zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
zomba kuweka record sawa: 11,154 - 6,000 = 5,154. Hizi ndio 5,154km ndio zimekamilika wakati wa awamu ya JK. Nimetumia neno "kukamilika" maana miradi mingi ya barabara ilikuwa tayari imeshaanza wakati wa Mkapa, na kama tuengeendelea na muundo ule ule wa Mkapa tungekuwa mbali sana.
Road fund ilikuwa inafanya vizuri sana, ndio maana hatukuwa tunasikia makandarasi wakisitisha kazi kwa sababu madeni. Tulikuwa na uwezo wa ndani tofauti na sasa amapo hela za nje ndio nyingi. Nakumbuka Raila Odinga alikuja Tanzania kujifunza namna tulivyokuwa tunaendesha hii wizara hasa kwa upande wa barabara, sasa hivi wamepiga hatua kubwa.
Kuna kosa kubwa lilifanyika (pengine sio kwa makusudi), mara baada ya uchaguzi mkuu baraza jipya la mawaziri lilikuwa kubwa sana lilikuwa na sura za wanamtandao. Kwa bahati mbaya wizara hii inayohusika na ujenzi wa barabara ikaenda, kwanza na Andrew Chenge na baadae kwa Shukuru Kawambwa. Wote wawili hakuwa na ubunifu au uwezo wa Magufuli na hapa ndipo mambo yalianza kuharibika maana gharama za ujenzi ziliongezeka mara 3 (cost/km)! na ubora wa kazi ukashuka.
Kwa sasa tunaanza ku-pick up lakini madeni yameathiri kwa kiasi kikubwa kasi ya ujenzi.
Hapana usizungushe, Magufuli kasema wazi bungeni ni 6,000 + 11,154 = 17,154 (Magufuli alisema zaidi ya 17,000). Kwanini hupendi ukweli?