Lowassa strikes back!

aliwajibika kwa makosa ya watu wengine si ya kwake kwani "hata mkiniamsha usingizini leo nitafanya maamuzi yale yale"
 
kwa kweli i hope.. TBC watawapa kina Mwakyembe nafasi ya kujibu hoja zao.. kwani bado anaamini kuwa suala zima lilikuwa ni "Uwaziri Mkuu", na anasema aliwajibika kwa makosa ya watu waliochini yake na kuwa yeye yuko "clean"

Na anaamini ilikuwa ni suala la uwaziri kuu wa lowassa
 
anasema wabunge wapinzani wachache ndiyo wamekuwa na mchango bungeni.. lakini zaidi ni wabunge wa CCM "ndiyo wamefanya kazi sana". Anatabiri kuwa CCM itakuwa na wabunge wengi zaidi kuliko 2005 na JK atashinda kwa zaidi ya kura za 2005.
 
Ni msafi kwa lipi wakati vimemo vya kuarakisha mchakato huo mchafu wa kupata richmond alisign yeye? Ni nanai alikuwa anamlazimisha injinia Manyanya apitishe ila akakuta mama ameona mbali?
 
Ni msafi kwa lipi wakati vimemo vya kuarakisha mchakato huo mchafu wa kupata richmond alisign yeye? Ni nanai alikuwa anamlazimisha injinia Manyanya apitishe ila akakuta mama ameona mbali?

Kwa kweli si kila mwenye uwezo wa kuandika anapaswa kuandika hata mambo hasioyajua...huyu ni mmoja wapo.................1.Anadai hapa kuwa kuna mtu alikuwa anamlazimisha injinia manyanya apitishe memo???????????how mbunge anapitisha memo ya waziri mkuu kwa ujinga wake anadhani manyanya alikuwa ni mtendaji pale tanesco wakati wa tanesco,...........2Hajasikiliza sijui au hajaelewa maelezo kuwa ni kweli alipush mchakato uende kwa haraka kwa kuwa tishio la umeme ni kubwa lilikuwa na anaamini ulikuwa ni wajibu wake
 
Fisadi Mtoto,
Naona umerudi kwa kasi kuwatetea wakubwa wako. Lowassa alikuwa anatawala kwa vitisho. Kama uamuzi haukubaliani na utashi wake alikuwa analazimisha utashi wake ufuatwe au uachishwe kazi. Hatuhitaji mtu kama huyu kushika usukani wowote wa uongozi katika nchi yetu.
 
...hivi kwani alihukumiwa/alishinikizwa na Kamati kujiuzuru au aliachiwa APIME NA KISHA AAMUE?!
..Lowassa is right hakutendewa haki...wekeni ushabiki kando....kauli ya Mwakyembe ya kumtaka achague mwenyewe ..wakati wanajuwa hawakumuhoji ilikuwa ya kiuonevu.....kama hawakumuhoji hawakuwa na haki ya kumuambia aamue hatima yake!!!

Lakini lazima mjue Lowassa aliokoa serikali nzima ya Kikwete kuanguka...kama angeng'ang'ania madaraka tulikuwa tunaelekea kutokea uchafuzi wa hali ya
hewa.......wanamkakati wapinzani wa Kikwete ndani ya chama kwa kujua kuwa Lowassa ndie alikuwa robot ya mtandao ....lengo lao lilikuwa kuangusha serkali ya Kikwete na kufanikiwa kujiuzulu kwa Lowassa ...lengo lilikuwa ni kuidhoofisha serikali ya Kikwete......

Naafikiri Kikwete na Lowassa ...they could achieve more together than what is claimed to be achieved today.....Lowassa anamjua vema Kikwete na udhaifu wake na alikuwa akiweza vema kuziba nyufa...ndio maana ....serikali ya Kikwete iliweza kuvuka ile miaka miwili migumu ya mwanzo....na bado wakaweza kujenga shule kila kata.............

Tusiwe wachoyo wa fadhila ......kwa kikwete na lowassa...as a team...

U
kiangalia kwa sasa kikwete anapwaya kwa sababu bado PINDA Hajamudu kuelewana vema ni Kikwete kikazi..... Pinda ni conservative ....civil servant, wakati Kikwete ni chakaram....sasa ukizingatia tena Shein ana sifa kama za Pinda .....basi kidogo imeleta gap......i mean wasaidizi wa rais mpole kama JK .....wanatakiwa wawe na ushawishi mkubwa .....na nguvu ya kisiasa....
 
sijataka mtu yeyote atetewa hapa lakini nataka watu wajenge hoja amabazo wanazielewa...........lazoma ata wewe uwe objective
 
Fisadi Mtoto,
Naona umerudi kwa kasi kuwatetea wakubwa wako. Lowassa alikuwa anatawala kwa vitisho. Kama uamuzi haukubaliani na utashi wake alikuwa analazimisha utashi wake ufuatwe au uachishwe kazi. Hatuhitaji mtu kama huyu kushika usukani wowote wa uongozi katika nchi yetu.
Nchi hiii inahitaji dikteta wa kiasi....apeleke watu mchakamchaka.......kubalini kataeni..sio lazima Lowassa, yeyote ambaye ni serious ...sio wauza sura na wanaojipodoa kama kina Membe.[aka: nyoka wa mdimu] maana ndiye anategemea urais 2015..na ameshaanza kujiandaa na kumuandaa mkewe kuwa first lady.....
 
Inashangaza mbado kuna wananchi misukule bado wanaitetea hii misukule origino pamoja na HASARA KUBWA walituingizia taifani. HII INAGHADHABISHA SANA.
 
Jamaa wajanja sana. Wamesubiri Bunge linaelekea ukomo wake ndipo wameanza kurusha mahojiano ya kujisafisha maana wanajua wangerusha kabla, swala lingerudi mjengoni na huenda mambo yangekuwa mabaya zaidi.

Lakini sasa wana uhakika kwamba hata wakiropoka hakuna kitakachorudi mjengoni. Come Nov 2010, Bunge litakuwa chini ya uongozi wa Spika mpya, ndipo sasa Richmond itakaporudishwa Bungeni Upya ili kukamilisha shughuli ya usafi na kuweka sawa mazingira kwa ajili ya 2015.

Kwa jinsi wabunge wetu wa CCM walivyo, wala sintashangaa iwapo watakaa kimya pindi ngoma ikirudishwa mjengo hapo 2011. Maana sijawahi kuona wabunge wa ajabu kama hawa wa CCM. Leo wanaweza kupitisha azimio/maamuzi fulani na serikali ikigoma kutekeleza, wao wanaufyata.

Kikwazo cha kurudisha hoja ya Richmond Bungeni ilikuwa ni Spika Sitta, kwa kuwa yeye anajinadi kuwa ni Mzee wa Kasi na Viwango, na kwamba ni mpambanaji wa ufisadi, asingekubali kurudisha hiyo hoja kwa ajili ya kumsafisha Lowassa. So, the right time is March/April 2011 chini ya Uongozi wa Spika Mpya na utasikia wanasema Lowassa alionewa. Wakati huo, si ajabu wajumbe wote waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mwakyembe watakuwa hawako mjengoni tena.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom