Chadema ndani ya mji mdogo wa Katoro/Buseresere

Mama .

Nyie wabunge mkiwa Bungeni mnalipwa posha kila siku. Je huko anawalipa nani Posho? na vipi hao wnaowahamasisha wanalipwa na nani? au ndio kuwadanganya watu wakati nyie mpo kazini?

Unawaza kulipwa tu,angalia usije "nunuliwa" na wewe pia
Uh,njaaa,lunch time
 
nadhani huyu aliyeandika hapa anakasumba mbay sana ya kutaka kulipwa kwa kila kitu ,na hiindo inaangamiza taifa na wewe ni mwajiriwa wa serikali unaepata hivi viposho vya kila mara

Mh Regia.

Ina maana wewe huna posho huko?
 
Orodheni huu Utumbo kwenye Mabango ya leo.

TICTS
RADAR (BIL 63)
NDEGE YA RAIS
SAFARI ZA NJE YA NCHI-UTADHANI YEYE NI WAZIRI WA MAMBO YA NJE
NGEREJA KULALA MKUTANONI PARIS HALAFU ANALIPWA kwa Kodi zetu
TWIN TOWERS BOT (BIL 300+)
MIKATABA ISIYO NA TIJA KWA NCHI(Migodi)
KAGODA(BIl 45)
MEREMETA
RICHMOND/DOWANS (BIL 94)
WAKUU WA MIKOA na WILAYA(Hao ni Watumishi wa CCM)
IPTL (3 BIL KAMA HAIFANYI KAZI, 8BiL KWA MWEZI IKIFANYA KAZI)
KIWIRA COAL MINES
NETGROUP SOLUTIONS (WALIKUSANYA CHAO WAKAENDA ZAO SOUTH)
MISAMAHA YA KODI(Nchi inakosa mapato)
ALEX STEWART (BIL 11)
BEI YA BIDHAA ie. UMEME na SUKARI (watanzania ndiyo wanaofidia misamaha ya kodi)
RITES (Tunadanywa ya India, wakati kila kitu ni jasho letu ikiwa pamoja na mtaji wa kampuni)
ALLIANCE AIR (Wameua ATC)
LOLIONDO IMEHUJUMIWA-WANYAMA WOTE WAMEKWISHA
NOTI MPYA KILA AWAMU-Nani kawaambia za zamani haziingii katika Pochi-Ni Ufisadi)
ALISTORM-Ililipwa na Umeme haupo Mwanza

Anayesema CDM ni wachochezi huyo ni fisadi.

Lazima tusiwaogope, CCM ni kichaka cha wezi.

Kinafuga na kulinda wezi, kinaandaa wezi wa kuendeleza fani ya wizi.

Songa Mbele Dr. Slaa,Mh.Mbowe, Mh.Regia, Mh. Sugu, Mh. Lema, Mh Mdee

Gooo please Go, Inchi imeelemewa, tunachopata chote tunakilipa kwa wapuuuuzi hawa.:rain:
 
CCM wapeleke hoja Bungeni ya kufuta ruzuku ya vyama vya siasa hata kama na wao wataathirika. Inaelekea CDM hawafanyi kosa na ruzuku yao; ruzuku inatumika kuibomoa CCM kisawasawa. Dawa ya kukomesha haya maandamano na mikutano ya CDM isiyosha ni kuwaondolea uwezo wa mapato. CCM wao si wana vyanzo vingine vya mapato kama viwanja vya mipira na majengo!!!!

Ikiondolewa ruzuku TUTACHANGIA.
 
CCM wapeleke hoja Bungeni ya kufuta ruzuku ya vyama vya siasa hata kama na wao wataathirika. Inaelekea CDM hawafanyi kosa na ruzuku yao; ruzuku inatumika kuibomoa CCM kisawasawa. Dawa ya kukomesha haya maandamano na mikutano ya CDM isiyosha ni kuwaondolea uwezo wa mapato. CCM wao si wana vyanzo vingine vya mapato kama viwanja vya mipira na majengo!!!!
hivi unajua hata sasa hivi kuna mvutano ndani ya chama baada ya ruzuku kupungua kutoka na CDM kupata viti vingi sasa wakiondoa ndiyo mwisho wao....
 
Mama .

Nyie wabunge mkiwa Bungeni mnalipwa posha kila siku. Je huko anawalipa nani Posho? na vipi hao wnaowahamasisha wanalipwa na nani? au ndio kuwadanganya watu wakati nyie mpo kazini?
CDM huwa hailipi waandamanaji wala kuwasomba kwa fusso kama nyie, nakwambia utaumia sana kwa sababu hii kitu si ya msimu ni mwendelezo kwa miaka mitano ijayo.
 
I praise CDM team for making people woke up and fight for their rights which has been sweendled by rulers and their allies for a long time. Cheyo and Mrema are dead polititians don't listen them. They are CCM messanaries, the voters back to their constitutions shall punish them for underleting them. The voters are wise enough to be cheated, they know what is CHADEMA is fighting for is for their survival.
Mr. Mbulando
 
poleni sana wana CCM! Chadema haiendeshwi na ruzuku...inaendeshwa na nguvu za wananchi...CCM igeni mfe!
 
Inaonesha Mkutano utakuwa mzuri sana kwani maandalizi mazuri yamefanyika.Baadhi ya Wabunge tuko hapa Twiga Lodge tunasubiri muda ufike.Jana nako Chato mambo yalikuwa mazuri sana.

Dada Regia kwa nini tusiwe na blog ambapo picha na yaliyojiri katika mikutani hii muhimu ya kutafuta uhuru wa nchi yetu kutoka kwa wakoloni wa weusi zitawekwa? Ni muhimu kwa ajili ya historia ya ukombozi wa nchi yetu. Mafisadi ni wakoloni wabaya kuliko wakoloni waliotutawala huko nyuma maana wao wana ngozi ya kizalendo (kondoo) lakini ndani ni wakoloni (mbwa mwitu) wabaya. Naomba suala hili lizingatiwe jamani. Wengine tuko mbali na maeneo husika lakini tunatamani tuone mwitikio wa ndugu zetu walioko huko
 
TRA siku hizi nao wamestuka...yaani wao wakusanye nyie mpeleke kwa Rostam Aziz? kwa taarifa yako siku hizi wakitumwa wanaleta taarifa in advance na kutoa majibu ambayo ni ultimatum!!

ccm imekula kwenu!
 
Wakati wa kampeni ya Uchaguzi, CCM ilitumia muda mwingi sana kuviita vyama vya upinzani kuwa vyama vya msimu au vyama vya uchaguzi. Sasa vyama hivyo vimeanza kufanya kazi full time! CCM inalalama nini tena? Hizo wanazofanya Chadema ndo siasa zenyewe na kwa hali inavyoonesha vurugu hazina nafasi hadi hapo serikali inapoamua kutumia polisi kuanzisha vurugu.

Sasa Chadema wanafanya siasa, basi na CCM wafanye siasa, si kulalamika kuwa eti Chadema inaikosanisha na wananchi. CCM inatarajia Chadema wafanye siasa gani kama si kuisema yale inayoshindwa kutelekeleza? Ukishindwa kutekeleza yale uliyoahidi ndo mtaji wa wapinzani wako na majukwaa ndo mahali pa wapinzani kupatumia.

CCM nayo, badala ya kutumia viongozi wa serikali, isimame kama CCM na waitetee serikali yake; hzo ndo siasa za kistaarabu. Kuendelea kulalamika kwa CCM kunaonesha kuwa hawako tayari kuona vyama walivyokuwa wakiviita vya msimu au vya uchaguzi vikiwa vya kudumu! Siasa ndo hizo, majukwaani. Kote wananchi wanatoka wanacheka na kuiona CCM chama cha wapuuzi. Badala ya CCM kutaka kutumia nguvu ya dola kuleta vurugu, waumize vichwa, na watafute majibu ya hoja za Chadema waende kwa wananchi wawaambie.

CCM wana midomo mingi sana! Lakini wakisimama wenyewe kama CCM wanajua kuwa hawana mvuto ndo maana wanalalamika. Lakini ulalamishi wao hauna uhalali wa kimkakati kwani wao ndo wamekuwa wakiongoza kwa kukejeli vyama vya upinzani kuwa vya msimu au vya uchaguzi. Sasa hizo ndo siasa za kudumu na Chadema haitakiwi walale! Waendeleze harakati hizo hadi 2015, CCM ikiendelea kulalamika tu, itavuna mabua. Wakitumia nguvu za dola ndo wamekwisha kabisa kwani watasakamwa na dunia nzima. Njia pekee ni wao kutumia majukwaa kama Chadema kueleza ya kwao; swali ni je yanaelezeka? Wanaweza kusimama mbele ya watanzania na kuwaambia kuwa Dowans ni halali? Au kuwa EPA haukuwa wizi?

Hapo ndo pagumu, ila inatakiwa wazoee kuwa siasa za upinzani za kudumu walizokuwa wanaziomba ndo zimeshaanza hizo! Fungate walilokuwa nalo toka 1992 mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa ndo limeisha rasmi! CCM wake up, or sleep for ever!
 
TRA siyo wajinga na si kitengo cha CCM kama unavyofikiri. Ndani TRA karibu wote pia wanakerwa na mambo ya CCM kama ambavyo CDM inavyokerwa. CDM aluta continue, we together. Wasira go to hell.
 
Mama .

Nyie wabunge mkiwa Bungeni mnalipwa posha kila siku. Je huko anawalipa nani Posho? na vipi hao wnaowahamasisha wanalipwa na nani? au ndio kuwadanganya watu wakati nyie mpo kazini?

Ufinyu wa ufikirifu au umettumwa na akina cjui nan wale wehu wenzio???????????????
 
CDM siyo chama cha wafanyabiashara wakubwa kama ilivyo ccm. Michango inayosemwa hapa ni hii ya walala hoi tu kama wewe, hata kwenye orodha ya TRA hawamo. Sasa hiyo kodi unayoisema watakadiria kubwa itatoka wapi. Taabu yenu mnaamini mno katika nguvu ya pesa. CDM ni chama cha wananchi wa kawaida kabisa, wakati wa kampeni kilizunguka nchi nzima wakati huo hata ruzuku haikuwepo. Kwa hiyo vyanzo vya mapato ni wanachama wenyewe.

CDM kina wanachama wasiopungua mil 4, fikiria kila mtu akichangia sh 200 tu, hesabu unayo. pesa hiyo haitoshi kufanyia mikutano??
 
CCM wapeleke hoja Bungeni ya kufuta ruzuku ya vyama vya siasa hata kama na wao wataathirika. Inaelekea CDM hawafanyi kosa na ruzuku yao; ruzuku inatumika kuibomoa CCM kisawasawa. Dawa ya kukomesha haya maandamano na mikutano ya CDM isiyosha ni kuwaondolea uwezo wa mapato. CCM wao si wana vyanzo vingine vya mapato kama viwanja vya mipira na majengo!!!!

Hapo kwenye RED, Hivyo viwanja vya mipira vilijengwa kwa nguvu za wananchi wala si vya CCM, Subiri utaona siku tunaichukua nchi vitawatokea puani!!! Kibanga ampiga mkoloni naikumbuka sana hii stori!! Sisi tutawapiga kwa sanduku la kura!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom