Ndoto za kupaa na kuelea hewani zinaashiria nini?

Rastad

Member
Oct 3, 2011
13
3
Jamani mimi mwenzenu naomba kuuliza. Mara nyingi nimekuwa naota ndoto ambapo katika ndoto hizo ni kwamba huwa ninakuwa na uwezo wa kuruka na kupaa hewani nikielea.

Tatizo ndoto hizi huwa naziota mara nyingi, bora ingekuwa naota mara moja moja lakini zinajirudia.

Zina maana gani?

=========

Similar cases:
Mmeshindaje wakuu,

Mara nyingi nimekuwa nikiota ndoto kama napaa hewani, imetimia miaka miwili sasa toka nianze kuota ndoto ya namna hii. Ndoto hii ninaiota atleast mara moja kwa mwezi, naota nikiwa katika mazingira tofauti nikawa nipo mitaani tu napaa hewani watu wananishangaa nikifika kwenye nyaya za umeme nina zikwepa nazidi kwenda juu zaidi.

Siku nyingine naota nipo kwenye ndege halafu ndege imepata ajali wengine wanapata madhara lakini mimi ninaendelea kuelea angani. Ili nipae angani huwa natakiwa niinyooshe mikono hewani dnipo napaa hewani zaidi na nikitaka kushuka chini nashusha mikono chini nikitaka kwenda angani tena nanyosha mikono juu.

Muda huo nikiwa angani huwa nakuwa na furaha sana na hatimae nikiamka asubuhi siku yangu huwa ya furaha sana.

Michango yenu wakuu, ni kawaida kuota ndoto inayojirudia rudia mara nyingi? Ndoto hii ina maana gani?
ASANTENI.

CC: MziziMkavu Pasco

Hii ndoto naota mara nyingi napaa angani ina maana gani? Nashindwa kuelewa kwani naiota mara nyingi sana nimetafuta maana yake nashindwa kupata jibu,nanyoosha mikono juu nakunja magoti kidogo,nikiinua magoti napaa na watu wengi wanakuja kushuhudia hilo,,maana yake nini ndugu zangu.
 
Jaman mi mwenzenu naomba kuuliza,mara nyingi nimekuwa naota ndoto ambapo katika ndoto hizo ni kwamba huwa ninakuwa na uwezo wa kuruka na kupaa hewan nikielea.tatizo ndoto hizi huwa naziota mara nyingi, bora ingekuwa naota mara moja moja lakini zinajirudia.

kuna kipind nilikuwa na ndoto kama zako, kwa sasa siot tena ila nilikuwa nainjoy sana
 
Jaman mi mwenzenu naomba kuuliza,mara nyingi nimekuwa naota ndoto ambapo katika ndoto hizo ni kwamba huwa ninakuwa na uwezo wa kuruka na kupaa hewan nikielea.tatizo ndoto hizi huwa naziota mara nyingi, bora ingekuwa naota mara moja moja lakini zinajirudia.

Ni kawaida hiyo hasa kipindi mambo yako yanapokuendea vizuri hali hii hujitokeza, wakati mwingine inakaa muda mrefu utadhani hauko ndotoni.
 
Hii ndoto naota mara nyingi napaa angani ina maana gani? Nashindwa kuelewa kwani naiota mara nyingi sana nimetafuta maana yake nashindwa kupata jibu,nanyoosha mikono juu nakunja magoti kidogo,nikiinua magoti napaa na watu wengi wanakuja kushuhudia hilo,,maana yake nini ndugu zangu.
 
Hii ndoto naota mara nyingi napaa angani ina maana gani?
Nashindwa kuelewa kwani naiota mara nyingi sana nimetafuta maana yake nashindwa kupata jibu,nanyoosha mikono juu nakunja magoti kidogo,nikiinua magoti napaa na watu wengi wanakuja kushuhudia hilo,,maana yake nini ndugu zangu
​@director1 ukiona dalili za kupaa uni pm ndotoni ili tupae wote mwana, haiwezekani uhondo uufaidi peke yako
 
Nenda hospital kapime afya kama ni mkirsto nenda kwenye maombi na kama ni mwislam kula nyama iliyochinjwa na mkristo(Siku nyingine ukiota jikague kama umepiga bao isijekuwa wakati wa finishing ndio unadhani unapaa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom