Jamani mimi mwenzenu naomba kuuliza. Mara nyingi nimekuwa naota ndoto ambapo katika ndoto hizo ni kwamba huwa ninakuwa na uwezo wa kuruka na kupaa hewani nikielea.
Tatizo ndoto hizi huwa naziota mara nyingi, bora ingekuwa naota mara moja moja lakini zinajirudia.
Zina maana gani?
=========
Similar cases:
Tatizo ndoto hizi huwa naziota mara nyingi, bora ingekuwa naota mara moja moja lakini zinajirudia.
Zina maana gani?
=========
Similar cases:
Mmeshindaje wakuu,
Mara nyingi nimekuwa nikiota ndoto kama napaa hewani, imetimia miaka miwili sasa toka nianze kuota ndoto ya namna hii. Ndoto hii ninaiota atleast mara moja kwa mwezi, naota nikiwa katika mazingira tofauti nikawa nipo mitaani tu napaa hewani watu wananishangaa nikifika kwenye nyaya za umeme nina zikwepa nazidi kwenda juu zaidi.
Siku nyingine naota nipo kwenye ndege halafu ndege imepata ajali wengine wanapata madhara lakini mimi ninaendelea kuelea angani. Ili nipae angani huwa natakiwa niinyooshe mikono hewani dnipo napaa hewani zaidi na nikitaka kushuka chini nashusha mikono chini nikitaka kwenda angani tena nanyosha mikono juu.
Muda huo nikiwa angani huwa nakuwa na furaha sana na hatimae nikiamka asubuhi siku yangu huwa ya furaha sana.
Michango yenu wakuu, ni kawaida kuota ndoto inayojirudia rudia mara nyingi? Ndoto hii ina maana gani?
ASANTENI.
CC: MziziMkavu Pasco
Hii ndoto naota mara nyingi napaa angani ina maana gani? Nashindwa kuelewa kwani naiota mara nyingi sana nimetafuta maana yake nashindwa kupata jibu,nanyoosha mikono juu nakunja magoti kidogo,nikiinua magoti napaa na watu wengi wanakuja kushuhudia hilo,,maana yake nini ndugu zangu.