Pupa ya kutaka kushika madaraka, itaiangusha CHADEMA tena

Mkuu, mimi sina chuki binafsi. I'm just stating the obvious, that's all.
 
Acha ubabaishaji mkuu, yaani unadhani watanzania bado wataendelea kudanganyika na makala yako ndefu iliyojaa chuki binafsi!!!. Huo umakini wa CCM uko wapi???, hao unaowaita viongozi wazuri wa CCM ya leo ndio akina nani?
Mkuu, mimi sina chuki binafsi. I'm just stating the obvious, that's all.
 
hivi wewe mpaka utukane huoni raha? Umeishiwa hoja? Si uombe msaada wa kujengewa hoja ili ujibu challenge uliyopewa hapo juu? Ndio maana ccm wamekataa kuhudhuria midahalo wanajuwa chadema wameshikwa na ugonjwa wa kichaa cha ikulu!!!
Thanks, kadogoo.
 
"A foolish consistency is the hobgoblin of little minds""~ Ralph Waldo Emerson

8D6U4371.jpg
 
BongoTz,
Mkuu wangu nyakati hizo zimepitwa na wakati.. Sasa hivi chama ni sera zake ambazo zinakubaliwa na wananchi wake kwa wingi. Enzi za Kikomunist ati chama kimeshika hatamu zimepita, huu ni wakati Katiba inayoongoza nchi haina mwenyewe na sote tunafuata Katiba na sio chama..

Leo hii Nguvu ya chama ni ushawishi wa sera zake kuuzika kwa wananchi kama vile unapeleka mazao yako sokoni. Ondoa kabisa yale mawazo ya wakati wa TANU ambayo watu walilazimika kuchagua TANU kwa sababu ndiye mtunzi wa katiba na mmliki wa njia kuu zote za uchumi na kila kitu..

Maadam system nzima ya kiutawala itamkubali mgombea fulani kuwa rais wao haijalishi tena nguvu ya chama kwani CCM sio Katiba ya nchi kiasi kwamba Majeshi yetu na Usalama lazima washiriki kupinga matokeo ya uchaguzi kwa sababu tu Chaderma sii imara kama CCM. Swala ni nani anayekubalika zaidi kwa wananchi kwa sera zake - Period!

Hofu kubwa ya Chadema na wananchi ni kama system (na majeshi yetu) haitamkubali Dr.Slaa baada ya ushindi lakini kama wao watampokea yeyote aloshinda basi CCM na JK hawana nguvu ya kufanya lolote dhidi ya vyombo hivi. Hofu yangu kubwa ipo hapo na sio CCM wala mtu mmoja kwani hata JK analindwa na katiba.
Mkandara, with all due respect, I think umekurupuka kujibu hoja hii bila ya kusoma makala nzima na kuelewa point niliyokuwa najaribu ku-make kuhusu TANU and stuff. I suggest that you go back and read the entire article again, then tutaendelea na mjadala huu...
 
Ishi kwa Historia, na kujiamini kwamba kwa sababu CCM ina matawi hadi kwenye vitongoji, then ndiyo chama pekee kinachoweza kuongoza dola sasa suburi ushangae hii ni 2010. Hayo matawi ndiyo yatapiga kura this time. Watanzania si wale wa miaka ya 70 hadi 90. Sasa hivi kuna mabadiliko makubwa sana ndani ya miaka 5 tu hii iliyopita. Tatizo CCM hamsomi alama za nyakati.
Well, kando na wananchi wa jimbo la Tarime na Karatu ambao kwa ujasiri wao wamezikataa sera mbovu za CCM, wananchi wengine wote wa Tanzania ni wale wale wa miaka ya 70 hadi 90.
 
Unakitega uchumi chochote? au una biashara usio ilipia kodi? nadhani chiligati ndugu yako manake akili zenu moja......
 
'Msingi imara wa chama cha TAA ulijengwa kutokana na harakati za machifu wa Tanganyika katika dhati ya kupambana wakiwemo baadhi yao kina Mangi Meli, Kinjikitile, Mirambo, Kimweri, Mkwawa, Makunganya, Bushiri na wengine--wakati kukubalika kwa chama cha TANU ni matokeo ya nguvu na juhudi za chama cha TAA.'

Unataka kutufanya kama hatufahamu historia? T.A.A. (Tanganyika African Association) kilikuwa ni jumuia ya kujadili mambo mbali mbali ya kijamii mjini Dar es salaam. Wanachama wake wa awali walikuwa wakazi wa Dar ambao chama hicho kilikuwa ni kama club. Katika kufanya hivyo, wakajikuta wakielekea kwenye kuongea zaidi kutaka ukombozi wa mwafrika zama zile. Baadae ndipo kikabadilishwa na kuwa TANU. Si lazima chama cha siasa kianza rasmi kwa wadhifa huo, kuna mifano mingi tu, kwa mfano vyama vya wafanyakazi.

Hivyo basi, Chadema, au shirikisho la watu wengine wale, wakiungana na wakiwa na malengo yanayofanana wanaweza kuwa na chama chao cha siasa. Hakuna chama kilichoundwa kikiwa tayari kinajua nyanja zote za kiuendeshaji kwa vile muundo wa chama na matokeo yake hutegemea vigezo vingi. Kusema kuwa ccm ndio chama tu kinachoweza kuongoza, huko ni kugandwa kwa wakati kwani ccm kimejiharibu chenyewe (self destruct) kutokana na kutoangalia na kufuata misingi ya kuanzishwa kwake. Itokeapo katika jamii ya kisiasa kuwa chama kinajiharibu chenyewe, matokeo halisi (logical conclusion) yake ni kutokea kwa vyama vingine ambavyo vitatekeleza matakwa ya watu wake.
Mkuu, elewa kwanza kinachozungumziwa kwenye paragraph kabla ya kukurupuka kutoa hoja: "Misingi imara ya chama cha TAA ilijengwa kutokana na harakati za machifu wa Tanganyika katika dhati ya kupambana..." Hakuna sehemu katika hiyo paragraph inayo-suggest kwamba hao machifu ndio waanzilishi wa chama cha TAA. Namna gani mkuu..!? Unaniangusha...lol
 
CCM original wenyewe wamechoka,wamekaa kimya maana wanajua chama chao kimevamiwa na mafisadi.Ili kuonesha uzalendo wanapigia kura upinzani.Wewe mganga njaa ndo bado unapiga kelele.
FYI-- I'm simply an independent observer. I've no affiliation with any political party in Tanzania. Kama ulishawahi kusoma makala zangu siku za nyuma, I am equally critical to CCM as I am with CHADEMA, CUF, NCCR and TLP.
 
Well, kando na wananchi wa jimbo la Tarime na Karatu ambao kwa ujasiri wao wamezikataa sera mbovu za CCM, wananchi wengine wote wa Tanzania ni wale wale wa miaka ya 70 hadi 90.

Hao Watanzania unaowaongelea kuwa bado ni wale wale wa miaka ya 70 hadi 90 ni nani hao. BongoTz, naomba nikuulize maswali mawili matatu, kulingana na tathmini yako tarehe 31 Octoba, Chadema ikishinda una maana wasipewe nchi ? Na kama unaamini kwa dhati kuwa hawawezi kushinda hizi nguvu zote, fulana zote, kofia zote, kanga zote, mabango yote na sasa vitisho vyote hadi vya jeshi vya nini ? Kulingana na tathmini zetu wengine hatuoni na hatuipi CCM nafasi yoyote ya kushinda uchaguzi wa nchi hii labda kwa kuchakachua, je ni hilo unalojaribu kutueleza ? Hebu soma na makala hii kutoka Habari Leo;

Chadema malalamiko yanawamalizia muda
na Steven Peter
WAKATI tukiwa tumebakiza wiki chache kupiga kura, tathmini inaonesha kuwa joto la uchaguzi linazidi kupanda. Hofu, shaka na wasiwasi vimeanza kutanda miongoni mwa vyama na wagombea wao. Bila shaka hofu hiyo ni ya kuogopa kushindwa. Kati ya vyama vilivyosimamisha wagombea ambavyo ni CCM, CUF, TLP, APPT-Maendeleo, NCCR-Mageuzi na Chadema; kwa maoni yangu Chadema ndicho kinachoonekana kushikwa na hofu na presha zaidi ya uchaguzi huo kuliko vyama vingine! Kwa nini?

Kwa sababu ndicho chama pekee hadi sasa kinachoongoza kwa kulalamika, kunung'unika na hata wakati mwingine kutoa vitisho dhidi ya vyama vingine, hususan CCM. Kadri siku za uchaguzi zinavyosogea, ndivyo viongozi na wagombea wa chama hiki wanavyozidisha lundo la malalamiko.

Mara watalalamikia hiki, mara watalalamikia kile! Ili mradi wao kutwa kiguu na njia kwenye vyombo vya habari kuzungumzia tuhuma na malalamiko yasiyo na kichwa wala miguu. Kimsingi, tabia hii ya Chadema ya kulalamika inatoa ishara mbaya kwa wapiga kura wao; ishara ya kushindwa na anguko baya. Kuna dhana maarufu tunayoiamini Waafrika wengi, kwamba mwanaume mwenye nguvu na anayejiamini, anapokuwa kwenye mapambano, hatakiwi kulalamikalalamika.

Anatakiwa asimame imara na kupambana hadi tone la mwisho la damu yake. Waafrika tunaamini kuwa ukiona mwanamume aliye katika mapambano, anaanza kulalamika, ni dalili ya woga, hofu, mashaka na kutojiamini. Matokeo yake ni kushindwa mapambano. Uchaguzi ni kama vita ya kusaka ushindi wa kuongoza Dola. Kila chama kilichoamua kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho kinatambua ukweli huu. Hakika, uchaguzi si lelemama.

Ni mapambano yanayohitaji kukaza buti ili kupata ushindi. Lakini ushindi huo hauwezi kupatikana kwa kuitisha mikutano ya waandishi wa habari na kuanza kulalamika, bali ushindi utapatikana kwenye "uwanja wa mapambano" yaani kwenye majukwaa ya kampeni ya kuwatangazia wananchi sera nzuri za chama chako, ili wakuchague. Nawashauri Chadema waache sasa lawama na malalamiko, kwani hayatawasaidia, wajikite zaidi kunadi sera kwa wananchi badala ya kupoteza muda mwingi kuorodhesha malalamiko.

Tangu kampeni zimeanza ni wao pekee wanaoongoza kwa kuorodhesha malalamiko. Walianza malalamiko yao kwenye mabango ya kampeni za CCM, kabla malalamiko hayo hayajatulia wakaibuka tena na malalamiko mengine kuhusu ahadi za mgombea urais wa CCM, eti hapaswi kuahidi kuhusu mishahara ya wafanyakazi na pia hapaswi kutoa ahadi ya kununua vivuko kwa wananchi. Hivi itawezekanaje mwanasiasa anayegombea, asitoe ahadi kwa wapiga kura?!

Kabla nayo hayajapoa vizuri, Chadema wakamrukia Mama Salma Kikwete, eti kwa nini anampigia kampeni mumewe. Ebo, kama asipompigia kampeni mumewe, walitaka ampigie nani? Isitoshe Mama Salma mbali ya kuwa na haki zote za kumuunga mkono mumewe na kumpigia kampeni, lakini pia anafanya hivyo kwa kutumia kofia yake ya uanachama halali wa CCM.

Ana haki ya kufanya hivyo kama ilivyo kwa mwanachama mwingine. Kama vile orodha ya malalamiko hayo haitoshi, wakaibuka tena na malalamiko mengine eti kashfa ya kupora mke wa mtu inayomwandama mgombea wao wa urais, Willibrod Slaa, ni mipango iliyosukwa na CCM! Haiingii akilini hata kidogo ni vipi CCM imzushie Slaa kashfa hiyo, wakati mtu aliyedai kuporwa mke yupo na alijitokeza hadharani akionesha vielelezo na ushahidi. Haieleweki CCM inahusika vipi na suala hilo!

Juzi tena wakaibuka na malalamiko mapya dhidi ya wahariri wa baadhi ya magazeti eti hayamwandiki vizuri mgombea huyo wa urais! Ilimradi orodha ya malalamiko ya chama hiki kwa wapinzani wao ni mengi.

Lipo pia hili la kulalamikia muda wa kumalizika kwa mikutano ya kampeni. Wakidai kuwa mgombea wa CCM, Rais Kikwete anapitisha muda wa kumaliza mikutano yake ya kampeni. Hata kama malalamiko hayo yana ukweli, lakini ni chama gani chenye jeuri ya kuthubutu kueleza hadharani kwamba tangu mikutano ya kampeni ilipoanza Agosti 21, hakikuwahi kupitisha muda wa kumaliza kampeni, saa 12 jioni, kutokana na jiografia ngumu na miundombinu mikoani? Ipo mifano kadhaa inayoonesha kuwa vyama vyote, ikiwamo Chadema yenyewe, vimepitisha mara kadhaa muda huo wa kumaliza mikutano ya kampeni, saa 12 jioni.

Vyovyote itakavyokuwa, hoja ya msingi ninayojaribu kuitoa hapa ni kuihadharisha Chadema iache kulalamika ovyo kwani inawapunguzia hadhi ya kuwa chama makini. Kinaweza kutafsiriwa kuwa ni chama kinachoonesha woga wa kushindwa hata kabla matokeo rasmi ya uchaguzi hayajatangazwa! Hakuna sababu ya kila siku kuwachosha wafuasi wao kulalamikalalamika.

Kitendo hicho, si tu kinachosha wafuasi hao, bali pia kinawakatisha tamaa, kinawapa hofu na mashaka ya kushindwa uchaguzi. Kwa lundo hili la malalamiko, ni kama vile chama hicho kinajichukulia anguko au pengine ni maandalizi ya kuwataka wafuasi wao wasiwe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi pindi watakaposhindwa.

Narudia tena, uchaguzi ni 'mapambano', Chadema wajiamini na wakaze buti. Waache kulalamika. Kama vile wanavyopambana CCM, CUF na vyama vingine. Malalamiko mengi ni dalili ya kukosa ushujaa. Kukosa kujiamini. Kila la kheri.

*Mwandishi wa Wazo hili anapatikana kwa simu: 0715199873
BongoTZ umeingia katika kundi hili la watathmini uchwara ambao sasa wamevamia JF kama Maggid Mjengwa na kuanza kumwaga upupu wao na kuyaita ya uchambuzi. Ukweli ulio wazi ni kuwa Watanzania wa leo wameamua kutodanganyika tena, sijui Chadema ikikamata dola tarehe 31 October mtaihama nchi. Lakini nakuhakikishia kuwa Raia mwema na safi hana sababu ya kumhofia Dr. Slaa ila wezi, mafisadi na wahujumu uchumi ambao hatakuwa na ubia nao madarakani kama huyu msanii wa sasa, kalagabaho !
 
hivi wewe mpaka utukane huoni raha? Umeishiwa hoja? ]


Yaani hata wale members wa miaka nenda rudi wa hapa ambao nilikuwa nawaheshimu kwa hoja, wameacha kutoa hoja na kutukana yanguoni. Inasikitisha kuona "wana-mageuzi" wa JF wana resort kwenye matusi. Inatia huruma. Wenyewe wanajiita great thinkers . Mtu na heshima yake anashindwa kuheshimu uhuru wa maoni na badala yake anakesha kutukana watu wanaopinga urais wa Dr Slaa....huyo ndio GREAT THINKER.
 
Yaani hata wale members wa miaka nenda rudi wa hapa ambao nilikuwa nawaheshimu kwa hoja, wameacha kutoa hoja na kutukana yanguoni. Inasikitisha kuona "wana-mageuzi" wa JF wana resort kwenye matusi. Inatia huruma. Wenyewe wanajiita great thinkers . Mtu na heshima yake anashindwa kuheshimu uhuru wa maoni na badala yake anakesha kutukana watu wanaopinga urais wa Dr Slaa....huyo ndio GREAT THINKER.
Nyie memba wa siku nyingi pia mnaofufuka wakati wa chaguzi mnastahili kupewa majibu haya maana mnaleta upupu wa 2005 wakati sasa ni 2010 mnategemea majibu yapi? Mara nyingine mnastahili hayo majibu.
 
Chama imara cha kisiasa ni lazima kwanza kiwe na muundo thabiti, mtandao mzuri wa kisiasa unaoanzia ngazi moja hadi nyingine pamoja na kuwa na mfumo unaosadifu wa kisera na kiitikadi na kutambulika, achilia mbali kukubaliwa na wananchi.

CHADEMA chama ambacho kwa bahati mbaya sana kimebahatika kukubalika kikanda na kuungwa mkono na kundi la kabila la Kichaga, bado hakijajipanga na kuonekana wazi kama "a real Political Party" ili kuivuta na kuishawishi hadhira kubwa inayoishi vijijini na mijini kwamba wao ndio wanaostahili kuiongoza Tanzania na sio CCM.


Mizizi na nguvu za CCM ni kubwa mno katika nchi yetu, anayepuuza ukweli huu ni mpuuzi jasiri asiyejua kupambanua baina ya mbivu na mbichi, na bila shaka hataki kwa makusudi kujua ukweli wa mambo ulivyo.


Msingi imara wa chama cha TAA ulijengwa kutokana na harakati za machifu wa Tanganyika katika dhati ya kupambana wakiwemo baadhi yao kina Mangi Meli, Kinjikitile, Mirambo, Kimweri, Mkwawa, Makunganya, Bushiri na wengine--wakati kukubalika kwa chama cha TANU ni matokeo ya nguvu na juhudi za chama cha TAA.


Kwa msingi huo kuimarika na kukubalika kwa CCM ni kutokana na kujijenga kwa vyama vya TANU/ASP ambavyo ni vyama viasisi vya siasa katika Tanganyika na Zanzibar tokea miaka ya 1954 na 1957.


CCM inatofauti sana kimtazamo na vyama kama UPC cha Uganda, MCP cha Malawi, na UNIP cha Zambia au KANU kilichokuwa kikitawala Kenya.


Vyama hivi navyo vilikataa kujikita na kuweka mizizi ili kulishika kundi la watu hasa mababa-kwabwela wanaoishi vijijini na kulazimishwa kutambua kwamba mafanikio na ujio wa uhuru wao ulitokana na vyama hivyo.


Kiuhalisia na kinadharia vyama hivyo mara baada ya uhuru vilibadilika na kuwa vyama vya kibwenyenye na kimwinyi kwa kuusahau kabisa kuutazama umma wenye nguvu za maamuzi na utafutaji wa ridhaa ya kudumu (CCM nayo ilijaribu kubadilika lakini sio kwa kasi kubwa ya kutisha kama ilivyokuwa kwa majirani zetu wa Uganda, Kenya, Malawi na Zambia. Shukrani za peee kwa hayati Kambarage Nyerere, mwasisi wa CCM).


Wanaojaribu kuitazama CCM kwa jicho rahisi wafanye pia utafiti mgumu ili kutambua matokeo kamili kabla na baada ya ujio wa vyama vingi huku wakiidurusu kwa weledi hali ya mambo na wakati ulikuwaje kwa nyakati hizo.


TANU haikupata kazi ya suluba ya kujenga matawi mapya toka mwaka 1954 kilipoanzishwa kuanzia kanda ya Mashariki, Lake zone ,Kaskazini na Kusini mwa Tanzania na hatimaye kusambaa nchi nzima, kutokana na kurithi matawi yoye toka kwa chama kikongwe cha TAA.


Kuzaliwa kwa CCM tarehe 5,2,1977 na kuenea kwake ilikuwa ni kama kuua tembo kwa bua kutokana na chama hicho kuiga tabia ya nyoka anayejibua gamba, na yeye kubaki akiwa ni nyoka yuleyule mwenye sumu kali.


TANU iliutumia vizuri mfumo wa chama kimoja na kueneza siasa zake hadi kwenye Taasisi za serikali, mashirika ya Umma, vyuo vikuu, sekondari hadi hata kwenye vikosi vya ulinzi na usalama.


Haikuwa kazi nyepesi inayoweza kuleta hasara haraka au kwa ulaini kama iliyovyazamwa na inavyoendelea kutazamwa na baadhi ya wahariri a mambo ya kisiasa.


Base ya TANU ni TAA. Base ya CCM ni TANU na ASP. CUF inatokana na vuguvugu la KAMAHURU, NCCR -Mageuzi ni mkusanyiko wa wanaharakati waliolilia mageuzi ya Kikatiba tokea miaka ya 1990. Lakini CHADEMA chimbuko lake halisi hasa ni nini na wapi? Au ndiyo ili iliyoelezwa kuwa something like "Chagga Develpement Manifesto"?


Takriban miaka 27 ilipita chini ya chama cha TANU kikiwaimbisha na kuwachezesha kwata wananchi chini ya zama ya nguvu ya chama kushika hatamu tangu pale mfumo wa vyama vingi ulipopigwa marufuku mwaka 1965; fursa na nafasi hii haikutumiwa ipasavyo huko Zambia, Uganda, Malawi na Kenya, na huu ndio ukweli wa mambo, ila anayetaka kubeza hawezi kuzuiwa.


CCM haikulala usingizi wa pono pale ulipoingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ilianzaa kujichimbia kisiasa, kuingiza wanachama wapya, kujinadi mbele ya umma na kuubeza upinzani kwa nguvu ya hoja.


Ni kweli serikali zake zimekuwa zikikabiliwa na matatizo mengi tokea awamu ya kwanza hadi hii ya sasa tuliyonayo--huku chama chenyewe kikijitutumua kwa bidii kulinda hadhi yake na kujivunia rasilimali watu.


Katika awamu ya kwanza mashirika yote ya umma yalifujwa, hakuna aliyefikishwa mahakamani, awamu ya pili walikamatwa watu wakisafirisha dhahabu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar ess Salaam, kesi ikayeyuka huku katika awamu ya nne tumeshuhudia mikataba mibovu ya madini na wizi katika akaunti ya EPA na BoT ikifanyika katika awamu ya tatu bila hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi ya waharifu/husika.


CCM mara kadhaa kimekuwa kikijikosoa na kujipanga kutokana na kupata msaada wa mtandao wake uliojengeka Tanzania nzima kwa miaka mingi.


Vyama vya Tanzania vina pupa ya kutaka kushika madaraka ya juu vianze kwanza kujijenga ndani ya halmashauri za wilaya, Bunge na Baraza la Wawakilishi huku vyenyewe vikitambua mitandao yao ili kupata ushindi ni dhaifu.


Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete imejitahidi kupambana na ubadhirifu wa mali ya umma, kukemea rushwa na kwa bahati nzuri kesi ziko mahakamani zikiwakabili vigogo wazito. Ingawa wengi wa hao wahusika wanataachiwa huru bila kupata adhabu wanayostahii, lakini hilo pekee ni jambo linalowaongezea wananchi mapenzi na hamu ya kuendelea kuiamini CCM, nje ya hilo ukifuatilia utekekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM toka awamu ya tatu hadi ya nne, Tanzania imepiga hatua (ingawa sio kubwa sana kimaendeleo).


Barabara, zahanati na huduma za maji safi zinatia moyo kinyume na miaka ile mara baada ya kupata Uhuru, vyama vya Bongo vijizatiti, viongozi wake wajitume na wasitegemee wao kuja kufaidi matunda ya nguvu zao, wafanye kama walivyofanya kina Mkwawa na Mangi Meli.


Kuimarika na kujengeka kwa CHADEMA kuna tofauti sana na kujengeka kwa CUF. Chadema mwanzo wake unatokana na safu ya waasisi wa chama hicho. Brown Ngululupwi, Edwin Mtei, Bob Makani, Costa Shinganya, na Kimesera. Hili lilikuwa ni kundi la masetla watupu na halikuwa la wanasiasa waliotambulika na kufanya kazi za kisiasa.


CUF ni chama kilichomega nguvu ya CCM Zanzibar baada ya wanachama wake vigogo wapatao saba walipofukuzwa mwaka 1988 akiwemo Seif Sharif Hamad mtu aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi wa SMZ.


Vigogo wengine ni Khatib Hassan Khatib aliyewahi kuwa mhazini wa CCM na MNEC--Hamad Rashid Mohamed ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mambo ya Ndani ya Nchi, Juma Ngwali na Masoud Omar wakiwa wakuu wa Mikoa.


Wanasiasa wengine waliopevuka kisiasa ni pamoja Musa Haji Kombo aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM, Juma Othman Juma aliyekuwa mjumbe wa NEC, Ali Haji Pandu Waziri wa Sheria katika SMZ, Soud Yusuf Mgeni Waziri wa Kilimo pamoja na Maulid Makame Abdallah aliyewahi kuwa Waziri mdogo wa Afya Zanzibar.


Kundi hili la CUF kwa kiasi kikubwa liliweza kuibana mbavu CCM kutokana na wao kuitambua misingi ya kuunda chama cha siasa na kukieneza kama taasisi.


Nieleweke wazi kwamba sikipigii chapuo chama cha CUF ila nimefanya utafiti na kuiona tofauti kubwa kati ya CCM, CHADEMA na CUF. CHADEMA wajenge kwanza mizizi na kundi lililopo sasa lisitegemee kula matunda ya juhudi hizo.


Chama cha CHADEMA na vingine katika Tanzania vinapaswa kujifunza na kupita katika barabara ya chama cha Liberal Party cha Uingereza amacho hakikuwa na papara ya kushika madaraka haraka bali kilitafuta kwanza amana na hatimaye kikaaminiwa.


CUF wanaelekea kuingia katika medani za serikali Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, hatua hiyo pekee ukiwa mtu mkweli utaweza kujua usahihi wa tathmini yangu.


Bado siamini kutokana na utafiti mdogo nilioufanya kwamba CHADEMA kimejiandaa na kimejijenga kimfumo, kisera na kimtandao kiasi kwamba kiweze kushinda katika uchaguzi wa mwaka huu na kuongoza dola.


Jambo hili kwa CHADEMA sitaki kabisa niliamini moyoni mwangu, naomba lisistawi kabisa kwenye mishipa ya fahamu zangu na kwenye ubongo wangu pia.


CHADEMA hakitashinda kutokana na kwamba bado ni kichanga, kiliwahi kusifiwa na Mwalimu Julius Nyerere kwamba kina sera zenye mwelekeo lakini kina upungufu wa wanasiasa, ni sawa tu na timu ya soka yenye nyota haba wa kuleta ushindi.


Safu ya kina Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, John Mnyika, Halima Mdee, Philemon Ndesamburo, Maulida Komu na Mabere Marando ni kundi la wasomi wa fani za kitaaluma wakikosa mtaji na ujuzi wa mizungu ya ufanyaji wa siasa.


Slaa ni mwanasiasa mahiri, mwepesi wa utambuzi wa mambo, hata kutoka kwake CCM baada ya kukatwa jina lake na kupachikwa kwa Patrick Qorro katika kura za maoni kulilalamikiwa sana na Mwalimu Julius Nyerere.


Slaa ni yeye peke yake kinara ndani ya CHADEMA akizungukwa na timu hafifu isiyo na uwezo ama ukomavu wa kisiasa wa kukiletea ushindi chama hicho. Kwa upande mwingine, CCM bado kina ngome kubwa, viongozi wengi wenye amana mbele ya umma ambao hawakuona umuhimu wa kujitoa ndani ya chama hicho kwa wingi na kujiunga na kambi ya upinzani.


Chadema, NCCR na TLP ni vyama vinavyoweza kuja kujiimarisha katika siku nyingi zijazo usoni, CUF kwa upande wa Bara nao wamo katika msafa wa vyama hivi vitatu, hawajawa na timu imara na pia Kiongozi wake Profesa Ibrahim Lipumba hajaungwa mkono na wasomi wenzake wa Chuo Kikuu cha Dare es Salaam kuonyesha kama anakubalika.


Hata yeye Lipumba anaonekana yuko peke yake. Ni sawa kabisa na kusema mchezaji nyota wa Brazil "Kaka" aamue kusajiliwa na Balimi ya Bukoba kisha timu hiyo ghafla itarajiwe kutandaza kabumbu safi uwanjani, aifungie magoli mengi timu hiyo, hata aiwezeshe ichukue ubingwa wa ligi kuu. Wa-da-nga-yi-ka wenzangu hebu tusijidanganye. Hiyo ni ndoto ya mchana. Hilo haliwezekani kwa mwaka huu na hata baada ya miaka kumi na tano ijayo, CHADEMA isitegemee kushinda kwasababu bado hakijajipanga vizuri.


Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!


P.S. [makala hii imeandikwa na Antar Sangali, mwandishi wa BongoTz.com]

Huyu throwback mwenye jina la ajabu ajabu TAA na ASP akahubirie makaburini labda wafu watamwelewa na siyo kizazi cha sasa.
 
Mkandara, with all due respect, I think umekurupuka kujibu hoja hii bila ya kusoma makala nzima na kuelewa point niliyokuwa najaribu ku-make kuhusu TANU and stuff. I suggest that you go back and read the entire article again, then tutaendelea na mjadala huu...
Mkuu wangu sikukurupuka hata kidogo isipokuwa nimeweza kueleza nguvu ya CCM kwa kifupi zaidi ktk karne hii na jinsi gani nguvu ile inaweza kutowa sababu ya kuwepo IKULU...

Wewe ndiye ulojumuisha pupa za chama na kwenda IKULU ukitumia historia ya CCM ambayo haihusu kabisa bali leo tunamchagua mtu baina ya Wagombea kutuongoza..Chadema wanaweza kushindwa uchaguzi wa majimbo mengi lakini bado Dr.Slaa akachukua IKULU kwa sababu nguvu ipo kwa wananchi na sio tena Chama tawala.

Kwa nguvu walokuwa nayo CCM ingekuwa wakati ule sidhani kama tungekuwa na mtu kama Dr.Slaa akiwavutia watu kuliko JK na bado wananchi wakaruhusiwa kwenda ktk mikutano yake. Kweli CCM bado wanajaribu sana kutumia nguvu ya dola na pengine umaarufu wake kuzuia mikutano lakini wananchi wameanza kuelewa haki zao hivyo hawadanganyiki tena. Na kama Watamchagua Dr.Slaa kwenda Ikulu sio kwa sababu ya pupa za Chadema isipokuwa wameridhika na sera za chama tofauti na wakati ule wa Nyerere ambapo tulimpigia kura Nyerere na kusisitiza zidumu Fikra za mwalimu..

Labda nikukumbushe tu kwamba anayekwenda IKULU ni rais ambaye amechaguliwa na wananchi kwa tiketi ya chama Chadema na atalindwa na Katiba ya Taifa sio katiba ya chama CCM wala Chadema. Historia ya CCM au ukubwa wake hakuna anayejali hilo tena isipokuwa SERA na mwakilishi wa sera hizo kuwa kiongozi wetu na sii mtawala.

Kifupi kama kuna pupa basi tuseme hizo Pupa ni za Dr.Slaa, na hao Chadema wanakwenda Bungeni kutetea sera zao kwa wawakilishi wa wananchi wote tofauti na nguvu ile ya CCM ambayo waliweza kuamua mambo yote wao pasipo upinzani toka Ikulu hadi vitongiji na wajumbe wa nyumba kumi kudumisha fikra za mwalimu. Leo hii huko vijijini tuna halmashauri na wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kuwaletea maendeleo na sio chama kimewaweka watu wake kwa niaba ya...
Huu ni wakati mwingine kabisa mkuu wangu...
 
[COLOR=red said:
Coach Parcells;1123636][/COLOR]

"Jambo hili kwa CHADEMA sitaki kabisa niliamini moyoni mwangu, naomba lisistawi kabisa kwenye mishipa ya fahamu zangu na kwenye ubongo wangu pia."

na kwenye uume wako pia.....

Umeanza makala yako kibaguzi, na ndio maana nimechukia. Niliposoma paragraph ya pili ya makala yako nikajua kuwa umetumwa au wewe ni mkabila. Chadema sio chama cha wachagga, bunge lililomaliza muda wake kulikuwa na mbunge mmoja tu wa Chadema wa kuchaguliwa kutoka Uchagani, sasa umetoa wapi hiyo bold evidence na kuitundika kwenye makala yako iliyojaa utoto kama vile hadithi anazondika mwanangu wa darasa la tatu

CCM haina misingi, unaona kuwa misingi kwa kuwa ndio chama kilikuwepo enzi na enzi. Mfumo wa vyama vingi ulianza juzi juzi tu. Kizazi kile cha chama kimoja kinafutika pole pole, kama unabisha angalia takwimu za wapiga kura wa mwaka huu, na miaka inayokuja, wengi ni waliozaliwa muda mfupi kabla ya mfumo wa vyama vingi kupiga hodi Tanzania. Hao ndio wanafanya makala yako hii kukosa hamu na ukweli, hawa ndo wapiga kura wa leo na kesho ambao hawajali kuwa CCM au lolote, hiyo mitandao ya CCM unayoisema ni ya wazee ambao wamechoka na wengine wamebaki kuongea tu hata kwenda kupiga kura hawaezi tena. So rudi darasani kachambue tena ukiwa NEUTRAL, and believe me ukifanya hivyo hii makala yako itabadilika kwa kiasi kikubwa
 
BongoTZ umeingia katika kundi hili la watathmini uchwara ambao sasa wamevamia JF kama Maggid Mjengwa na kuanza kumwaga upupu wao na kuyaita ya uchambuzi. Ukweli ulio wazi ni kuwa Watanzania wa leo wameamua kutodanganyika tena, sijui Chadema ikikamata dola tarehe 31 October mtaihama nchi. Lakini nakuhakikishia kuwa Raia mwema na safi hana sababu ya kumhofia Dr. Slaa ila wezi, mafisadi na wahujumu uchumi ambao hatakuwa na ubia nao madarakani kama huyu msanii wa sasa, kalagabaho !
Mag3, mimi simhofii Dr.Slaa. Na hakuna kitu ningependa kama kuona chama kingine chenye nguvu, mvuto, dira na sera za kueleweka kikiiongoza nchi. I'm tired of CCM, too. But let's be realistic here: 'kuongoza dola sio jambo la mchezo.' I mean, nchi haiogozwi na mtu mmoja... Plus, kama umesoma makala yote hadi mwisho, utaona jinsi makala nzima inavyo paint positive image kuhusu this Slaa guy unayemzungumzia. So unaweza ukaendelea kung'ang'ania ushabiki wako wa kitoto for the natural term of your life, but nobody is forcing you ukubaliane na tathmini ya hapo juu.
 
Back
Top Bottom