Hivi vile vyama 13 vya upinzani, vilivyoamua kuungana na CCM, kuwapinga Chadema, wanajisikiaje hivi sasa baada ya kuona maandamano hayo yamefanikiwa?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Baada ya Mwenyekiti wa Chadema kuutangazia Umma kuwa chama chake kinategemea kufanya maandamano ya amani jijini Dar tarehe 24 mwezi huu, kama kawaida viliibuka baadhi ya vyama, wakiongozwa na CCM kuyapinga maandamano hayo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti Freeman Mbowe, maandamano hayo ya amani, yalikuwa na madhumuni yafuatayo:-

1. Kuitaka serikali kuiondosha miswada 3 ya uchaguzi, ambayo hivi sasa imefikishwa bungeni, kutokana na wananchi walio wengi, kutosikikilizwa hoja zao.

2. Kuwataka serikali kuangalia gharama za maisha, zinazopanda kila kukicha, zikiwemo bei za sukari, bei ya nauli na gharama nyingine, wakati kipato cha mtanzania, kimebaki palepale.

3. Serikali hii ya CCM iweze kuondoa matumizi ya anasa katika serikali yake, wakati wananchi walio wengi, wakiishi katika maisha ya ufukara wa kutisha!

Kwanza aliibuka Mkuu wa Mkoa wa Dar, Albert Chalamila, aliyedai kuwa askari wa JWTZ zaidi ya 8,000 na askari 5,000 wa Jeshi la Polisi, siku hiyo iliyotangazwa maandano, tarehe 24, watashiriki kufanya usafi jijini Dar

Sikushangazwa na kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar kuyapinga maandamano hayo, kwa kuwa ni kawaida ya viongozi wa CCM, kutumia mbinu hiyo ya kuwatisha wananchi wake, kila pale yanapotangazwa maandamano ya amani.

Hata hivyo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1)(2) maandamano hayo ya amani yanaruhusiwa kwa mujibu wa Katiba hiyo.

Lakini kilichonishangaza zaidi, ni pale vyama 13 vinavyojiita ni vya upinzani, kujitokeza hadharani na kuyapinga maandamano hayo ya amani!

Niviulize hivyo vyama vinavyojiita ni vyama vya upinzani (wakati katika hali halisi, hivyo vyama tunapaswa kuviita ni CCM -B) je nyinyi hamuoni hoja za msingi zikizotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ya kuitaka serikali hii ya CCM, kutafakari kwa makini jinsi wanavyotutawala, kwa kuwa hivi sasa, maisha ni magumu mno kwa mwananchi wa kawaida, kutokana na kupandisha kila wakati gharama za maisha, mathalani kupanda kwa bei ya sukari na kupanda kwa nauli za mabasi na kukatika kwa umeme bila mpangilio?

Najua kuwa chama tawala kina mbinu nyingi, zikiwemo za kugawa (maokoto) kwa baadhi ya vyama vya upinzani, ili ionekane, hizo hoja zilizotolewa na Chadema, zionekane kuwa siyo za watanzania walio wengi.

Hata hivyo baada ya maandamano hayo ya amani ya Chadema, kufanikiwa sana hapo jana, vyama hivyo vinavyojiita vya upinzani, vijaandalie makaburi yao, kwa kuwa wananchi tumebaini kuwa, wao si watetezi wetu, badala yake, vimeungana na CCM, katika kuyaangamiza maisha ya umma wa watanzania wanyonge!

Mungu ibariki Tanzania
 
Baada ya Mwenyekiti wa Chadema kuutangazia Umma kuwa chama chake kinategemea kufanya maandamano ya amani jijini Dar tarehe 24 mwezi huu, kama kawaida viliibuka baadhi ya vyama, wakiongozwa na CCM kuyapinga maandamano hayo...

Chama kama ACT ambacho nacho kinataka kuaminika upande wa bara …nimeshangaaa kutosema chochote …au nao walikuwa sehemu Yao Hao 13? Bora mzee Hashim Rungwe Sipunda …Huwa Ana msimamo Yule mzee
 
Hao ni puppets wa CCM, sasa Mungu amewaonesha rangi zao ili muwatambuwe.

Aibu yao.
Wakiongozwa na "chief of oomedians" Chalamila, aliyewataka marubani wa JWTZ, waliokwenda mafunzoni kuzirusha Jet fighters, eti waje awakabidhi "hard brooms" ili walisafishe Jiji!😁
 
Baada ya Mwenyekiti wa Chadema kuutangazia Umma kuwa chama chake kinategemea kufanya maandamano ya
vinajiskia vizur sana na actually vitaungana tena katika umoja wao kumuunga mkono na kumnadi mgombea urasi wa CCM oct.2025 🐒

utajiskiaje wew na chama chako 🐒
 
Baada ya Mwenyekiti wa Chadema kuutangazia Umma kuwa chama chake kinategemea kufanya maandamano ya amani jijini Dar tarehe 24 mwezi huu, kama kawaida viliibuka baadhi ya vyama, wakiongozwa na CCM kuyapinga maandamano hayo.


Mungu ibariki Tanzania
Ni vyama vya upinzqni ndio demokrasia ndio maana ya kila chama kuwa na katiba na sera tofauti si lazima mburuzwe kwenye tenga moja!
 
Baada ya Mwenyekiti wa Chadema kuutangazia Umma kuwa chama chake kinategemea kufanya maandamano ya amani jijini Dar tarehe 24 mwezi huu, kama kawaida viliibuka baadhi ya vyama, wakiongozwa na CCM kuyapinga maandamano hayo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti Freeman Mbowe, maandamano hayo ya amani, yalikuwa na madhumuni yafuatayo:-
WAMEJIDHIHIRISHA SIO VYAMA VYA UPINZANI NI VYAMA TANZU NA CCM

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom