Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 38
Mulama, kuoa ni jambo jema kwa jamii na kwa wawili wapendanao. Kuna halalisha na kuhakikisha kuwa, watoto watakaopatikana kwenye ndoa watapata malezi bora zaidi. Na pia kunathibitisha uwezo, na nia ya wawili kuendelea kupendana, kuvumiliana na kuheshimiana.
Ndoa ni mzigo kwa wanaoingia bila kuwa na sababu za msingi za kufanya hivyo. Kuingia kwenye ndoa ili kuifurahisha jamii peke yake, ni sawa na kujinyima furaha ya maisha. Ndoa lazima itokane na nia thabiti inayosukuma mioyo ya watu wawili kuona maisha bila kuwa karibu hayana raha. Ndoa ya namna hiyo haizuiliki.
Mulama, sio lazima kwa yeyote kuoa au kuolewa. Mtu anaweza na ni haki yake kuamua aina ya maisha anayotaka kuishi (ndoa au bila ndoa). wapo watu wengi walioteseka sana ndani ya ndoa, na wapo waliofurahia sana kuwa ndani ya ndoa. Maisha ni kupanga, na kupanga ni kuchagua.
Ili kuwa na watoto, si lazima kuoa au kuolewa. Hakuna ndoa iliyofungwa wakati Adam na Hawa walipopewa amri ya kwenda na kuijaza dunia. Lakini ili maisha yawe ya kistaarabu, na ili watoto wapate malezi bora, ni vyema wawili wenye nia ya kuzaa wakaoana.