Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh umekuwa mhandisi sasa! I don't understand what you want! no consistence in what you're saying. One minute you want feeder roads the next you want outer roadsnjia mojawapo ya kupunguza foleni badala ya kutengeneza mabarabara ya juu kwa juu ni kujenga outer drives...
Nilibahatika kufika Nairobi japo sikukaa siku nyingi lakini nilibahatika kuangalia hizo fly over jinsi zilivyo nikajiuliza hii idea ya kujenga fly over hapa Dar nikaona sijui itakuaje maana zinahitaji space ya kutosha hasa ukizingatia kuna sehemu wanalundika udongo umbali flani ili wapate slope ya kiana wakati gari linapanda. Huwa najiuliza kwa Dar sijui itakuaje na sidhani kama kuna ambao walijiuliza kuhusu hili unless kama majengo mengine mengi yavunjwe ndio mradi huu ukamilike
Ungeisoma hiyo habari mpaka mwisho ungekutana na hiki:
"The Arusha Minjingu Road (90 km) which is part of the Great North Corridor is fully funded by the World Bank. The rehabilitation of this project will be of a contract amount of Tshs. 75,510,520,575.86 excluding Value Added Tax (VAT) and is expected to be completed by October 2013."
Nadhani usingeuliza swali lako. Tatizo hamsomi mkaelewa au huwa mnakurupuka.
Hili suala linaitaji taaluma sio siasa...kila mwanasiasa akija na mawazo yake hakuna kitakachofanyika..
zomba, lugha mtihani...inanipiga chenga.
Siku hizi watu hawana "excuse" hiyo. Unabandua kipande usichokijuwa unakibandika "google translate" mambo swaafi kabisa. Mie hata Wachina wakiniandikia Kichina nawajibu Kiswahili tunaelewana na kila mtu happy 快乐.
Chukuwa hilo neno la kichina libandike hapa uone mwenyewe kwa raha zako: Google Translate
Mie CCM damu ila siko sana kisiasa kwenye masuala ya kitaalamu! Magufuli, some points to chew bro!
Zipo flyover hizo za kujaza udongo na zipo za kujenga maguzo ya concrete. Nyumba zingine inabidi ziondoke. Gharama za kutokuwa na maendeleo ya barabara za uhakika ni kubwa kuliko majumba yanayobomolewa.
Tatizo letu hapo kwenye kubomoa nyumba kwani majengo mengi ya serikali yakiwa kwenye hifadhi tu ya barabara mara nyingi hayabomolewi lakini kiukweli kuna mitaa mingine Dar nyumba mtaa mzima zinatakiwa zibomolewe warekebishe miundo mbinu lakini kwa kuwa nchi inaongozwa na wanasiasa wasiojiamini utasikia hawa ni wapiga kura wangu inabidi serikali iangalie namna ya kuwasaidia matokeo yake hazibomolewi. Hii nchi wanasiasa wakikubali kuitwa wanoko kisa wanasimamia sheria na maamuzi nadhani mabadiliko yanawezekana maana fly over inahitaji space na si lazima katikati ya jiji tu hata nje ya jiji mambo yanawezekana pia
Kupanga ni kuchagua!
Ukitaka kila gari linalotoka jijini kuelekea Morogoro lipite UBUNGO, basi unahitaji barabara za juu kwa juu pale makutano ya UBUNGO. Lakini ukiwa na ubunifu kwamba si kila aendaye Moro ni lazima apite UBUNGO, basi utaanza na kile kilicho katika uwezo wako - tengeneza barabara mbadala kutoka maeneo mbalimbali kuelekea Kimara, Mbezi, bagamoyo, Kibaha, nk.
ndiyo 'na sisi tumo'
Research ilifanywa na iko dizaini kamili ya namna ya kupunguza msongomano dar. Tena nakumbuka ilifanywa na wajapani wakishirikiana na wataalaam wa chuo kikuu na wengineo. Na hii ni mwanzo tu wakutekeleza yaliyomo.
Pitia pitia mitandao utaupata huo utafiti, niliusoma kwenye mtandao lakini sikuweka kumbukumbu ni muda mrefu.
Barabara za juu zinapunguza sana msongamano, hilo halina ubishi.
Mabadiliko ya miundombinu yameanza kwa kasi kipindi cha Kikwete kuliko wakati wowote ule na tunayaona.
I agree with you Ritz...halafu lini tutaanza kuboresha miundo mbinu kama hatuna moyo wa uthubutu na nia ya kurekebisha makosa yaliyokwisha fanywa kabla. Miji yetu mingi haikupangiliwa na ndio chanzo cha matatizo leo tunapoanza kuona ongezo la watu na vitendea kazi mbali mbali. Kama bado tunaendesha fikra kisiasa tutaendelea kukwama maana siasa inataka kuenzi fikra za chama kwanza.
Naunga mkono hii step ya kuamua kujaribu kufanya kitu tofauti