RC wa MBEYA atuhumiwa kuhujumu maandamano ya CHADEMA Mbeya

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amekuwa akiandaa njama za kudhoofisha maandamano ya chama hicho yaliyopangwa kufanyika jijini Mbeya Jumanne, Februari 20.2024

Akizungumza na wanahabari kwenye Ofisi za CHADEMA Kanda ya Nyassa zilizopo Kadege Mbeya leo, Jumapili Februari 18.2024 Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya nje wa chama hicho Taifa John Mrema ameeleza kuwa Homera kwa kushirikiana na baadhi ya wazee wa mkoa huo wamekusudia kuitisha kikao cha wanahabari ili wautangazie umma kuwa Jumanne, Februari 20.2024 wanakusudia kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya kimkakati jambo ambalo CHADEMA imetafsiri kuwa ni njama iliyoandaliwa ili wananchi wasitoke kwenye maeneo yao kushiriki maandamano

Mrema amesisitiza kuwa jambo hilo halijawastua kwa kuwa njama kama hiyo ilijitokeza walipoandaa maandamano ya kwanza Dar es Salaam ambapo Mkuu wa mkoa huo Albert Chalamila alitangaza siku iliyopangwa kufanyika maandamano ya CHADEMA kuwa siku ya usafi lakini mpango huo haukufanikiwa

Ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Machifu na wazee wa Mbeya kwa ushiriki wao katika kuhakikisha maandamano hayo yanafanikiwa sambamba na kufafanua kuwa chama hicho kinaratibu maandamano hayo kwa ajili ya umma.

Credit - JamboTv
 
Haiwezi kuwa kweli hayo mambo Rais ndio karidhia hakuna mteule wake wa kuweka vikwazo, hata polisi kutoa ushirikiano sio bahati mbaya. Ni vizuri kuwa na hoja za kisayansi
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amekuwa akiandaa njama za kudhoofisha maandamano ya chama hicho yaliyopangwa kufanyika jijini Mbeya Jumanne, Februari 20.2024

Akizungumza na wanahabari kwenye Ofisi za CHADEMA Kanda ya Nyassa zilizopo Kadege Mbeya leo, Jumapili Februari 18.2024 Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya nje wa chama hicho Taifa John Mrema ameeleza kuwa Homera kwa kushirikiana na baadhi ya wazee wa mkoa huo wamekusudia kuitisha kikao cha wanahabari ili wautangazie umma kuwa Jumanne, Februari 20.2024 wanakusudia kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya kimkakati jambo ambalo CHADEMA imetafsiri kuwa ni njama iliyoandaliwa ili wananchi wasitoke kwenye maeneo yao kushiriki maandamano

Mrema amesisitiza kuwa jambo hilo halijawastua kwa kuwa njama kama hiyo ilijitokeza walipoandaa maandamano ya kwanza Dar es Salaam ambapo Mkuu wa mkoa huo Albert Chalamila alitangaza siku iliyopangwa kufanyika maandamano ya CHADEMA kuwa siku ya usafi lakini mpango huo haukufanikiwa

Ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Machifu na wazee wa Mbeya kwa ushiriki wao katika kuhakikisha maandamano hayo yanafanikiwa sambamba na kufafanua kuwa chama hicho kinaratibu maandamano hayo kwa ajili ya umma.

Credit - JamboTv
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya awajibike kwa kudhamiria kwa makusudi kumdhalilisha Naibu Waziri Mkuu kwa kumpitisha kwenye njia iliyoruhusiwa Maandamo ya Chadema.
 
Back
Top Bottom