Lowassa strikes back!

Mkuu wa Kaya,sidhani kama Lowassa atakuwa radhi kusema ukweli wake katika hili. Ila pia bado sijaelewa ni picha gani ambayo inaendelea hapa. Ngoja tutafika tu mwisho wake maana si ndio likizo ya kuomba kazi tena wameshaianza...

Mkuu Lusajo,

Mzee Mwanakijiji aliwahi kuota hii njozi!
Naona kama ana kipaji cha kufunuliwa vile.... maana picha invyoanza inaelezea mwisho wake...

Kweli bongo tambarare.
 
PM..

a. kwanini Lowassa hakutoa hoja Bungeni siku ile asubuhi na kutaka Bunge liahirishwe ili aweze kupitia hoja za wabunge zilizotolewa jana yake na kutoa majibu?

b. Kwanini hakutoa hoja kuishutumu kamati teule kuwa haikumpa nafasi ya kujitetea na kuomba Spika ampe muda mbele ya Kamati hiyo iweze kumhoji kabla haijachukuliwa hatua nyingine?

c. Kwanini Lowassa baada ya kuona Bunge limegawanyika hakutoa utetezi wake wa kile alichokifanya/kutokifanya kuhusu Richmond na baadaye kutaka Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani naye?

d. Kwanini licha ya kutoitwa na Kamati Teule, Lowassa hakujitetea mbele ya Bunge ambalo ndilo lilikuwa na nguvu na lina nguvu kama Kamati Teule kwa mujibu wa Kanuni za Bunge? Kwa kukataa nafasi yake ya kujitetea mbele ya Bunge (aidha kama Bunge au kama Kamati) yawezekana alijinyima yeye mwenyewe nafasi ya kujitetea aliyoiomba na kupewa?

...mzee wapinzani wa mtandawo walikuwa wamejipanga kweli kweli....na aina yoyote ya kujitetea asingeeleweka...na rais alishafanywa behind the scene ashindwe au aogope kumtetea ......so Mwanajijiji in general Taarifa za kijasusi alizopewa Lowassa kuhusu hali halisi zilimshtua sana..na zilikuwa za ghafla....ie Plan B ya kina Mwakyembe ilikuwa tishio kwa utawala mzima...

...naamini kabisa Lowassa angepata taarifa mapema ya kinachopangwa ....angekuwa waziri mkuu hadi leo ...kwani hata angepata taarifa ndani ya masaa 24 au 48 kabla ya tukio ...angekuwa na uwezo wa kubadilisha kabisa..hali ile na kuwapanga watu wa kumtetea na namna ya kujitetea au hata lolote lingeweza kutokea ......ni wazi tume ya Mwakyembe ilichomudu ni USIRI mkubwa!!!
 
Kwa kweli si kila mwenye uwezo wa kuandika anapaswa kuandika hata mambo hasioyajua...huyu ni mmoja wapo.................1.Anadai hapa kuwa kuna mtu alikuwa anamlazimisha injinia manyanya apitishe memo???????????how mbunge anapitisha memo ya waziri mkuu kwa ujinga wake anadhani manyanya alikuwa ni mtendaji pale tanesco wakati wa tanesco,...........2Hajasikiliza sijui au hajaelewa maelezo kuwa ni kweli alipush mchakato uende kwa haraka kwa kuwa tishio la umeme ni kubwa lilikuwa na anaamini ulikuwa ni wajibu wake
Fisadi Mtoto sikiliza, injinia Manyanya alikuwa bado mfanyakazi wa Tanesco hata alipokuwa mbunge. Alipoingia katika kamati ya Mwakyembe ndipo alijiuzuru kazi.

Na wewe usiandike mashambulizi bila kufanya utafiti wako kuhusu ukweli wa unachoandika.
 
Wakuu wangu, hata tufanye nini the EL is back. Tena kwa nguvu kubwa kama tetemeko la HAITI.

Watch and see. Unadhani hakukuwa na makubaliana kabla ya JK kuchukua fomu? Wacha tununue pop corn movie ndo kwanza lianaanza.

Tatizo letu tunaongea sana, hadi mapovu yanatutoka mdomoni, kwanini hatutaki kuchukua hatua? Watu wakijaribu tu, sisi wenyewe tunawarudisha nyuma. Hatutaki kusaidiana kujenga base kubwa ya kuwashawishi wapiga kura wa nchi hii. CCM wanajua udhaifu wetu watatuchapa tu....
 
bado anasimamia masuala ya richmond na anasema pasipo utata kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu ulikuwa ni sahihi na jinsi alivyoshughulikia suala la richmond hakuna ambacho angebadilisha "hata chembe".

Mzee wa kijiji nahisi ile ripoti ya Mwakyembe ilikuwa ya kimazingara na ilikuwa na mapungufu fulani na ililenga jambo ambalo mpaka leo sijui msingi wake.

Jana EL kasema kuwa kulikuwa na mgogoro na anampongeza sana Mwinyi kwa kufanikiwa kupunguza siasa za chuki ndani yao. Kama Mwinyi aliridhika kuwasuluhisha bila kumtaka EL awaombe msamaha waTZ, basi ana haki ya kutetea alichokianzisha na hasa njia za utatuzi wa sakata la umeme.

Naona bado ana nguvu hasa na sijui nani atakayeweza kumsimamisha safari hii.
 
Atamaliza sabuni tu, labda akaoge kwenye tindikali ndio atasafishika! Baba wa ufisadi, Richmond ni matokeo ya baraka zake and he knew every thing and he was party of the deal!
 
wANA JF, NIMESHINDWA KUMWELEWA HUYU NDUGU KUWA ALIKUWA NA AKILI TIMAMU AU LA, NIMESHINDWA KUELEWA JINSI ANAVYOISIFIA RICHMIOND KAMA NDIYE YEYE KWELI ALISEMA KAONEWA. hABARI KAMILI, TIZAMA TBC1 SAA 2 NA NUSU USIKU HUU MAOJIANAO NA TIDO MUNDA YATARUSHWA LIVE. mLIOKO NYUMBANI TUJUZENI BAADA YA KUTAZAMA
NAJISIKIA UCHUNGU SANA .
Mimi nimeskiliza vizuri sana mheshiwa na nilivyomuelewa ni kuwa katika mazingira tuliyokuwa nayo kipindi kile na maamuzi aliyoyachukua hali kama hali ile ingejurudia tena kwa mazingira yaleyale angechukua hatua zilezile alizochukua wakati ule
 
..Lowassa is right hakutendewa haki...wekeni ushabiki kando....kauli ya Mwakyembe ya kumtaka achague mwenyewe ..wakati wanajuwa hawakumuhoji ilikuwa ya kiuonevu.....kama hawakumuhoji hawakuwa na haki ya kumuambia aamue hatima yake!!!

Lakini lazima mjue Lowassa aliokoa serikali nzima ya Kikwete kuanguka...kama angeng'ang'ania madaraka tulikuwa tunaelekea kutokea uchafuzi wa hali ya
hewa.......wanamkakati wapinzani wa Kikwete ndani ya chama kwa kujua kuwa Lowassa ndie alikuwa robot ya mtandao ....lengo lao lilikuwa kuangusha serkali ya Kikwete na kufanikiwa kujiuzulu kwa Lowassa ...lengo lilikuwa ni kuidhoofisha serikali ya Kikwete......

Naafikiri Kikwete na Lowassa ...they could achieve more together than what is claimed to be achieved today.....Lowassa anamjua vema Kikwete na udhaifu wake na alikuwa akiweza vema kuziba nyufa...ndio maana ....serikali ya Kikwete iliweza kuvuka ile miaka miwili migumu ya mwanzo....na bado wakaweza kujenga shule kila kata.............

Tusiwe wachoyo wa fadhila ......kwa kikwete na lowassa...as a team...

U
kiangalia kwa sasa kikwete anapwaya kwa sababu bado PINDA Hajamudu kuelewana vema ni Kikwete kikazi..... Pinda ni conservative ....civil servant, wakati Kikwete ni chakaram....sasa ukizingatia tena Shein ana sifa kama za Pinda .....basi kidogo imeleta gap......i mean wasaidizi wa rais mpole kama JK .....wanatakiwa wawe na ushawishi mkubwa .....na nguvu ya kisiasa....

Haya maelezo ni matamu sana. Na uhalisia wake unawezekana pale tu, kazi/cheo kinapotolewa kishkaji. Vinginevyo ni vigumu sana kuyamkinika
 
Hivi unajua dhana ya uwajibikaji na utawala bora? May be tuambie wewe the best case/ worst case scenario ilitakiwa nani awajibihswe na malaika lowaasa abaki?

Na ukiseama JK na EL can achieve More 2gether una maanisha Personal achievement ??? Au kwa kuwa Lowassa akiitisha harambee ya kujenga shule basi zinakusanywa bil 1 na akiitisha Pinda au Shein basi vinakusanywa vimilioni vichache. Unasema Lowasa anamjua sana Kikwete na Udhaifu wake . Uki reverse hiyo reaction inaweza kuwa JK anamjua sana Lowassa na Uchu wake wa madaraka.

If it was Pinda ningemuelewa kuwa aliingizwa mjini. lakini mtu smart kwenye utendaji kama tulivyoaminishwa na mwenye network kubwa mambo yemehaibika anasema hausiki. Inachekesha sana. Akubali hiyo ni part of collective responsibility
 
Ebo,

Kumbe PM ni mpiga debe mkuu wa kisiasa na anajua siri zote za mambo yanayohusu Lowasa na utawala wa Kikwete kwa jumla?
 
Lowassa ameanza kampeni .....

na akirudi anachukua nafasi yake ya waziri Mkuu
 
Hivi ni lazima EL awe Rais ???
Si naskia ana mijisenti... awe Mjasiariamali...
Hata akiupata huo U-Rais anaoutolea macho utakuwa cursed...
Come Oct 30...
 
Hivi ni lazima EL awe Rais ???
Si naskia ana mijisenti... awe Mjasiariamali...
Hata akiupata huo U-Rais anaoutolea macho utakuwa cursed...
Come Oct 30...

Kwa EL Urais ni moja kati ya Agenda zake kubwa, Inaonekana kuwa kuna makubaliano fulani kati ya muungwana na EL, Sasa yanafanyika sasa ni kumuosha ili awe safi na wakati wa kuuzwa ukifika basi asiwe ananuka tena.
 
lakini bwana EL ana roho ngumu kweli kweli
Mmasai yule! Ndo sifa za mwanaume wa kimasai kuwa mgumu na mvumilivu hata akipigwa sime au mkuki. Na alama ya nje ya ujasiri wao ni circumcision bila ganzi! Upo hapo!
 
Mmasai yule! Ndo sifa za mwanaume wa kimasai kuwa mgumu na mvumilivu hata akipigwa sime au mkuki. Na alama ya nje ya ujasiri wao ni circumcision bila ganzi! Upo hapo!

Kama ana roho ngumu kweli kweli ya Kimasai (pamoja na Umasai wake kuwa na utatata) kwa nini alijiuzulu? Aliwekewa bastoal kichwani? Angekataa kujiuzulu na kupigana kijasiri (kama kweli ni jasiri) akiwa humo humo ndani na tungeona iwapo swahiba wake angemtimua au la. Hana ujasiri wowote!
 
Wadau huyu mtu alipewa nafasi yakujitetea on the spot lakini aliishia kusema nimeonewa sana namedhalilishwa sana nakadhalika nakadhalika...... Sasa sisi tumueleweje? Huyu jamaa ni msanii kwa kweli. Lets wait! will see.
 
Na afadhali basi yule mwenzake (No 3 katika ile triumvirate) -- RA. Immediately baada ya ripoti ya Mwakyembe kuanikwa huyu aling'aka na kusema kaonewa na kupanga kutoa hoja Bungeni. Huyu anayekazania kuwa ni Mmasai yeye alitimkia Monduli na kujigharamia sherehe kubwa ya mapokezi! -- kwamba ni shujaa, kumbe kule Bungeni hakuonyesha ushujaa wowote.
 
Mimi nadhani hata Muungwana hamtaki swahiba wake kurithi kiti 2015. Angekuwa anataka, angefanya juu chini Dr Bilal (aliyekuwa anapigiwa debe na RA na EL) kupata uteuzi wa kugombea urais wa Zanzibar. Kwani strategy ya RA na EL ilikuwa kwamba kama Rais wa Zanzibar, Dr Bilal angekuwa Vice Chairman wa CCM, nafasi ambayo ingemuwezesha ku-control wajumbe wengi kutoka Visiwani wa NEC na General Congress ya CCM ili (pamoja na wengine wa Bara) kuweka nguvu ya kumpitisha EL mwaka 2015.

Bilal kukosa nafasi hiyo ni pigo kubwa kwa mikakakti ya akina EL na swahiba wake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom