Ukilewa sana kisha ukalala unaweza kuota ndoto ndani ya ndoto na ukiwa kwenye hiyo ndoto ukaota tena ndoto ila process ya kuamka inaweza kukuchizisha

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,054
Hello bosses and roses,

Leo niko kwenye mood ya kuandika so nimeona niandike hii experience nliopitia mwaka fulani.

Kuna siku miaka ya zamani kdg nililewa sana zaidi ya kawaida. Mie nna alcohol torelance ya ajabu sana. Hata nilewe vipi huwa sipotezi fahamu, nitayumba kutembea lkn ukinipa kazi ndo ntaifanya kwa speed ya ajabu hadi utashangaa. Na nikilewa sana huwa napata usingizi mtamu balaa ila kwa muda mfupi tu. Naweza kulala kama masaa matatu tu lkn usingizi murua sana. Inshort huwa nakua na consciousness fln amazing sana ambayo ngumu kuwa nayo kwa siku za kawaida.

Sasa bwana hio siku ikatokea nimelewa balaa, nikarudi zangu ghetto nikaendeleza kunywa tena huku nacheki movie fln hv hadi nikapitiwa na usingizi. Kwenye huo usingizi sasa niliexperience hii situation ambayo sijawahikuipata hapo kabla na kidogo niwe chizi aisee.

Kwanza niliota ndoto ya kwanza nimegeuka kuwa TAI (Eagle), nikawa napaa juu naona mambo nafurahia tu, nikazidi kupaa zaidi na zaidi nikaona mambo ambayo nakumbuka kwenye hio ndoto niliyaelewa lkn baada ya kutoka kwenye ndoto sikuyaelewa tena. Ile kupaa juu zaidi mawinguni nikawa napishana na mawingu tu ghafla misuli ikabana nikasikia maumivu makali nikaanza kushuka bila control kwa free fall kama mzoga wa ndege.

Sasa muda huo niko na hofu nini kitafuata mara nikapoteza fahamu (Nikiwa kama TAI, Eagle) na nikaingia kwenye Ndoto nyingine kuwa nimegeuka kuwa Simba. Kwenye Kuwa simba nikawa naona mambo mengi porini na kuyaelewa (wakati huo kwenye ndoto ila baada ya kutoka nikawa siyaelewi tena). Ile naperuzi tu mapori na vichaka naona mambo mengi sana lkn ukatokea ukame na nikawa na njaa sana hadi nikalala usingizi mzito na ndani ya huo usingizi nikaota tena nimekua Popo (Bat).

Sasa hii ya kuwa Popo ndio nnayotamani ningekua nachukua notes uingizini sababu niliona mambo mengi sana, hatari nyingi sana lkn kama kawaida baada ya kutoka kwenye hio ndoto sikuweza kuzikumbuka wala kuzielewa. Si tunajua Popo anatumia sana masikio yake kupata taarifa zaidi hata ya macho au sensory organ yyt ile, pia ana uwezo wa kujua dalili za matetemeko na hatari nyingine. Sasa kwenye hii ndoto niliona mambo mengi sana lkn kitu pekee nnachokumbuka niliona hatari kubwa sana ikija huku viumbe vingine vikichukulia poa na kitendo hicho kikafanya niwe na hofu kweli na ndipo nikazinduka kutoka kwenye hio ndoto ya kuwa Popo nikarudi kuwa simba mwenye njaa (kule nilipotoka)

Nikikumbuka nachekaga sana, yaan ile feeling ya kutoka kwenye ndoto ukiwa binadam ndio hio hio nilikua naipata nilipoanza kurudi reverse yaani nilipotoka kwenye ndoto ya kuwa Popo na kurudi kuwa Simba. Sasa hapo nikiwa nashangaa kwa nn niko simba na nna njaa kali ndipo nikazinduka tena kutoka kwenye ndoto ya kuwa simba na nikarudi kuwa Tai (Eagle). Kumbuka kwenye Eagle niliishia nikiwa nashuka kwa free fall baada ya misuli kufeli na nikapoteza fahamu. Sasa fahamu zikarudi bado nipo kwenye hio free fall, huku najiuliza ni nini hiki mbona na-move kwa speed sana huku mwili ukiwa mdg na mwepesi ndipo nikafika chini na kujigonga kwenye jiwe moja nikapata maumivu kweli kichwani lkn hapo hapo nikashtuka nikarudi kuwa binadamu. Aisee nilipanic nakushtuka nikidhan mto nliokuwa nmelalia ndio hilo jiwe nilioangukia. Nilikua na maumivu makali ya kichwa na nimechoka zaidi ya kawaida.

Kwa dakika kumi baada ya kushtuka kidogo nichizi pale kitandani sababu kichwa kwanza kilikua kinauma lkn kimejaza information nyingi ambazo sikuweza kuzielewa tena, huku nikiwa na hamu ya kuelewa ndipo zikazidi kupotea mdg mdg hadi nikabaki empty set.

Nilikaa wiki nzima najiuliza maswali mengi. Ikafikia muda nikajiuliza AU kuwa binadamu nayo ni ndoto pia, yaan nimezinduka kutoka kwenye ndoto hizo nyingine ili niendelee na hii ndoto kuu. Inafikirisha sana....

Hii ilitokea miaka mingi iliopita, nimekumbuka leo nimeona nishare hape. Je na wewe ulishawahi kuota ndoto ndani ya ndoto ndani ya ndoto?
 
Kuna mmoja alikua anakula mihogo mixer kachumbari, ukwaju na pilipili kama 10 anazikatiamo. Baada ya hapo anaenda kukata K-Vant.
Basi kunasiku alikuja analalamika kwamba anaharisha dam, mie jibu nikawa nishalipata.
huyo anatafuta kifo

Mie mbona nlikua nimekula vzr tu. Makange kilo nzima
 
Back
Top Bottom