monde arabe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 8,490
- 13,022
Habar zenu ndugu zangu,
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikiota ndoto nyingi tofauti tofauti ambazo binafsi sina uwezo wa kuzitafsiri hata kidogo.Miongoni mwa ndoto hizo ni pamoja na hizi;
1. Nimewahi kuyaota maeneo tofauti tofauti ambayo tangu nilipozaliwa sikuwa nimeenda kutembelea kwenye maeneo hayo wala sikuwahi kupita kwenye maeneo hayo na wala sikuwa nayafahamu maeneo kwa majina wala kwa lolote. Mwanzoni mwa mwezi January, 2024 nilienda kutembea Mkoani Geita sehemu moja inaitwa Msalala (nilitembelea maeneo mengi sana kama vile Bukwimba,Bulangale na Msalala mjini/Msalala Center kisha nilienda Geita mjini).
Wakati naenda Msalala nilipitia Solwa,Mwakitolyo Mgodini na gari (gari la Hokas) lilitembea umbali mrefu sana then tukatokezea Msalala.Nikiwa njiani kutoka Mwakitolyo to Msalala niliziona Leaching Plants nyingi sana hasa Leaching Plant ya Wagogos ambayo imezunguwa na miti mingi na iko fenced.Maeneo yote hayo hasa hiyo Leaching Plant nilikuwa tayari nimekwisha kuiona kupitia ndoto kabla hata sijapanga safari ya kwenda Msalala then Geita.
Pia wakati natoka Msalala nilipitia Geita mjini (sikurudi na njia niliyokuja nayo mwanzo ya Solwa to Msalala) nilipofika Geita mjini nililala Lodge/guest house ili kesho yake niweze kuendelea na safari.Mida ya saa sita za mchana (kesho yake/kulipokucha) nilipanda bus la kampuni ya 'Africa raha' lililokuwa linatokea Bukoba kuelekea Mwanza mjini kupitia kivuko cha Busisi lkn,kabla hatujafika kwenye daraja la Busisi nililiona eneo ambalo tayari nilikuwa tayari nimeshaliona ndotoni kabla sijapanga hata hiyo safari ya Mwakitolyo to Msalala then from Msalala to Geita then Geita to Usagara via Busisi
Vilevile,kuna maeneo ninaweza nikaenda leo na maeneo hayo/eneo hilo sijawahi kwenda hata mara moja wala sijawahi kupita kwenye eneo hilo wala sijawahi kulisikia eneo hilo lkn,nikifika kwa mara ya kwanza nahisi kama niliwahi kufika kwenye eneo hilo japo nakuwa sikumbuki ni lini nilifika kwenye eneo hilo
2. Nimekuwa nikiota nazungumza na watu maarufu mara nyingi sana.Baadhi ya watu hao ni pamoja na hawa;
I. Magufuli,huyu jamaa japo sikuwa nampenda lkn,kuna kipindi niliwahi kuota namshauri lkn,akaukataa ushauri wangu.Siku hiyo wakati namshauri alikuwa amevaa suruali jeusi na shati la kijani (long sleeve) japo sikumbuki nilikuwa namshauri nini.
II. Kuzungumza na wasanii wa Bongo flavour mfano Diamond Platnumz na wengineo wengi.
III. Kuota nachota maji kwenye kisima nakujaza kwenye ndoo.
IV. Kuota nimepanda gari la abiria (bus) nasafiri.
V. Kuota natembea juu ya maji na sizami (maji yenyewe ni mengi sana ni kama vile nipo Ziwani au Baharini).
VI. Kuota nafundisha wanafunzi wengi sana (nipo ubaoni nimeshikilia kitabu nawafundisha wanafunzi wengi sana na wananisikiliza kwa umakini sana).
VII. Kuota naendesha bus la abiria na abiria wamejaa sana kwenye bus.Pia,nimekuwa nikiota naendesha magari tofauti tofauti au nimepanda kwenye pikipiki na anaendesha mtu mwingine.
VIII. Kuota napaa angani na nipo mbali sana lkn,ni kupaa kwa namna ya kwenda horizontally na kuna muda naganda angani kama ndege then natazama chini naona ni mbali sana.
XI. Kuota nimekaa mahali na yanakuja maji mengi sana kama mafuriko lakini, hayanidhuru wala kuniathiri kwa lolote.
XII. Kuota naokota fedha au napewa fedha au nahamisha fedha kutoka kwenye mfuko mmoja wa suruali kwenda mfuko mwingine.
Kwa kifupi ni ndoto nyingi sana lkn,naomba mnisaidie kutafsiri hizo ndoto chache kwa leo kwa wale wenye maarifa au elimu ya kuweza kufanya hivyo
Asanteni!