CHADEMA kufanya Maandamano Mbeya 20 Feb, maandalizi yakamilika

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mbeya kimesema kimekamilisha maandalizi ya kufanyika kwa maandamano ya amani yanayotarajiwa kufanyika Jumanne, Februari 20.2024 ambapo viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa wakitarajiwa kuongoza maandamano hayo

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Mbeya mjini Fokile Mwadende Shitambala wakati akizungumza na wanahabari katika Ofisi za chama hicho Kanda ya Nyasa jijini Mbeya kuhusu maandalizi ya maandamano hayo

Shitambala amesema tayari wamefanya maandalizi hayo kwa asilimia kubwa ambapo kutakuwa njia kubwa tatu za Mbalizi, Uyole na Isanga zikikusanya watu kwenda katikati ya jiji kisha mkutano wa hadhara katika uwanja wa Ruanda Nzovwe

Mwenyekiti huyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuungana pamoja kwenda kufikisha ujumbe wao kwa serikali ambayo anadai haizingatii haki na utawala bora wala kuheshimu haki za watu wake ambao ndio wenye nchi

Kwa upande wake Katibu wa CHADEMA mkoa wa Mbeya Hamadi Mbeyale amesema hali ngumu ya maisha, madai ya Katiba mpya na kupinga miswada mitatu iliyopitishwa Bungeni hivi karibuni sambamba na masuala mengine yanayokuwa kero kwa wananchi

Mbeyale amewaasa wananchi kujitokeza Februari 20.2024 ili kuandamana kwani ni haki yao kikatiba ambayo itawezesha kufikisha ujumbe wao.
 
Maandamano ya siku moja hayatabadili kitu, Ni sawa na carnival, aka mdundiko, mbeya waandamane kwa siku tatu usiku na mchana madai ya chadema yatasikilizwa. Lengo sasa liwe ni kusimamisha nchi.
 
Back
Top Bottom