Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,834
- 18,835
Kuna chaguzi ndogo zilizofanyika katika maeneo mbalimbali nchini, na Chadema waliamua kutoshiriki, ACT wao wakafanya maamuzi yao kama chama huru cha siasa kushiriki, ACT wamelalamika na kusema kuna ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi zimefanyiwa kwenye chaguzi hizo.
Maajabu ni kuwa viongozi wa chama kingine cha upinzani, CHADEMA, akiwemo mwenyekiti wao wa kanda ya kaskazini Godbless Lema wamekuwa wakishangilia hayo madhila waliyofanyiwa ACT na dola, huku wao wakitarajia kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao katika mazingira haya haya.
Maswali yangu ni;
CHADEMA wao wamekuwa wakishiriki uchaguzi mkuu kila mwaka katika mazingira haya haya lakini ACT wao wakishiriki inawaona ni wasaliti, tawi la CCM.
CHADEMA haiamini katika uhuru wa vyama vingine vya siasa? Kwamba vyama vingine vya siasa vikifanya maamuzi kama wanavyofanya wao (kama kushiriki uchaguzi mkuu uliopita na ujao) wanakuwa ni tawi la CCM?