LiverpoolFC
JF-Expert Member
- Apr 12, 2011
- 11,348
- 3,219
Kawaambie wazuie ruzuku yao. Halafu tuone!
Serikali ya CCCM imekuwa ikiwapatia CDM mamilioni ya shilingi kama ruzuku ya chama hicho kujijenga kidemokrasia na kuleta chachu ya maendeleo nchini lakini CDM wamekuwa wakitumia fedha hizo za walipa kodi kwa kutalii mikoa kadhaa huku wakipoteza nguvu ya rasilimali watu, nchi hii inahitaji wachapakazi na wenye kuleta chachu ya maendeleo na si watalii.
Mtachoka tu kuandamana li-nchi likubwa sana hili. Kodi zetu ndio zinateketea hivo. Tofauti kati yenu na CCM kwa matumizi ya fedha za UMMA haipo. Watoto wetu waendelee kusoma chini ya miti na kukalia mawe. Tuendelee kuigharamia SIASA mpaka basi.
mimi nafikiri ujui unachoonge.maandamano yamesaidia kwa kwa kiasi kikubwa na cha umuhimu watu wapate elimu na watambue haki zao ili itapofikia wakati wa uchaguzi wafanye maamuzi boro.
Hivi hawa Chadema sisi Watanzania tunawashangaa sana kila kukicha maandamano, saizi watu wapo makazini, viwandani, mashambani, wao wapo barabarani wanafanya usumbufu kwa Watanzania, wanatumia vibaya pesa zetu walipa kodi 'ruzuku' wanagawana posho kila baada ya maandamano. viongozi wa juu Dk Slaa na wenzake kila mmoja poso yake milioni mbili, hawa wengine kina Lema na wenzake milioni moja, huyo dada mbunge wa kupewa wa maandamo Regia Mtema yeye na wenzake laki tano, huyu dada yeye kila kukicha kiguu na njia kwenye maanamano, hili swala Zitto akubaliani nalo ndio maana umuoni kwenye maandamano yao, Chadema wamefanikiwa lakini kwenye maandamano kimekuwa chama cha kwanza dunia kufanya maandamano mengi wastani kila mwezi wanaitisha maandamano. wamo kwenye Guinness book Record in the World, chama cha maandamano
Tusimpuuze WildCard,Kwa wanafunzi mmekwisha wawini. Matawi mnafungua sana kisha mnayatelekeza. Ruzuku yote kwenye maandamano na uendeshaji makaomakuu!
Wakuu,
Hivi sasa ndio tunajipanga ili kuanza Maandamano yetu. Mji umejaa hamasa kubwa kila ukipita bendera za CHADEMA na ishara ya vidole viwili ndio vimetawala.
Watu wamependeza sana na Kombati na Sare nyingine za Chama. Tunatarajia kuanza Maandamano mida ya saa sita. Magari yote ya msafara yako hapa Forest yakipiga nyimbo mbalimbali za chama. Maandamano yanatarajiwa kuanza maeneo ya Mafiat njia ya Uwanja wa Ndege yataelekea Viwanja vya Ruandanzovwe Mwanjelwa.
Leo tutatembea Kilomita Mbili tu.
Pata picha za Awali.
Aluta Continua
Kutoka Mbeya Forest
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
Wazo zuri ni kweli maandamano yaendane na kuonyesha kwamba wanaweza kuaminiwa kwa vitendoNawambieni CHADEMA msipoonyesha kwa vitendo kufanya yale ambayo CCM yamewashinda, watu wa kawaida watashindwa kuwatofautisha nao. Maandamano hata CCM wanayaweza sana. Onyesheni kwa vitendo na kauli zenu kwamba mnaweza kuyabadili maisha ya Watanzania hata kwa ruzuku hii ndogo mnayopata.
Pumba nyingine!Duh ! ww mama bado una post vitu humu JF ? watu hawana imani na ww humu kwa upotoshaji unaofanya na kulinda maslahi yako badala ya taifa
Asante Dada Regia Mtema,Hivi sasa ndo tumetoka kuzindua tawi la wanafunzi chuo kikuu cha Teofilo Kisanji.Tunaelekea kuzindua Ofisi yao Majengo tukitoka hapo tunaendelea na maandamano kuelekea uwanjani.Watu ni wengi sana.Aluta Continua.
CHADEMA sio CCM tumeona ilivyojengwa na jinsi gani wamezitumia rasilimali zetu kwa ajiri ya kuendeleza matubo yao na familia zao(UFISADI)Kwa ziara za kwenda nje na kuwakumbuka wananchi wakati wa uchaguzi kwa kuwazadia walalahoi pea za khanga fulana na pilau.Utakijengaje chama kwa kukaa Dar na kutanua.HAMA KWELI CCM KICHEKESHO HAWA VIWAVI ILIOWATUMA HAPA JAMVINI KUWATEA HAWANA HOJA WANAKURUPUKA .Serikali ya CCCM imekuwa ikiwapatia CDM mamilioni ya shilingi kama ruzuku ya chama hicho kujijenga kidemokrasia na kuleta chachu ya maendeleo nchini lakini CDM wamekuwa wakitumia fedha hizo za walipa kodi kwa kutalii mikoa kadhaa huku wakipoteza nguvu ya rasilimali watu, nchi hii inahitaji wachapakazi na wenye kuleta chachu ya maendeleo na si watalii.
Nazidi kushangaa wadau, kuna babu mmoja hapa nimekaa naye jirani anaonekana anawasubiri kwa mori viongozi wakuu wa chama, muda wote macho barabarani na jukwaani, naona pia kuna mama watu wazima wana mori sana pia na mabadiriko, kuna mabinti wenye wenye ari, akina mama wanazidi kuongezeka, wanavyoonekana wamekuja kwa dhamira za kweli kabisa, vijana ndo wengi zaidi, mabango yalikuwepo mengi sana, baadhi yalikuwa yana bedha hatua ya kujivua magamba ccm wakati nyoka ataendelea kuwa yuleyule, pia yamembedha shitambala kwa unafiki na njaa yake, uwanja unazidi kujaa kwa kasi hapa.