Pupa ya kutaka kushika madaraka, itaiangusha CHADEMA tena

mi naona we umechoka na maisha huna la kuwaambia wana jf,ccm ndo wanapupa ya madaraka,we hujiulizi kwanini familia nzima inapiga kampeni?
 
dokii2.jpg
Kwa hiyo? Hiyo ni CCm au CHADEMA?
 
Mkuu, mimi sina chuki binafsi. I'm just stating the obvious, that's all.
The obvious is that CCM's confidence is based on its control of the election management organs (NEC, returning officers, voting stations supervision, etc.) and the coercive forces of the state (Police, JWTZ, TISS, etc.). It has nothing to do with CCM popularity or organisation. History has nothing to do with it either. 65% of TZ population now is youth of between 15 - 45 years of age. They are not so much into historical sentiments. So if anybody is living in dreamland, it must be BongoTz and his CCM.
 
chadema wanataka madaraka hata kwa kupitia umwagaji wa damu wa wananchi!!! Nani atakubali amwage damu yake!! Viongozi wa chadema uongozi haupatikani kwa kutumia nguvu bali hoja!!!

miaka nenda miaka rudi ccm imekuwa kinara wa kumwaga damu za mamilioni ya watanzania wanyonge wanaopoteza maisha kwa kukosa huduma za afya, akina mama wanaokosa huduma za kujifungua salama, utapiamlo wa watoto, maganjwa yanyosababishwa na matumizi ya maji machafu kama vile kipindipindu, kuhara n.k, wazee kukosa matunzo, na vilema kukosa misaada ilihali nchi imejaaliwa utajiri lukuki unaofisadiwa na viongozi wa ccm kwa kushirikiana na watu kutoka nje ya nchi

ccm inahusika moja kwa moja na damu za mamilioni ya watanzania wanapoteza maisha kila mwaka katika ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva waliopata leseni za udereva bila ya kupata mafunzo na kufaulu mitihani ya udereva wa magari, pikipiki, bajaj, magari, malori na mabasi ya abiria kutokana na rushwa inayofungwa na serikali ya ccm.

ccm inahusika moja kwa moja na umwagaji wa damua za watanzania waliofukiwa katika migodi, iliyokuwa mbioni kuuzwa kwa wawekazaji uchwar.

ccm inahusika maoja kwa moja na umagaji wa damu za wakulima na wafugaji waliohusika katika mapiagano katika sehemu mbali mbali za nchi yetu kutokana na vitendo vya rushwa vya baadhi ya viongozi wake kuwamilikisha wawekezaji uchwara ardhi ya wafugaji ya loliondo, ngorongoro n.k na wafugaji kulazimika kuhamia na mifugo yao katika sehemu za wakulima.

hata hivi tunavyozungumza ccm inaendelea kumwaga damu za watanzania wanaopoteza maisha katika zahanati, vituo vya afya, hospitali n.k kwa kukosa madawa, huduma na vifaa vya utabibu ilihali ccm ikitumia bilioni 50 katika kampeni za uchaguzi ikilipia bango moja shilingi milioni tatu kwa siku n.k.
 
Nimeisoma makala yako kuhusu vyama na ni dhahiri kuwa huipendi CHADEMA. Unaiita CHADEMA kuwa "Chagga Development Manifesto" wakati unaorodhesha waanzilishi wake kuwa ni "Brown Ngululupwi, Edwin Mtei, Bob Makani, Costa Shinganya, na Kimesera". Hiyo orodha ya waanzilishi hainishawishi kukubaliana na mtazamo wako kuhusu ukabila wa CHADEMA.
 
Mag3, mimi simhofii Dr.Slaa. Na hakuna kitu ningependa kama kuona chama kingine chenye nguvu, mvuto, dira na sera za kueleweka kikiiongoza nchi. I'm tired of CCM, too. But let's be realistic here: 'kuongoza dola sio jambo la mchezo.' I mean, nchi haiogozwi na mtu mmoja... Plus, kama umesoma makala yote hadi mwisho, utaona jinsi makala nzima inavyo paint positive image kuhusu this Slaa guy unayemzungumzia. So unaweza ukaendelea kung'ang'ania ushabiki wako wa kitoto for the natural term of your life, but nobody is forcing you ukubaliane na tathmini ya hapo juu.
Mi nafikiri kama Nguvu chadema wanazo,kama mvuto wanao wakutosha tu,kama Dira inaonekana wazi na sera za kueleweka wanazo wengi wa waTZ tunapenda vitu laini bila ya jasho, wengi sasa wanawasiwasi CCM iking'oka watakula wapi? maana wamezoea Ujomba na ubabaishaji.
nilishaandika humu "CCM ikitaka kupona lazima ijifanyie mapinduzi yenyewe kwanza, wakishindwa mapinduzi yatatokea nje na hayo yatakua mabaya maana yatawamaliza kabisa".
iwe isiwe hata kama sio mwaka huu they will go down, THE THING IS DEAD MY BROTHER!
 
WASTED:llama:
natafuta uhusiano wa picha zako na thread huwa sipati jibu.. sijui ni ufinyu wa mawazo au unahitaji elimu zaidi..

Hii tabia ya kuchafuachafua suruali ni matatizo ya kubaleghe nyakati za uchaguzi! :tonguez:
 
The obvious is that CCM's confidence is based on its control of the election management organs (NEC, returning officers, voting stations supervision, etc.) and the coercive forces of the state (Police, JWTZ, TISS, etc.). It has nothing to do with CCM popularity or organisation. History has nothing to do with it either. 65% of TZ population now is youth of between 15 - 45 years of age. They are not so much into historical sentiments. So if anybody is living in dreamland, it must be BongoTz and his CCM.
"Those who cannot learn from history are doomed to repeat it." ~ George Santayana.
 
...vipi ndugu yangu ujasiri wa nyumbani Tarime uko wapi......

He he he....ujasiri wa nyumbani Tarime bado upo ndugu yangu....lol

...hivi tulikosea sana kuchagua chama tofauti na CCM eehh.............
No, hamkukosea kuchagua chama tofauti na CCM. Point ni kwamba, huwezi ukalinganisha ubunge na urais...
 
Chama imara cha kisiasa ni lazima kwanza kiwe na muundo thabiti, mtandao mzuri wa kisiasa unaoanzia ngazi moja hadi nyingine pamoja na kuwa na mfumo unaosadifu wa kisera na kiitikadi na kutambulika, achilia mbali kukubaliwa na wananchi.

CHADEMA chama ambacho kwa bahati mbaya sana kimebahatika kukubalika kikanda na kuungwa mkono na kundi la kabila la Kichaga, bado hakijajipanga na kuonekana wazi kama "a real Political Party" ili kuivuta na kuishawishi hadhira kubwa inayoishi vijijini na mijini kwamba wao ndio wanaostahili kuiongoza Tanzania na sio CCM.


Mizizi na nguvu za CCM ni kubwa mno katika nchi yetu, anayepuuza ukweli huu ni mpuuzi jasiri asiyejua kupambanua baina ya mbivu na mbichi, na bila shaka hataki kwa makusudi kujua ukweli wa mambo ulivyo.


Msingi imara wa chama cha TAA ulijengwa kutokana na harakati za machifu wa Tanganyika katika dhati ya kupambana wakiwemo baadhi yao kina Mangi Meli, Kinjikitile, Mirambo, Kimweri, Mkwawa, Makunganya, Bushiri na wengine--wakati kukubalika kwa chama cha TANU ni matokeo ya nguvu na juhudi za chama cha TAA.


Kwa msingi huo kuimarika na kukubalika kwa CCM ni kutokana na kujijenga kwa vyama vya TANU/ASP ambavyo ni vyama viasisi vya siasa katika Tanganyika na Zanzibar tokea miaka ya 1954 na 1957.


CCM inatofauti sana kimtazamo na vyama kama UPC cha Uganda, MCP cha Malawi, na UNIP cha Zambia au KANU kilichokuwa kikitawala Kenya.


Vyama hivi navyo vilikataa kujikita na kuweka mizizi ili kulishika kundi la watu hasa mababa-kwabwela wanaoishi vijijini na kulazimishwa kutambua kwamba mafanikio na ujio wa uhuru wao ulitokana na vyama hivyo.


Kiuhalisia na kinadharia vyama hivyo mara baada ya uhuru vilibadilika na kuwa vyama vya kibwenyenye na kimwinyi kwa kuusahau kabisa kuutazama umma wenye nguvu za maamuzi na utafutaji wa ridhaa ya kudumu (CCM nayo ilijaribu kubadilika lakini sio kwa kasi kubwa ya kutisha kama ilivyokuwa kwa majirani zetu wa Uganda, Kenya, Malawi na Zambia. Shukrani za peee kwa hayati Kambarage Nyerere, mwasisi wa CCM).


Wanaojaribu kuitazama CCM kwa jicho rahisi wafanye pia utafiti mgumu ili kutambua matokeo kamili kabla na baada ya ujio wa vyama vingi huku wakiidurusu kwa weledi hali ya mambo na wakati ulikuwaje kwa nyakati hizo.


TANU haikupata kazi ya suluba ya kujenga matawi mapya toka mwaka 1954 kilipoanzishwa kuanzia kanda ya Mashariki, Lake zone ,Kaskazini na Kusini mwa Tanzania na hatimaye kusambaa nchi nzima, kutokana na kurithi matawi yoye toka kwa chama kikongwe cha TAA.


Kuzaliwa kwa CCM tarehe 5,2,1977 na kuenea kwake ilikuwa ni kama kuua tembo kwa bua kutokana na chama hicho kuiga tabia ya nyoka anayejibua gamba, na yeye kubaki akiwa ni nyoka yuleyule mwenye sumu kali.


TANU iliutumia vizuri mfumo wa chama kimoja na kueneza siasa zake hadi kwenye Taasisi za serikali, mashirika ya Umma, vyuo vikuu, sekondari hadi hata kwenye vikosi vya ulinzi na usalama.


Haikuwa kazi nyepesi inayoweza kuleta hasara haraka au kwa ulaini kama iliyovyazamwa na inavyoendelea kutazamwa na baadhi ya wahariri a mambo ya kisiasa.


Base ya TANU ni TAA. Base ya CCM ni TANU na ASP. CUF inatokana na vuguvugu la KAMAHURU, NCCR -Mageuzi ni mkusanyiko wa wanaharakati waliolilia mageuzi ya Kikatiba tokea miaka ya 1990. Lakini CHADEMA chimbuko lake halisi hasa ni nini na wapi? Au ndiyo ili iliyoelezwa kuwa something like "Chagga Develpement Manifesto"?


Takriban miaka 27 ilipita chini ya chama cha TANU kikiwaimbisha na kuwachezesha kwata wananchi chini ya zama ya nguvu ya chama kushika hatamu tangu pale mfumo wa vyama vingi ulipopigwa marufuku mwaka 1965; fursa na nafasi hii haikutumiwa ipasavyo huko Zambia, Uganda, Malawi na Kenya, na huu ndio ukweli wa mambo, ila anayetaka kubeza hawezi kuzuiwa.


CCM haikulala usingizi wa pono pale ulipoingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ilianzaa kujichimbia kisiasa, kuingiza wanachama wapya, kujinadi mbele ya umma na kuubeza upinzani kwa nguvu ya hoja.


Ni kweli serikali zake zimekuwa zikikabiliwa na matatizo mengi tokea awamu ya kwanza hadi hii ya sasa tuliyonayo--huku chama chenyewe kikijitutumua kwa bidii kulinda hadhi yake na kujivunia rasilimali watu.


Katika awamu ya kwanza mashirika yote ya umma yalifujwa, hakuna aliyefikishwa mahakamani, awamu ya pili walikamatwa watu wakisafirisha dhahabu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar ess Salaam, kesi ikayeyuka huku katika awamu ya nne tumeshuhudia mikataba mibovu ya madini na wizi katika akaunti ya EPA na BoT ikifanyika katika awamu ya tatu bila hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi ya waharifu/husika.


CCM mara kadhaa kimekuwa kikijikosoa na kujipanga kutokana na kupata msaada wa mtandao wake uliojengeka Tanzania nzima kwa miaka mingi.


Vyama vya Tanzania vina pupa ya kutaka kushika madaraka ya juu vianze kwanza kujijenga ndani ya halmashauri za wilaya, Bunge na Baraza la Wawakilishi huku vyenyewe vikitambua mitandao yao ili kupata ushindi ni dhaifu.


Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete imejitahidi kupambana na ubadhirifu wa mali ya umma, kukemea rushwa na kwa bahati nzuri kesi ziko mahakamani zikiwakabili vigogo wazito. Ingawa wengi wa hao wahusika wanataachiwa huru bila kupata adhabu wanayostahii, lakini hilo pekee ni jambo linalowaongezea wananchi mapenzi na hamu ya kuendelea kuiamini CCM, nje ya hilo ukifuatilia utekekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM toka awamu ya tatu hadi ya nne, Tanzania imepiga hatua (ingawa sio kubwa sana kimaendeleo).


Barabara, zahanati na huduma za maji safi zinatia moyo kinyume na miaka ile mara baada ya kupata Uhuru, vyama vya Bongo vijizatiti, viongozi wake wajitume na wasitegemee wao kuja kufaidi matunda ya nguvu zao, wafanye kama walivyofanya kina Mkwawa na Mangi Meli.


Kuimarika na kujengeka kwa CHADEMA kuna tofauti sana na kujengeka kwa CUF. Chadema mwanzo wake unatokana na safu ya waasisi wa chama hicho. Brown Ngululupwi, Edwin Mtei, Bob Makani, Costa Shinganya, na Kimesera. Hili lilikuwa ni kundi la masetla watupu na halikuwa la wanasiasa waliotambulika na kufanya kazi za kisiasa.


CUF ni chama kilichomega nguvu ya CCM Zanzibar baada ya wanachama wake vigogo wapatao saba walipofukuzwa mwaka 1988 akiwemo Seif Sharif Hamad mtu aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi wa SMZ.


Vigogo wengine ni Khatib Hassan Khatib aliyewahi kuwa mhazini wa CCM na MNEC--Hamad Rashid Mohamed ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mambo ya Ndani ya Nchi, Juma Ngwali na Masoud Omar wakiwa wakuu wa Mikoa.


Wanasiasa wengine waliopevuka kisiasa ni pamoja Musa Haji Kombo aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM, Juma Othman Juma aliyekuwa mjumbe wa NEC, Ali Haji Pandu Waziri wa Sheria katika SMZ, Soud Yusuf Mgeni Waziri wa Kilimo pamoja na Maulid Makame Abdallah aliyewahi kuwa Waziri mdogo wa Afya Zanzibar.


Kundi hili la CUF kwa kiasi kikubwa liliweza kuibana mbavu CCM kutokana na wao kuitambua misingi ya kuunda chama cha siasa na kukieneza kama taasisi.


Nieleweke wazi kwamba sikipigii chapuo chama cha CUF ila nimefanya utafiti na kuiona tofauti kubwa kati ya CCM, CHADEMA na CUF. CHADEMA wajenge kwanza mizizi na kundi lililopo sasa lisitegemee kula matunda ya juhudi hizo.


Chama cha CHADEMA na vingine katika Tanzania vinapaswa kujifunza na kupita katika barabara ya chama cha Liberal Party cha Uingereza amacho hakikuwa na papara ya kushika madaraka haraka bali kilitafuta kwanza amana na hatimaye kikaaminiwa.


CUF wanaelekea kuingia katika medani za serikali Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, hatua hiyo pekee ukiwa mtu mkweli utaweza kujua usahihi wa tathmini yangu.


Bado siamini kutokana na utafiti mdogo nilioufanya kwamba CHADEMA kimejiandaa na kimejijenga kimfumo, kisera na kimtandao kiasi kwamba kiweze kushinda katika uchaguzi wa mwaka huu na kuongoza dola.


Jambo hili kwa CHADEMA sitaki kabisa niliamini moyoni mwangu, naomba lisistawi kabisa kwenye mishipa ya fahamu zangu na kwenye ubongo wangu pia.


CHADEMA hakitashinda kutokana na kwamba bado ni kichanga, kiliwahi kusifiwa na Mwalimu Julius Nyerere kwamba kina sera zenye mwelekeo lakini kina upungufu wa wanasiasa, ni sawa tu na timu ya soka yenye nyota haba wa kuleta ushindi.


Safu ya kina Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, John Mnyika, Halima Mdee, Philemon Ndesamburo, Maulida Komu na Mabere Marando ni kundi la wasomi wa fani za kitaaluma wakikosa mtaji na ujuzi wa mizungu ya ufanyaji wa siasa.


Slaa ni mwanasiasa mahiri, mwepesi wa utambuzi wa mambo, hata kutoka kwake CCM baada ya kukatwa jina lake na kupachikwa kwa Patrick Qorro katika kura za maoni kulilalamikiwa sana na Mwalimu Julius Nyerere.


Slaa ni yeye peke yake kinara ndani ya CHADEMA akizungukwa na timu hafifu isiyo na uwezo ama ukomavu wa kisiasa wa kukiletea ushindi chama hicho. Kwa upande mwingine, CCM bado kina ngome kubwa, viongozi wengi wenye amana mbele ya umma ambao hawakuona umuhimu wa kujitoa ndani ya chama hicho kwa wingi na kujiunga na kambi ya upinzani.


Chadema, NCCR na TLP ni vyama vinavyoweza kuja kujiimarisha katika siku nyingi zijazo usoni, CUF kwa upande wa Bara nao wamo katika msafa wa vyama hivi vitatu, hawajawa na timu imara na pia Kiongozi wake Profesa Ibrahim Lipumba hajaungwa mkono na wasomi wenzake wa Chuo Kikuu cha Dare es Salaam kuonyesha kama anakubalika.


Hata yeye Lipumba anaonekana yuko peke yake. Ni sawa kabisa na kusema mchezaji nyota wa Brazil "Kaka" aamue kusajiliwa na Balimi ya Bukoba kisha timu hiyo ghafla itarajiwe kutandaza kabumbu safi uwanjani, aifungie magoli mengi timu hiyo, hata aiwezeshe ichukue ubingwa wa ligi kuu. Wa-da-nga-yi-ka wenzangu hebu tusijidanganye. Hiyo ni ndoto ya mchana. Hilo haliwezekani kwa mwaka huu na hata baada ya miaka kumi na tano ijayo, CHADEMA isitegemee kushinda kwasababu bado hakijajipanga vizuri.


Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!


P.S. [makala hii imeandikwa na Antar Sangali, mwandishi wa BongoTz.com]

Mawazo kama haya yanamsaidia tu mwandishi kupata malupulupu ya kuishi yeye na famila yake na siyo kuijenga Tanzania ya leo. Watanzania lazima tuwe na uchungu jinsi nchi yetu inavyotafunwa chini ya chama kinachosemekana kuwa sera nzuri na ni imara kabisa (kinadharia)! Kutokana na umaskini tulio nao na sifa za sera nzuri za chama tawala, hakuna uwiano wowote. Ndiyo maana hata kama kuna chama kichanga kama mwandishi anavyodai ni bora kiongoze nchi kuliko chama kilicho imara lakini umaskini unazidi kuongezeka - ukianzia, pamoja na mambo mengine, na jiji la Dar es Salaam kunuka kinyesi kila siku!
 
Huo ushauri wa kuongoza dola si jambo la mchezo ungempa Kikwete 2005. Angalia alipotufikisha. Hata kama Chadema si perfect, nakuhakikishia they will do a better job in government than this clown.
Jasusi, I respectfully disagree with your assumption.
 
Ndiyo maana hata kama kuna chama kichanga kama mwandishi anavyodai ni bora kiongoze nchi kuliko chama kilicho imara lakini umaskini unazidi kuongezeka - ukianzia, pamoja na mambo mengine, na jiji la Dar es Salaam kunuka kinyesi kila siku!
No, umasikini wa watanzania unachangiwa na watanzania wenyewe kuwa wavivu. Nani anakuzuia kujiajiri mwenyewe kama unashindwa kupata ajira serikalini ama kwenye private sector. Watanzania wanachokijua ni kukaa vijiweni na kupiga porojo siku nzima wakitegemea kuwa serikali itawafanyia kila kitu. Hizo zama za zamani zimepitwa na wakati. There ain't no such thing as a free lunch hapa duniani. Na kuhusu "jiji la Dar es Salaam kunuka kinyesi kila siku," unategemea Kikwete ndo' aje kukusafishia? C'mon! Mbona watu mnaongea pumba sana humu jukwaani. Serikali haiwezi ikawafanyia kila kitu. Wewe unachafua jiji mwenyewe, unategemea matokeo yake yawe nini? Jiji lijisafishe lenyewe????
 
Kasome katiba ya taifa....

I knew it .... huna data za kusapoti maelezo yako na yet unataka watu wakuchukulie serious.

Nilianza kukuona myeyushaji baada ya kuanza kujibu as if wewe ni Antari Sangari (mwandishi wa hii habari). Huwezi kutoa credit mwanzoni mwa thread na ukaanza kuchukua credit kati kati ya thread unless unataka kusema kuwa wewe ni Antari Sangari (which of course you are not).
 
No, umasikini wa watanzania unachangiwa na watanzania wenyewe kuwa wavivu. Nani anakuzuia kujiajiri mwenyewe kama unashindwa kupata ajira serikalini ama kwenye private sector. Watanzania wanachokijua ni kukaa vijiweni na kupiga porojo siku nzima wakitegemea kuwa serikali itawafanyia kila kitu. Hizo zama za zamani zimepitwa na wakati. There ain't no such thing as a free lunch hapa duniani. Na kuhusu "jiji la Dar es Salaam kunuka kinyesi kila siku," unategemea Kikwete ndo' aje kukusafishia? C'mon! Mbona watu mnaongea pumba sana humu jukwaani. Serikali haiwezi ikawafanyia kila kitu. Wewe unachafua jiji mwenyewe, unategemea matokeo yake yawe nini? Jiji lijisafishe lenyewe????

Bongotz, kuna kitu kinaitwa kodi ... kazi yake ni kufanya kazi kama hii - kusafisha jiji.
Kijana mbona una pumba sana leo?
 
Bongotz, kuna kitu kinaitwa kodi ... kazi yake ni kufanya kazi kama hii - kusafisha jiji.
Kijana mbona una pumba sana leo?
To paraphrase Joe Walsh, you are a sick mind Mwafrika. And I can't argue with a sick mind.
 
Back
Top Bottom