Barabara za Juu kwa Juu kweli ni kwa ajili ya kupunguza msongamano?

zomba kuweka record sawa: 11,154 - 6,000 = 5,154. Hizi ndio 5,154km ndio zimekamilika wakati wa awamu ya JK. Nimetumia neno "kukamilika" maana miradi mingi ya barabara ilikuwa tayari imeshaanza wakati wa Mkapa, na kama tuengeendelea na muundo ule ule wa Mkapa tungekuwa mbali sana.

Road fund ilikuwa inafanya vizuri sana, ndio maana hatukuwa tunasikia makandarasi wakisitisha kazi kwa sababu madeni. Tulikuwa na uwezo wa ndani tofauti na sasa amapo hela za nje ndio nyingi. Nakumbuka Raila Odinga alikuja Tanzania kujifunza namna tulivyokuwa tunaendesha hii wizara hasa kwa upande wa barabara, sasa hivi wamepiga hatua kubwa.

Kuna kosa kubwa lilifanyika (pengine sio kwa makusudi), mara baada ya uchaguzi mkuu baraza jipya la mawaziri lilikuwa kubwa sana lilikuwa na sura za wanamtandao. Kwa bahati mbaya wizara hii inayohusika na ujenzi wa barabara ikaenda, kwanza na Andrew Chenge na baadae kwa Shukuru Kawambwa. Wote wawili hakuwa na ubunifu au uwezo wa Magufuli na hapa ndipo mambo yalianza kuharibika maana gharama za ujenzi ziliongezeka mara 3 (cost/km)! na ubora wa kazi ukashuka.

Kwa sasa tunaanza ku-pick up lakini madeni yameathiri kwa kiasi kikubwa kasi ya ujenzi.

Hapana usizungushe, Magufuli kasema wazi bungeni ni 6,000 + 11,154 = 17,154 (Magufuli alisema zaidi ya 17,000). Kwanini hupendi ukweli?
 
Mkuu Jodoki Kalimilo huoni barabara mpya wakati wa JK? Korogwe - handeni, mkata - handeni, tunduma - sumbawanga, namtumbo - songea - mbinga, tunduru - matemanga, tuliani - magole - kilosa, tabora - nzega, manyoni - itigi - tabora, kigoma - kidahwe - uvinza, daraja la malagalasi, sumbawanga - kizi - kibaoni, dodoma - babati, minjingu - babati - hydom - singida, nk. Katika ujenzi wa barabara kunakuwa na design period ambapo ikifika unatakiwa ufanye rehabilitation ama reconstruction hivyo hizo unazozisema zimeisha muda wake wa kuishi na inabidi ama zifanyiwe reconstruction au rehabilitation. Ukiziacha zinarudi kwenye vumbi na mashimo yake yanakuwa ni mabaya kwelikweli.Twende mbele turudi nyuma JK amejitahidi sana kwenye miundombinu hasa ya barabara asiyeona hataki tu kukubali huo ukweli. Na ikumbukwe kuwa kuna barabara nyingi tu zinajengwa kwa pesa za ndani bila ufadhili toka brettonwoods.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: FJM
Mkuu FJM usichanganye mambo. Hela ya Road Fund asilimia kubwa inaenda kwenye kitu inaitwa maintenance na wala siyo construction of new roads. Hizo za road fund zimekuwa ringfenced kwa ajili hiyo, pesa za construction aidha zinatoka kwa wafadhili ama consolidated fund ya jumla (najua road fund nayo ni CF lakini iko specific)
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: FJM
Jodoki Kalimilo amma kwa makusudi kabisa umechukuwa baadhi tu ya takwimu. tazama pia kwenye on going projects ambayo ndio theme ya nyuzi hii.

Isitoshe, kuna miradi mingi ambayo haikumaliziwa na awamu ya Mkapa ambayo Kikwete kaimalizia.

Miradi mingi ya barababara tayari hela zilishalipwa/tengwa wakati JK anaingia. Kumbuka rais anaingia madarakani November wakati Financial Year inaanza July. Mkapa angekuwa ni mtu visasi hasa kipindi kilichopita 2005-10 ambapo kuna watu CCM walikuwa wanamwandama angeweza kabisa kumwaga mboga kuhusu miradi ya barabara.

Unajuwa wakati mwingine ni rahisi sana watu kusema hata Mlimani City imejengwa wakati wa JK.

Nirudie point yangu ya awali, kama hatukubalisha uongozi wa wizara ya Ujenzi mwaka 2006 tungekuwa mbali sana. Hela zimetafunwa mno pale ujenzi hadi Magufuli aliporudi. Na angalia nchi yoyote kuna corruptio kubwa sana constuction.
 
Sijakataa Kimbunga nilichokuwa nachangia kuhusu hizo kilometre 11,154 alizojenga JK kama alivyoleta zomba kuna ambazo mchakato ulianza before kuingia madarakani otherwise kazi naziona
 
Last edited by a moderator:
Sijakataa Kimbunga nilichokuwa nachangia kuhusu hizo kilometre 11,154 alizojenga JK kama alivyoleta zomba kuna ambazo mchakato ulianza before kuingia madarakani otherwise kazi naziona

Mkuu nashukuru kama unaona hilo. Tuweke mambo vizuri ni kwamba awamu ya Mkapa na Awamu ya JK barabara zimejengwa katika nchi hii. Watu wa kanda ya ziwa wanakumbuka jinsi walivyokuwa watalii wa kenya na hata uganda bila utashi wao. Naungana na zomba kwamba wakati wa JK imeanzishwa na inatekelezwa miradi mingi ya barabara kuliko wakati wowte ule wa historia ya Tanganyika kuanzia wakati wa Protectorate.
 
Last edited by a moderator:
Miradi mingi ya barababara tayari hela zilishalipwa/tengwa wakati JK anaingia. Kumbuka rais anaingia madarakani November wakati Financial Year inaanza July. Mkapa angekuwa ni mtu visasi hasa kipindi kilichopita 2005-10 ambapo kuna watu CCM walikuwa wanamwandama angeweza kabisa kumwaga mboga kuhusu miradi ya barabara.

Unajuwa wakati mwingine ni rahisi sana watu kusema hata Mlimani City imejengwa wakati wa JK.

Nirudie point yangu ya awali, kama hatukubalisha uongozi wa wizara ya Ujenzi mwaka 2006 tungekuwa mbali sana. Hela zimetafunwa mno pale ujenzi hadi Magufuli aliporudi. Na angalia nchi yoyote kuna corruptio kubwa sana constuction.

Tatizo kubwa ulilokuwa nalo ni uelewa usio mpana.
 
Mkuu nashukuru kama unaona hilo. Tuweke mambo vizuri ni kwamba awamu ya Mkapa na Awamu ya JK barabara zimejengwa katika nchi hii. Watu wa kanda ya ziwa wanakumbuka jinsi walivyokuwa watalii wa kenya na hata uganda bila utashi wao. Naungana na zomba kwamba wakati wa JK imeanzishwa na inatekelezwa miradi mingi ya barabara kuliko wakati wowte ule wa historia ya Tanganyika kuanzia wakati wa Protectorate.

Mie binafsi niliwahi kusafiri njia ya kati mara tatukKutoka Mwanza Arusha na Mwanza Dar, miaka ile ya 2001 - 2003 mara nyingi ilikuwa tunalala Singida au Misigiri kesho yake mnaendelea na safar aliyezunguka nairobi unakuta amefika. Lakini siku ni shwari.
 
Kama wapi ambapo uelewa wangu sio 'mpana?

Ni pale ambapo unashindwa kuelewa kuwa unaweza kuwa na plani lakini usiitimize akaja mwenzako akaitimiza kiurahisi sana. Kila mmoja na uwezo na upeo wake.

Mfano Nyerere alishindwa kupata hata mafuta ya kuweka kwenye magari na tukawa na mgao wa mafuta, gari Jumapili hazitembei, ingawa alikuwa ni msemaji mzuri sana. alipokuja mwinyi mafuta bwerereee.

Sasa kama Mkapa aliweza kuwa na plan akashindwa kuzitimiza akaja Kikwete akazitimiza kwa kasi zaidi akaongeza na zake kwa ari na nguvu zaidi huoni kuwa ni neema hiyo?
 
Ni pale ambapo unashindwa kuelewa kuwa unaweza kuwa na plani lakini usiitimize akaja mwenzako akaitimiza kiurahisi sana. Kila mmoja na uwezo na upeo wake.

Mfano Nyerere alishindwa kupata hata mafuta ya kuweka kwenye magari na tukawa na mgao wa mafuta, gari Jumapili hazitembei, ingawa alikuwa ni msemaji mzuri sana. alipokuja mwinyi mafuta bwerereee.

Sasa kama Mkapa aliweza kuwa na plan akashindwa kuzitimiza akaja Kikwete akazitimiza kwa kasi zaidi akaongeza na zake kwa ari na nguvu zaidi huoni kuwa ni neema hiyo?

Ah, nadhani hukusoma vizuri nilichoandika. Nimesema miradi mingi ilishatengewa fedha wakati JK anaingia madakrani. Na nimesema kwa taratibu za kwetu rais anaingia madarakani November wakati Financial Year inaanza July, meaning kama JK aliingia November 2005 maana yake hela za miradi ya Jan-Jul 2006 ilikuwa tayari imeshapitishwa na bunge la bajeti 2005/06. Siongelei PLAN kama ambavyo umetaja naongea allocation of project funds.
 
Ah, nadhani hukusoma vizuri nilichoandika. Nimesema miradi mingi ilishatengewa fedha wakati JK anaingia madakrani. Na nimesema kwa taratibu za kwetu rais anaingia madarakani November wakati Financial Year inaanza July, meaning kama JK aliingia November 2005 maana yake hela za miradi ya Jan-Jul 2006 ilikuwa tayari imeshapitishwa na bunge la bajeti 2005/06. Siongelei PLAN kama ambavyo umetaja naongea allocation of project funds.

Sasa ukishakuwa na hiyo bajeti ndio nini? hujui kuwa bajeti zinabadilika? jaribu kuwa na uono mpana zaidi. Hata juzi bungeni tumesikia kuna miradi ilisitishwa kutatuwa tatizo la njaa.

Hata wewe katika matumizi yako unaweza kuwa na bajeti uliyojipangia lakini inaweza kuingiliana na mabo mengine. Kuwa na bajeti sio kutumia tu bajeti ina kupata vilevile. Unaweza kupanga upate 100 mazao yakazaa vizuri ukapata 120 au yasizae vizuri ukapata 80.

Muhimu ni kipi umefanya iwe kwa plan yako au ya mwenzako. Kwa barabara tusibishane, liko wazi kabisa kuwa hakuna kipindi kilichojengwa barabara nyingi za lami, za kokoto, kama kipindi hiki cha Kikwete. Usitake tuzungushane kwa maneno.

11,154 KM kipindi chake tu. Sasa kama alichiwa pesa na Nyerere, Mwinyi na Mkapa hilo mimi halinisumbuwi, wao mbona wote kwa ujumla wao hawakufanya hata nusu ya alizofanya yeye? tuwe wakweli.
 
No research,wanakurupuka tuu kishamba shamba

Mfamaji you are very right Tanzania mambo mengi zimamoto na huwa hatufanyi research ya kutosha hizi barabara zilizopo tu zenyewe kuzitunza zimetushinda lami zina vishimo,lami zina mawimbi ila watu wanataka kujenga za juu kwa juu....simple let's do the basics first barabara ziwe katika hali nzuri taa za kuongozea magari ziwe sawa ,ukaguzi wa magari ufanyike vizuri kwani asilimia 60 ya magari yanayotembea humu barabarani haswa daladala ni mabovu tukimaliza hapo tutakua tumejua kama tunahitaji hizo za juu juu
 
Mkuu wangu wala hili halina Ubishi.. barabara za juu kwa juu zinapunguza sana trafic kwa sababu nyingi sana..
Kwanza hazina traffic lights wala makutano ya njia panda hivyo magari yote yanaenda kwa mwendo wa kasi kufuatia exits zilizopo ambazo mara kwa mara huwa zinapishana kwa maili moja au mbili. Pili, mara nyingi hujengwa na lane zaidi ya mbili kila upande nchi nyingine hufikia hadi sita hivyo upo urahisi sana kwa kutoka mijini..

Sasa ukitazama miji mingi ya Marekani unakuta beltway ambazo hujengwa kuuzunguka mji na hivyo kurahisisha kutoka na kuingia mjini kulingana na sehemu unayokwenda. Japokuwa kuna misongamano pia ktk nchi hizo lakini tusisahau tu ya kwamba miji mikubwa ya Ulaya na Marekani ina population kubwa sana na pengine kila nyumba ina gari japokuwa moja. Mbali na hivyo wana subway (treni za chini kwa chini), za juu na streetcars lakini bado msongamano upo lakini sii kama wa Dar -es salaam.

Hivyo tunazungumzia magari yasiyopungua nusu ya population. Tanzania registered cars in total sidhani kama zinafika hata millioni au mbili kwa nchi nzima. Kwa hiyo barabara za juu kwa juu zinaweza kbaisa kuondoa msongamano sana tu kwani Dar safari ya maili 20 tu say Bahari hadi mjini utachukua saa nzima meaning mkimbiaji wa Olimpic ktk Marathon anaweza kufika mjini kabla yako.


Mwisho mkuu wangu jaribu kufikiria hivi, Juu ya barabara ya Morogoro Road ijengwe fly over ambayo exit yake ya kwanza ni Magomeni Mapipa wakati hiyo ya chini ipo, halafu exit nyingine Manzese, Mwenge na ikifika karibu na Kimara inashuka. Nyingine inatoka Kigamboni (kufuatia daraja) inakwenda kando kando ya bahari na kuuungana na Ali Hassan Pale Salender ubalozi wa Marekani zamani. Amini maneno yangu traffic itapungua kwa kasi kikubwa sana na gharama zake zitakuwa ndogo kuliko kujenga reli za street cars au subway..tatizo sisi mipango mibovu tu hatuna cvision zaidi ya urefu wa mkono uendao kinywani.. Maisha ni ya leo kesho siku nyingine.

Ulichosimulia sio kinachotaka kufanywa na JPM & Co. Kwa mfano @ Tazara junction, Mandela Rd itaanza kuinuliwa taratibu kusini mwa Uhuru junction na itapita juu ya Pugu road kabla ya kurudi chini taratibu. Hakuna Barbara mpya itajengwa zaidi ya kusema unachofanyika ni matengenezo ya makutano! Kiutaalamu suluu inataliwa kuangali mahitaji na uwezo wa miundombinu, njia mbadala, na vitu vitavyotufanya tuache Corolla zetu nyumbani.
Ukiangalia jiji la bongo limepangwa vibaya toka mkoloni, pia njia zake zote zinakutanika mji kati. Daraja la magogoni litaongeza matatizo ya Barbara katikati ya jiji. Nashindwa kuamini kama mipango miji ilishirikishwa, nk nk. PIA aliepeleka makao makuu Dodoma aliona mbali sema ndio kola mtu anang'ang'ania Dar. Fikiria kama ikulu ingekuwa Dom, waDar wasingekuwa wanapata kadhia ya kusimamishwa njia nzima kupisha wakuu wanchi wapite kola siku, na wale mishemishe wangehamia Dom kama waganga wa usiku walivyorundikana bungeni sass hivi.
 
Hivi nchi ambazo zina barabara za juu kwa juu hazina msongamano wa magari? Je kuna njia nyingine rahisi ya kupunguza msongamano wa magari Jijini Dar bila kuanza ujenzi wa mabarabara ya juu kwa juu? Ni kitu gani kingine basi kilicho nyuma ya push hii ya kuwa na mabarabara ya juu kwa juu? Yawezekana ni kwa ajili ya picha (postcards) au kusema na "sisi tunazo"?

What do U want? Wewe uko USA wacha sisi tuungue na JUA kinachokuuma nini? Why kila kitu unaponda?
 
Hawajakurupuka, utafiti wa kina umefanyika. Na si barabara za juu tu zinazokuja ni pamoja na mabasi ya kwenda kasi (ikimaanishwa kuwa yatakuwa na lane yao tu na hayataoingiliana na lane za magari mengine) ujenzi umeshaanza. Pantoni za kubeba watu kwa wingi kutoka bagamoyo na zikiwa na vituo vinane tofauti. Barabara za juu. Kupanuliwa baadhi ya barabara (Ali Hassan Mwinyi imeshaanza kutoka kawe mpa juu huko. Feeder road ya Mbezi Goba imeshaanza kuwa designed. Train za abiria za mjini kutka ubungo mpaka posta kuanza kabla ya mwisho wa mwaka.

Magufuli anasema, barabara hazina siasa, wa chadema anapita humo hata maandamano anafanya humo akimaliza anakwenda kulala.
Mwenyekiti nimeipenda sana hoja hii. Kusemaukweli hii haitaleta ufumbuzi Wa muda mrefu. Kama kunautafiti umewahi kufanyika basi kulikuwa na influence. Badala ya kuangalia wapi kunasababisha foleni ili kutatua ingelikuwa kwanini hapo pana foleni??? Jibu lake Ni rahisi sana. Wote wanaelekea mjini, yaaani, mabenki, maofisi ya serikali, wahindi na biashara zoo ambao ndiko kwenye Dili nk nk nk.
Kwa hiyo nini kifanyike, hamisha shughuli za serikali na kuziweka tofauti na msongamano wa traffick. Huko zinakohamishiwa, Unakuwa mji mpya. Why not, badala ya hii siasa. Mifano Ni mingii. Niishie napa, lakini yote Ni ubabaishaji, ambao Kizazi kijacho kitalipia, I am sorry to say.
 
Juzi tu hapa kulikua na uzi kuhusu wa Kenya kujenga Fly over, ukiufuata huo uzi then uusome utaona wabongo tulivyo wanafiki! yaani kule tumewasifia wakenya wanaweza then huku tunaponda eti hazina tija! Wabongo khaa.
 
Flyover ni muhimu kwetu, sasa haina maana zikijengwa tu ndio mwisho wa msongamano ila ni hatua kuelekea kupunguza msongamano. Kupunguza msongamano ni vita itaendelea kwa muda mrefu sana, maana jamii yetu bado inaendelea na ni asilimia kidogo sana ya raia wetu wana magari kwa sasa.
Mwanzo niliona wachina wakijenga flyovers kwa sululu (beijing 2nd ring) nadhani ni muda umefika kampuni za KITANZANIA zikapewa tenda - ili mradi wajenge imara, uzuri utafuata baadaye baada ya uzoefu.
 
Nchi haina wachumi

mimi ingawa kitaaluma ni mhandisi lakini sina budi sasa kuomba kazi ya kuishauri serikali kiuchumi.

maendleo hayakimbiliwi bali unatengeneza mfumo yanakuja yenyewe.

ni wapi mmeona barabara za juu zinapita kwenye makazi kama ya manzase , magomeni,

ili kupata kibarua hiki nawashauri serikali kuunda mamlaka ya uchumi sambamba na TRA ili wafanye tathmini ya kama taifa tufanye nini kwa wakati gani.

tatizo la msongamano wa magari kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya kutokuwa na udhibiti wa uchumi, fedha yote inayoingia tanzania inaishia kwenye magari, tunahesabu utajiri kwa magari

tukibalansi uchumi wetu ili fedha inayopatikana isambae katika sekta muhimu kwanza kama nyumba hatutahitaji barabara za juu kwa sasa.
wewe jiulize kama unataka gari kama ni mtumishi wa serikali serikali yenyewe inakukopesha, na inakusamehe kodi ila ukitaka kujenga inakuuzia kiwanja si chini ya milioni nne.

kwa wachumi wa kweli wanaojua mzunguko wa fedha wanatambua athali za kiuchumi kwa kununua magali kwa wingi na fedha ikaishia huko na kwa fedha kkujenga nyumba na fedha hiyo ikabaki kwenye mzunguko wetu. kumbuka ukinunua gari kila mwaka unapeleka fedha ngapi nje kununa mafuta na vipuri.
 
Back
Top Bottom