mcrounmj
JF-Expert Member
- Feb 26, 2016
- 380
- 885
Nianze kwa kusema 'much respect to you all hustlers'. No matter what you're going through.... but you're the future billionaire. Hiyo ni salamu yangu kwenu watafutaji mliojipata, ambao hamjajipata na mnaamini katika kesho.
Uzi huu ni mwendelezo wa nyuzi nne zilizotangulia zikielezea mapambano yangu ya kiuchumi na namna ambavyo niliamua kujiingiza kwenye shughuli za dhahabu, mafanikio niliyoyapata na namna ambavyo niliweza kupanga mipango ya baadae. Nimeelezea historia ya maisha yangu ya huko nyuma...nikitokea familia masikini na kujikuta mhanga wa kukosa ajira baada ya kuhitimu chuo kikuu.
Yapo mengi nimeyaelezea ambayo yalinifanya niwe na ari na hamasa kubwa ya kuusaka utajiri. Lakini kubwa zaidi niliamua ku share na jamii ya jukwaa hili nikiamini, uzoefu wangu na mawazo yangu yatabadilisha mitazamo ya watu wengi namna ya kuwaza, kuamka na kuingia tena kwenye uwanja wa mapambano.... lakini mahususi nilitaka kuwasanua watu kuhusu rasilimali adhimu ambayo ni dhahabu.
Kutoka kuwa kibarua wa kuajiriwa mgodini, mpaka kufikia hatua ya kumiliki mgodi...si jambo dogo na sikuonyesha katika namna ya ujivuni bali ilikuwa kuonyesha kwamba kila kitu kinawezekana kama ukidhamilia. Guys, nikiri tu kwamba sehemu ambayo utajiri upo nje nje ni kwenye dhahabu.
Kwasababu andiko hili ni utangulizi wa sehemu ya mwisho..... Niahidi kuwa sehemu ya mwisho itakuwepo hapa jukwaani mapema juni mwaka huu 2024. Katika kipindi chote ambacho nimekuwa nikishea nanyi safari yangu ya mapambano, wapo watu ambao walihamasika na kunifata inbox. Wachache niliwajibu, na hata hao niliowajibu sikuwapa nafasi ya kuonana nao. Hii ilikuwa ni sababu yangu mahususi na mara kadhaa niliandika hapa kwamba napendelea niendelee kubakia kichakani kwa masirahi yangu binafsi. Hivyo sasa kwa sababu pale ambapo ilikuwa tamaa yangu kufikia is already done... The last season will reveal my cover, nitakuwa tayari kuwasiliana na yeyote na kumkaribisha nyumbani kwangu kama atataka kuja kujifunza.
Lakini pia kwa opposers na wakatisha tamaa... Nikiri tu kuwa ninyi ni watu mhimu mno kwenye jukwaa hili hata jamii kwa ujumla. Ninyi hamkubali katika juhudi za watu na mpo kutabili kuwa hawafiki popote. Nakumbuka uzi wangu wa kwanza nilipoonyesha kuwa mtaji wangu umekua maradufu kutoka million tatu mpaka kumi ndani ya miezi sita, mlitabili kuwa 'vina muda basi'. Lakini ilivyo ajabu nimekuwa nikiyatumia maneno yenu kupanda juu zaidi. Pia wapo ambao walihisi uzi huu ni namna ya kwenda kuwapiga watu pesa... yaani utapeli, haya naomba niliyemtapeli ajitokeze!
Kwa kumalizia niseme tu kuwa.... for whatever you're doing, do it in high spirit. Focus, consistency and determination will brought you into success. Amini kwenye unachokifanya, kifanye kwa ufasaha na na uwe na nidhamu ya matumizi.
Guys meet you at the top 'cheers'