Simulizi ya kweli: Nilitaka kukupenda ila sikuweza kabisa

Tmainitvp

Member
Mar 25, 2019
64
119
SEHEMU YA KWANZA.......01

BASED ON SOMEONE’S TRUE STORY
(simulizi ya mtu yenye uhalisia ndani yake)
simu: 0684024387
na TUMAINI ERNEST STANSLAUS

June 1, 2019.

“Maskini Happy!!!!!, looh!!!!!!, nisamehe mimi Rafiki ako pengine mimi ni
Zaidi ya walio kuumiza, mpaka nakuandikia haya, sina uhakika kama yatakufikia au
laah maana sijui hata nikupatie wapi, uwe hai au umekufa ,popote ulipo nisamehe
Rafiki yako.’’
Nilimaliza kuandika ujumbe mfupi kisha nikauweka mfukoni, nikajilaz
kitandani kwangu chali, dakika moja nikajigeuza tena nikakumbuka kijikaratasi
nilicho mwandikia Happy nika kichomoa tena mfukoni ili niweze kuusoma tena
lakin sikufanikiwa baada ya kamasi jepesi kutoka mapuani mwangu na kuchungulia
nje, ni wazi sasa nilikuwa natokwa na kilio cha chini cha kwikwi, nilikuwa nikiwaza
nitampatia wapi Happy, nikaamua kuirudisha mfukoni, mara hii nikaamua
kunyanyuka kitandani na kuisogelea meza ndogo ilio kuwa ndani ya chumba
changu. Sikujua hata nimeenda kufanya nini pale mezani, roho iliniuma sana tena
saaana, nikajikuta natokwa na kilio cha wazi kabisa “haaaaappy……. Haaappy”
Nilijikuta napiga piga kifua roho iliniuma saana, pengine sikuwahi kulia kiasi
kile hapo kabla happy aliniumiza saana, si kwa alicho nifanyia lahasha, ni hatia
yangu ya kumuumiza mtoto wa watu. Akili ikaja sasa, ni namna ya kumpata lucy
japo aniambie kitu kuhusu Happy ndio ukwel huo nilikuwa nikiuhangaikia katika
Maisha yangu.
Kabla sijachukua simu yangu nimpigie lucy sikuwa na uhakika wowote kama
hata lucy atapokea simu yangu. Tayari nilikuwa nimeharibu kila kitu, kila kitu katika
Maisha. Si yule wala huyu kila mmoja nilikuwa nimemkosea. wacha kwanza nivute
pumzi kabla cjakwambia kitu.
Naitwa Tumain jina pekee alilo nizawadia mama yangu kipenzi,wengi
walipenda kuniita Tvp kutokana na kazi niliokuwa nikiifanya ni mwanafunzi wa
chuo kikuu cha Dodoma. Maisha yangu ya uandishi ndiyo yananifikisha hapa nilipo.
Kila dogo nililolisikia katika mapenzi nilipata shauku la kuliandika. Na katika
maandishi yangu najikuta najiingiza katika maisha ya mtoto mzuri happy.
Ni happy huyo huo ambae alipaswa kunilaumu mimi mkosaji mkubwa nisie
sitahili msamaha wowote katika dunia hii, ingawa walau ninasababu ambayo kiufupi
haikuwa na maana yoyote masikioni mwa happy, lakini ninge fanya nini mimi mtotoiii
wa mwanamke mwenzake nilie na moyo, tena moyo wa nyama, wenye kusikia kila
aina ya machungu na furaha oooh! Happy. Siwezi kukulaumu popote ulipo
nisamehe,
***

May 10,2018

KATORO, GEITA.
Anna ; huyu alikuwa msichana wa kwanza kabisa katika Maisha yangu , ni
kutokana na kutokuwa na uelewa wa mapenzi nilitokea kumpenda Anna kuliko kitu
chochote katika Maisha yangu kabla hata Anna sijamwambiwa kama nampenda,
Anna alikuwa asubuhi na jioni yangu, nilikuwa siambiwi chochote kuhusu Anna, si
kwa kingine Zaidi ya alicho kuwa nacho Anna, hakuna aliepinga kuwa Anna
alikuwa binti mzuri, rangi yake ilimsaidia kuvaa kila aina ya nguo aliyo ipenda, sura
na umbo tuachane navyo maana sina neno la kuelezea juu yake, Anna alivutia bana
Ikawa ni foleni ya wanaume kulisaka penzi la Anna, kila siku ana alilisikia
neno NAKUPENDA masikioni mwake, atamuamini nani, kila mmoja alikimbilia
nakupenda, huyu alikuja kwa miguu mwingine kwa lift, wengine kwa gari na
mwingine funguo mkononi, ilimradi tu anna apendwe, ndio pale zamu yangu ilipo
fika, sikuwa na chochote Zaidi ya nguo nzuri nilizokuwa nimevaa nikiamini
zitasaidia kumshawishi mrembo huyu, maskini mimi, ninge mwambia nini Anna,
sina chochote sina kila kitu, naishia kuambiwa tu “nikupeleke wapi?”.
Moyo uliuma sana sikujua nifanye nini, pengine sio kosa lake, kosa langu
kupenda penda ovyo, hakuna siku nilio wahi umia kama siku hiyo, niliwaza
ntafanyaje ili niweze kumpata anna sikuwa na cha kufanya, hali haikuniruhusu,
nikapiga moyo konde, nikaulaani labda ni umaskini wetu ndio ulio nifanya
nikataliwe, nikajiangalia vizuri, nikweli ndio kwanza nilikuwa nikila na kulala kwa
nyumba ya mzee, sina nilicho kuwa nazalisha, umri wangu ningempeleka wapi
mtoto mzuri kama yule. Nafsi iliniambia Tuma tafuta hela.
Nikiwa bado katika maumivu ya kukataliwa na mpenzi nilie tokea kumpenda,
si mbali na nyumbani kwetu wanatokea mabinti wawili mmoja alionekana mdogo
kwa mwenzake. Hawa waliishi mita kama mia hivi toka katika mahali tulipo kuwa
tukiishi, ni ndani ya mji mdogo tu, mji wa katoro, mji usio kuwa na mawaa ndani ya
mkoa wa Geita. Ni katika safari yangu ya kusubiri kuendelea na masomo yangu ya
elimu ya juu, Queen ndugu yake Leah anatokea kunipenda yote haya nikutokana na
mazoea tulio kuwa tumeanza kuyaweka, muda wake mwingi akaumalizia nyumbaniiv
kwetu akicheza na mimi michezo mingi sana anachana na zile movie za kifilipino
tulizo kuwa tunaziangalia pamoja na kusababisha hisia kukutana, taratibu Queen
akaanza kunifanya nimsahau Anna hii ni kutokana na mapenzi ya dhati niliyo anza
kuyaona moyoni mwa Queen, kweli Queen alinipenda, alinipa kila nilicho hitaji
kidogo maskini moyo wangu mwepesi, moyo ulioumbwa kupenda haraka, bila
kujari Queen nikawa nimemuweka moyoni.
Haikuwa siri tena mamayangu akawa mtu wa kwanza kuelewa ukaribu wetu
mimi na Queen, kwel tuliendana nikafungua dunia mpya ya mapenzi, nikahakikisha
naingia moyoni mwa Queen, ni kwel Queen akawa kwel malkia, mimi nikawa
Queen, Queen akawa mimi, ikawa hata nikimuona tu moyo unaadunda haswaa,
damu inachemka wacha weee, mapenzi yakawa mapenzi, asikusimulie mtu, mapenzi
yetu yakawa mamenoga kila mtu akatamani walau awe kama sisi, mapenzi yetu
yakawa ya kikorea sasa, yalee ya ki tamthiria, yale ya nikikosea tu nakukumbatia
unanisamehe.
Akatokea Leah dada yake Queen, huyu mpaka hapa naamini alikuwa mwiba
na shetani mkubwa wa penzi letu, ni katika safari yetu ya kupendana, mimi na Queen
tukaanza kuweka mipango ya mbeleni, kubwa kabisa nikaridhia kumuoa Queen,
kwanza alikuwa mzuri kabisa sio tu wa sura na umbo hata mama yangu aliipenda ile
tabia yake nzuri ya heshima, kitendo cha mama kuwa ana msifia Rafiki yangu
anatabia nzuri ikawa na suluhisho tosha la mimi na Queen kuoana. Lakini ntamuoaje
mtoto wa watu angali ndio kwanza tunasubiri amalize kusoma, na ndio mwanya huo
alio utumia leah kuangamiza penzi letu, mwanya uliotokana na jinamizi baya la
wivu, mapenzi niliyo mwonyesha Queen leah akatamani ayapate, dah! Vitisho
vikawa vingi juu ya Queen, ukizingatia leah alikuwa binti mkubwa akawa juu ya
Queen kila alicho kisema Queen alikifata, heshima aliyo kuwa ameiweka Queen juu
ya dadayake hakutaka kuiondoa, akaambiwa aachane na mimi, Queen hakusikia
akaapa kamwe hatokuja kuniacha, na kwel moyo wake ulukuwa na ukwel mtupu,
Queen alinipenda.
Lakini atafanyaje sasa, ndio kwanza dadake leah alikuwa ametamani penzi
langu, akili yake ikawa ni jinsi gani atatutenganisha, vitisho havikutosha tu kwani
tayari tamthiriya za kikorea zilikuwa zime muathiri. Leah akaamua kabisa
kututenganisha, uamzi wake wa kumuongopea mdogo wake ukawa umefanikiwa, ni
baada tu ya kumsemea kwa baba yao kipenzi mzee omary, mzee ambae ni watu
wachache tu walitokea kuwa na utani nae maranyingi ukumwona amecheka basi
kulikuwa na sherehe kwake au sikukuu, ukali huo uliwafanya majilani na hatav
Watoto wake wawili wapendwa wamuogope sana, si kwa kuto kucheka 2 bali hata
maamuzu yake magumu ambayo huwa anayachukua.
Queen akaonywa sana, akazuiwa kabisa, kuonekana na mimi, ikawa ina pita
siku hatuonani, wiki, ikafikia hatua mpaka mwezi, niliumia sana, kisasi kikawa juu
ya mwanamke mbaya maishani mwangu, Leah Omar, achana na kipigo alicho kipata
mpenzi wangu Queen, kilicho niuma Zaidi ni kuhamishwa kabisa na kupelekwa
sehemu ambayo mpaka sasa cjui Queen wangu alipo enda.
Nikajiapiza kamwe ctokuja kupenda, maskini mapenzi, utausemea moyo
mpaka lini, ndio kwanza napoteza mtu wa pili katka Maisha yangu nilio wapenda,
ntapenda wangapi mimi, lakini nikawa na matumaini huenda Queen atarejea lakini
wapi, Queen yule nilie msubiria sikumuona tena, ikawa ivo mpaka nafanikiwa
kujiunga na masomo yangu ya juu.


November 1, 2018

CHUO KIKUU CHA DODODMA, TANZANIA

Ndani ya kitivo cha biashara na sharia, sikuwa nakingine kikubwa kilicho
nileta Zaidi ya masomo yangu ya biashara ndan ya chuo kile kikubwa jijini Dodoma,
sehemu ambayo nilijifunza mengi kuliko hata yale nilio jifunza awali kabla ya kufika
jijini Dodoma, nikaona mengi yakitendeka,

ITAENDELEAAA.........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom