Jaribio la kuiba dhahabu katika mgodi wa Geita (GGM) lazimwa

siku haya MANYANI yanayotutawala wakijua kuwa hata sisi NGEDERE ni ndugu zao itakuwa kilio na kusaga meno.
 
Asante Mungu magamba wameanza kuumbuliwa! Hapo maswali yatakuwepo kwa wingi. Je TRA walikuwa wapi? Na wanataarifa ya huo mzigo?!
 
Kama majambazi wanaweza kuiiba hiyo dhahabu na kwenda kuuza, kwanini sisi wenyewe hatuwezi kufanya hivyo hadi kaburu aje?

Ni kweli hao majambazi will come up with a better one, however na hao makaburu nao watatumia mabilioni mengine kujijengea ulinzi, haya mambo ya kuchota haya madini na kuondoka nayo pia noumer kwa sana, sijui kwanini zisiwe proccessed hapo hapo, tena hilo lingekuwa mojawapo ya sharti kwa wanaotaka kuwekeza kwenye madini.

Sasa yanapochimbwa na kuondolewa haraka haraka inakuwa kama na wao wanayaiba vile, hakuna amani.
 
mimi yananiuma hayo madini tu...yaani mali yetu hiyo inakwenda kumnufaisha kaburu. Hii ngozi nyeusi ni shida tupu.
 
Safi sana, wafanye jitahada waende na north mara, ila wasibugi step kama walivyochemka GGM.
 
GOOD ATTEMPT. Kama waliofanikisha kulizima sakata hilo ni WATANZANIA, KIFO HALALI YAO. Nategemea waliohusika kuzima watanzania kuchukua MADINI YAO kuwa ni wazungu tu, kwani wanapeleka kwao

uko sahihi mkuu maana wameona kwakuwa hawalipi kodi ni bora waichukue kwa nguvu, nawapa pole hao majambazi, ila nawaomba wajipange tena kwani kuna migodi mingi sana ya kuiba hasa ya Barrick.
 
I see nchi inaliwa hii yaani vitofali 34 na kila kitofa kina kilo 24kg sijui TRA wapo? au wapo kwa kazi ya kufukuzana na wauza viosk mitaani?

kila kilo 1 ni 70 milion kwa bei ya sasa ya dhahabu, 34*24*70=57,120,000,000/=Tsh (Tsh bilion 57.12) hiyo ni dhahabu inayozalishwa kwa kila wiki. mkuu hiyo ni kwa mjibu wa tunaofanya kazi mgodini.
 
Kuna wakati mtu waweza kufurahia ujambazi kwa kweli.................
Poleni Familia za MAJAMBAZI waliokufa wakitafuta dhahabu YAO!
 
Inabidi wakajipange upya,ila nadhani walistahili kufanikisha mission yao,sijui waliikosea wapi.maana hizo kg 400 ukilinganisha na zilie zilizokwisha ondoka ni afadhali za leo washikaji hawa wangefanikiwa kuzichukua,nashangaa hata waliopambana mpaka kufa kuokoa mali iliyogeuka kuwa ya mzungu.
Itabidi wasahihishe mpango iko siku watafanikiwa tu.naamini zingeingia kwenye mzunguko hapa bongo tungeambulia sasa zinavyokwenda huko mmmm sijui kama tutanusa
 
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha nzito za kivita, wamevamia Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), na kuiteka ndege ndogo iliyokuwa imebeba dhahabu kutoka mgodini hapo, kwa ajili ya kuikisafirisha kwenda nje ya nchi.

Tukio hilo limetokea hii leo majira ya saa 5:55 asubuhi, katika uwanja wa ndege wa mgodi huo uliopo umbali wa kilomita 5 kutoka katikati ya mji wa Geita, na kwamba majambazi hayo yaliyodaiwa kujifunika nyuso zao, yaliishambulia ndege hiyo kwa risasi za moto, kwa lengo la kutaka kupora dhahabu hizo zenye mabilioni ya fedha.

Habari kutoka eneo la tukio zilizoifikia FikraPevu, zinaeleza kwamba, wakati majambazi hayo yakiimiminia ndege hiyo risasi, huku yakifyatua ovyo risasi nyingine hewani, askari polisi Wilaya ya Geita walifanikiwa kufika eneo hilo haraka, kisha kuanza kupambana na watu hao kwa risasi za moto, kabla majambazi hayo hayajakimbia na kuliua jambazi moja.

Katika majibizano hayo ya risasi, askari polisi walifanikiwa kuliua jambazi moja baada ya kulimiminia risasi kifuani, na kwamba kabla ya jambazi hilo kuuawa na polisi lilikuwa limejeruhiwa vibaya na mmoja wa walinzi wa mgodi huo ambaye ni raia wa nchini Afrika Kusinia.

Dhahabu iliyonusurika kuporwa na majambazi hao inadaiwa kuwa ilikuwa ni zaidi ya kilo 1,000, ambapo ilikuwa imegawanywa katika maboksi 16 huku kila boksi moja likiwa na matofali manne ya dhahabu, na kwamba kila tofari moja linadaiwa lilikuwa na ujazo wa kilo 25.

jambazi-geita.jpg


Pichani: Wakazi wa Wilaya ya Geita mkoani Mwanza, wakiangalia mwili wa mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi (jina hajafahamika), akiwa ni mmoja wa watu wanne waliyovamia mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), akiwa amekufa baada ya kupigwa risasi na askari polisi katika jaribio hilo la kutka kupora dhahabu jana. (Picha na Sitta Tumma)

Habari zaidi - http://www.fikrapevu.com/biashara-n...shambulia-ndege-ya-dhahabu-geita-mmoja-auwawa
 
twashukuru kwa habari hii ila kuna mada kama hii imeshawekwa tangu asbh ungeunganisha habari yako,zitafute utaona.
 
I see nchi inaliwa hii yaani vitofali 34 na kila kitofa kina kilo 24kg sijui TRA wapo? au wapo kwa kazi ya kufukuzana na wauza viosk mitaani?
That is one week shipments. Folks this shipment is done every week. Currently one ounce is sold $1608. 1 ounce = 31.1g. It means 1g of gold is $51.7042. 1kg of gold=$51704.2. 30 bricks of gold x 24 = 720Kg.
Weekly shipment = 51704.2x720= $37,227,024
Monthly shipment 37,227,024x4.3=$160,076,203.2
Annual shipment = $160,076,203.2x12=$1,920,914,438.4

Those are the approximate production. it can be more or less than that by few dollars because it is believed that between 500kg and 1200Kg is shipped every week.
I just want to know how many kg is declared by GGM? We are told that mining is contributing a single digit percent in the GDP is it still the same with this figures of one goldmine among many mines in the country?
With all these huge resources being exploited GGM did not pay income taxes since
commencement of Geita mine in the year
2000.
Apart from that GGM and other mining companies are not paying taxes on all imports they make on machines n other production materials. Even fuels they consuming free of taxes. GGM for example consumer about 6-8 milion litres of fuel monthly duty free.

Do we need to go to New York city or London or to beg Chinese with these abundant
resources. The country is being robbed while the leaders are enjoying shopping by Arab thieves in London


Production done by GGM in 2011 has already surpassed their 2012 targets. In other words GGM can sleep and pay their employee in 2012, pack their machines in the year 2012 but still enjoy their accrued profit in 2011.

Can African get angry if mzungu calls us a continent of dead brains?
 
Kwa nini huyo Mzungu asingekufa? kwa nini wasingemuua? washenzi hawa wanasafirisha mali yetu kavu kavu!
 
Duh! Huu wizi ungefanikiwa ungekuwa mtakatifu!!! Inavyosemekana Vitofali 68 vya dhahabu vyenye thamani ya Shilingi 130 Billioni!!!!
 
RIP Mpambanaji Mtanzania/Mgeni kutoka nchi jirani nasi... umekufa kishujaa... CCM ndio wametufikisha hapa... Angalau tumejua tunavyoibiwa na hawa Makaburu...


GO TO HELL NGELEJA.
GO TO HELL MALIMA.
GO TO HELL JAIRO(mwizi mstaafu)
GO TO HELL KAFUMU

NIMESKITISHWA SANA NA MAUAJI YA HUYU KAMANDA...
 
Back
Top Bottom