kazi hivyo ku-rejuvenate economy.... And so, Obama kitu kingine kinachomfanya awe kwenye msukosuko ni blowback ya kucheza nice na republican wingnuts na kuwaachia nafasi wajenge narrative bandia kwenye mainstream media na kwenye pysches za wamarekani kuwa yeye ni socialist, sio mkristo, and stuff like that... Moreover, you can't deny the fact that, there's such pure form of racism toka kwenye segment kubwa ya electorate.
Mkuu wangu maelezo marefu wakati hujui kinachowasibu ni kujaribu kujaza debe upepo. Tunazungumzia wananchi jinsi wanavyomtazama kiongozi na serikali yake sii swala ya kisayansi au dhana.

Kwanza Healthcare utata upo kwenye gharama yake kubwa na sio sijui Liberal hawaipendi kutokana na vipengele gani..
Pili, umezungumzia stimulus ni kwa sababu haiku create ajira kama walivyotegemea kulingana na ahadi za Obama lakini ukweli ni kwamba Stimulus ilikuwa lazima kuepuka total collapse. Psipo stimulus ajira zingepotea kwa kasi ile aloiacha Bush, hivyo kidogo imeweza kuuweka uchumi ktk hatua ya kati.
Tatu, Independent hawajali kabisa Domocratic wanasimamia nini zaidi ya ahadi walizopewa wao nje ya itikadi. Ni ahadi (sera) ambazo zinakidhi mahitaji yao lakini maadam Obama na Democratic hawakuzipa kipaumbele ndio maana Independent wanampinga. Kati ya maswala mazito ni pamoja na gay rights, Immigration na kubadilisha muundo wa White house unavyofanya kazi.
Nne, Reagan aliface matatizo ya Unemployment ambayo aliyarithi kutokana na uchumi wa nchi hiyo kushuka mwaka 1980 chini ya Carter.. Na ndiyo sababu kubwa aliweza kumwangusha Carter ambaye alikuwa rais wa awamu moja kama itakavyokuwa kwa JK mwaka huu. Na sijui kama unakumbuka vizuri ktk kampeni zake Reagan aliwahi kusema kwamba:- "The government is not the solution to our problems, The government is the problem." akimaanisha utawala wa Carter ambao uchumi ulikuwa ukishuka ghafla.. Pengine nisema tu kwamba kushuka kwa Uchumi wowote ule kunaathiri Ajira, inflation na kadhalika haya ndio matunda ya uchumi mbaya.

Kwa hiyo, siku zote tunasema utavuna ulichopanda. Kama mbinu za kiuchumi zikiwa mbaya matokeo yake unapoteza ajira kwa viwanda na mashirka kufungwa na ndivyo unavyopoteza ajira. Kutokana na urithi ule wa depression ya Carter, wananchi waliona bora Reagan kuliko kubakia na Carter kama ilivyotokea kwa Obama ambaye watu walishamchoka Bush na Republican ktk downfall ya uchumi..

Reagan alichaguliwa tena kwa sababu nyingi sana, kwanza Mandale was a weak candidate, yaani hanunuliki na pili kama unakumbuka Reagan aliendelea kusema kwamba amerithi uchumi mbaya toka kwa Carter hivyo aliomba muda zaidi ili sera zake zifanye kazi. Aliweza kuwashawishi wananchi wakafanya subira na kweli alikuja fanya maajabu kushusha hadi 5.5 au point 7..(a record).

Na Obama huyu anaweza kupata kipindi kingine cha kuongoza ikiwa wananchi wataelewa alichopanda kwani at the end of the road wananchi wanataka kuona ajira kwani ndio matunda ya Utawala bora kwa wananchi. Lakini usinambie ati Ajira inawalazimu wananchi kujishughulisha na chochote pasipo kuwepo mfumo bora unaowawezesha wananchi ku posper.. Aim kubwa ya mbinu za kukuza uchumi ni kupata matunda bora zaidi ambayo Ajira ni mojawapo na maadam JK ameshindwa kuja na mbinu ambayo italeta matunda hayo kutokana na uchovu wa mikakati yake ya kiuchumi ndio maana tunasema hatuwezi vuna ajira.
 
CHADEMA chama ambacho kwa bahati mbaya sana kimebahatika kukubalika kikanda na kuungwa mkono na kundi la kabila la Kichaga, bado hakijajipanga na kuonekana wazi kama "a real Political Party" ili kuivuta na kuishawishi hadhira kubwa inayoishi vijijini na mijini kwamba wao ndio wanaostahili kuiongoza Tanzania na sio CCM.

Mkuu ni Aidha Hauko Nchini kwa Muda Mrefu au unazungumzia Siasa za mwaka 92
 
Mkuu, mimi sina chuki binafsi. I'm just stating the obvious, that's all.

Kapimwe ..... una kasoro kwenye ubongo wako. The obvious my foot! You wouldn't recognise the "obvious" even if it hit you with a one metre pole. Sick dog!!
 
Kwanza Healthcare utata upo kwenye gharama yake kubwa na sio sijui Liberal hawaipendi kutokana na vipengele gani..
Mkuu, kama hujui jambo, uliza usaidiwe lol. Utata wa Healthcare haupo kwenye gharama.In fact, polls nyingi zinaonyesha kuwa wananchi wengi wanadai kuwa healthcare reform haikuenda mbali vyakutosha (didn't go far enough). And so please allow me to educate you on this issue kidogo: Ah, score ya CBO (Congressional Budget Office) juu ya Healthcare ilikuwa kama ifuatavyo: overall cost projection for ten years ilikuwa $940 billion (but it will reduce the deficit by $130 billion over the same period). And most of all, it will cut the deficit by $1.2 trillion over the second ten year period (pretty cool stuff, huh lol!). So ukiangalia hizo projections, utaona kuwa gharama sio kubwa sana kama ambavyo "tea party supportes" wamekufanya uamini.

Pili, umezungumzia stimulus ni kwa sababu haiku create ajira kama walivyotegemea kulingana na ahadi za Obama lakini ukweli ni kwamba Stimulus ilikuwa lazima kuepuka total collapse. Psipo stimulus ajira zingepotea kwa kasi ile aloiacha Bush, hivyo kidogo imeweza kuuweka uchumi ktk hatua ya kati.
No, don't twist my words. Nilichosema ni kwamba "Stimulus package aliyoipitisha mara tu baada ya kushika madaraka, haikuenda mbali kama ambayo liberal economists wengi walivyotarajia." In other words, stimulus haikuwa big and bold enough to inspire confidence. And nobody amesema kwamba stimulus haikusaidia kuepusha total collapse ya financial institutions.

Tatu, Independent hawajali kabisa Domocratic wanasimamia nini zaidi ya ahadi walizopewa wao nje ya itikadi. Ni ahadi (sera) ambazo zinakidhi mahitaji yao lakini maadam Obama na Democratic hawakuzipa kipaumbele ndio maana Independent wanampinga. Kati ya maswala mazito ni pamoja na gay rights, Immigration na kubadilisha muundo wa White house unavyofanya kazi.
Mkuu, unajua kweli unachokizungumzia hapa lol!!? Geez, you never cease to disappoint me!! Ah, vitu vyote ulivyovitaji hapo juu ni core issues za liberals. Independents wanajali zaidi kuhusu economy na deficit reduction. Ndo' maana Ross Perot alilamba kura nyingi sana za Independents mwaka 1992/1993 kwasababu centerpiece ya kampeni yake ilikuwa based juu ya deficit reduction.

Nne, Reagan aliface matatizo ya Unemployment ambayo aliyarithi kutokana na uchumi wa nchi hiyo kushuka mwaka 1980 chini ya Carter.. Na ndiyo sababu kubwa aliweza kumwangusha Carter ambaye alikuwa rais wa awamu moja kama itakavyokuwa kwa JK mwaka huu. Na sijui kama unakumbuka vizuri ktk kampeni zake Reagan aliwahi kusema kwamba:- "The government is not the solution to our problems, The government is the problem." akimaanisha utawala wa Carter ambao uchumi ulikuwa ukishuka ghafla..
Yeah, hata Obama amerithi matatizo ya high unemployment toka kwa Bush. No, Reagan hakusema hayo maneno ktk kampeni zake. Maneno hayo aliyasema kwenye inaugural address yake [January 20, 1981].
 
Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete imejitahidi kupambana na ubadhirifu wa mali ya umma, kukemea rushwa na kwa bahati nzuri kesi ziko mahakamani zikiwakabili vigogo wazito. Ingawa wengi wa hao wahusika wanataachiwa huru bila kupata adhabu wanayostahii, lakini hilo pekee ni jambo linalowaongezea wananchi mapenzi na hamu ya kuendelea kuiamini CCM, nje ya hilo ukifuatilia utekekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM toka awamu ya tatu hadi ya nne, Tanzania imepiga hatua (ingawa sio kubwa sana kimaendeleo)

Serikali Hiyohiyo inawashitaki, Serikali hiyo hiyo Inasema Jamaa Wamesingiziwa! Kweli Ukipenda Chongo Huita kengeza ona sasa unavyojichanganya
 
Serikali Hiyohiyo inawashitaki, Serikali hiyo hiyo Inasema Jamaa Wamesingiziwa! Kweli Ukipenda Chongo Huita kengeza ona sasa unavyojichanganya
Ndege ya Uchumi, how old are you? I mean, kama ningekuwa Dr. Slaa, ningeikataa kura yako. Maana kama unashindwa kuelewa ninachokizungumzia kwenye hiyo paragraph (ambayo inajieleza yenyewe), then you are not fit kuwa mpiga kura.
 
Chama imara cha kisiasa ni lazima kwanza kiwe na muundo thabiti, mtandao mzuri wa kisiasa unaoanzia ngazi moja hadi nyingine pamoja na kuwa na mfumo unaosadifu wa kisera na kiitikadi na kutambulika, achilia mbali kukubaliwa na wananchi.

CHADEMA chama ambacho kwa bahati mbaya sana kimebahatika kukubalika kikanda na kuungwa mkono na kundi la kabila la Kichaga, bado hakijajipanga na kuonekana wazi kama "a real Political Party" ili kuivuta na kuishawishi hadhira kubwa inayoishi vijijini na mijini kwamba wao ndio wanaostahili kuiongoza Tanzania na sio CCM.

Mizizi na nguvu za CCM ni kubwa mno katika nchi yetu, anayepuuza ukweli huu ni mpuuzi jasiri asiyejua kupambanua baina ya mbivu na mbichi, na bila shaka hataki kwa makusudi kujua ukweli wa mambo ulivyo.

Msingi imara wa chama cha TAA ulijengwa kutokana na harakati za machifu wa Tanganyika katika dhati ya kupambana wakiwemo baadhi yao kina Mangi Meli, Kinjikitile, Mirambo, Kimweri, Mkwawa, Makunganya, Bushiri na wengine--wakati kukubalika kwa chama cha TANU ni matokeo ya nguvu na juhudi za chama cha TAA.

Kwa msingi huo kuimarika na kukubalika kwa CCM ni kutokana na kujijenga kwa vyama vya TANU/ASP ambavyo ni vyama viasisi vya siasa katika Tanganyika na Zanzibar tokea miaka ya 1954 na 1957.

CCM inatofauti sana kimtazamo na vyama kama UPC cha Uganda, MCP cha Malawi, na UNIP cha Zambia au KANU kilichokuwa kikitawala Kenya.

Vyama hivi navyo vilikataa kujikita na kuweka mizizi ili kulishika kundi la watu hasa mababa-kwabwela wanaoishi vijijini na kulazimishwa kutambua kwamba mafanikio na ujio wa uhuru wao ulitokana na vyama hivyo.

Kiuhalisia na kinadharia vyama hivyo mara baada ya uhuru vilibadilika na kuwa vyama vya kibwenyenye na kimwinyi kwa kuusahau kabisa kuutazama umma wenye nguvu za maamuzi na utafutaji wa ridhaa ya kudumu (CCM nayo ilijaribu kubadilika lakini sio kwa kasi kubwa ya kutisha kama ilivyokuwa kwa majirani zetu wa Uganda, Kenya, Malawi na Zambia. Shukrani za peee kwa hayati Kambarage Nyerere, mwasisi wa CCM).

Wanaojaribu kuitazama CCM kwa jicho rahisi wafanye pia utafiti mgumu ili kutambua matokeo kamili kabla na baada ya ujio wa vyama vingi huku wakiidurusu kwa weledi hali ya mambo na wakati ulikuwaje kwa nyakati hizo.

TANU haikupata kazi ya suluba ya kujenga matawi mapya toka mwaka 1954 kilipoanzishwa kuanzia kanda ya Mashariki, Lake zone ,Kaskazini na Kusini mwa Tanzania na hatimaye kusambaa nchi nzima, kutokana na kurithi matawi yoye toka kwa chama kikongwe cha TAA.

Kuzaliwa kwa CCM tarehe 5,2,1977 na kuenea kwake ilikuwa ni kama kuua tembo kwa bua kutokana na chama hicho kuiga tabia ya nyoka anayejibua gamba, na yeye kubaki akiwa ni nyoka yuleyule mwenye sumu kali.

TANU iliutumia vizuri mfumo wa chama kimoja na kueneza siasa zake hadi kwenye Taasisi za serikali, mashirika ya Umma, vyuo vikuu, sekondari hadi hata kwenye vikosi vya ulinzi na usalama.

Haikuwa kazi nyepesi inayoweza kuleta hasara haraka au kwa ulaini kama iliyovyazamwa na inavyoendelea kutazamwa na baadhi ya wahariri a mambo ya kisiasa.

Base ya TANU ni TAA. Base ya CCM ni TANU na ASP. CUF inatokana na vuguvugu la KAMAHURU, NCCR -Mageuzi ni mkusanyiko wa wanaharakati waliolilia mageuzi ya Kikatiba tokea miaka ya 1990. Lakini CHADEMA chimbuko lake halisi hasa ni nini na wapi? Au ndiyo ili iliyoelezwa kuwa something like "Chagga Develpement Manifesto"?

Takriban miaka 27 ilipita chini ya chama cha TANU kikiwaimbisha na kuwachezesha kwata wananchi chini ya zama ya nguvu ya chama kushika hatamu tangu pale mfumo wa vyama vingi ulipopigwa marufuku mwaka 1965; fursa na nafasi hii haikutumiwa ipasavyo huko Zambia, Uganda, Malawi na Kenya, na huu ndio ukweli wa mambo, ila anayetaka kubeza hawezi kuzuiwa.

CCM haikulala usingizi wa pono pale ulipoingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ilianzaa kujichimbia kisiasa, kuingiza wanachama wapya, kujinadi mbele ya umma na kuubeza upinzani kwa nguvu ya hoja.

Ni kweli serikali zake zimekuwa zikikabiliwa na matatizo mengi tokea awamu ya kwanza hadi hii ya sasa tuliyonayo--huku chama chenyewe kikijitutumua kwa bidii kulinda hadhi yake na kujivunia rasilimali watu.

Katika awamu ya kwanza mashirika yote ya umma yalifujwa, hakuna aliyefikishwa mahakamani, awamu ya pili walikamatwa watu wakisafirisha dhahabu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar ess Salaam, kesi ikayeyuka huku katika awamu ya nne tumeshuhudia mikataba mibovu ya madini na wizi katika akaunti ya EPA na BoT ikifanyika katika awamu ya tatu bila hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi ya waharifu/husika.

CCM mara kadhaa kimekuwa kikijikosoa na kujipanga kutokana na kupata msaada wa mtandao wake uliojengeka Tanzania nzima kwa miaka mingi.

Vyama vya Tanzania vina pupa ya kutaka kushika madaraka ya juu vianze kwanza kujijenga ndani ya halmashauri za wilaya, Bunge na Baraza la Wawakilishi huku vyenyewe vikitambua mitandao yao ili kupata ushindi ni dhaifu.

Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete imejitahidi kupambana na ubadhirifu wa mali ya umma, kukemea rushwa na kwa bahati nzuri kesi ziko mahakamani zikiwakabili vigogo wazito. Ingawa wengi wa hao wahusika wanataachiwa huru bila kupata adhabu wanayostahii, lakini hilo pekee ni jambo linalowaongezea wananchi mapenzi na hamu ya kuendelea kuiamini CCM, nje ya hilo ukifuatilia utekekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM toka awamu ya tatu hadi ya nne, Tanzania imepiga hatua (ingawa sio kubwa sana kimaendeleo).

Barabara, zahanati na huduma za maji safi zinatia moyo kinyume na miaka ile mara baada ya kupata Uhuru, vyama vya Bongo vijizatiti, viongozi wake wajitume na wasitegemee wao kuja kufaidi matunda ya nguvu zao, wafanye kama walivyofanya kina Mkwawa na Mangi Meli.

Kuimarika na kujengeka kwa CHADEMA kuna tofauti sana na kujengeka kwa CUF. Chadema mwanzo wake unatokana na safu ya waasisi wa chama hicho. Brown Ngululupwi, Edwin Mtei, Bob Makani, Costa Shinganya, na Kimesera. Hili lilikuwa ni kundi la masetla watupu na halikuwa la wanasiasa waliotambulika na kufanya kazi za kisiasa.

CUF ni chama kilichomega nguvu ya CCM Zanzibar baada ya wanachama wake vigogo wapatao saba walipofukuzwa mwaka 1988 akiwemo Seif Sharif Hamad mtu aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi wa SMZ.

Vigogo wengine ni Khatib Hassan Khatib aliyewahi kuwa mhazini wa CCM na MNEC--Hamad Rashid Mohamed ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mambo ya Ndani ya Nchi, Juma Ngwali na Masoud Omar wakiwa wakuu wa Mikoa.

Wanasiasa wengine waliopevuka kisiasa ni pamoja Musa Haji Kombo aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM, Juma Othman Juma aliyekuwa mjumbe wa NEC, Ali Haji Pandu Waziri wa Sheria katika SMZ, Soud Yusuf Mgeni Waziri wa Kilimo pamoja na Maulid Makame Abdallah aliyewahi kuwa Waziri mdogo wa Afya Zanzibar.

Kundi hili la CUF kwa kiasi kikubwa liliweza kuibana mbavu CCM kutokana na wao kuitambua misingi ya kuunda chama cha siasa na kukieneza kama taasisi.

Nieleweke wazi kwamba sikipigii chapuo chama cha CUF ila nimefanya utafiti na kuiona tofauti kubwa kati ya CCM, CHADEMA na CUF. CHADEMA wajenge kwanza mizizi na kundi lililopo sasa lisitegemee kula matunda ya juhudi hizo.

Chama cha CHADEMA na vingine katika Tanzania vinapaswa kujifunza na kupita katika barabara ya chama cha Liberal Party cha Uingereza amacho hakikuwa na papara ya kushika madaraka haraka bali kilitafuta kwanza amana na hatimaye kikaaminiwa.

CUF wanaelekea kuingia katika medani za serikali Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, hatua hiyo pekee ukiwa mtu mkweli utaweza kujua usahihi wa tathmini yangu.

Bado siamini kutokana na utafiti mdogo nilioufanya kwamba CHADEMA kimejiandaa na kimejijenga kimfumo, kisera na kimtandao kiasi kwamba kiweze kushinda katika uchaguzi wa mwaka huu na kuongoza dola.

Jambo hili kwa CHADEMA sitaki kabisa niliamini moyoni mwangu, naomba lisistawi kabisa kwenye mishipa ya fahamu zangu na kwenye ubongo wangu pia.

CHADEMA hakitashinda kutokana na kwamba bado ni kichanga, kiliwahi kusifiwa na Mwalimu Julius Nyerere kwamba kina sera zenye mwelekeo lakini kina upungufu wa wanasiasa, ni sawa tu na timu ya soka yenye nyota haba wa kuleta ushindi.

Safu ya kina Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, John Mnyika, Halima Mdee, Philemon Ndesamburo, Maulida Komu na Mabere Marando ni kundi la wasomi wa fani za kitaaluma wakikosa mtaji na ujuzi wa mizungu ya ufanyaji wa siasa.

Slaa ni mwanasiasa mahiri, mwepesi wa utambuzi wa mambo, hata kutoka kwake CCM baada ya kukatwa jina lake na kupachikwa kwa Patrick Qorro katika kura za maoni kulilalamikiwa sana na Mwalimu Julius Nyerere.

Slaa ni yeye peke yake kinara ndani ya CHADEMA akizungukwa na timu hafifu isiyo na uwezo ama ukomavu wa kisiasa wa kukiletea ushindi chama hicho. Kwa upande mwingine, CCM bado kina ngome kubwa, viongozi wengi wenye amana mbele ya umma ambao hawakuona umuhimu wa kujitoa ndani ya chama hicho kwa wingi na kujiunga na kambi ya upinzani.

Chadema, NCCR na TLP ni vyama vinavyoweza kuja kujiimarisha katika siku nyingi zijazo usoni, CUF kwa upande wa Bara nao wamo katika msafa wa vyama hivi vitatu, hawajawa na timu imara na pia Kiongozi wake Profesa Ibrahim Lipumba hajaungwa mkono na wasomi wenzake wa Chuo Kikuu cha Dare es Salaam kuonyesha kama anakubalika.

Hata yeye Lipumba anaonekana yuko peke yake. Ni sawa kabisa na kusema mchezaji nyota wa Brazil "Kaka" aamue kusajiliwa na Balimi ya Bukoba kisha timu hiyo ghafla itarajiwe kutandaza kabumbu safi uwanjani, aifungie magoli mengi timu hiyo, hata aiwezeshe ichukue ubingwa wa ligi kuu. Wa-da-nga-yi-ka wenzangu hebu tusijidanganye. Hiyo ni ndoto ya mchana. Hilo haliwezekani kwa mwaka huu na hata baada ya miaka kumi na tano ijayo, CHADEMA isitegemee kushinda kwasababu bado hakijajipanga vizuri.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!

P.S. [makala hii imeandikwa na Antar Sangali, mwandishi wa BongoTz.com]

Mpuuzi usitudanganye,Hatudanganyiki na mawazo yako mafupi.Unauhakika hatujajipanga,kwa taarifa yako tumejipanga na kama serikali itakuwa yamfano dunia nzima.Mwambieni kikwete Msimdanganye kama Kaunda alivyodanganywa mpaka dakika za mwisho ndivyo atakavyokuwa Mkwere wenu,mmeishiwa sera mpaka Mnatumia jeshi hata wewe usalama useless nasasa Umoja wa mataifa lazima uwatazame.
 
Ndege ya Uchumi, how old are you? I mean, kama ningekuwa Dr. Slaa, ningeikataa kura yako. Maana kama unashindwa kuelewa ninachokizungumzia kwenye hiyo paragraph (ambayo inajieleza yenyewe), then you are not fit kuwa mpiga kura.

Kilichotokea ni Kwamba Hata wewe huelewi nini umeandika au unamaanisha katika Paragraph hiyo, subiri nitakuelza nini unamaanisha
 
Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete imejitahidi kupambana na ubadhirifu wa mali ya umma, kukemea rushwa na kwa bahati nzuri kesi ziko mahakamani zikiwakabili vigogo wazito. Ingawa wengi wa hao wahusika wanataachiwa huru bila kupata adhabu wanayostahii, lakini hilo pekee ni jambo linalowaongezea wananchi mapenzi na hamu ya kuendelea kuiamini CCM, nje ya hilo ukifuatilia utekekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM toka awamu ya tatu hadi ya nne, Tanzania imepiga hatua (ingawa sio kubwa sana kimaendeleo)

Yaani kwa Lugha Rahis ni Kwamba, Mimi Nimeshtaki Mtu, Halafu Mimi huyo huyo kesho yake nasimama Jukwaani nikimshika Mkono yule niliyemshtaki kwamba ni Mtu safi amesingiziwa ( Sasa sijui amesingiziwa na nani) Huu si Uzuzu au wewe huoni hilo

Ameingilia Uhuru wa Mahakama Iringa ( Mwakalebela)
Rombo( Basili Mramba)
Bariadi( Chenge)

Wewe huoni hilo halafu unataka watu wakuone eti Uko makini

Jebu hoja bana acha maneno ya kashfa
 
Ingawa wengi wa hao wahusika wanataachiwa huru bila kupata adhabu wanayostahii, lakini hilo pekee ni jambo linalowaongezea wananchi mapenzi na hamu ya kuendelea kuiamini CCM,
Yaani Umewaona Watanzania ni Mazuzu kwamba Waendelee Kujenga Imani na Serikali inayowatete watuhumiwa ambayo yenyewe Serikali Imewashtaki

Waombe Radhi Watanzania
 
Back
Top Bottom