Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Mimi nadhani hata Muungwana hamtaki swahiba wake kurithi kiti 2015. Angekuwa anataka, angefanya juu chini Dr Bilal (aliyekuwa anapigiwa debe na RA na EL) kupata uteuzi wa kugombea urais wa Zanzibar. Kwani strategy ya RA na EL ilikuwa kwamba kama Rais wa Zanzibar, Dr Bilal angekuwa Vice Chairman wa CCM, nafasi ambayo ingemuwezesha ku-control wajumbe wengi kutoka Visiwani wa NEC na General Congress ya CCM ili (pamoja na wengine wa Bara) kuweka nguvu ya kumpitisha EL mwaka 2015.
Bilal kukosa nafasi hiyo ni pigo kubwa kwa mikakakti ya akina EL na swahiba wake.
Kama ni kweli usemayo, kweli ni pigo kubwa. Lakini hapajaharibika kitu kwani cheo cha Umakamu wa Urais wa Jamhuri ni only one step of becoming full President, according to the Union Constitution. Chochote chaweza kutokea, Mungu apishie mbali!