Maandamano ya CHADEMA Jiji la Mbeya-Picha na Matukio

Mtachoka tu kuandamana li-nchi likubwa sana hili. Kodi zetu ndio zinateketea hivo. Tofauti kati yenu na CCM kwa matumizi ya fedha za UMMA haipo. Watoto wetu waendelee kusoma chini ya miti na kukalia mawe. Tuendelee kuigharamia SIASA mpaka basi.

Acha majungu. Kwani Chadema wanakusanya kodi? unaweza kutuambia shilingi ngapi zimetumika?
 
mulikuwa munauhadaa ulimwengu kuwa Tanzania kuna demokrasia ya vyama vingi. Pumba (cuf, nccr, tlp, udp, nra, tadea, dp) zimejitenga.

chama cha siasa cha upinzani ndiyo hicho sasa kimejipambanua. mnatamani hata ruzuku ifutwe. lol!

na bado.
Hapo kwenye red, Ruzuku ikifutwa ujue ndiyo msumari wa mwisho kabisa kwenye jeneza la ccm. CCM hakuna mkutano wala maandamo bila wahudhuriaji kulipwa na kusafirishwa na malori. Pia hata kuiba kura itakuwa tabu
 
Nawambieni CHADEMA msipoonyesha kwa vitendo kufanya yale ambayo CCM yamewashinda, watu wa kawaida watashindwa kuwatofautisha nao. Maandamano hata CCM wanayaweza sana. Onyesheni kwa vitendo na kauli zenu kwamba mnaweza kuyabadili maisha ya Watanzania hata kwa ruzuku hii ndogo mnayopata.

Ninani amekwambia ruzuku ya Chama ndo inatumika katika Maandamano!!Ushaambiwa wabunge wa cdm wanatoa michango kutoka katika posho zao na mishahara yao ili kuimarisha chama nakutoa elimu ya Uraia kwa wananchi ili waamke kudai Haki zao zinazonyonywa na kuibiwa na Mafisadi.Ruzuku ya Chama Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) lazima akague zimetumika vipi na lazima kuna mwongozo juu ya Matumizi yake so acha kupotosha Wananchi.
 
hivi ukisema watanzania tunawashangaa unajumuika na watanzania wep hao kuishangaa nguvu ya umma? Mind thc wanaondamana ni watanzania hao hao unaosema waniashangaa CDM! Gamba gambuka kwnza ndo uingize miguu yko humu ndan
 
...mji wote umezizima,ni maelfu ya watu!! Wanafunzi wameacha masomo kuiunga mkono CDM!!

Thats a problem. Do we rise awareness, do we build our nationt that way?!!
Mkuu, siyo jambo la kushabikia hilo (kama unashabikia)
 
Haya maandamano yanagharimu kiasi kikubwa sana cha fedha, kuanzia magari, ukodishaji wa magari, mafuta, chakula, malazi, POSHO za viongozi n.k, fedha hivi zingetumika kununua madawati kwenye mojawapo ya shule za msingi zilizo karibu na ofisi ya CDM pale kinondoni au hata kununua dawa mahospitalini.

Wewe na chama chako cha magamba hamna moral authority ya kutoa kauli kama hizi. Mara hii umeshasahau kwamba serikali ya CCM ilishawahi kutenga bl 18 kwa vinywaji?
 
wildcard huna hoja na hushirikishi ubongo......kaa utulie...mmeshindwa kujichuna huko kwenu magamba sasa mnaweweseka tu......
 
Wakuu,

Hivi sasa ndio tunajipanga ili kuanza Maandamano yetu. Mji umejaa hamasa kubwa kila ukipita bendera za CHADEMA na ishara ya vidole viwili ndio vimetawala.

Watu wamependeza sana na Kombati na Sare nyingine za Chama. Tunatarajia kuanza Maandamano mida ya saa sita. Magari yote ya msafara yako hapa Forest yakipiga nyimbo mbalimbali za chama. Maandamano yanatarajiwa kuanza maeneo ya Mafiat njia ya Uwanja wa Ndege yataelekea Viwanja vya Ruandanzovwe Mwanjelwa.

Leo tutatembea Kilomita Mbili tu.

Pata picha za Awali.




Aluta Continua
Kutoka Mbeya Forest

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
Pamoja tutafika mkuu endelea kutujuza mpaka walie wajivua magamba.
 
Wewe na chama chako cha magamba hamna moral authority ya kutoa kauli kama hizi. Mara hii umeshasahau kwamba serikali ya CCM ilishawahi kutenga bl 18 kwa vinywaji?

Mkuu makosa mawili hayafanyi kuwa sahili, CDM hawazezi kuendelea kuchoma moto kodi zetu simply because serikali nayo hukosea.
 
Nalipa kodi kwa serikali. Serikali inawapa CHADEMA karibu 1bn kila mwezi kama RUZUKU. Dr Slaa alifanya kazi kubwa mwaka jana kuipandisha ruzuku hii.

Haya ndiyo matatizo ya kuwa m-CCM "mbumbumbu". Hivi ni nani kati ya CCM na CHADEMA aliyekuwa anapokea bilioni 1 kila mwezi 2005-2010, na sasa amechanganyikiwa mapato kushuka? Inawezekana vipi serikali ya CCM kuwa na upendo wa ajabu namna hii kuwapa CHADEMA bil 1 kasoro kidogo na CCM kupunjwa wakati inajulikana wabunge wa CCM ni wengi kuliko wa CHADEMA?

Kuhusu kazi ni kweli Dr Slaa alifanya. Lakini ukimuuliza yeye na viongozi wengine makini wa CHADEMA watakwambia wananchi ndiyo waliofanya kazi kubwa mno. Huu ndiyo ukweli zaidi. Ni wananchi walioikataa CCM, walihamasishana, walitambua nani adui yao mkubwa, waliokwenda kupiga kura, waliolinda kura na walishinikiza matokeo halali yatangazwe. Ni waliosema hatuna bunduki, risasi wala mabomu lakini nguvu yetu itatupa ushindi wetu ambao CCM inataka kutupora. Ni wao ambao jana, leo na hadi kesho wanawaunga mkono viongozi wawapendao wa CHADEMA katika maandamano haya kote nchini.

Msione wivu, CCM jaribuni basi na ninyi kuyafanya angalau ya mita 100 mkiwaalika watu bila ya kuwasomba kwa magari muone nguvu iliyopo ndani ya mioyo ya watu.
 
Serikali ya CCCM imekuwa ikiwapatia CDM mamilioni ya shilingi kama ruzuku ya chama hicho kujijenga kidemokrasia na kuleta chachu ya maendeleo nchini lakini CDM wamekuwa wakitumia fedha hizo za walipa kodi kwa kutalii mikoa kadhaa huku wakipoteza nguvu ya rasilimali watu, nchi hii inahitaji wachapakazi na wenye kuleta chachu ya maendeleo na si watalii.

Watanzania wengi wamelala. Wamelewa usingizi wa CCM. Kama kodi yangu ninayokatwa kila mwezi inatumika kuamsha waliolala, sina pingamizi.
 
Thats a problem. Do we rise awareness, do we build our nationt that way?!!
Mkuu, siyo jambo la kushabikia hilo (kama unashabikia)

Raha sana kuona mnaumia hvi... 2nawatakia kila la kheri kwenye harakati za kuvuana magamba.
 
Na tayari vyama vimeshaelezwa kuwa vipeleke mapato na matumizi yao kwa mkaguzi mkuu wa serikali,nadhani kama kuna ubadhilifu ama kuna matumizi tofauti tutapata tu taarifa kwani kwa sasa na mkubali sana mkaguzi mkuu wa serikali kwa upande wake anafanya kazi ipasavyo,tatizo ni serikali kuzitumia hizo ripoti atowazo mkaguzi mkuu
kwa upande wa chadema na dhani watakuwa makini sana na matumizi kwani wao ndio vinala wa kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya pesa kwa hiyo wakienda kinyume hatuta WAELEWA KABISA
kazi njema wanaharakati
 
Wazo zuri ni kweli maandamano yaendane na kuonyesha kwamba wanaweza kuaminiwa kwa vitendo
Ni vitendo gani unataka, hujasikia muziki wa madiwani uliomtoa mkuruganzi wa moshi nduki. Na bado huko Arusha Mh Lema kafanya kweli na ndio maana viongozi wa serikali walimsusia. Sitaki kumaliza uhondo. Tuambie CCM walichokifanya zaidi ya kuonyeshana ubabe ya kwamba kila mmoja na mjuaji na kutafuta masifa.

Tanzania haitajengwa na wanafiki au na watu wenye tamaa. People's powerrr!!!!!!. Mpaka kieleweke.:israel:
 
Thats a problem. Do we rise awareness, do we build our nationt that way?!!
Mkuu, siyo jambo la kushabikia hilo (kama unashabikia)

wewe ulitaka wasifurahie, na wasiandamane?........jamani kama hamjapata lunch nawashauri mle
 
Kila la kheri jamani tunaamini mashujaa wa taifa letu (Tanganyika) mtaendelea kutuwakilisha huko, natamani sana ningekuwepo kwani mimi ni mzailwa wa Soweto (Mby) jirani kabisa na eneo la viwanja vya Ruanda Nzovwe.... ukombozi unazidi kukaribia
 
Back
Top Bottom