Maandamano ya CHADEMA Jiji la Mbeya-Picha na Matukio

Ng'wanza Madaso

kaka umelowanisha msimamo?!!! hivi unadhani wildacard anajua anachokisema?......hana hoja ya msingi anajikwaruza tu ukutani hana lolote
 
Tumeshafungua Tawi Chuo Cha Teofil pamoja na ofisi ya Tawi hilo.Hivi sasa tuko robo ya safari kwa maandamano tukielekea uwanja wa Ruandanzovwe ambao watu wa Mbeya wameupata jina la uwanja wa Dr Slaa.Watu ni wengi sana,Polisi nao wametanda kila kona ya mji.Wamejaa hao.Kwa kweli hali ni nzuri sana na watu wanahamasa sana. Watu wa rika zote na jinsia zote wanaandamana kwa furaha kabisa.

Hakika Ukombozi Uko Njiani.

Kutoka Soweto.

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
 
mulikuwa munauhadaa ulimwengu kuwa Tanzania kuna demokrasia ya vyama vingi. Pumba (cuf, nccr, tlp, udp, nra, tadea, dp) zimejitenga.

chama cha siasa cha upinzani ndiyo hicho sasa kimejipambanua. mnatamani hata ruzuku ifutwe. lol!

na bado.

Na hata ruzuku ikifutwa cdm bado itaendelea kunawiri.
 
quote_icon.png
Originally Posted by WildCard

Halmashauri ipi hiyo. Mnatakiwa kufanya zaidi ya hizo halmashauri zenu. CHADEMA ni ya WATANZANIA wote. Natamani nisilipe kodi nchi hii ambako fedha zinagharamia siasa na wanasiasa kupita kiasi.

Wildcard kumbe hujui hata Halmashauri zinazoongozwa na Chadema? pole,,, sasa humu JF unafanya nini hata basic info za siasa hujui,,, nenda kwenye vijiwe kahawa nadhani ndio saizi yako... haya mabo nadhani yanakuzidi kimo

Serikali yetu masikini imekuwa ikiwapatia CDM mamilioni ya shilingi kama ruzuku ya chama hicho kila mwezi kujijenga kidemokrasia na kuleta chachu ya maendeleo nchini lakini CDM wamekuwa wakitumia fedha hizo za walipa kodi kwa kutalii mikoa kadhaa huku wakipoteza nguvu ya rasilimali watu kwa maandamano, nchi hii inahitaji wachapakazi na wenye kuleta chachu ya maendeleo na si watalii.

Babu wa Loliondo ameomba apelekewe wafungwa, ila hakuanisha ni wafungwa wa aina gani anawataka, yaweza kuwa ni wafungwa wa akili kama wewe gamba jipya. Hivyo subiri iwapo serikari itaridhia yaweza ukapata msaada wa kusafirishwa kwenda unyweshwe kikombe hata kwa nguvu.
Huna huruma na watanzania, na hulipi kodi yoyote.
 
Serikali yetu masikini imekuwa ikiwapatia CDM mamilioni ya shilingi kama ruzuku ya chama hicho kila mwezi kujijenga kidemokrasia na kuleta chachu ya maendeleo nchini lakini CDM wamekuwa wakitumia fedha hizo za walipa kodi kwa kutalii mikoa kadhaa huku wakipoteza nguvu ya rasilimali watu kwa maandamano, nchi hii inahitaji wachapakazi na wenye kuleta chachu ya maendeleo na si watalii.

Na ukizingtia ruzuku inatumiwa vibaya na watu wa makao makuu. Huku mkoa nilipo mie sio siri viongozi wa CDM wanalalamika sana ukizingatia hawana vitendea kazi, na ofisi zenyewe za shida wanadaiwa kodi za pango. Kwa kweli CDM makao makuu ijiangalie sana na haya maandamano yataleta mgawanyiko mkubwa sana kwenye chama !. Hivi fikiria pesa za maandamano laiti zingetumika kununulia vitendea kazi , tatizo hili lingepungua kwa kiasi kikubwa
 
Hizo za CCM ambazo zimetokana na kodi zetu na wizi wa rasilimali zetu zimewekezwa wapi?Au ndio zinatumika kuwalipa watu kama wewe kuwatete Mafisadi.CHADEMA wanatumie pesa waliyopata kama ruzuku kuwahamasisha wananchi ,kuwafumbua macho kwa wizi unaofanywa na mafisadi,kua karibu ya wananchi na kusikiliza matatizo yao.Ata wakiulizwa pesa ilitumika vipi watatoa maelezo.CCM inapata ruzuku kubwa zaidi ya CHADEMA,inatuibia rasilimali zetu,haifanyi mikutano wala maandamano.Waulize pesa zinakwenda wapi?Nape:" Nikwambie ukweli, hali ilivyo ndani ya Chama watendaji wanafanya kazi kwa mazoea. Hali ya uchumi katika Chama ni mbaya. Huwezi kuamini kwamba kwamba katika mazingira ambayo tuna mali zenye thamani takriban Sh bilioni 50, kinachoingia kwa maana ya mapato ni takriban Sh. bilioni moja hivi. Ni lazima sasa tujiimarishe katika sehemu zote; sio tu kimaadili na kisiasa lakini pia kiuchumi".Nape Mnauye akiojiwa na gazeti Raiamwema.

Mkuu nachojaribu kuelezea ni kwamba, kodi zetu wanazopewa kama ruzuku zitumike kwa utashi wa hali ya juu, wawekeze kwenye ofisi za majimbo, wilaya, mikoa na taifa, ili come 2015 wawe wametapakaa kiutendaji sio kuuza sura tuu.
 
MIE NIPO HAPA MBEYA WATU NI WACHACHE SANA, LEO WAMEFULIA; HUYO RM ANONA AIBU KUONYESHA PICHA ZA TUKIO. SHITAMBALA KAWAMALIZA:A S cry:

Uko Mbeya Sehemu gani kaka na hao watu wachache, mimi nipo hapa mama Joni, watu ni wengi balaaaa, sikuweza kuamini macho yangu. Kweli chama cha magamba wana kazi mwaka huu. Doo hii hatari sana, bendera, sare za Cdm na vidole juu ndivyo vilivyotawala. Kaazi kweli kweli
 
Mh Regia E Mtema, sisi wapenzi wa CDM tunapagawa zaidi tukipata picha ndani ya jukwaa hili, tubandikie picha kadhaa ili thread itembee zaidi.
 
Regia, mnapochelewa ku-upload picha mnatusababishia usumbufu wa kipuuzi kama huu hapa chini.

MIE NIPO HAPA MBEYA WATU NI WACHACHE SANA, LEO WAMEFULIA; HUYO RM ANONA AIBU KUONYESHA PICHA ZA TUKIO. SHITAMBALA KAWAMALIZA:A S cry:
 
Tumeshafungua Tawi Chuo Cha Teofil pamoja na ofisi ya Tawi hilo.Hivi sasa tuko robo ya safari kwa maandamano tukielekea uwanja wa Ruandanzovwe ambao watu wa Mbeya wameupata jina la uwanja wa Dr Slaa.Watu ni wengi sana,Polisi nao wametanda kila kona ya mji.Wamejaa hao.Kwa kweli hali ni nzuri sana na watu wanahamasa sana. Watu wa rika zote na jinsia zote wanaandamana kwa furaha kabisa.

Hakika Ukombozi Uko Njiani.

Comrade turushie japo picha mbili tujisikie kushirikishwa.
 
MIE NIPO HAPA MBEYA WATU NI WACHACHE SANA, LEO WAMEFULIA; HUYO RM ANONA AIBU KUONYESHA PICHA ZA TUKIO. SHITAMBALA KAWAMALIZA:A S cry:

Aibu yenu. Anguko lenu. Magamba mmeshajivua na sasa mmeanza kuchunana ngozi, ndo kifo chenyewe hicho.
 
Weka picha mkuu
kuna wapinzani humu washaanza kuleta maneno mbofumbofu,,,,,
 
Kuandamana ni kutoa hisia kupitia mkutano wa hadhara, unataka cdm ifanye nini wewe zuzu la siasa? Huoni mambo ambayo cdm wameishinikiza CCM na ikafanya pasipo utashi wao au nikukumbushe
1. Katiba
2. Kuwafukuza makamba na wenzie
3. Safari za JK kupungua kwa 90% (kwa kuwa hazikuwa na tija)
4. Kuwabana mafisadi (japo kisanii)
5. Kushusha bei ya sukari

Subiri ya Mbeya ujue tunashinikiza nini, pia ccm lazima itafanya kwani chadema ndio inaongoza nchi kwa remote control, nadiriki kusema Slaa ndiye Rais na Mbowe Waziri Mkuu

Arusha vipi siku 21 zimeisha mbona hakuna lolote tena mkuu ? mna piga magoti saa hizi kuwaomba serikali mfanye nao mazungumzo. Na mmekubali kuwa umeya ni wa CCM na nyie mnaomba japo unaibu meya mpewe nyie kwa miaka 4, na mwaka 1 awe TLP
 
Na muwaachie wana-Mbeya wachague wao mwenyekiti pasipo viongozi wa kitaifa kupindisha kanuni na kubatilisha maamuzi.
 
Tumeshafungua Tawi Chuo Cha Teofil pamoja na ofisi ya Tawi hilo.Hivi sasa tuko robo ya safari kwa maandamano tukielekea uwanja wa Ruandanzovwe ambao watu wa Mbeya wameupata jina la uwanja wa Dr Slaa.Watu ni wengi sana,Polisi nao wametanda kila kona ya mji.Wamejaa hao.Kwa kweli hali ni nzuri sana na watu wanahamasa sana. Watu wa rika zote na jinsia zote wanaandamana kwa furaha kabisa.

Hakika Ukombozi Uko Njiani.

Kutoka Soweto.

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Nimeipenda hiyo ya polisi nao kujiunga na maandamano.
Kila la kheri bros and sis'.
 
MIE NIPO HAPA MBEYA WATU NI WACHACHE SANA, LEO WAMEFULIA; HUYO RM ANONA AIBU KUONYESHA PICHA ZA TUKIO. SHITAMBALA KAWAMALIZA:A S cry:
Inawezekana upo Mbeya Sokomatola kwenye ofisi za ccm mkoa, hapo lazima pawe na watu wachache sana ama hawapo kabisa kwa sababu wana-Mbeya wote wenye kuipenda nchi yao wanaelekea Ruandanzovwe.
 
Back
Top Bottom