Jaribio la kuiba dhahabu katika mgodi wa Geita (GGM) lazimwa

siku ingine wakitaka kufanya tena watuupdate ili tutoe ushirikiano,siyo vizuri kufeli kuchukua hizo dhahabu zetu alizotupa mungu kutoka kwa hao makaburu
 
Mhhh hizo kilo nyingi kweli! mbona sijasikia afisa wa TRA au TMAA aliyejeruhiwa...je ni free export?
 
I think next time they will come with better tactics and get away with the dough!
Hao waliokufa nawaita MASHUJAA!
Atakaye hachoki!
Aisee, hii mitizamo si ya kuifagilia kabisa. Majambazi wenyewe usishangae ni wasomali au wakenya or wanyarwanda. Na walijua kabisa kwamba pale kuna walinzi, watanzania wenzao, ilikuwaje hadi wajitose na maslaha makubwa makubwa kiasi hicho kwenda kuwazuru watanzania wenzao. Wizi ni wizi tu wakuu, hakuna cha kufagilia hapa.
 
Hii inatisha!
hivi serkali haiwezi kuitaifisha na kumiliki migodi yote inayomilikiwa na wageni?

Unasemaje? Wazungu watatuita majina yote mabaya, na watatumia baadhi yetu kutupiga na kutubebesha madeni makubwa kama ya NTC Libya! ikishafikia hapo hata mfumko wa bei, vitu kupatikana itakuwa nouma. Inabidi kujipanga kabla ya kuitafisha.
 
Mhhh hizo kilo nyingi kweli! mbona sijasikia afisa wa TRA au TMAA aliyejeruhiwa...je ni free export?
Hawawezi kuwapo hao, kwa nini wawepo wakati Ngereja,Jairo,Jakaya wameshachukua mgao wao,sii wamekataa kulipa kodi bwana
 
Duh, kilo 816 ni USD ngapi? Hii itakuwa imewapa uzoefu fulani hawa jamaa, wakajipange waangalie ni wapi wamefanya makosa, wakifanikiwa next time inaweza kuwa neema kwetu kama hiyo pesa itawekezwa TZ badala ya kwenda kunufaisha makaburu huko south.
 
Yule mzungu aliyejeruhiwa ameshapaishwa kuelekea NAIROBI kwa matibabu, jamaa alimtupia risasi kama tatu hivi ila ni kwenye mguu na mkono,huyo ndie aliyemuua jambazi mmoja.
 
Wangechukua ingekuwa safi sana,maana tunaachiwa mashimo tu kaburu anaondoka na mali.Kiukweli inauma sana.
 
Bad move, gold ni nzito sana kuweza kuisafirisha kutoka kati namna hiyo, labda kama waliandaa usafiri wa anga. Id go for Diamonds pale mwadui wale jamaa wanasema wanaendesha mgodi kwa hasara na hawaachi mwaka hadi mwaka. Ambaye yuko interested aseme! hahahaa
 
Dhahabu hiyo tofali 34 zenye kilo 24 kila moja jumla ni kilo 816. Thamani yake ni dola 442340564.17 sawa na bilionsh.688 na zaidi je trip hizi wanafanya "mara ngapi kwa mwezi na je royalty ya asilimia nne imelipwa na cooperate tax wameanza kulipa !
 
Naona baadhi ya Watanzania wameamua kuchukua mali yao directly kwani hawanufaiki nayo.
Ingawa hawakutakiwa kuua.
 
SI kweli kuwa watanzania wengi hatuwapendi wawekezaji. Ukisoma kati ya mistari ya michango ya wanabodi hapa utaona kuwa kinachochukiwa zaidi ni taratibu za kuwapatia hayo marasilimali na badala ya kuwa wawekezaji wamegeuka kuwa wawekezwaji. Nchi masikni lakini inaruhusu capital flight. Hata matajiri wamerekani na wachina wa siku hizi hawawezi kuruhusu upuuzi huu kutendeka nchini mwao.
Kwa mujibu wa post nilizosoma hapa,wachangiaj weng(hasa walojinasibisha na utanzania)walitaka gold ibebwe na majambaz,hili ni changam0to kwa serikali,watanzania wengi hatuwapend wawekezaj na uwekezaj,wadau boreshen sera za uwekezaji
 
I see nchi inaliwa hii yaani vitofali 34 na kila kitofa kina kilo 24kg sijui TRA wapo? au wapo kwa kazi ya kufukuzana na wauza viosk mitaani?

Kwaufupi ni kama bil 65.3, simchezo, next time inabidi warudie na silaha kali zaidi zikiwemo silaha za kutungua ndege au hata ikibidi JWTZ waonyeshe uzalendo wao kwakutumia yale masilaha waliotuonyesha siku ya uhuru.
 
Mhhh hizo kilo nyingi kweli! mbona sijasikia afisa wa TRA au TMAA aliyejeruhiwa...je ni free export?

Waliokuwa wanaiba ndio hao wanaosafirisha kwa ndege. Je wamelipia kodi kiasi gani hili liinchi bwana ngoja aje mkombozi 2015.
 
Wasingekuwa wameiba wangekuwa wamechukuwa mali yao kuliko ikataifishiwa S A
 
Back
Top Bottom