zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Mkuu mimi nimefanya kazi na wajapan na miradi yao ya JICA. kuna siku moja bosi wangu aliniambia kuwa JICA huwa wanakaa na wakandarasi wao na kudesign miradi kwenye nchi masikini na kuishauri serikali yao ili hela itoke na waom wapate fungu hapo. Its purely business.
Hebu tuwe wakweli, pale TAZARA ukiweka hizo flyovers. zitaenda mpaka wapi? pale KAMATA kwenda kariakoo ni foleni tu, kwenda city centre ni barabara zile zile
Hata pale Ubungo mataa, ukifika jangwani utaenda wapi au ukifika pale Bahama mama unapita wapi mpaka ufike mbezi na kiluvya?
Suluhishmla kwanza ilitakiwa serikali ihakikishe magari ya umma (dala dala) ziwe na hadhi y mtu kupanda amevaa suti bila bugudha. we jaribu kupanda gari ya mbagala pale posta mpya au kivukoni jioni uone balaa lake.
Then city centre ilitakiwa magari yaingie kwa vibali maalum. sasa hata boda boda utaziona zinapita pale nje ya ikulu. sasa hapo foleni zitaishia wapi wakati city centre haina utaratibu wa kuingia?
Kama public transport ingekuwa reliable naamini wengi tungeacha magari yetu home.
Kwani wakienda huko nje hawaoni wenzao wanavyofanya?
Tatizo serikali etu uwezo wake wa kufikiria unaishia kwenye kiwango cha familia za watendaji wakuu wa serikali
Nadhani hujaiona master plan kamili, barabara zote kuanzia Kilwa Road (mbele ya Mbagala) mpaka Kariakoo, Kimara mpaka Ferry, Pugu Mpaka Kariakoo, Magomeni mpaka Morocco. Tegeta mpaka Morroco, zote zinapanuliwa kwa phases na patapokuwa na ma flyover ni sehemu nyingi tu, lakini lakini kama anavyosema Magufuli "kuchaguwa ni kupanga". Isitoshe kuna mradi wa Daraja la Kigamboni na barabara mpya kuania huko itayolizunguka jiji (ring road). Usifikiri huu ni mradi wa siku mbili tatu, inakadiriwa kuwa utakwisha mwaka 2030 (miaka 18 kuanzia sasa) ni mambo ya muda mrefu lakini inabidi yaanzie mahali fulani na ndiyo yameanza kama uonavyo.
Kuhusu JICA kutengeneza fedha, hilo halina tatizo mradi wanafanya kazi zinazoridhisha na hawamuibii mtu.