Lowassa strikes back!

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
wANA JF, NIMESHINDWA KUMWELEWA HUYU NDUGU KUWA ALIKUWA NA AKILI TIMAMU AU LA, NIMESHINDWA KUELEWA JINSI ANAVYOISIFIA RICHMIOND KAMA NDIYE YEYE KWELI ALISEMA KAONEWA. hABARI KAMILI, TIZAMA TBC1 SAA 2 NA NUSU USIKU HUU MAOJIANAO NA TIDO MUNDA YATARUSHWA LIVE. mLIOKO NYUMBANI TUJUZENI BAADA YA KUTAZAMA
NAJISIKIA UCHUNGU SANA .
 
Lowassa ana kila haki kutafuta haki yake katika hili jambo. Nimekuwa nikiwaeleza hapa jamvini toka mwanzo kwamba Lowassa alionewa katika hili suala, hakupewa muda kabisa wa kujieleza mbele ya tume ya Mwakyembe. Tume ya Mwakyembe ilikuwa na madaraka ya kumuita mtu yeyote bila kujali cheo, rangi, kabila wala mali kwani ilipewa mamlaka hayo na Mkuu wa nchi.

Kwanini tume Iliweza kuwasikiliza na kuwatembelea watuhumiwa wote isipokuwa Lowassa?. Jamani huwezi kumuhukumu mtu bila kumsikiliza ama kumpa nafasi ya kujieleza. Na ningeomba muelewe kwamba uzuri wa shillingi ni kuiangalia pande mbili na wala si pande moja. Welldone Lowassa.
 
Lowasa tena!
Bado yumo tu.
Laiti ningepata nafasi ya kumshauri, ningemwambia aachane na siasa, imetosha sana.
 
wANA JF, NIMESHINDWA KUMWELEWA HUYU NDUGU KUWA ALIKUWA NA AKILI TIMAMU AU LA, NIMESHINDWA KUELEWA JINSI ANAVYOISIFIA RICHMIOND KAMA NDIYE YEYE KWELI ALISEMA KAONEWA. hABARI KAMILI, TIZAMA TBC1 SAA 2 NA NUSU USIKU HUU MAOJIANAO NA TIDO MUNDA YATARUSHWA LIVE. mLIOKO NYUMBANI TUJUZENI BAADA YA KUTAZAMA
NAJISIKIA UCHUNGU SANA .

Haaaaa! Kumbe mkakati wa kutushangaza ndo umeanza? ama kweli inji hii inawenyewe.
Yaani TBC ya kodi zetu ndo yakusafishia nomino kwa wezi wetu? yaani milioni 152 kwa siku?
 
Lowassa hakuitaji tume wala nini; alitakwa kujiuzulu kabla hata tume haijaundwa.

Hapo ndipo Lowassa anaponyimwa haki yake. Kwanini basi tume iliundwa?. Kwanini tume iliweza kuwaita na kuwatembelea wahusika wote wa nje na ndani ya Tanzania na kumwaacha Lowassa aliyekuwa na ofisi mtaa pili tu toka ofisi ya tume hiyo?.

Jamani, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Welldone Lowassa, kaza buti mpaka kieleweke.
 
Kidatu.. unajua madaraka ya waziri mkuu kule Bungeni na nafasi yake? Kama hakutendewa haki alitakiwa kulazimisha haki itendeke kwake badala ya kuweka manyanga chini. Kwani alipigiwa kura ya kutokuwa na imani? Lowassa ni mzungumzaji mzuri angeweza kabisa kujenga hoja na kulaizmisha bunge lipige kura ya kuwa na imani naye au la hakufanya hivyo. Aliamua kuweka manyanga chini.

Lowassa alijionea mwenyewe na kujidhulumu mwenyewe. Jaribio lolote la kuhamisha lawama toka kwa Lowassa litashindwa kabla halijajaribiwa.
 
Lowassa ana kila haki kutafuta haki yake katika hili jambo. Nimekuwa nikiwaeleza hapa jamvini toka mwanzo kwamba Lowassa alionewa katika hili suala, hakupewa muda kabisa wa kujieleza mbele ya tume ya Mwakyembe. Tume ya Mwakyembe ilikuwa na madaraka ya kumuita mtu yeyote bila kujali cheo, rangi, kabila wala mali kwani ilipewa mamlaka hayo na Mkuu wa nchi.

Kwanini tume Iliweza kuwasikiliza na kuwatembelea watuhumiwa wote isipokuwa Lowassa?. Jamani huwezi kumuhukumu mtu bila kumsikiliza ama kumpa nafasi ya kujieleza. Na ningeomba muelewe kwamba uzuri wa shillingi ni kuiangalia pande mbili na wala si pande moja. Welldone Lowassa.

sikiliza ndugu yangu. Tume ile haikuwa na mamlaka ya kumtoa Lowasa madarakani; jukumu lake lilikuwa ni kutafuta ukweli. Lowasa alijiondoa madarakani ili kujizuia na aibu iwapo tume itatoa hadharani mambo ambayo yalikuwa yanamhusu yeye. Kuna wakati tuliilaumu ile kamati kwa vile ilikiri kuwa kuna mambo ambayo hawakuyatoa hadharani kulinda heshima ya serikali.

Asiyekubali kushindwa si mshindani.

Kwanini alijiuzuru wakati anajua anasimamia ukweli?
Good questions
 
Hivi kwa nini wanasiasia wote:

  • neno smahani /sorry kwao ni gumu sana. Hata kwenya hotuba ya JK bungeni umeona hili. subiri mwaka 2015 utasikia ana generalise kuomba kusamehewa pale alipokosea kama alivyofanya Ben Mkapa

  • Kwanini wanasiasa hawana utamaduni wa kuonyesha kuwajibika?
  • Kwa nini wanasiasa wote wanataka waonekane kama malaika?
Kumjua mwanasiasa yeyote mkweli na Honest swali hili ni muhimu
Maamuzi /ushauri gani mbovu aliwai kufanya/kutoa?

Sijui kama Tido Mhando alimuuliza swali hili? Na
 
wANA JF, NIMESHINDWA KUMWELEWA HUYU NDUGU KUWA ALIKUWA NA AKILI TIMAMU AU LA, NIMESHINDWA KUELEWA JINSI ANAVYOISIFIA RICHMIOND KAMA NDIYE YEYE KWELI ALISEMA KAONEWA. hABARI KAMILI, TIZAMA TBC1 SAA 2 NA NUSU USIKU HUU MAOJIANAO NA TIDO MUNDA YATARUSHWA LIVE. mLIOKO NYUMBANI TUJUZENI BAADA YA KUTAZAMA
NAJISIKIA UCHUNGU SANA .
No matter how the issue is ? we real need Lowassa to expose each and every thing out, Kwani Richmond walishazika Mbungeni bila kujua Mkosaji ni nani, itakuwa jambo lamaana kama Lowassa atasema ukweli.
 
Mkuu wa Kaya,sidhani kama Lowassa atakuwa radhi kusema ukweli wake katika hili. Ila pia bado sijaelewa ni picha gani ambayo inaendelea hapa. Ngoja tutafika tu mwisho wake maana si ndio likizo ya kuomba kazi tena wameshaianza...
 
WanaJF mliopo Nyumbani, kwenye maojiano na TBC1 , Mh.waziri mkuu mstaafu kasemaje kuhusu rich mond?
 
Namwangalia hapa.. he is coming back for sure! anajitahidi sana.. nadhani ilirekodiwa baada tu ya Mkutano Mkuu..
 
anapewa ujiko wa ujenzi wa shule za sekondari huku Mhando akidai baada ya Lowassa kuondoka msisimko wa ujenzi umepungua; Lowassa anasema hana uhakika umepungua kwa kiasi gani.
 
Yeye anasahihisha kauli mbiu ya JK kuhusu "Kilimo kwanza" yeye anasema ni "Elimu kabla, kilimo kwanza".. anasema ni lazima tuanze na elimu na siyo kilimo. Hatuwezi kufundisha watu kilimo kwanza kama hawana elimu.
 
bado anasimamia masuala ya richmond na anasema pasipo utata kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu ulikuwa ni sahihi na jinsi alivyoshughulikia suala la richmond hakuna ambacho angebadilisha "hata chembe".
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom