Barabara za Juu kwa Juu kweli ni kwa ajili ya kupunguza msongamano?

Malori makubwa yanaopita barabara za Mandela na Mororgoro yana mchango mkubwa sana kuongeza foleni katika jiji hili. Njia ya haraka kupunguza foleni ki kuweka muda maalumu malori kusafiri mfano yatoke bandarini kuanzia saa tatu usiku na yaruhusiwe kuingia mjini (kutoka Kibaha) muda huo huo. Ila kufanikisha hilo kitengo cha kutoa magari bandarini kifanye kazi hadi saa sita usiku. Pia kuna umuhimu wa vitengo vya TRA pale Bandarini na kule Posta vifanye kazi angalau hadi saa sita usiku kwa ajili ya watu ku process documents.

Pia Askari traffic waache kuongoza magari sehemu zenye mataa wafanye hivyo kwa muda maalumu labda kama kuna msafara. kazi yao iwe kudhibiti wanaotanua na kutoheshimu taa. Mfumo wa kuongoza magari ulifaa wakati ule kulipokuwa na uneven distribution ya magari lakini hivi sasa magari ni mengi kila upande, hakuna barabara isiyo na foleni. Uwepo wa trafiki unasababisha foleni kwa vile wanavuta sana upande mmoja na kuacha upande mwingine. Pia huwa wanapigiwa simu za jamaa zao kuvuta magari ya upande mmoja.......

Kwa gharama za mafuta zilivyo panda, nisingependa kuja na gali yangu katikati ya jiji kama tungukuwa usafiri wa uhakika wa magali ya abilia. Serikali inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa msururu wa magali kama ingeweza kuzitumia kikamilifu reli zetu kwa kusafirisha watu wakati wa asubuhi na jioni. Kwa kufanya hivyo baadhi yetu hatutakuja na magari hapa katikati ya jiji na baadhi ya madaradara yatahama.
 
Back
Top Bottom