CHADEMA mkivuka 2025 kwa mafaniko mtakuwa katika ligi yenu, tofauti na hapo ni mwisho wenu

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Ukifuatilia Historia za vyama vikuu vya upinzani Tanzania vingi huwa vinaibuka na kupotea kama mvua za msimu, havidumu.

Vyama vikubwa vingi vya upinzani Tanzania viliundwa mwaka 1992. NCCR ilikuwa ya kwanza kuwa chama kikuu cha upinzani ikaipa tabu sana CCM katika uchaguzi wa mwaka 1995, mwaka 2000 NCCR ikaenda katika kaburi la kisiasa na haijafufuka mpaka leo.

CUF wao walikuwa na ushawashi Tanzania mwaka 2000 na 2005, baada ya hapo kikabaki kama chama cha Zanzibar zaidi. ACT nao inaonekana wanafuata mkondo huo .

CHADEMA pekee yake ndio chama cha upinzani ambacho kilianzishwa mwaka 1992 kinachoonekana kuendelea kukua na kuwa ushawashi katika siasa za Tanzania, hata baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 CHADEMA kinaonekana bado kimebakiwa na nguvu za kupambana na kurejesha heshima yake kama chama serious cha siasa cha kitaifa.

Uchaguzi wa mwaka 2025 ni mtihani mkubwa sana kwa uhai wa CHADEMA na demokrasia ya nchi hii.
 
Ukifuatilia Historia za vyama vikuu vya upinzani Tanzania vingi huwa vinaibuka na kupotea kama mvua za msimu, havidumu...

Wacha kuilinganisha CHADEMA na upuuzi wako ulioutaja.

CHADEMA ni tumaini la watanzania hivyo dua zao zipo kila siku ndiyo maana hadi leo cdm ipo
 
Kwanza nakushauri punguza njaa zako lwa kufanya kazi kwa bidding.

Pili wacha kuilinganisha CDM na upuuzi wako ulioutaja.

CDM ni tumaini la watanzania hivyo dua zao zipo kila siku ndiyo maana hadi leo cdm ipo
Hata CCM pia kuna Watanzania wanaiombea dua kila siku, labda ndio sababu bado ipo pia.
 
Back
Top Bottom