Jaribio la kuiba dhahabu katika mgodi wa Geita (GGM) lazimwa

hii habari ni mpya na inaibua mawazo mapya pia!
Kwani katika tafsiri na uelewa wa kawaida, kati ya hawa wawili nani hasa ni mwizi!?
Na kama upande 'ulioshindwa' ni waliotaka kuzuia madini yasisafirishwe nje ya nchi ili wayafaidi wao, basi ni wapi Watz wengi wataegemea!?
 
Angalau watu wenye kuona mambo kwa usahihi wamejaribu kufanya tendo la maana, hata kama hawakufanikiwa!! Nawaombea wasikamatwe na vibaraka wa mkoloni...!
 
Habari kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa GGM ni kwamba hali sasa imetulia na wamefanikiwa kuiniusuru dhahabu isiibwe.......dahh nimesikitika sana kusikia hili, siku nyingine tuwape msaada wa kisilaha wananchi wachache wanaojitolea kuwanyang'anya hawa makaburu mali zetu walizojichukulia kirahisi
 
watanzania waliotengenezwa na nyerere sio waliozalishwa na mfumo wa mwinyi, mkapa na kikwete, vizazi vitatu hivi wana hasira na wizi unaotendeka ndani ya nchi yao. usijidanganye eti sio watanzania, labda wanyarqwanda wanahusika kufanikisha upatikanani wa armaments tu, lakini uchoraji wa ramani na utekelezaji ni kizazi cha Mwinyi, Mkapa na Mrisho

They may have the will......but guts?....no way......it was like HIGH NOON you know
 
next time wajipange vema ili wafanikiwe
hakuna haja madini yanasafirishwa kwenda kwa makaburu wananchi tunabakiwa na mashimo
hivi kuna udhibiti gani wa serikali hapo kuhakikisha kiasi cha madini kilichopatikana na kodi inayolipwa?
poleni wapedwa siku nyingine mtafanikiwa walau mtauza nasi tutafaidi mzunguko wa hela.
 
Hivi hizo dhahabu wanavyo pakia na kuondoka nazo juu kwa juu kunakuwepo maafisa wa TRA, TBS, Usalama wa Taifa na watu wengine?
 
Polisi wamefika eneo la tukio na kwa sasa wanawakamata wakata mbao, wachungaji na wachoma mkaa wakiwatuhumu kwa ‘ujambazi' wakati wapiga deal halisi wameisha sepa , walinzi 8 wa mgodini ( wa kitanzania) wameahidiwa 10,000 USD kila mmoja kwa kuweza kulinda mali ya ' mwekezaji', huku mlinzi mzungu akisafilishwa kurudi RZA kwa matibabu ( huyu jamaa amepigwa kama risasi 3 mkononi na mguuni, na huyu ndio aliyeuwa jambazi baada ya kukabiliana naye uso kwa uso).

Polisi wamekabidhiwa sub machine gun 3, mabomu ya mkono 9 ( moja lilirushwa lakini halikulipuka vizuri) magazine zaidi ya 5 zikiwa na risasi zaidi 100, bullet proof vest 2.

Polisi wanasomeshwa wakubali kuwa wao ndio waliopambana na ku uwa majambazi ili hawa jamaa wanakwepa lawama za mauaji kimtindo, Mwili wa jambazi (kipande cha jibaba lenye asili ya kisomali inaaminiki ndiye alikuwa kiongozi wa uvamizi) umepelekwa mortuary, nikifanikiwa nita upload picha ya maiti yake.

Hali ya hewa imetulia kidogo na shuguli za kumtumikia kaburu zimeanza mnamo 1330hrs, kwa ujumla kulikuwa na vitofali 34 vya dhahabu ( kila kitofali kina 24KG) vilivyo pona pona kutembea ( ila nawalaumu hawa ma intruders kwa uchoyo wao!)
 
majambazi yamevamia wakati wakisafirisha dhahabu airport. wamekufa watu 2 askari wa mgodi ntawajuza kadri navopata. Source aliekua eneo la tukio
 
Hali ya hewa imetulia kidogo na shuguli za kumtumikia kaburu zimeanza mnamo 1330hrs, kwa ujumla kulikuwa na vitofali 34 vya dhahabu ( kila kitofali kina 24KG) vilivyo pona pona kutembea (ila nawalaumu hawa ma intruders kwa uchoyo wao!)
Uchoyo wa nini Mkuu?
Wa kugawa risasi kwa walinzi?
 
kwa ujumla kulikuwa na vitofali 34 vya dhahabu ( kila kitofali kina 24KG) vilivyo pona pona kutembea ( ila nawalaumu hawa ma intruders kwa uchoyo wao!)

I see nchi inaliwa hii yaani vitofali 34 na kila kitofa kina kilo 24kg sijui TRA wapo? au wapo kwa kazi ya kufukuzana na wauza viosk mitaani?
 
Mkuu wee acha tu, hata mimi sielewi mwizi ni nani hapa, maana kama mtu ana uwezo wa kuruka na ndege kuanzia mgodini hadi huko aendako na hakuna ukaguzi wowote mahali popote hii haingii akilini kabisa. Juzi nilikua nimetoka safari na viroba vinne vya mkaa na kitanda kimoja nilipofika kibiti nikasimiamamishwa na kuanza kukaguliwa eti nilipie ushuru....pumbafu kabisa, wachukue tu kwanza tuwaite Majasiri na mashujaa wa taifa hili hao waliojaribu. Halafu nione kijitu kinasimama kwenye Luninga na kujifanya kuua majambazi.
hii habari ni mpya na inaibua mawazo mapya pia!
Kwani katika tafsiri na uelewa wa kawaida, kati ya hawa wawili nani hasa ni mwizi!?
Na kama upande 'ulioshindwa' ni waliotaka kuzuia madini yasisafirishwe nje ya nchi ili wayafaidi wao, basi ni wapi Watz wengi wataegemea!?
 
Nimeongea na jamaa yangu aliyekuwepo eneo la tukio amesema mmoja wa watu waliotaka kuchukua dhahabu ameuawa na walinzi wa mgodi. Katika mapambano hayo Kaburu mmoja (Sniper) pia amepigwa risasi na kujeruiwa vibaya.
 
Mkuu wee acha tu, hata mimi sielewi mwizi ni nani hapa, maana kama mtu ana uwezo wa kuruka na ndege kuanzia mgodini hadi huko aendako na hakuna ukaguzi wowote mahali popote hii haingii akilini kabisa. Juzi nilikua nimetoka safari na viroba vinne vya mkaa na kitanda kimoja nilipofika kibiti nikasimiamamishwa na kuanza kukaguliwa eti nilipie ushuru....pumbafu kabisa, wachukue tu kwanza tuwaite Majasiri na mashujaa wa taifa hili hao waliojaribu. Halafu nione kijitu kinasimama kwenye Luninga na kujifanya kuua majambazi.

Kama dege la jeshi lilitua na kupakia Twiga, swala, fisi na kuruka huku wanao jiita usalama wa mafisadi wakisinzia huko kwenye migodi si ndo balaa tupu mtu anatua anapakia vitofali na anaruka navyo anako kujua yeye yaani tutaendelea kutembeza bakuri mpaka siku tupapaswe makalio.
 
siku moja nilikuwa naongea na injinia wa mgodini, nMtanzania mwenye mapozi hivi, aisee! anakubaliana na wizi wa madini yetu, halafu anapotosha ukweli eti madini hayawezi kutuinua kwenye tope la umaskini, wangekalenga kenyewe kwanza kafie mbali

Ntamaholo, mbona kenyewe tu hapo kalipo ni kamarehemu kafe mara ngapi?
 
Wadau,nasikia GGM kunawaka moto sasa hivi,majambazi wamevamia mgodini na hivi sasa nasikia wanapambana na polisi pamoja na walinzi wa mgodi.Wamevizia msafara wa kusafirisha dhahabu, mtu mmoja ameuwawa na mwingine amejeruhiwa vibaya na hali bado haijakaa sawa.Nitawajuza zaidi endapo waliopo mgodini watanipa taarifa mapema.

Kanta, kwa sasa mambo ni shwari worry bro. Na alie uawa ni jambazi si mfanyakazi.
 
Back
Top Bottom